Gwajima: Taifa tumekosa maono, inakuwaje kujenga reli kabla ya kuchimba chuma? Waziri Mwigulu ampinga

Mimi nimejibu kama mchumi tena professsional yeye amezungumza kama layman asiyeelewa abc za uchumi



Mimi nimechangia kama,mchumi yeye amazungumza kama layman .
Ndio umuhimu wa watanzania mlioelimika kama wewe kuchukua point Kwa Hawa wanasiasa wachumia tumbo na kujenga hoja ya kukomboa taifa letu na kushauri njia sahihi
 
Sidhani kama nyanya zimevunwa na zipo tayari ni kwamba eneo la kulima tunalo na maji ya kuwagilizia yapo...., cha kujiuliza tukienda kununua kwa jirani je ni gharama nafuu / ndogo kuliko tukilima sisi na kumwagilizia (ingekuwa bora kama tungelima na sisi tukamuuzia jirani ila kwa utunzaji wetu na gharama za bili za maji je tukishavuna tutaweza kuuza kwa bei anayouza yeye)?

Hayo ni maswali muhimu sana katika kungalia opportunity costs
 
Hiyo Gwajima hajui anachoongea hicho chuma kina Siasa zake za kitaalam ambazo ukisubiri hautakuja kujenga hiyo Reli, mbona hashangai tunachimba gas lakini bei ya kuinunua ikojuu?
 
Na.hii ndio sababu wanamchukia January.
 
Wewe unadharaulisha sana ubongo wako,chuma kipo,hutaki kuchimba,unaagiza nje,ni akili hiyo?
 
Bila shaka wewe ni mwanaccm.Suala alilosema Mch.Gwajima ni sahihi.Tungeokoa US$2.2 billion=Tshs ngapi?Hicho chuma cha Mchuchuma/Liganga pekee kingechimbwa kikamilifu ingefanya Tanzania ijenge reli hadi vijijini na wilayani badala ya kuhangaika na lami.Tungeweza kuwa na Network ya reli kuunganisha nchi yetu lakini kwa kukosa Dira/Maono ya Taifa tunaagiza chuma.
Tunazo raslimali za gesi asilia lakini tunaagiza gesi,mbolea na mafuta.Tanzania kuna uwezekano wa kuzalisha umeme wa jua,upepo,joto ardhi au biogas,lakini serikali inawaza tozo na kuongeza kodi.
Hakuna Dira/maono ya kitaifa na Mch.yupo sahihi,at least kwa hoja hiyo.
 
H
Wewe unadharaulisha sana ubongo wako,chuma kipo,hutaki kuchimba,unaagiza nje,ni akili hiyo?
Hata Nyerere aliamua, tusichimbe kwanza madini maana,hayaozi tusubiri hadi tutakapokuwa na,uwezo ili yaweze kutunufaisha. Nadhani unaelewa kilichotokea baada ya Nyerere kutoka madarakani, mikataba ya ovyo iliingiwa na awamu zilizofuata hasa ya JK ambapo ni kama wawekezaji walisomba madini burexkwa kulipa kodi kiduchu hafi JPM aliporekebisha mikataba ya madini ndipo walau tunapata kiasi cha kuridhisha.
 
Ndugu yangu uchumi hauko hivyo.
Natamani nikupe lecture lakini muda hauruhusu.
 
Wewe unadharaulisha sana ubongo wako,chuma kipo,hutaki kuchimba,unaagiza nje,ni akili hiyo?
Hatuna uwezo wa kuchimba, kuprocess na mtaji, kama unakumbuka hata kiwanda cha karatasi cha,Mgololo, Mufindi kilitushinda kuendesha.
 
Swali gani la ajabu unauliza. Kwani wapi kwenye katiba wamesema kuna mtu anaitwa Gwajima ndio anatakiwa kuzungumzia matatizo yote ya nchi hii?

Yeye kaamua kuzungumzia chuma, jibu hoja yake sio kuuliza kwanini hajazungumzia viberiti sijui pamba wala utapiamlo wa watoto wenu. Kwahiyo angesemea hiyo dhahabu napo ungekuja kuuliza mbona hajasema chuma?
Cha kusikitisha hizi akili ndizo mnatumia kuendesha familia
 
Kipi kinafanya uchimbaji wa iron ore ya Tanzania uwe wa gharama kubwa ila hiyo hiyo ore inasafirishwa kwenda nje inatengeneza vyuma na vinauzika soko la kimataifa?
Japan inasafirisha iron ore kutoka duniani kote inazalisha vyuma na kuuza kisha sisi tumeyalalia tu.

