Habibu B. Anga (The Bold) Mungu akupe maisha marefu sana, afya njema pamoja na baraka tele. I sincerely appreciate your writings brother. All the best

Nilimkubali sana mwanzo huyo jamaa na nilikuwa big fan wake ila alivoanza kusimulia nusunusu mara aende kumalizia hadithi zake kwenye group la WhatsApp ambalo sijui member ili wajoin walipie nikaona apa kuna kitu Story mara isimuliwe wiki mbili hata haieleweki itaisha lini nikaona isiwe tabu nikapotezea kufatilia afu alikuja kuungana na Mzee wa Canada Tycoon Ontario nkapunguza speed kumfatilia mpaka now simfatilii kabisa ila yupo vizuri kwenye data collection na Kuzi merge ili zileta Attractive storu shida yake ameshindwa kujua approach sahihi ya kuingiza pesa kupitia JF na Kalamu anayotumia
 
mzee baba umeandika pasipo kuweka nukta hata moja.
 
Huyu mshkaji naskia alisilimu nikweli mkuu? The bold, and now anaitwa Habibu.
Ni muislam wa kuzaliwa msichunguze chunguze vitu visivyowahusu muhimu soma kile anachokiandika kama ni mkristo muislam au buddha ita utakavyoita ila acheni kutaka kuyafahamu hayo hayakuongezei maarifa yoyote.

Nikuulize....hivi unadhani na unaamini kabisa kwamba kama kweli ipo siku walimwengu tutahukumiwa unadhani Mungu atazingatia hiki kipengele cha dini?umekuwa mkristo au muislam kama hukutenda utu jinsi utashi uliopewa ulivyokuelekeza jua moto ni wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Ndugu zangu Watanzania huyu Habibu B. Anga (The Bold) Mungu ampe maisha marefu sana, afya njema pamoja na baraka tele. I sincerely appreciate his writings here on JF. I wish him all the best.

Ninapenda kutumia wasaa huu kutuma salama zangu za pongezi pamoja na heartfelt appreciation kwa ndugu yangu Habibu B. Anga kwa makala zake nzuri sana humu JF ambazo honestly nimekuwa nikijifunza mambo mengi sana mema na mazuri ambayo nilikuwa sijawahi kuyafahamu hapo kabla.

Mimi pia ni mwandishi wa makala kule jukwaa la Jamii Intelligence ila Habibu B. Anga anajua sana kusimulia na kupangilia story zake. Kwa kweli ananikosha sana. Ona hii sasa;

Christiano Ronaldo (CR7) alipokuwa bado anachezea Real aliwahi kuwapiga hat trick Atletico Madrid katika uwanja wa nyumbani wa Santiago Bernabeu kwenye mechi ya kwanza ya league kuu wa Spain (La Liga)

Kwenye mechi ya Round ya Pili katika uwanja wa nyumbani wa Atletico Madrid wa Estadio Metropolitano Ronaldo akapiga tena hat trick.

Baada ya kuona vile mashabiki woooote wa Atletico Madrid kwa heshima kubwa wakaamua kunyanyuka juu ya viti vyao na wote kwa pamoja kuanza kumpigia makofi CR7 baba lao.

Habibu ndio CR7 wa Jamiiforums kwa sasa.

Mkuu, endelea kutupa ladha pasipo kuchoka.

Long live Habibu. Long live JamiiForums.
upo vizuri sana kijana kama unajua kutoa appreciation. ubarikiwe na wewe
 
Ni muislam wa kuzaliwa msichunguze chunguze vitu visivyowahusu muhimu soma kile anachokiandika kama ni mkristo muislam au buddha ita utakavyoita ila acheni kutaka kuyafahamu hayo hayakuongezei maarifa yoyote.
well said bro.@
 
Tangu nakuwa tunaambiwa hivi hasa sisi Waswahili "Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni". Katika vitu ambavyo namkubali mdau ni namna ya usimuliaji wake, yaani mambo ya kitafiti anakuwa ana yaandika kama story. Hili nafsi yangu huwa shahidi kwamba anajua sana.

Lakini kitu kingine ambacho anatakiwa akiweke sawa au anaweza kutuambia akiona hili ninalo liandika ni kwamba hizi habari huwa anazipata wapi na je huwa anatumia njia gani kujua aidha habari anazoziweka humu ni za kweli au si za kweli. Mathalani ukisoma makala yake ya "UNIT 15" anasimulia jambo kama yeye ni mtu katika hilo tukio au ameshuhudia hilo tukio au amesimuliwa na muhusika, wakati kiuhalisia si kweli, na makala kama hizi kwa uadilifu anapaswa kutuonyesha wapi amenukuu, kwani kwa watu watafiti na wenye kuhoji mambo, huwa anawaondolea mzuka, yaani ile hamasa na kuwapa gagaiko na huchukulia kama kiburudisho tu. Nini maanisha hapa, haoa alitakiwa awe ana tuambia "Anasimulia fulani katika kitabu chake fulani..... ", hii ingezidi kumjengea uaminifu zaidi na zaidi.

Lakini kadhalika kuna makala yake moja, hii makala alitakiwa kuipitia upya, ni ile makala inayo husu "Hukumu ya kuchinjwa watu kwenye kadamsi" au kama alivyo andika,ile makala ina dosari nyingi sana, kuanzia kwenye kichwa cha makala mpaka yale yaliyomo ndani.
 
Makala ya kuchinja watu inadosari gani mkuu utujuze ?
 
Back
Top Bottom