Steel imeanza kuzalishwa kabla ya uzalishaji wa umeme. Mapinduzi ya viwanda yaliletwa na steel na engine si umeme. Hapo nilikuwa nakupa mfano jinsi steel ilivyo muhimu. Labda kwa tech ya sasa inaweza isiwe sawa kuzalisha bila umeme lakini steel ilianza kabla ya umeme.
Hiyo $1bln umesema ni wastani. Maana yake tunaweza kuwa na mills zinazotumia $ 400m au 500m kwa mwaka na kucover mahitaji yetu kwanza.
Na mwisho, chuma ni kama hospitali, barabara au shule. Si rahisi kupima faida za kifedha za hospitali.
Hakuna investment isiyokuwa na monetary value in economics ata public goods kama taa za barabarani unaweza pima faida zake kwa idadi ya uporaji uliopungua, gharama za matibabu kwa wahanga wa vibaka, thamani ya vitu vilivyookolewa, gharama zilizokolewa kufanya upelelezi na polisi, gharama kesi za kuendesha kesi mahakamani and so forth; uka justify jamii inaokoa kiasi kadhaa cha fedha kwa sababu taa zimepunguza uporaji wa usiku.
Na unapotaka kukiweka chuma kwenye merit good or anyother investment faida zake unapima on cascading effects za baadae kuna monetary value pia.
Sasa kuna faida gani ya kutumia $1-4 billion kujenga kiwanda cha chuma (hapo atujazungumzia gharama za mineral extraction investment ambazo na zenyewe zipo in billion of dollars).
Halafu baada ya kuwekeza utumie na zaidi ya $600 million dollars kwa mwaka kama ruzuku ili tu useme unakiwanda cha chuma.
Wakati unaweza agiza chuma kwa gharama za $400 million tena hiyo ni kwa sababu ya miradi mikubwa miwili ikiisha uagizaji kwa ukuaji wa uchumi leo hiko kiwango kinashuka bila ya shaka.
Ni hivi kuna vitu vina minimum investment costs watu wakisema kiwanda cha kati wanapiga hesabu zote machine, gharama za kiwanda and other necessary components awajisemei tu steel mill ina cost kati ya dollar billion 1 mpaka 4 kutoka vichwani mwao.
Na wanaposema running costs wanazingatia productions costs zote wanakuja na average; hiyo research imeangalia viwanda 350 vya chuma duniani wamekuja na wastani wa dollar billion moja kukiendesha kiwanda cha kati kwa mwaka.
Sasa watanzania kama ilivyo hulka yetu badala ya ku deal na facts tunaanza kutengeneza hadithi vichwani mwetu na kuondoka kwenye uhalisia na kuanzisha mijadala ya kujifurahisha tu kama huu.
Unataka kuzungumzia uzalishaji chuma zama za kale ni nishati pia ilitumika ya makaa ya mawe ambazo gharama zake leo ukilinganisha na bei ya umeme hakuna mtu mwenye akili zake timamu atatumia hizo mbinu.
Halafu kama ujawahi kuangalia documentaries za uzalishaji wenyewe wa zamani utaki kujua uvunjifu wa haki za binadamu humo ndani na average life expectancy ya wafanyakazi the whole thing was barbaric ambayo binadamu wa dunia ya leo awawezi kukubali kabisa.
Tatizo letu tunapenda kuona vitu ni rahisi kweli ingekuwa ivyo si nchi za africa zingekuwa na ivyo viwanda by ku refine crude oil, chuma na nonsense zingine kubwa kubwa tunazotamani bila ya uwezo.
Tutafika huko siku moja lakini embu tujikite na tunayoyaweza kwanza na yaliyo muhimu kukuza chumi zetu.