Gwambina FC 0-1 Simba SC | Simba yapaa kileleni

Gwambina FC 0-1 Simba SC | Simba yapaa kileleni

Kuhusu ubingwa!!!

Mpaka Sasa Yanga kabakiza Mechi 8.anatakiwa ashinde mechi zote huku akiombea simba apoteze mechi Tatu, msimamo unakuwa [emoji1313][emoji1313][emoji1313]
Yanga point 81
Simba 79
Azam 74

Azam kabakisha mechi 8, anatakiwa ashinde zote huku akiombea Yanga apoteze mechi tatu kati ya mechi nane na Simba apoteze Mechi tano kati ya mechi 11 alizobaki nazo
Msimamo unakuwa
[emoji1313][emoji1313][emoji1313][emoji1313][emoji1313][emoji1313][emoji1313][emoji1313]
Azam point 74
Simba point 72
Yanga point 71

Simba amebakiwa na Mechi 11 mkononi, ili awe bingwa anatakiwa ashinde Mechi 9 na afungwe Mechi mbili.Wakati huo Yanga na Azam washinde game zote nane
Msimamo unakuwa [emoji1313][emoji1313][emoji1313][emoji1313][emoji1313][emoji1313][emoji1313][emoji1313][emoji1313]
Simba point 82✓
Yanga Point 81✓
Azam point 74✓

Mpaka Sasa Simba ana 89% ya kuwa bingwa..Mechi 11 mkononi Ni faida kubwa✓

Kabla ya mechi ya leo, apo tumebakisha mechi 10
Uchambuzi wako naudhamini.
Nimejiridhisha pasinachembe ya shaka ntauuza kwa mashabiki wa Simba na kupata faida.
Njoo inbobo tuyajenge tufunge mkataba.

Simba mabilioni sports club mpaka mashabiki tunafunga mikataba huku.
Yanga bakini na Albadiri zenu.
 
Pongezi ziende kwa Simba hasa benchi la ufundi na wachezaji wote kwa ujumla wao kwani "game plan' imefanya kazi vizuri kutokana na uwanja kuwakaba wasicheze aina yao mpira. Leo wangejichanganya kidogo tu wajitie kucheza biriani ingekula kwao. Leo mapungufu yalikuwa kidogo sana hasa kwa Muzamiru anakaba vizuri lakini alikuwa anakosa maamuzi ya haraka na mara nyingine alikuwa anapoteza pasi kwa adui. Pia Boko na Kagere walikosa mawasiliano kukawa haijulikani nani anakaba na kurudi chini kidogo kuchukua mpira na nani atazunguka ndani ya 18 za Gwambina kuwanyima raha mabeki wakati wa Gwambina. Na pili nani anaruka na mabeki wakati nani anakimbiza "second ball". Hii iliwapa nguvu sana Gwambina kwani mabeki wao wawili wa kati kwa sehemu kubwa ya mchezo walikuwa huru sana mpaka alipoingia "mtunza mali" Mugalu. Baada ya kuingia Mugalu walau Simba ndio walianza kupata nguvu kutokana na uwezo wake kutunza mpira mpaka wenzake wafike .

Na Gwambina walicheza vizuri sana lakini walikosa uzoefu kidogo na hawakuwa na mtu wa kuamua matokeo. Kwa mmiliki wa Gwambina akiweza kuwazuia hawa vijana alionao sasa hivi halafu akaongeza wachezaji wazoefu kama watatu hivi nafikiri mwakani watakuwa wanapambania "top four" badala ya kugombania kushuka daraja kama mwaka huu. Kikubwa wapambane hasa ili timu isishuke daraja mwaka huu ili mwakani waje kivingine.
 
20210424_21034539846.jpg
20210424_21034539846.jpg
 
CEO
 

Attachments

  • 67e465848e324c80b12102d6d4b7fbb6.mp4
    541.7 KB
Back
Top Bottom