H.E.Bobi Wine to appear in the USA top congress

H.E.Bobi Wine to appear in the USA top congress

Move ya huyu jamaa imekuwa boosted na Museveni mwenyewe, popularity ya jamaa imekuwa juu kiasi museven hawezi tena kuzima moto
 
Dogo ana akili sana, halafu na yule lawyer wake Robert Amsterdam ni balaa kwenye issue za dizaini hii.
Nilipitia CV ya huyo lawyer, nikasema naam!
Dogo anaakili sana. angalia anajibu maswali bila kuumauma, yaani anaakili za kuzaliwa. Huwezi fananisha na wapinzani wa hapa kwetu. wapa kwetu wanajiangalia wao tu.
 
Tatizo letu ni woga as you have put it. tunaogopa ku sacrifice maisha yetu for the benefit of coming generations! Watu wametupwa kwenye sanadarusi , hakuna kilichokemewa, hata kuifanya international community ipate taarifa of these atrocities!

Yule mdada kule USA sialianzisha vuguvugu fulani mwanzoni mwa mwaka huu ! Si labda ndio pangekua pa kuanzia pazuli au ?
 
Na tujiandae kupokea wakimbizi toka Uganda ! maana alishagasema yeye ni quarter pin ya baiskeli, kuingia kwa nyundo na kutoka kwa nyundo...
Teknolojia imebadilika tokea miaka hiyo ya early 80's labda tumpokee yeye kama mkimbizi
 
Erythrocyte tatizo letu sisi wabongo (Tz) ni uoga. Kwa tatizo la kufanana na hilo la Bobi Wine (TAL), na hata lile la UKUTA ilitakiwa maandamano ya nguvu. Na sauti ya dunia kukemea ingekuwa kubwa sana.
Hili la Bobi Wine waganda wameionyesha dunia kuwa hawakubaliani na matendo ya watawala .
mkuu hata Waganda wamechelewa sana, Besigye kateswa miaka mingi mno kupita hata Mateso ya Watz, tukiachilia la TL.
ni suala la muda.
Hata Tz kitawaka siku moja hutaamani.
Wahenga wanasema usimwamshe aliyelala, Ipo siku watu wataamka kwa pamoja kama moto wa majani mabichi.
Ole wake kiongozi wa enzi hizo za mlipuko hakuna rangi ataacha kuona.
binafsi naona uvumilivu wangu ni mwembamba zaidi ya uzi, naomba Mungu wajinga hawa wasije nigusa kwa namna yoyote dunia yote itajua
 
Aisee...

Lissu nae aalikwe jamani.
Sio rahisi ki hivyo kwani hayo ni matokeo ya reaction ya waganda baada ya tukio la bobi wine!!sisi hapa tunazidiwa hata na waganda?!!!JISAIDIE NAWE UTASAIDIWA!!
 
Bobi Wine amchukue Tundu lissu awe best-man wake katika kutoa hio speech[emoji18]
Lisu apambane na hali yake kwanza.
Siku akiruhusiwa hospital tutarajie dunia yote kutikiswa na vyombo vya habari, jamaa hayuko Ubeligiji kwa bahati mbaya, subiri ni suala la wakati, wekeni akiba ya maneno
 
“US Top Congress”

Jinsi habari ilivyoandikwa tu unajua ni fake news
 
Tatizo letu ni woga as you have put it. tunaogopa ku sacrifice maisha yetu for the benefit of coming generations! Watu wametupwa kwenye sanadarusi , hakuna kilichokemewa, hata kuifanya international community ipate taarifa of these atrocities!
Boss nisikilize,
mwanadamu asipochokozwa kiwango cha kuchokozeka huwa ni mpole au hata huonekana mjinga.
Wakuu hakuna mahali patawaka moto kama Tz, uzuri hii post itakaa milele yote ya uhai wa jf.
kuna siku itarejewa, Tz inakwenda kuwaka kwa trend ya yanayoendelea, yote yaliyotokea ya viroba, saa8, ,Azoveri, TL, Ulimboka jumlisha na yajayo ni majani yanayosubiria kiberi yalipuke, Tusidanganyike, malipo ya ubaya ni ubaya.
Nawaonea huruma viongozi watakao shuhudia hasira za Watanzania.
 
Back
Top Bottom