Habari mbaya kwa walaji wa Kitimoto: Huenda wengi wao wakaja kupata kifafa!

Habari mbaya kwa walaji wa Kitimoto: Huenda wengi wao wakaja kupata kifafa!


Hakika ni kuwa Agano la Kale katika Biblia imekataza ulaji wa nguruwe na akafanywa

kuwa ni haramu: “
Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu ni najisi. Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama yao wala msiguse mizoga yao” (Walawi 11: 7 – 8).

Agizo hilo limerudiwa katika Kumbukumbu la Shari’ah 14: 7 – 8 na pia Isaya 66: 17.

Na katika Agano Jipya, Yesu naye amesema
kuwa hakuja kutangua shari’ah na mafundisho ya manabii bali kukamilisha (Mathayo 5: 17). Kwa ibara hiyo ni kuwa Yesu pia aliharamisha ulaji wa nguruwe.

Ndg yaliyoelezwa hapo si nguruwe tu, kuna Samaki wasio na Magamba, wadudu (mfano kumbikumbi), n.k. Tena yaliyoamriwa ktk agano la kale ni mengi hasa TORATI Sharia ya Mussa mfano siku ya sabato yakupasa utembee umbali unaoweza kutupa jiwe tu! Na si zaidi mbona hii hatuizungumzii! Hapa ndo patamu kibiblia.
Aidha mimi kama mimi na uelewa wangu katika Biblia mambo ya sheria (Sharia) hayana nafasi toka Yesu afe msalabani. Natamani niingie ukurasa wa dini.....................
Loading..........................
 
Vipi kuhusu yule kitimoto wa polini maana yeye hujitafutia chakula mwenyewe!

hilo nalo nenoooo!!!!!!!!!!!!!! na naipendaje kitimoto pori sijui inauzwaga wapi jamani tusaidiane, MziziMkavu tusaidie, au hata huyu ni hatariiiii??????????
 
hizi ni mbwembwe tu za chuo Kikuu cha sua.. kulikua kuna haja kweli ya kusema wamegundua au ya kufanya utafiti???.. wakati tafiti zilishafanyika kitambo na vitabu vimeandikwa na watu tunajua kwamba taniea solium anasababisha neurocysticosis ambayo inasababisha kifafa (jacksonian epilepsy).....hapa wangesema tu kwamba kumekua na ongezeko wa maambukizi kwa nguruwe kwa hiyo watu wawemakini...sio kutafuta umaharufu wa kuvumbua
 
Ngombe Hali kinywesi wala mizoga!!kesi yake tofauti na kiti moto!!kuna tinnea sollium hao ndo minyoo tegu!!yaaani haiteguki ni balaaa!!!!

kwa taarifa yako: ngombe anapata minyoo hii kutokana na kula mayai yaliotoka kwenye kinyesi cha binaadamu hasa wale wenye tabia ya kujisaidia vichakani, maporini na kwenye majani hasa maeneo watu hawajengi vyoo, wakachimbaji dawa porini wanaotoka kwenye mabasi ya safai na kwenda kujisaidia haja kubwa zenye mayai ya hawa tegu(T.sagnata).hapa unaweza ukapima kama ng'ombe hali mavi anakula nini sasa.tofauti na nguruwe anayefugwa ndani na kupewa pumba, na makombi ya vyakula.hii inamaana kuwa kama binadamu wakijenga vyoo na kuachana tabia ya '''kunya'' nje, hopefully ng'ombe watanusurika.
 
Tafiti nyingine kukatana stimu tu...kwani kutibu kifafa bei gani bhanaa...
220px-Sweet_and_sour_pork.jpg


Hii maneno acha kabisa!
 
