Habari za huku kaka zangu na dada zangu ninawazo kidogo la biashara naombeni ushauri wenu.

calvin priva

Member
Joined
Jan 24, 2014
Posts
9
Reaction score
3
Nimewaza sana kutafuta ufadhili wa kampuni yoyote ili inijengee hostels za kisasa zenye vyumba hamsini lakini nimeona ni vyema nilete wazo langu hapa na baada ya hapo ndo nichukue maamuzi, malipo ya deni la kampuni tutakatana ndani ya miaka kadhaa hadi pesa yao imalizike na haitaniumiza kwasababu katika vyumba hamsini hao watachukua kodi ya vyumba arobaini kila mwaka hadi wamalize deni lao then mimi nitabaki na vyumba kumi kwaajili ya matumizi yangu baada ya kumaliza deni lao nyumba nzima inakuwa yangu.. Je, ufadhili kama huo unawezekana?
 
Je hizo hostel utazijenga eneo gani?
Utatoza kodi ya kiasi gani kwa chumba?
Eneo unalo tayari au ni la kununua?

Kupata ufadhili inategemea na project plan yako na ushawishi wako, ila kwa ushauri ni vizuri uwe na mtaji wa kianzia atleast....hakuna mtu anaweza kukupa ela kwa idea ambayo hata wewe umeshindwa kuigharamia kidogo.

All the best.
 
je unakiwanja kariakooo au??? he he he ongeza nyama kumfanya mdhamini akujengee wewe na amuache mwingine
 
Asanteni sana kwa ushirikiano.. sina kiwanja ila gharama ya chumba kimoja ni Tsh.70,000 kwa mwezi then watalipia kwa miezi minne (awamu 3 kwa mwaka) that means ni sawa na Tsh.280,000 na kila chumba kimoja watakaa watu wanne. Ukiangalia hesabu ya mwaka mmoja kwa vyumba arobaini vya mdhamini ambavyo vitakuwa na watu 160 (kila chumba kimoja watu 4) na ada ya mtu mmoja kwa mwaka ni Tsh.840,000 that means ada ya mwaka mmoja kwa wanafunzi 160 wa hivyo vyumba arobaini ni sawa na Tsh.33,600,000 hivyo mdhamini atakata kiasi hicho cha pesa kila mwaka hadi kumaliza deni lake na baada ya hapo atanikabidhi umiliki wa jengo.
 
Mkuu tupe kwanza wewe una noni special mpaka wakujengee?

Je unakiwanja kipo karibu na chuo au eneo ambalo watu wanahitaji hizo hostel au?
Hapana ndugu sina kiwanja ila nipo eneo ambalo kuna uhitaji mkubwa wa hostel
 
je unakiwanja kariakooo au??? he he he ongeza nyama kumfanya mdhamini akujengee wewe na amuache mwingine
Hapana, sina kiwanja kariakoo maana sehemu ambapo kuna uhitaji wa hostel hiyo ni maeneo ya sinza na watu wengi sana wanahangaika kutafuta hostel
 
Asante sana ndugu.. Hostel nimeplan iwe sinza kama nitafanikiwa maana hostel nyingi za huku hazikidhi vigezo na husababisha wanafunzi wengi kuzikimbia hivyo kuna uhitaji mkubwa wa hostel, gharama ya chumba kimoja ni elfu sabini kwa mwezi na italipwa kwa awamu tatu yaani laki mbili na themanini kila baada ya miezi minne. Chumba kimoja watakaa wanafunzi wanne.
 
soko la hostel sio zuri kiasi hicho.. maana kuna wanafunzi wanapanga mitaani pia... mwanafunzi akupe 70 kwa mwezi akae hostel ya kushare wanne wakati hiyo hiyo 70 yake inamruhusu kupanga chumba cha peke yake mtaani?

sinza kuna hostel nyingi sana na hakuna hata moja inayojaa na hapo wanachaji chini ya hiyo bei kwa kitanda....


 
Ni kweli kaka ila mimi nilikuwa nakaa hostel zilizopo mori na bei zilkuwa juu ya 70 halafu sababu za wanafunzi wengi kukimbia niliziona baadhi ndio maana nimeamua kufanyia tu hukohuko sinza ila nitafuatilia zaidi kutokana na ushauri wako kaka, asante.
 