Kipi kinafanya production cost za steel ziwe kubwa kwa Tanzania hii. Kuna maajabu gani kwenye steel ukishakuwa na umeme na raw materials, yani kutengeneza matairi ni vigumu kuliko kutengeneza steel.

Uganda wako mbioni kutuzidi kwenye hii sekta. Hakuna nchi iliwahi endelea bila chuma hatutakiwi kuwa na visingizio. Kuanzia China na Uturuki walioanza na textile manufacturing, kuja Japan na South Korea kwenye shipbuilding, kuja Germany kwenye automobile au Russia wenye extensive railway systems hakuna aliyenunua chuma nje.

Tukizalisha sisi wenyewe tunachukua malighafi kwenye machimbo yetu hapo gharama inakuwaje kubwa kushindikana kuwa controlled
 

Everything you need to know about the industry breakdown.


Average investment costs za kujenga steel mills (plant) kuvuka $4 billion sio jambo la ajabu kabisa.


Average running costs ya large steel mill ni $1 billion dollars
..........

Na kuna costs zingine luluki ata kuziongelea ni shida.

Sasa ni hivi tukirudi kwenye dunia ya ukweli:

Tanzania inanunua chuma kwa wastani wa $400 million kwa mwaka; reli ikiisha na mradi wa bwawa hiyo level itashuka. Wakati expenses tu kuendesha kiwanda kikubwa cha chuma $1 billion kwa mwaka. Kwa hali ya sasa tungekuwa na kiwanda serikali ingekuwa inatoa ruzuku $600 kuwa na kiwanda tu; can you see why nikaongelea maswala ya break even.

Pili hakuna bank wala donor itakayoipa Tanzania hela ya kuwekeza kwenye hiyo mill in the first place; na hakuna hayo mapato ya ndani ya ku fund hiyo project.

Tatu ata tukiweza kuwekeza kwenye Mills, inabidi tujenge kwanza which might take years, halafu baada ya hapo tutafute hela tena za kujenga hiyo reli sums which might amount to 10s of billions na muda mrefu sana kabla ya kuanza kuona matunda ya reli yenyewe (be it ni ndoto za mchana kwa mazingira ya sasa).

Huyo Gwajima porojo zake abaki nazo huko huko kwenye kanisa lake, sio kuichosha dunia kusikiliza upuuzi wake; hakuna lolote la maana aliloongea zaidi ya ujinga mtupu.
 
Bora umenisaidia kumjibu huyo asiyejielewa
Shida wametanguliza chuki kwa mtu binafsi mpk wanashindwa kuona logic ya anachokiongea!
 
Sasa Mwigulu hiyo vision 2025 ndio mpango wa muda mrefu? Unajua tofauti ya short na long term Plans? Miaka 25 huwezi kuita long term ni makosa! Projections za miaka angalau 50 ijayo would suffice. Inakupa maono ya jinsi mnavyotegemea nchi iwe!
Ni mpango wa mda wa Kati,haujaanza leo kutekelezwa.
 
Hakuna benki ya kimataifa au donor atakupa pesa ujenge steel mill. hili limeandikwa sana. Dunia ipo hivyo. Na kazi ya chuma si kujenga reli tu kwamba reli ikiisha kitakosa soko. Chuma ni muundombinu ambao si rahisi kuuwekea monetary value. Ni kama vile shule au hospitali. Hakuna nchi imeendelea bila kujitosheleza kwa chuma. Leo unaagiza chuma China, halafu China anaingia mgogoro na Australia. Unafikiri utakuwa kwenye hali gani? Chuma ni muhimu kuliko umeme maana mapinduzi ya viwanda yanaweza tokea bila umeme ila hayawezi kutokea bila chuma. Lakini watu huwa hatuulizi sana bei ya power plants maana tunajua faida yake. Sasa chuma ni zaidi ya umeme.

Gwajima katika hili yupo sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…