hizi ni mbwembwe tu za chuo Kikuu cha sua.. kulikua kuna haja kweli ya kusema wamegundua au ya kufanya utafiti???.. wakati tafiti zilishafanyika kitambo na vitabu vimeandikwa na watu tunajua kwamba taniea solium anasababisha neurocysticosis ambayo inasababisha kifafa (jacksonian epilepsy)...
definitely yes:A S thumbs_up:, au pengine magazeti ndio yame-exaggurate hii taarifa ili yaweze kuuzika kwa wingi
 
kimsingi hata ng'ombe wanao minyoo wa aina hii wenye cyst wanaokaa kwenye nyama/misuli na moyo, ambapo kwa ng'ombe wanaitwa cystercercuss bovis (CB)na kwa nguruwe wanaitwa cystercercus cellulosae (CC). hivyo ngoma droo, wote walao nyama kwa ujumla wanakuwa katika hatari hii. pengine kwa nguruwe inaweza kuwa hatari kwakuwa sijajua machinjio ya nguruwe na ukaguzi wake na inaweza kuwa sio hatari kwakuwa maambukizi hayajafika kwenye eneo la mfugaji husika vilevile sio nyama zote za ng'ombe zinazoliwa zinapita kwenye machinjio pia.
stop worrying and start living.

We wadanganye tu wenzio ina maana hao wataalamu wa sua na denmark hawajui kitu hadi wakaja na conclusion hiyo kuhusu nguruwe? Na hii siyo mara ya kwanza kwa researchers kutoa onyo kuhusu nguruwe, remember no research no right to speak, kafanye na wewe reasearch siyo unaburuzwa kwa uchu wako wa kula nguruwe
 
Ndg yaliyoelezwa hapo si nguruwe tu, kuna Samaki wasio na Magamba, wadudu (mfano kumbikumbi), n.k. Tena yaliyoamriwa ktk agano la kale ni mengi hasa TORATI Sharia ya Mussa mfano siku ya sabato yakupasa utembee umbali unaoweza kutupa jiwe tu! Na si zaidi mbona hii hatuizungumzii! Hapa ndo patamu kibiblia.
Aidha mimi kama mimi na uelewa wangu katika Biblia mambo ya sheria (Sharia) hayana nafasi toka Yesu afe msalabani. Natamani niingie ukurasa wa dini.....................
Loading..........................
ndugu kirwanga, i hope kahtaan ( zamani tuliita mkonge)na Gavana( asiyepoteza jimbo kwenye uchaguzi), crabat, khawarizm wanakusikia, ningependa waanzie hapa, manake wao ndio wanaijua sabato vizuri. (sisi tuliopewa jina la 6 na wapiga ramli wakina khawarizm kwasababu ya rizim zao, hatusemi kitu kwakuwa tunataka urais) ha ha ha ha
........loading..................................
..................kwetu pazuuuuuuuri nimeshapakumbukaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.......................la la la la la la
 
We wadanganye tu wenzio ina maana hao wataalamu wa sua na denmark hawajui kitu hadi wakaja na conclusion hiyo kuhusu nguruwe? Na hii siyo mara ya kwanza kwa researchers kutoa onyo kuhusu nguruwe, remember no research no right to speak, kafanye na wewe reasearch siyo unaburuzwa kwa uchu wako wa kula nguruwe
we naona unarudisha mada nyuma, kwa taarifa yako research hiyo ilisha fanyika very longtime na ndio maana mchangiaji fidelis zul zorander akajikuta anasema hizo ni mbwembwe tu, mbona si jambo geni hili na research hii ipo hadi kwenye vitabu miaka mingi, na inasomwa na wanafunzi wasomao mifugo na madaktari wotewa mifugo nchini wanajua hii kitu in detail , nothing special here to pin point
 
Hizi tafiti siku hizi kila kitu hakifai.Jana tu mwingine kanitumia kwamba tusiweke vyakula vya moto kwenye vyombo/vifaa vya plastik tutapata kansa hujakaa vizuri chumvi sukari sio nzuri mwishowe sasa tutaambiwa kulala kwenye nyumba ya bati sio nzuri kwa afya yako.

Ni kweli siku hizi kila kitu ni hatari kuanzia vyakula vya mezani mpaka chumbani! Usafiri kuanzia baharini mpaka barabarani, mwenda kwa miguu mpaka mpanda bodaboda. Mazao ya GMO mpaka mayai na kuku wa kisasa, bidhaa za mchina mpaka madawa ya phamacy! mwanajeshi feki mpaka usalama wa taifa feki, trafiki feki mpaka daktari feki, madereva ndo usiseme, wanasiasa feki ni wengi mpaka mawaziri mizigo!

