Habari za za Simba kupewa nafasi badala ya Mbeya City

Habari za za Simba kupewa nafasi badala ya Mbeya City

Jasho atoke mwingine....kula ale mwingine....bure kabisa soka la Africa mashariki
 
Club zote za ligi (hasa zile less privileged) zinapaswa kulaani jambo hili. Kwa hali hii hata ligi kuu ingebaki na timu tatu tu. Timu za TFF
 
Hii ni sababu soka la Tanzania halitaendela kamwe.Ujinga na upumbavu huu wanoufanya viongozi wa TFF unakera sana.huyu mtu anaitwa Jamal Malinzi na kundi lake wamekuja kutuharibia mpira kabisa.
 
Simba watakuwa wamehonga walipe madeni yao kushiriki Kagame cup
 
Jamal malinzi ..aibu ya tff naiona mm...duuuu hatutaendelea kamwe,
 
Kama kweli jambo hilo lipo basi halina msingi,hv kama unamuweka simba eti kwa sababu ya uzoefu timu kama mbeya city ikichukua ubingwa watapelekwa champion ligi eti kwavile iliwah kufika robo fainal ktk mashindano hayo? Swala hili halikubaliki na wala halitakiwi,musonyo na huyo mwanasimba mwenzie mwesigwe watafuta chanzo kingine cha mapato na si kwa njia hii ambayo inadidimiza soka la afrika mashariki badala ya kulikuza.
 
Nibebe nibeeebe nibebe simb (in the voice of Rose Muhando).......... ndo opportunity pekee ya simba iliyobakia
 
Walichoangalia hapo TFF ni namna ya kupiga mpunga tu...

Hizo mbwembwe sijui Simba ana historia ni sarakasi tu...
 
Hao wanataka mapato ya getini, shortsighted aka chicken vision kama kawaida yao .
 
Basi kumbe timu zingine hazina maana kukomaa kushika nafasi za juu sababu Zina wenyewe?
 
mimi nilisoma jana kwa Shafii dauda . hiyo habari .kimsingi TFF hawana jipya badala ya kuinua soka la #Tanzania wao wanadidimiza soka letu
 
Halafu wataanza kusema tuthamini ligi za nyumbani,huu ni undezi,hivi ujinga kama huu na kwa wenzetu mbele upoo?
 
Hivi viti maalum balaa...hadi kwenye mpira khaaaa!
 
Sasa nimepata jibu la kwann nafasi ya yanga kwenye kagame alipewa azam....njaa huzaa magumashi....
 
Kwa nini mbeya city wasikate rufaa FIFA.??

mkuu ile habari kwa maelezo ya katibu wa TFF amesema mwenye haki ya kushiriki moja kwa moja ni #AZAM kwakuwa TANZANIA ndio wa andaji wa mashindano wamepewa nafasi ya upendeleo kuingiza timu 3 . kasema hizo timu 2 wanachaguwa wao mwenyewe

sidhani kama TFF kwa kigezo walicho kitumia kwa kumuingiza SIMBA badala ya MBEYA CITY ni sawa.

hakuna timu inayo penda kukaa bila ubingwa ila kwa bahati mbaya TANZANIA ligi yetu niya SIMBA na YANGA....
 
Mwaka jana kagame cup..Rwanda nao walitumia kigezo hiki..
APR...Rayon..na Police Rwanda...kazi iko mpira east africa pasua kichwa
 
Kama wanataka Simba ashiriki wafanye timu nne si ashiriki kwa gharama ya kumtosa Mbeya City halafu hii itazivunja nguvu timu bora na chipukizi na kuzifanya timu kubwa kama Simba kubweteka halafu hii habari si iliisha kipindi cha FAT.
 
Back
Top Bottom