Gwajima: Taifa tumekosa maono, inakuwaje kujenga reli kabla ya kuchimba chuma? Waziri Mwigulu ampinga

Gwajima: Taifa tumekosa maono, inakuwaje kujenga reli kabla ya kuchimba chuma? Waziri Mwigulu ampinga

Mawazo ya Gwajima ni potofu na ya unafiki. Kiuchumi sio lazima nchi iwe na chuma ndio ijenge reli wala hata kama ina chuma sio lazima kwanza kuchimba chuma ndipo nchi ijenge reli. Kila ntu sasa anajifanya mchumi!.
Ziko nchi nyingi tu zimejenga reli na hazina hicho chuma.

Unapotaka kujenga reli unatangaza tenda baada ya kuwa umefanya tathmini reli itajengwa vipi na costs ni kiasi gani. Mkandarasi akishapatikana ndiye anajua vyuma atanunua wapi na kwa bei gani; sisi tunachotaka tukabidhiwe reli iliyojengwa kwa viwango na kwa wakati.

Hicho chuma ikitokea kimechimbwa siku moja kitauzwa kwa wateja wanaohitaji wa nje na ndani ya nchi na kitaingiza mapato ya fexha za kigeni na pia shilingi.

Hakuna nchi inazalisha kila kitu yenyewe na sio lazima kiuchumi tuzalishe kila kitu, vingine tutaagiza tupende tusipende; ndio maana kuna kitu kinaitwa comparative advantage katika biashara ya kimataifa sio suala la kuzalisha tu
Loh, hapana! Ingawa Gwajima anaelezea nini kianze kati ya reli na kuchimba chuma, wewe umepotoka kabisa kufikiri kuwa chuma ni bidhaa kama zingine tu. Ukiacha Uingereza, nchi ya kwanza kuwa na viwanda, nchi zingine zote zilizoendelea zimeendelea kutokana na chuma na makaa ya mawe. Soma kuhusu Ruhr Valley na maendeleo ya viwanda vya Ufaransa na Ujerumani. Jikumbushe kiu ya Uchina ya makaa ya mawe na chuma ya hivi karibuni. Makaa ya mawe, pamoja na uchafuzi wake wa mazingira, ndiyo prime fuel ya viwanda. Viwanda huendelezwa na metal-working industries. Metal working industries chakula chake ni chuma.
 
Hakuna benki ya kimataifa au donor atakupa pesa ujenge steel mill. hili limeandikwa sana. Dunia ipo hivyo. Na kazi ya chuma si kujenga reli tu kwamba reli ikiisha kitakosa soko. Chuma ni muundombinu ambao si rahisi kuuwekea monetary value. Ni kama vile shule au hospitali. Hakuna nchi imeendelea bila kujitosheleza kwa chuma. Leo unaagiza chuma China, halafu China anaingia mgogoro na Australia. Unafikiri utakuwa kwenye hali gani? Chuma ni muhimu kuliko umeme maana mapinduzi ya viwanda yanaweza tokea bila umeme ila hayawezi kutokea bila chuma. Lakini watu huwa hatuulizi sana bei ya power plants maana tunajua faida yake. Sasa chuma ni zaidi ya umeme.

Gwajima katika hili yupo sahihi.
Sahihi
 
Mbona sukari ya ndani ina bei kuliko na nje? hatujiulizi kwanini? nchi hii inashida kwenye mifumo ya tax sio attractive nchi inatoza kodi kubwa sana haivutii ni rahisi kuwa na kiwanda china kuliko hapa ndio maana unakuta bidhaa za ndani zinabei kuliko za nje pamoja na ushuru. Nchi ina cheap labour lakini kwanini viwanda vinashindwa kushindana mp
Hili siyo tatizo la taxation tu, kuna umasikini wa fikra ambao ndiyo msingi wa shida zote.
Ni lazima kuweka uhuru wa kukuza teknolojia kwa wazawa badala ya kutegemea Kila kitu kutoka nje.
Hata chuma kutoka mradi wa Liganga na Mchuchuma chaweza kuwa ghali kwa sababu hizo hizo za umasikini wa fikra.
Gharama za uzalishaji zaweza kupandishwa hadi kuwa ghali kuliko impotation.
 
