NairobiWalker
JF-Expert Member
- Oct 31, 2012
- 14,267
- 14,890
Soma vizuri, kuwa na bajeti kubwa siyo kigezo pekee cha wananchi wake kuwa na maisha mazuri. Ndiyo maana narudia hakuna tofauti kubwa kimaisha kati ya wananchi wa Tanzania na Kenya hivyo hizi kelele zenu hazina maana.
Mfano Hakuna m-Ethiopia mkimbizi wa kiuchumi anataka kukaa Kenya ndiyo maana wanaelekea South Afrika kupitia Kenya au vijana wenye nguvu zao wa- Eritrea / Watanzania /Wa-Uganda n.k wenye kutafuta maisha wote wanaelekea nchi zingine siyo Kenya sababu kuu ni kuwa hakuna tofauti kubwa kimaisha hilo lazima ukubali.
Wanajamvi heshima sana.
Naomba tujikite katika hoja kwanza badala ya kukimbuilia kurushiana madongo pasipo sababu za msingi.
Ni kweli bajeti ya Kenya ni kubwa ukilinganisha na nchi zote za Afrika Mashariki.Hilo halina ubishi hata kidogo.Kenya ina uchumi mkubwa ukilinganisha na nchi zingine za Afrika Mashariki.
Wakati Jumuiya ya Afrika Mashariki inafufuliwa tena na Marais Ali Hassan Mwinyi wa Tanzania,Daniel Arap Moi wa Kenya na Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda bajeti ya Kenya ilikuwa kubwa mara nne zaidi ya bajeti ya Tanzania.Kenya ilikuwa ikiuza bidhaa katika soko la EC huku nchi nyingine zikibaki kama soko la bidhaa za Kenya,ukiangalia sekta ya utalii Kenya ilikuwa ikipokea watalii mara mbili hadi tatu zaidi ya watalii walikuokuja Tanzania.Kwa ujumla kila sekta Kenya ilikuwa imetawala na kuziacha nchi nyingine mbali sana.
Bajeti ya mwaka 2016/17 pengo baina ya Kenya na Tanzania limezidi kupungua sana,bajeti ya Kenya ni 22.62 bilion na Tanzania 13.51 bilion dollar ya USA. Ukitazama hili pengo ni U$ 9 billion litazidi kupunguzwa kila mwaka mfano tukichukua sekta ya gas pekee yake inatarajiwa kuingiza taifa zaidi ya u$ 2.5 billion kila mwaka.Usafirisha wa mafuta ya Uganda unatarajiwa kuliingizia taifa (Tanzania) u$ 1.022 billion hapo bado sijaguza mipango ya Tanzania kuuza umeme nje ya nchi na sekta ya utalii inayotarajiwa kukua hadi kufikia watalii 2 million.Kenya bado ina kimbembe cha Alshabab bajeti yake itajikita zaidi katika masuala ya ulinzi na usalama.Isitoshe mradi wake wa Lapsset uliobuniwa na Rais Kenyatta upo katika hali mbaya baada ya nchi washirika katika maradi huo kuukimbia.Mfano Ethiopia imekimbilia Djibuti,Uganda,Rwanda na Congo DRC zimetorokea Tanzania ambayo ina ukomavu wa siasa ukilinganisa na Kenya inayotarajiwa kufanya uchaguzi wake 2017.
Naomba kuwasilisha kwa mjadala wa afya na hoja zenye maana si viroja.
Wakati wa Moi bajeti ya Kenya hata haikufika $5B, sahii pengo kati ya bajeti ya Kenya na Tz ni $9B na bado unasema pengo linapunguka. Hivi wewe unafikiria kwa akili ama kwa mapua?
we dont know but as a person am pretty sure haikua _$2B ndio imake hiyo difference ya $7B iko sahii....unless thats true then its obvious the gap inaongezekaHivi umeandika Kiswahili au kikuyu.Kama wakati wa Moi bajeti ilikuwa haifiki $ 5B, umewahi kujiuliza wakati wa A H Mwinyi bajeti ya Tanzania ilikuwa $ ngapi ?.
Wakati wa Moi bajeti ya Kenya hata haikufika $5B, sahii pengo kati ya bajeti ya Kenya na Tz ni $9B na bado unasema pengo linapunguka. Hivi wewe unafikiria kwa akili ama kwa mapua?
Hawa akina Ngongo ni wakuhurumiwa tu, yaani tangu lini tofauti ya bajeti ya Kenya na Tanzania ikawa zaidi ya ilivyo sasa. Yaani tofauti ya sasa ya $9B
bajeti yetu leo ni karibia mara mbili ya bajeti yao halafu wanasema pengo linazidi kupungua. Hawa watu vioja na wakuhurumiwa.
Euro Bonds ni nini?Euro Bonds ni sehemu ya hiyo budget?
Duh hawawezi kujibu hii.Euro Bonds ni sehemu ya hiyo budget?
Nimepita Kibaigwa juzi Wakenya kibao wamefata mahindi, nichukue fursa hii kuwakumbusha wahusika zile mashine za kupepeta mahindi mkazitengenezeWe Towashi wa 2, hebu nipe elimu yako kwanza? Eti Tanzania inawategemea Kenya kwa mazao ghafi, unaweza kuleta ushahidi wa unachosema! Kenya hii yenye njaa kila mwaka?
Wako hoi....walikopa wakitegemea bomba la mafuta linapita kule. ..kama hela wamekula itawanyolosha muda sio mrefuDuh hawawezi kujibu hii.
Mkopo wa masharti magumuEuro Bonds ni nini?
masharti kama yapi hivi?Mkopo wa masharti magumu
Inategemea....just Google to learn about itmasharti kama yapi hivi?
Just tell people what you know manInategemea....just Google to learn about it
hehe mi napita hapa nikicheki majaabu tuHehehe huwa mnatia huruma.
ficha ujinga wako...wahurumishaHapo 50% inatumika kwenye military kupambana na Al Shabeeeebbbb...interesting