Wanajamvi heshima sana.
Naomba tujikite katika hoja kwanza badala ya kukimbuilia kurushiana madongo pasipo sababu za msingi.
Ni kweli bajeti ya Kenya ni kubwa ukilinganisha na nchi zote za Afrika Mashariki.Hilo halina ubishi hata kidogo.Kenya ina uchumi mkubwa ukilinganisha na nchi zingine za Afrika Mashariki.
Wakati Jumuiya ya Afrika Mashariki inafufuliwa tena na Marais Ali Hassan Mwinyi wa Tanzania,Daniel Arap Moi wa Kenya na Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda bajeti ya Kenya ilikuwa kubwa mara nne zaidi ya bajeti ya Tanzania.Kenya ilikuwa ikiuza bidhaa katika soko la EC huku nchi nyingine zikibaki kama soko la bidhaa za Kenya,ukiangalia sekta ya utalii Kenya ilikuwa ikipokea watalii mara mbili hadi tatu zaidi ya watalii walikuokuja Tanzania.Kwa ujumla kila sekta Kenya ilikuwa imetawala na kuziacha nchi nyingine mbali sana.
Bajeti ya mwaka 2016/17 pengo baina ya Kenya na Tanzania limezidi kupungua sana,bajeti ya Kenya ni 22.62 bilion na Tanzania 13.51 bilion dollar ya USA. Ukitazama hili pengo ni U$ 9 billion litazidi kupunguzwa kila mwaka mfano tukichukua sekta ya gas pekee yake inatarajiwa kuingiza taifa zaidi ya u$ 2.5 billion kila mwaka.Usafirisha wa mafuta ya Uganda unatarajiwa kuliingizia taifa (Tanzania) u$ 1.022 billion hapo bado sijaguza mipango ya Tanzania kuuza umeme nje ya nchi na sekta ya utalii inayotarajiwa kukua hadi kufikia watalii 2 million.Kenya bado ina kimbembe cha Alshabab bajeti yake itajikita zaidi katika masuala ya ulinzi na usalama.Isitoshe mradi wake wa Lapsset uliobuniwa na Rais Kenyatta upo katika hali mbaya baada ya nchi washirika katika maradi huo kuukimbia.Mfano Ethiopia imekimbilia Djibuti,Uganda,Rwanda na Congo DRC zimetorokea Tanzania ambayo ina ukomavu wa siasa ukilinganisa na Kenya inayotarajiwa kufanya uchaguzi wake 2017.
Naomba kuwasilisha kwa mjadala wa afya na hoja zenye maana si viroja.