Hakuna benki ya kimataifa au donor atakupa pesa ujenge steel mill. hili limeandikwa sana. Dunia ipo hivyo. Na kazi ya chuma si kujenga reli tu kwamba reli ikiisha kitakosa soko. Chuma ni muundombinu ambao si rahisi kuuwekea monetary value. Ni kama vile shule au hospitali. Hakuna nchi imeendelea bila kujitosheleza kwa chuma. Leo unaagiza chuma China, halafu China anaingia mgogoro na Australia. Unafikiri utakuwa kwenye hali gani? Chuma ni muhimu kuliko umeme maana mapinduzi ya viwanda yanaweza tokea bila umeme ila hayawezi kutokea bila chuma. Lakini watu huwa hatuulizi sana bei ya power plants maana tunajua faida yake. Sasa chuma ni zaidi ya umeme.

Gwajima katika hili yupo sahihi.
Chuma na umeme sio kitendawili cha kuku na yai kipi kimetangulia.

Uwezi kuwa na steel industry kama huna umeme wa kupeleka viwandani. Hiyo running cost kiasi kikubwa ni umeme na hizo ni nchi zenye unit costs ndogo za umeme kushinda Tanzania.

Halafu hoja ya msingi ni kwamba kuna minimum costs ambazo lazima uzalishe zaidi ya hapo vinginevyo ni hasara. Sasa umeshaambiwa average running costs za kiwanda cha wastani ni $1 billion kwa mwaka na sisi kama nchi at the height of importation tulikuwa tunaagiza $400 million worth of steel.

How do you account for that $600 million production costs deficit annually? Utatoa ruzuku ya tsh 1.5 trillion mwaka ama?

Wakati huo huo ungesaidia labda kutueleza hizo hela za kujenga kiwanda zitatoka wapi kwa sasa kama hakuna mwekezaji wa kutoka nje na kama yupo ebu mtaje.

Mkuu embu tujikite kwenye mijadala ya maendeleo iliyo size yetu; reli ikiisha inauwezo wa kuzalisha trillion plus kirahisi annually kama mapato ya kibiashara plus other taxes serikali ikiwa mmiliki wa biashara kwa asilimia 100.
 
Akumbushwe kupeleka wapiga kura Bamingam
Mimi nilihama mkoa, nikahamia jimboni Kawe, nikiwa na safari ya matumaini BIRMINGHAM!
Aache Kuongea pumba akitumwa na investors!

Sasa anataka tuchimbe Chuma, tuna smelter!? Au ndiyo anafanya udalali hapo wa wasafirishaji udongo!?
 
Steel imeanza kuzalishwa kabla ya uzalishaji wa umeme. Mapinduzi ya viwanda yaliletwa na steel na engine si umeme. Hapo nilikuwa nakupa mfano jinsi steel ilivyo muhimu. Labda kwa tech ya sasa inaweza isiwe sawa kuzalisha bila umeme lakini steel ilianza kabla ya umeme.

Hiyo $1bln umesema ni wastani. Maana yake tunaweza kuwa na mills zinazotumia $ 400m au 500m kwa mwaka na kucover mahitaji yetu kwanza.

Na mwisho, chuma ni kama hospitali, barabara au shule. Si rahisi kupima faida za kifedha za hospitali.
 
Pamoja na utapeli wa Gwajima, kuanzia kwenye Imani ( ukristo) hadi ubunge unaolalamikiwa kwa wizi wa kura, bado ana hoja za msingi ambazo lazima tumuunge mkono.
Gwajima ana mambo chanya ambayo tunatakiwa tuungane naye na pia hasi yanayohitaji tuyapuuze.
 
Hiyo Liganga na Mchuchuma tokea nianze kuisikia, sijui ni miaka mingapi imepita bila kuona matokeo...
 
Mawazo ya Gwajima ni potofu na ya unafiki. Kiuchumi sio lazima nchi iwe na chuma ndio ijenge reli wala hata kama ina chuma sio lazima kwanza kuchimba chuma ndipo nchi ijenge reli. Kila ntu sasa anajifanya mchumi!.
Ziko nchi nyingi tu zimejenga reli na hazina hicho chuma.

Unapotaka kujenga reli unatangaza tenda baada ya kuwa umefanya tathmini reli itajengwa vipi na costs ni kiasi gani. Mkandarasi akishapatikana ndiye anajua vyuma atanunua wapi na kwa bei gani; sisi tunachotaka tukabidhiwe reli iliyojengwa kwa viwango na kwa wakati.