Hivi tufanyeje sasa, maana haya yote ni sawa na mnyunyu ya mvua "hayakwepeki" ukikwepa hapa unavurugwa pale! Aaagh tuleni tu kitimoto labda watafute condomu za kuvalisha kabla ya kula! Vinginevyo kandamiza tu hospitali zipo!
 
Aaah wapi mzigo umekaangwa kwenye futa lake afu tena akauroast huyo tegu ata survive vipi labda kama ni robotic tegu..
Mapishi ya ile kitu acha kabisa ni next level labda wala mishikaki ya ng'ombe ndio wako hatarini ila Noah ni safe kabisa.
"Mangi leta kilo ila tenganisha nusu ikaushe nusu fanya roast na ndizi mbili..fasta basi...afu mwambie muhudumu alete kinana mbili baridiii..."
 
Ni kweli siku hizi kila kitu ni hatari kuanzia vyakula vya mezani mpaka chumbani! Usafiri kuanzia baharini mpaka barabarani, mwenda kwa miguu mpaka mpanda bodaboda. Mazao ya GMO mpaka mayai na kuku wa kisasa, bidhaa za mchina mpaka madawa ya phamacy! mwanajeshi feki mpaka usalama wa taifa feki, trafiki feki mpaka daktari feki, madereva ndo usiseme, wanasiasa feki ni wengi mpaka mawaziri mizigo!

Hivi tufanyeje sasa, maana haya yote ni sawa na mnyunyu ya mvua "hayakwepeki" ukikwepa hapa unavurugwa pale! Aaagh tuleni tu kitimoto labda watafute condomu za kuvalisha kabla ya kula! Vinginevyo kandamiza tu hospitali zipo!
hapa umenigusa aisee.:A S thumbs_up:
 
Haya bana hospitali zipo, wapi TZ wanakopasua kichwa badala ya mguu kweli ndo tujivunie? Ngoja mimi nichukue tahadhari lakini si ya kuacha kula kitimoto bali uandaaji wake
 
Nguruwe ambapo katika mwili wake hukusanyika jumla ya vijiumbe maradhi visivyoondoka kwa kuoshwa

Mdomo ni maficho ya vijidudu, bakteria na virusi vinavyokwenda kwa binadamu na wanyama.


Baadhi yake vinamhusu nguruwe, mfano wa kidudu kiitwacho Trchinella, nywelenywele ziitwazo

Balantidium Dysentery, wadudu wa tumbo (Taenia Solium) na mchango wa nguruwe (Spiralis).

Baadhi yake huingizwa kwenye maradhi mengi ya pamoja baina ya binadamu ( Cysticercosis & Influenza) na wanyama.


Minyoo (Ascaris na Fasciolopsis Buski) hupatikana kwa wingi nchini China.

Maradhi ya Balantidiasis hupatikana kwa wachunga nguruwe na wenye kuchanganyika nao, na

yanaweza kuenea kwa sura ya mlipuko kama ilivyotokea katika moja ya visiwa vya bahari ya Pacific

baada ya kimbunga. Maradhi yanakuwepo panapokuwepo nguruwe katika nchi zilizoendelea

kiviwanda kinyume na madai ya uwezekano wa kuushinda uchafu wake kwa kutumia teknolojia

mpya zinazoharamisha kula nyama bila ya kibali, hasa nchini Ujerumani, Ufaransa, Philippines na Venezuela.

Kwa kula minofu ya nyama ya nguruwe, (Trichinellosis) hupatwa na ugonjwa wa Balantidium

Dysentery. Kwani mke hubungua kuta za matumbo kwa ajili ya kuweka mayai ambayo yanafikia

kiasi cha 10,000. Mayai hayo huingia kwenye misuli kupitia damu na kugeuka kuwa ni vijiyai vyenye kuambukiza.

Ama kupata maradhi kupitia mchango wa nguruwe, ni kuwa hiyo hupatikana baada ya kula minofu ya nguruwe mwenye ugonjwa.

