Hadi bajeti ya Tanzania, Uganda na Rwanda ziunganishwe ndio zifikie ya Kenya

Hadi bajeti ya Tanzania, Uganda na Rwanda ziunganishwe ndio zifikie ya Kenya

Soma vizuri, kuwa na bajeti kubwa siyo kigezo pekee cha wananchi wake kuwa na maisha mazuri. Ndiyo maana narudia hakuna tofauti kubwa kimaisha kati ya wananchi wa Tanzania na Kenya hivyo hizi kelele zenu hazina maana.

Mfano Hakuna m-Ethiopia mkimbizi wa kiuchumi anataka kukaa Kenya ndiyo maana wanaelekea South Afrika kupitia Kenya au vijana wenye nguvu zao wa- Eritrea / Watanzania /Wa-Uganda n.k wenye kutafuta maisha wote wanaelekea nchi zingine siyo Kenya sababu kuu ni kuwa hakuna tofauti kubwa kimaisha hilo lazima ukubali.

Saa zingine mie huchoka kujibu umburula
 
Wanajamvi heshima sana.

Naomba tujikite katika hoja kwanza badala ya kukimbuilia kurushiana madongo pasipo sababu za msingi.

Ni kweli bajeti ya Kenya ni kubwa ukilinganisha na nchi zote za Afrika Mashariki.Hilo halina ubishi hata kidogo.Kenya ina uchumi mkubwa ukilinganisha na nchi zingine za Afrika Mashariki.

Wakati Jumuiya ya Afrika Mashariki inafufuliwa tena na Marais Ali Hassan Mwinyi wa Tanzania,Daniel Arap Moi wa Kenya na Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda bajeti ya Kenya ilikuwa kubwa mara nne zaidi ya bajeti ya Tanzania.Kenya ilikuwa ikiuza bidhaa katika soko la EC huku nchi nyingine zikibaki kama soko la bidhaa za Kenya,ukiangalia sekta ya utalii Kenya ilikuwa ikipokea watalii mara mbili hadi tatu zaidi ya watalii walikuokuja Tanzania.Kwa ujumla kila sekta Kenya ilikuwa imetawala na kuziacha nchi nyingine mbali sana.

Bajeti ya mwaka 2016/17 pengo baina ya Kenya na Tanzania limezidi kupungua sana,bajeti ya Kenya ni 22.62 bilion na Tanzania 13.51 bilion dollar ya USA. Ukitazama hili pengo ni U$ 9 billion litazidi kupunguzwa kila mwaka mfano tukichukua sekta ya gas pekee yake inatarajiwa kuingiza taifa zaidi ya u$ 2.5 billion kila mwaka.Usafirisha wa mafuta ya Uganda unatarajiwa kuliingizia taifa (Tanzania) u$ 1.022 billion hapo bado sijaguza mipango ya Tanzania kuuza umeme nje ya nchi na sekta ya utalii inayotarajiwa kukua hadi kufikia watalii 2 million.Kenya bado ina kimbembe cha Alshabab bajeti yake itajikita zaidi katika masuala ya ulinzi na usalama.Isitoshe mradi wake wa Lapsset uliobuniwa na Rais Kenyatta upo katika hali mbaya baada ya nchi washirika katika maradi huo kuukimbia.Mfano Ethiopia imekimbilia Djibuti,Uganda,Rwanda na Congo DRC zimetorokea Tanzania ambayo ina ukomavu wa siasa ukilinganisa na Kenya inayotarajiwa kufanya uchaguzi wake 2017.

Naomba kuwasilisha kwa mjadala wa afya na hoja zenye maana si viroja.

Wakati wa Moi bajeti ya Kenya hata haikufika $5B, sahii pengo kati ya bajeti ya Kenya na Tz ni $9B na bado unasema pengo linapunguka. Hivi wewe unafikiria kwa akili ama kwa mapua?
 
Wakati wa Moi bajeti ya Kenya hata haikufika $5B, sahii pengo kati ya bajeti ya Kenya na Tz ni $9B na bado unasema pengo linapunguka. Hivi wewe unafikiria kwa akili ama kwa mapua?

Hivi umeandika Kiswahili au kikuyu.Kama wakati wa Moi bajeti ilikuwa haifiki $ 5B, umewahi kujiuliza wakati wa A H Mwinyi bajeti ya Tanzania ilikuwa $ ngapi ?.
 
Hivi umeandika Kiswahili au kikuyu.Kama wakati wa Moi bajeti ilikuwa haifiki $ 5B, umewahi kujiuliza wakati wa A H Mwinyi bajeti ya Tanzania ilikuwa $ ngapi ?.
we dont know but as a person am pretty sure haikua _$2B ndio imake hiyo difference ya $7B iko sahii....unless thats true then its obvious the gap inaongezeka
 
Wakati wa Moi bajeti ya Kenya hata haikufika $5B, sahii pengo kati ya bajeti ya Kenya na Tz ni $9B na bado unasema pengo linapunguka. Hivi wewe unafikiria kwa akili ama kwa mapua?

Hawa akina Ngongo ni wakuhurumiwa tu, yaani tangu lini tofauti ya bajeti ya Kenya na Tanzania ikawa zaidi ya ilivyo sasa. Yaani tofauti ya sasa ya $9B
bajeti yetu leo ni karibia mara mbili ya bajeti yao halafu wanasema pengo linazidi kupungua. Hawa watu vioja na wakuhurumiwa.
 
Wa Tzn tuache kukomaa na Kenya wakati ukweli uko wazi wameendelea kupita sie,turudi kujadili mambo yetu mfano hivi nini economical rationale ya kuwapa wachina prime area ya kurasini eti wajenge magodwns ya bidhaa zao ndio tuwe tunaenda kununua hapo badala ya China.Naomba kuuliza hivi hiyo ndio project ya kujenga uchumi wa viwanda au upuuzi mtupu? Tubishane kwa mambo haya sio kuhusu bajeti ya Kenya
 
Kenya, mmeshalipa Euro bonds? Waangalieni Ghana na Mozambique wanaendeleaje
 
Hawa akina Ngongo ni wakuhurumiwa tu, yaani tangu lini tofauti ya bajeti ya Kenya na Tanzania ikawa zaidi ya ilivyo sasa. Yaani tofauti ya sasa ya $9B
bajeti yetu leo ni karibia mara mbili ya bajeti yao halafu wanasema pengo linazidi kupungua. Hawa watu vioja na wakuhurumiwa.

Euro Bonds ni sehemu ya hiyo budget?
 
We Towashi wa 2, hebu nipe elimu yako kwanza? Eti Tanzania inawategemea Kenya kwa mazao ghafi, unaweza kuleta ushahidi wa unachosema! Kenya hii yenye njaa kila mwaka?
Nimepita Kibaigwa juzi Wakenya kibao wamefata mahindi, nichukue fursa hii kuwakumbusha wahusika zile mashine za kupepeta mahindi mkazitengeneze
 
Back
Top Bottom