Hicho chuma ikitokea kimechimbwa siku moja kitauzwa kwa wateja wanaohitaji wa nje na ndani ya nchi na kitaingiza mapato ya fexha za kigeni na pia shilingi.

Hakuna nchi inazalisha kila kitu yenyewe na sio lazima kiuchumi tuzalishe kila kitu, vingine tutaagiza tupende tusipende; ndio maana kuna kitu kinaitwa comparative advantage katika biashara ya kimataifa sio suala la kuzalisha tu
Pamoja na yote uliyoandika na kuchambua hujaeleweka ktk hoja ya Gwajiboy.Msikilize vizuri
 
Steel imeanza kuzalishwa kabla ya uzalishaji wa umeme. Mapinduzi ya viwanda yaliletwa na steel na engine si umeme. Hapo nilikuwa nakupa mfano jinsi steel ilivyo muhimu. Labda kwa tech ya sasa inaweza isiwe sawa kuzalisha bila umeme lakini steel ilianza kabla ya umeme.

Hiyo $1bln umesema ni wastani. Maana yake tunaweza kuwa na mills zinazotumia $ 400m au 500m kwa mwaka na kucover mahitaji yetu kwanza.

Na mwisho, chuma ni kama hospitali, barabara au shule. Si rahisi kupima faida za kifedha za hospitali.
Hakuna investment isiyokuwa na monetary value in economics ata public goods kama taa za barabarani unaweza pima faida zake kwa idadi ya uporaji uliopungua, gharama za matibabu kwa wahanga wa vibaka, thamani ya vitu vilivyookolewa, gharama zilizokolewa kufanya upelelezi na polisi, gharama kesi za kuendesha kesi mahakamani and so forth; uka justify jamii inaokoa kiasi kadhaa cha fedha kwa sababu taa zimepunguza uporaji wa usiku.

Na unapotaka kukiweka chuma kwenye merit good or anyother investment faida zake unapima on cascading effects za baadae kuna monetary value pia.

Sasa kuna faida gani ya kutumia $1-4 billion kujenga kiwanda cha chuma (hapo atujazungumzia gharama za mineral extraction investment ambazo na zenyewe zipo in billion of dollars).

Halafu baada ya kuwekeza utumie na zaidi ya $600 million dollars kwa mwaka kama ruzuku ili tu useme unakiwanda cha chuma.

Wakati unaweza agiza chuma kwa gharama za $400 million tena hiyo ni kwa sababu ya miradi mikubwa miwili ikiisha uagizaji kwa ukuaji wa uchumi leo hiko kiwango kinashuka bila ya shaka.

Ni hivi kuna vitu vina minimum investment costs watu wakisema kiwanda cha kati wanapiga hesabu zote machine, gharama za kiwanda and other necessary components awajisemei tu steel mill ina cost kati ya dollar billion 1 mpaka 4 kutoka vichwani mwao.

Na wanaposema running costs wanazingatia productions costs zote wanakuja na average; hiyo research imeangalia viwanda 350 vya chuma duniani wamekuja na wastani wa dollar billion moja kukiendesha kiwanda cha kati kwa mwaka.

Sasa watanzania kama ilivyo hulka yetu badala ya ku deal na facts tunaanza kutengeneza hadithi vichwani mwetu na kuondoka kwenye uhalisia na kuanzisha mijadala ya kujifurahisha tu kama huu.

Unataka kuzungumzia uzalishaji chuma zama za kale ni nishati pia ilitumika ya makaa ya mawe ambazo gharama zake leo ukilinganisha na bei ya umeme hakuna mtu mwenye akili zake timamu atatumia hizo mbinu.

Halafu kama ujawahi kuangalia documentaries za uzalishaji wenyewe wa zamani utaki kujua uvunjifu wa haki za binadamu humo ndani na average life expectancy ya wafanyakazi the whole thing was barbaric ambayo binadamu wa dunia ya leo awawezi kukubali kabisa.

Tatizo letu tunapenda kuona vitu ni rahisi kweli ingekuwa ivyo si nchi za africa zingekuwa na ivyo viwanda by ku refine crude oil, chuma na nonsense zingine kubwa kubwa tunazotamani bila ya uwezo.

Tutafika huko siku moja lakini embu tujikite na tunayoyaweza kwanza na yaliyo muhimu kukuza chumi zetu.
 