Minyoo hukua kwenye mchango wa binadamu na urefu wake unaweza kufikia meta saba, na

unakuwa na kichwa chenye miba inayosababisha kukwaruzika kwa kuta za michango na mchupo

mkubwa wa damu, na ana mirija minne na shingo. Aina za mke huzaliwa kama kwamba ni

wanyama pekee na hufikia maelfu. Na katika kila mmoja kati ya mnyama, huzaliwa zaidi ya mayai

elfu moja iwapo utakula Cysticercosis.

Kupatwa na ugonjwa wa minyoo ya tumbo la binadamu, hutokana na kula chakula kilichoingia

mayai na kutoa lava, na huingia katika damu kupitia kiungo chochote. Na hatari yake hukisiwa kwa

mujibu wa umuhimu wake.

Maradhi haya hayatokei kabisa kutokana na kupatwa na mchango usio na miba katika kichwa na

wenye madhara madogo


kabisa Taenia Saginata ya ng'ombe. Chanzo.MziziMkavu



KIIMANI
kwa upande wa Quran
"Yeye Amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilichotajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu" (2: 173).


KWA UPANDE WA BIBILIA
"Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu ni najisi. Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama yao" wala msiguse mizoga yao (Walawi 11: 7 – 8).

 
: ABC News: It's Not a Tumor, It's a Brain Worm

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Nyama ya nguruwe.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimehadharisha walaji wa nyama ya nguruwe nchini, kuwa wanakabiliwa na hatari ya kupata kifafa.

Utafiti wa kisayansi uliofanywa na SUA, umebaini kuwa baadhi ya nguruwe wana minyoo aina ya tegu ambao nyama yao ikiliwa bila kuiva vizuri, mlaji atapata minyoo hiyo ambayo huingia kichwani na kusababisha kifafa.

Akizungumza na mwandishi hivi karibuni, Mhadhiri na Mtafiti wa Idara ya Sayansi ya Wanyama na Uzalishaji ya SUA, Profesa Faustine Lekule, alisema sampuli za utafiti huo kutoka Mbeya, zimebaini nguruwe wengi wakiwamo wanaosafirishwa katika miji mikubwa wameathirika na minyoo hiyo.

Kwa mujibu wa Profesa Lekule, wataalamu wa SUA wanaosimamia Mradi wa Utafiti wa Kuboresha Ufugaji wa nguruwe kwa mkoa wa Mbeya ili kuinua pato la kaya, unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Denmark (DANIDA), walibaini hatari hiyo baada ya kuchukua sampuli ya nyama ya nguruwe kwa ajili ya vipimo.

“Majibu ya sampuli ambazo wataalamu wamezichukua kutoka kwa nguruwe wa wafugaji kwenye baadhi ya vijiji, wamebainika kukumbwa na hatari hii.

“Lazima jitihada za makusudi zichukuliwe katika kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili kati ya watafiti na Serikali,” alisema Profesa Lekule.

Alisema maambukizi ya tegu au minyoo ya nguruwe yanatokana na tabia za baadhi ya wafugaji kutozingatia ufugaji bora kwa kuwaacha kujitafutia chakula na maji mitaani na kula kinyesi cha binadamu.

Kwa mujibu wa Profesa Lekule, baadhi ya wafugaji wamekuwa wakijisaidia vichakani na kuwaacha nguruwe kutafuta malisho katika vichaka na kula kinyesi chao, hali inayochangia ongezeko la maambukizi ya minyoo ya tegu hao.

Baada ya kula kinyesi minyoo humwingia mwilini na kumdhoofisha na baadaye binadamu anapokula nyama ambayo haijaiva vizuri, minyoo hiyo humwingia na kusababisha kifafa baada ya kuingia kichwani.

Alisema athari za kuenea kwa maambuziki hayo inaweza kutokea katika miji mikubwa ikiwamo Dar es Salaam kwa kuwa nguruwe wa Mbeya husafirishwa na kuuzwa maeneo hayo.

“Hatua hii inaweza kusababisha kusambaa kwa ugonjwa huu, hivyo ushirikiano kati ya wafugaji, wafanyabiashara, Serikali na wataalamu wa afya katika kufikia hatua ya kumaliza changamoto hii unahitajika,” alibainisha Profesa Lekule
 
MziziMkavu waambie bana nyama zipo kibao wanahangaika na kitimoto tu bora nile nyoka kuliko huyu anaefanana na wazungu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom