Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MZEE KIUNYA ANAOMBA KUMUONA MHE RAIS: HAAMINI MACHO YAKE KUONA SHULE MPYA IKIJENGWA KWENYE KITONGOJI CHAO
Kijiji cha Kigera cha Musoma Vijijini kimepokea Tsh 348,500,000 (Tsh 348.5m) kutoka Serikalini kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi mpya (Mradi wa BOOST) ambayo itakuwa ya pili, na inajengwa kwenye Kitongoji cha Kusenyi
Mzee Kiunya, mzaliwa na mkazi wa Kitongoji cha Kusenyi, kwa furaha tele ya kupata shule kwenye Kitongoji chao, amemtuma Mbunge Prof Muhongo "ampelekee hapo Kitongojini Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan" akafungue shule hiyo inayokamilishwa ujenzi. Mzee huyo ameongea kwa lugha ya "Kikwaya."
Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa yenye taarifa za shukrani nyingi, ikiwemo ya Mzee Kiunya, kutoka Kijijini Kigera, Kata ya Nyakatende, Musoma Vijijini.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumatano, 23.8.2023