Gwajima yupo sahihi. Ni kazi sana kwa nchi kuendelea bila chuma. Ukiwa na chuma utajenga reli kwa bei rahisi, utajenga nyingi, utajenga mabehewa. Na itakuwa rahisi kwako kurekebisha. Hao wakina Mwigulu wamekalia porojo za LNG utafikiri ni mtambo wetu!!
Huo umeme wa kuyeyusha hicho chuma mnao?au mnafikili hicho chuma kinategea umeme kama viwanda vya pale mwenge kwa waindi,chuma hiyo inaitaji mtaji mkubwa ndio maana wawekezaji wanapakimbia,kama pangekuwa ni laisi hiyo biashara ingefanyika tokea enzi za mkapa.
 
Ndugu yangu uchumi hauko hivyo.
Natamani nikupe lecture lakini muda hauruhusu.
Muda wa kunipa lecture hauna lakini wa kuitetea CCM unao,kusifia Royal Tour upo na kupinga Katiba Mpya mnao.
Uchumi ukoje kama hatuwezi kuwekeza katika raslimali zinazoweza kuuinua uchumi wetu.Chuma tunacho ila tunajenga reli kwa kuagiza chuma?Uchumi gani unaoufahamu wewe hadi unipe lecture!
 
Huo umeme wa kuyeyusha hicho chuma mnao?au mnafikili hicho chuma kinategea umeme kama viwanda vya pale mwenge kwa waindi,chuma hiyo inaitaji mtaji mkubwa ndio maana wawekezaji wanapakimbia,kama pangekuwa ni laisi hiyo biashara ingefanyika tokea enzi za mkapa.
Unapotosha ama upo serious?Mungu aliweka chuma chetu pamoja na makaa ya mawe,unataka umeme wa nini tena?
 
Mbunge wa Kawe akiwa bungeni, Joseph Gwajima amesema kwa miaka mitano Taifa limelipa fedha za kigeni dola za kimarekani bilioni 2.2, Gwajima amesema kwa mtu yoyote mwenye akili na anajua kuzitumia jambo hili hawezi kuruhusu kufanyika.

Gwajima amesema nchi imeanza na reli ambayo hayupo kinyume nayo lakini ameshangaa kuanza na reli ambayo 'component' kubwa ni chuma kwa kukiagiza nje ya nchi badala ya kuchimba chuma kisha kujenga reli.

Gwajima amesema kinachosumbua ni kukosa maono ya Taifa, mipango ya Taifa na dira.

Gwajima amesema Taifa linahitaji maono ya pamoja na hakuna nchi duniani iliyoendelea kwa miaka mitano au kumi.

Kingu-Taarifa
Kingu akichangia kupitia taarifa, amesema hadi tume ya kutengeneza mipango ya muda mrefu imefutwa. Amesema Taifa halina tume ya mipango kuanzia miaka 50.

Mwigulu akanusha
Waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba amekanusha na kusema Taifa lina mipango ya muda mrefu na tangu uhuru limeongozwa na viongozi wenye maono na ndio maana kuna dira ya 2025 kutoka kwa Mkapa.

Mwigulu amesema nchi imeongozwa kwa maono ndio maana ipo ilipo. Mwigulu amemaliza kwa kusema Rais ameshaweka utekelezaji wa miradi mikubwa, yote inaenda kutekelezwa ya Liganga, LNG.
Haya asingesema kipindi cha Magu na hakuyasema. Au ana maana maono yameanza kukosekana awamu ya sita.
 
Pamoja na utapeli wa Gwajima, kuanzia kwenye Imani ( ukristo) hadi ubunge unaolalamikiwa kwa wizi wa kura, bado ana hoja za msingi ambazo lazima tumuunge mkono.
Gwajima ana mambo chanya ambayo tunatakiwa tuungane naye na pia hasi yanayohitaji tuyapuuze.
Matapeli siku zote huonekana wana mambo ya msingi! Ndiyo maana halisi ya utapeli!
Deep down wana personal interests za binafsi kuliko ubinafsi!

Hapo Kawe kuna matatizo ya kutosha. Kutwa kuongelea mada za kujipigia chapuo za udalali!

Tapeli ni tapeli. Hukawii kukuta kuna watu huko anawapiga akiwahakikishia atalisimamia jambo lao la chuma!
 
Back
Top Bottom