Habari mbaya kwa walaji wa Kitimoto: Huenda wengi wao wakaja kupata kifafa!

Habari mbaya kwa walaji wa Kitimoto: Huenda wengi wao wakaja kupata kifafa!

Nchini Tanzania nyama ya nguruwe ni maarufu katika maeneo mbali mbali ya starehe na imepewa majina mengi ,kama vile mkuu wa meza, kiti moto na mengineyo mengi.

Hata hivyo utafiti wa kisayansi kutoka chuo kikuu cha kilimo cha sokoine ( SUA), umebaini kuwa walaji wa nyama ya nguruwe wako katika hatari ya kupata magonjwa kama vile kifafa kutokana na mnyoo Tegu uliopo kwenye nyama ya nguruwe.

Mwandishi wa BBC Maximiliana Mtenga amezungumza na mtafiti wa magonjwa ya binadamu na wanyama Dkt. Boa Mathias Emanuel kutoka chuo kikuu cha SUA, na kwanza amemuuliza ueneaji wa ugonjwa huu.


Chanzo: BBC Swahili

Asante kwa kunikumbusha mboga ya kula leo
 
Hizi tafiti siku hizi kila kitu hakifai.Jana tu mwingine kanitumia kwamba tusiweke vyakula vya moto kwenye vyombo/vifaa vya plastik tutapata kansa hujakaa vizuri chumvi sukari sio nzuri mwishowe sasa tutaambiwa kulala kwenye nyumba ya bati sio nzuri kwa afya yako.
Aisee tafiti uchwara zimekuwa nyingi....!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ANGALIA SIFA ZA NGURUWE HATA KATIKA BIBLIA!! - HAFAI- NI NAJIS, NI KHARAM. BIG UP WAISLAM NA WASABATO
Mambo ya Walawi 11:7 Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.

Kumbukumbu la Torati 14:8 na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.

Zaburi 80:13 Nguruwe wa msituni wanauharibu, Na hayawani wa kondeni wanautafuna.

Mithali 11:22 Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, Kadhalika mwanamke mzuri asiye na akili.

Isaya 65:4 waketio kati ya makaburi, na kulala katika mahali pao pa siri; walao nyama ya nguruwe, na mchuzi wa vitu vinichukizavyo u katika vyombo vyao;

Isaya 66:3 Yeye achinjaye ng'ombe ni kama yeye amwuaye mtu; na yeye atoaye dhabihu ya mwana-kondoo ni kama yeye avunjaye shingo ya mbwa; na yeye atoaye matoleo ni kama yeye atoaye damu ya nguruwe; na yeye afukizaye uvumba ni kama yeye abarikiye sanamu; naam, wamezichagua njia zao wenyewe, na nafsi zao zafurahia machukizo yao.

Isaya 66:17 Watu wale wajitakasao, na kujisafisha katika bustani, nyuma yake aliye katikati; wakila nyama ya nguruwe, na machukizo, na panya; watakoma pamoja, asema Bwana.

Mathayo 7:6 Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.

Mathayo 8:30 Basi, kulikuwako mbali nao kundi la nguruwe wengi wakilisha.

Mathayo 8:31 Wale pepo wakamsihi, wakisema, Ukitutoa, tuache twende, tukaingie katika lile kundi la nguruwe.

Mathayo 8:32 Akawaambia, Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! Kundi lote wakatelemka kwa kasi gengeni hata baharini, wakafa majini.

Marko 5:11 Na hapo milimani palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, wakilisha.

Marko 5:12 Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao.

Marko 5:13 Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini.

Marko 5:16 Na wale waliokuwa wameona waliwaeleza ni mambo gani yaliyompata yule mwenye pepo, na habari za nguruwe.

Luka 8:32 Basi, hapo palikuwa na kundi la nguruwe wengi wakilisha mlimani; wakamsihi awape ruhusa kuwaingia wale. Akawapa ruhusa.

Luka 8:33 Pepo wakamtoka mtu yule wakawaingia nguruwe, nalo kundi lilitelemka gengeni kwa kasi, wakaingia ziwani, wakafa maji.

Luka 15:15 Akaenda akashikamana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe.

Luka 15:16 Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu.

2 Petro 2:22 Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.
 
Mi ningekuwa nishapata zaman maana ni ngumu siku kupita bila kupata walau nusu kilo na ndizi mbili, na sitaacha kama ni kufa acha nife tu, kwan wale waliokutwa wanaelea baharini kwenye viroba nao walikula KITIMOTO??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitimoto hata aliyeipiga marufuku alikuwa anaipiga vizuri tu......
 
Kwanza makinika nami vizuri kuhusu hizi picture hapa chini:-

dawa%2Bya%2Bminyoo..jpg


images-1.jpeg


images.jpeg


images-3.jpeg


images-2.jpeg




Sasa twende kwenye upotoshaji wa SUA kuhusu huyu mdudu:-

Nchini Tanzania nyama ya nguruwe ni maarufu katika maeneo mbali mbali ya starehe na imepewa majina mengi kama vile mkuu wa meza, kiti moto na mengineyo mengi.

Hata hivyo utafiti wa kisayansi kutoka chuo kikuu cha kilimo cha sokoine( SUA) umebaini kuwa walaji wa nyama ya nguruwe wako katika hatari ya kupata magonjwa kama vile kifafa kutokana na mnyoo Tegu uliopo kwenye nyama ya nguruwe.

Mwandishi wa BBC Maximiliana Mtenga amezungumza na mtafiti wa magonjwa ya binadamu na wanyama Dkt. Boa Mathias Emanuel kutoka chuo kikuu cha SUA na kwanza amemuuliza ueneaji wa ugonjwa huu.


SUA wanafanya makusudi sana.
 
Back
Top Bottom