Hamna mtu atakaa hostel ya 70,000/= af wakae wanne

Sent from my iPhone6 using JamiiForums mobile app
 
Ndugu yangu naomba kwanza elewa hakuna taasisi inayoweza kukukopesha pesa hali yakuwa huna chochote mkononi angalau ungekuwa na kiwanja na ukajenga kozi kadhaa halafu ikakushinda hapo sawa waweza enda mahala ukakopa


Na hiyo 70k mwanachuo ni ngumu kutoa kwenye chumba cha kushare wakati mtaani anaweza pata room saaaf ya peke ake Kwa bei hiyo.....biashara ya hostel Kwa sasa si nzuri sana kwani hao wanachuo siku hizi hawazitumbui kama zamani, yani ujasiliamali umeanza kuwabeba

invest what you are willing to lose
 
Wazo lako zuri lakini zingatia haya ili uwe na ushawishi kwa kampuni/mwekezaji wa mradi wako
1. Eneo la hostel
Nimepitia majibu yako unasema unataka iwe Sinza. Sababu zipi zimefanya uamue Sinza na si sehemu nyingine kama Mwenge, Kijitonyama nk?
2. Huduma
Katika eneo hilo utakalo kujenga unatarajia kuweka huduma zipi zilizo rahisi kwa wateja/wanafunzi ambazo ni bora na za kipekee kiasi cha kufanya kila awazae hostel basi aje kwako
3. Urahisi wa usafiri
Asili ya wapangaji wengi hupenda kutumia basi moja kutoka anapokaa hadi mahala pa kazi/masomo. Je hili kwa eneo lako linawezekana au una ushawishi gani wenye mabasi kuja kuqnzisha huduma ya mabasi ya kwenda chuo/ mjini kutokea kwako
4. Kodi ya pango
Maeneo yanayozunguka Sinza na karibu na Sinza na Sinza yenyewe kumejaa utitiri wa hostel na nyumba za kupanga. Je kodi yako ushaifanyia upembuzi yakinifu kuwa ipo chini na itaweza kukidhi kugharamia huduma zote za kijamii na za ziada
5. Utulivu
Mtu anaesoma anapenda mazingira yaliyotulivu na hakuna kelele. Sinza kwa hili bado ni changamoto. Umeliona hili?
6. Mtaji za uwekezaji
Mradi huu naamini unaweza kuwa rahisi kwako kutekelezeka kama nawe ungekuwa na mtaji. Mtaji huu unajumuisha pesa kiasi au hata kiwanja kikubwa na kipo katika eneo 'potential' ss angalia hili
7. Mwisho
Mawazo yako mazuri yaandike na uanze kutengeneza mipango na shirikisha wadau wewe uwe na shea kiasi tu
Nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahio mtu akujengee hostel, halafu akupe room kumi uwe unakula hela tu. Baada ya investment yake kurudi akuachie hilo jengo bure kabisa. Who are you???

Simuoni mtanzania mwenye roho ya hivyo kwa kweli,,,tafta namna ya kutoka tu!
 
hakuna mtu duniani mjinga kiasi hicho.. dogo hachangii chochote eti na bado apewe vyumba kumi bure... angalau angekuwa na kiwanja ingesound...


Kwahio mtu akujengee hostel, halafu akupe room kumi uwe unakula hela tu. Baada ya investment yake kurudi akuachie hilo jengo bure kabisa. Who are you???

Simuoni mtanzania mwenye roho ya hivyo kwa kweli,,,tafta namna ya kutoka tu!
 
hakuna mtu duniani mjinga kiasi hicho.. dogo hachangii chochote eti na bado apewe vyumba kumi bure... angalau angekuwa na kiwanja ingesound...
Eeh man, yani nimesoma uzi wake nikakaa nikatafakari kwa utulivu sana. Its a good idea ila kwa bongo hakuna mtu atafanya kitu cha kijinga hivyo,

maybe amuombe mwenye jengo baada ya project kukamilika amlipe freshi kwa mwezi, akiwa kama manager wa hostels hizo! Hata M na nusu freshi, na hio ni bonus ya kumpa kickstart idea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…