Habari nauza nguo za mtumba nipo Dar es salaam wapi nikitembeza naweza nikapata soko kirahisi naombeni ushauri wenu

Habari nauza nguo za mtumba nipo Dar es salaam wapi nikitembeza naweza nikapata soko kirahisi naombeni ushauri wenu

Tembeza mitaa yote, dsm ni jiji kubwa jipangie
1. Jtatu nenda kigamboni
2. Jnne nenda chanika
3. J5 magwepande
4. Alhamisi mbagala mbande
5. Ijumaa pugu mnadani
6. Jmosi vikindu na kisemvule
7. Jpili pumzika.
Linda kipato chako kuza mtaji kisha anza kuuza mtumba wa jumla, kata mabaro yanatajirisha balaaa mapointa wengi, mtaji ukikua zaidi uza baro zima zima jumla, mtaji ukikua zaidi safiri nenda Dubai, canada na china utuletee makondena ya mitumba, kila la kheri ndugu mjasiriamali
 
Dar es Salaam popote kambi, lakini kutembeza mitaani nadhani inasaidia sana sana mitaa ambayo kuna makazi ya watu, achana na mitaa ya mishemishe.

Ushawahi kufikiria kufanya na online shopping?
 
Ukiweza kujiongeza na mashati ya mtumba itakuwa vizuri, point makali yanayovutia.

Ikifika lunch time kuanzia saa 6 mchana uwe unazunguka karibu na maeneo yalipo maofisi makubwa kama TPA, PSSF, n.k

NB: BEI IWE YA KAWAIDA ILI ZITOKE HARAKA KULIKO KUWEKA BEI KUBWA MZIGO UTAKUDODEA.
KILA LA HERI MKUU
 
Back
Top Bottom