Habib Kyombo ameomba kuvunja mkataba, tumemkubalia

Habib Kyombo ameomba kuvunja mkataba, tumemkubalia

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
1,016
Reaction score
2,195
taarifa black.jpg

Watu wa Soka,

Taarifa iwafikie kuwa Mshambuliaji wetu Habib Haji Kyombo yuko huru kujiunga na timu yoyote baada ya kuamua kuvunja mkataba na timu yetu.

Kila kitu kimeenda sawa na kupitia yeye tunatarajia kujenga mahusiano imara na klabu atakayoenda.

Aidha, tutatoa taarifa zaidi kuhusu maboresho tuliyoyafanya kwenye safu yetu ya ushambuliaji hivi karibuni.

Tunamtakia Habib Haji Kyombo kila la kheri katika safari yake ya Soka.
 
Ningekuwa mchezaji, kabla sijaenda Simba au Yanga, lazima wanihakikishie kucheza mechi nyingi angalau kuanza mechi 10 kwenye msimu
Kucheza mechi zote angalau dakika 30 kama sijaanza
 
Hata Kama KIWANGO chako kimeshuka?
fanya bidii mazoezini ukiwa mechi piga kazi uone Kama utakaa benchi
Ila ukizingua utasugua tu benchi watu wanataka utendaji
Ningekuwa mchezaji, kabla sijaenda Simba au Yanga, lazima wanihakikishie kucheza mechi nyingi angalau kuanza mechi 10 kwenye msimu
Kucheza mechi zote angalau dakika 30 kama sijaanza
 
Simba ya msimu ujao inafurahisha na kuchekesha. Habib Kiyombo alitakiwa abakie hapo hapo Singida Big Stars. Kwa sababu bado hajarudi katika kiwango cha miaka ile alipokuwa Mbao Fc!

Tamaa ya hela na kukosa ushauri sahihi bila shaka vimempoteza. Atasugua benchi huyo mpaka akome. Na msimu ujao msimsajili hata kwa mkopo.
 
Ni mchezaji gani wa maana ambaye amevunjiwa (amepambaniwa) mkataba na Yanga,...? We taja hata mmoja tu[emoji23]
Akitaja nitag[emoji23][emoji23][emoji23]

Majamaa yanabeba free agent tu(wachaezaji wa bure) wanaishia kubeba kina kambole,morisson,ki azizi, n.k hawawezi kununua mkataba hao

Sent from my PBBM00 using JamiiForums mobile app
 
Ni mchezaji gani wa maana ambaye amevunjiwa (amepambaniwa) mkataba na Yanga,...? We taja hata mmoja tu[emoji23]
Yule ambaye klabu yake ilishindwa kwenye masharti ya mkataba mpya baada ya Tajiri wa timu kukosa fedha za mshahara mpya na kupiga magoti uku akimwomba mchezaji apunguze mpaka milioni Saba kutoka 11.

Mchezaji aka mwambia Tajiri nenda Kwa Habib Kyombo utampata Kwa milioni 10 na mshahara wa laki Saba.
Tajiri akaufanyia kazi ushuri na sasa Wana Simba wanafuraha.
 
Hussein Massanza, niliku eleza kwenye ule uzi wako wa kwanza kuhusiana na huyu mchezaji, lakini ukaona kama naku challenge hivi, hatimaye yametimia…….
 
Yule ambaye klabu yake ilishindwa kwenye masharti ya mkataba mpya baada ya Tajiri wa timu kukosa fedha za mshahara mpya na kupiga magoti uku akimwomba mchezaji apunguze mpaka milioni Saba kutoka 11...
Ni kwamba mpaka sasa hamjasajili mchazaji yoyote wa maana.
 
Akitaja nitag[emoji23][emoji23][emoji23]

Majamaa yanabeba free agent tu(wachaezaji wa bure) wanaishia kubeba kina kambole,morisson,ki azizi, n.k hawawezi kununua mkataba hao

Sent from my PBBM00 using JamiiForums mobile app
Unakuta mtu antamba eti wamesajiki wachezaji wa gharama, ilhali hakuna hata mmoja ambae wamemvunjia mkataba.

Wale wa mwaka jana wote walikuwa ni reject wa team zao za zamani, hawa wa sasa hivi karibia wote ni free agent na hata huyo Aziz Ki ni wa kawaida ila kwasababu aliwafunga Simba Sc ndio akaonekana mzuri.

Mchezaji wa maana pale ASEC alikuwa ni Konate tu.
 
Unakuta mtu antamba eti wamesajiki wachezaji wa gharama, ilhali hakuna hata mmoja ambae wamemvunjia mkataba...
Mtaje mchezaji wa Sasa au miaka 20 iliyopita namba 10 mwenye uwezo wakucheza eneo lote la mbele apo Simba kama K. Aziz
 
Back
Top Bottom