Hadi Kenya inabezwa kanisani kule Tanzania, ndugu zetu huu ujasiri mnautoa wapi?

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Mchungaji huyu ambaye huenda kushauri hadi ikulu anadiriki kuchekelea idadi ya waathirika Kenya, halafu watu wanamshabikia, mtu kama huyu ndiye anategemewa kuongoza taifa kwenye maombi.

Huu ni wakati wa kuchukua tahadhari, acheni vya hovyoo, hiki kirusi hakijui mipaka wala utaifa, hata maombi sidhani kama yatafanya kazi maana dunia imejaa maasi.

Hii video inauma kwa kweli.

Facebook

hqdefault.jpg

michuzijr_60972817_148512542951570_1144757953477379838_n.jpg
 
Mkuu, ukipata news update zingine za Tz nijuze. Yaonekana unajua mengi sana ya tz na unafuatilia sana mambo ya huku zaidi yangu.

Updates za Tz ziko nyingi sana, ni vigumu kuleta humu, tutajaza server za watu bure.
Hapa naleta ambazo kiaina zinaigusa Kenya au kwa namna moja au nyingine zina kitu kinachoweza kujadiliwa na Wakenya, kama hii mnabeza Kenya mpaka makanisani halafu mnasema mnaomba.
 
Useless thread,,

Mnaambiwa mrudi kanisani msali wakenya mtajifungia ndani hadi lini?

Wakat huo mnamwita magufuri kaidi,
Wakat rais wenu yuko bae anakunywa Gongo.huku akiwambia wananchi wake mjifungie...

Kanisa sio majengo, ila ipo ndani ya mioyo yetu, rais wetu alishatuagiza tuendelee kuomba ila tukiwa kwenye nyumba zetu, nyie mumeambiwa muombe ila mkikusanyika huko huko kansani na kupumuliana.
Kama wewe ni Mkristo kasome Hosea 4:6
 
Mwili upo KENYA roho ipo TANZANIA

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
Mkuu Sio huyu tuu, Wakenya wengi wanaifuatilia sana Tz kuliko nchi yao. Kuna jamaa mmoja anaitwa Miguna..huyo bora tumpe uraia wa lazima maana Tz imemkaba koo haswa.
Ila kuna usemi, "mti wenye matunda hulengwa mawe"
 
Mwili upo KENYA roho ipo TANZANIA

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
Huyu jamaa nahisi ana vimelea vya Tz, hata kiswahili chake kimenyooka kama cha wabongo. Najua wamombasa tunafanana nao kwa mengi ila huyu kazidi.
Updates za Tz ziko nyingi sana, ni vigumu kuleta humu, tutajaza server za watu bure.
Hapa naleta ambazo kiaina zinaigusa Kenya au kwa namna moja au nyingine zina kitu kinachoweza kujadiliwa na Wakenya, kama hii mnabeza Kenya mpaka makanisani halafu mnasema mnaomba.
Mkuu, suala la kubeza usitegemee kila mTz au kila binadamu ataongea vizuri kuhusu kenya. Hata nyie mbona mmemuita rais wetu stuborn ila freshi tu. Ni neno la kawaida hilo ila chombo kikubwa cha habari kumuita rais wa jirani hivyo ni fedheha, hatujamaindi kivile sababu tunajua ndio binadamu walivyo, wataongea watakavyo na huwezi wazuia.
hivyo basi tulieni nanyi kwenye kiti cha salumi kama mnamyolewa mkisikiliza MAWAIDHA ya huyo mchungaji mwenye maono makali akiwanywesha dawa.
 
Jua kutofautisha kati ya jambazi anaekukwida na mtu mjanja mjanja anaekutoa pesa yako mfukoni kwa maneno tu..
Na hicho ndicho unachokiona hapo ni brainwash tu ili apige chake maisha yasonge.. swala la kutumika kenya na Tanzania ni kielelezo tu cha kuvutia zaidi ili kuwahadaa ni hivyo tu watu wanachumia tumbo.
 
Huyu jamaa nahisi ana vimelea vya Tz, hata kiswahili chake kimenyooka kama cha wabongo. Najua wamombasa tunafanana nao kwa mengi ila huyu kazidi.

Mkuu, suala la kubeza usitegemee kila mTz au kila binadamu ataongea vizuri kuhusu kenya. Hata nyie mbona mmemuita rais wetu stuborn ila freshi tu. Ni neno la kawaida hilo ila chombo kikubwa cha habari kumuita rais wa jirani hivyo ni fedheha, hatujamaindi kivile sababu tunajua ndio binadamu walivyo, wataongea watakavyo na huwezi wazuia.
hivyo basi tulieni nanyi kwenye kiti cha salumi kama mnamyolewa mkisikiliza MAWAIDHA ya huyo mchungaji mwenye maono makali akiwanywesha dawa.

Rais kusemwa akikaidi mbona inasemwa kote, Trump alikaidi na kupuuza maoni ya wataalam, kirusi kimeipiga Marekani mpaka wigi zimemsimama, leo anasemwa sana.
Hilo sio tusi ukiangalia kwa mtazamo wa Kikenya, maana huku tumezoea kumsema rais wetu akiboronga, matamko ya rais wenu kuruhusu muendelee na mibanano kwenye makanisa, hapo ni wazi alikadi na kupuuza ushauri wa kitaalam na ingetamkwa na rais wetu Uhuru aisei angetafuta pakutokea maana angesemwa na Wakenya hadi achoke.
Tatizo kwenu mumesahau urais ni taasisi ya umma mpaka mumekua too personal, hamtaki kumshauri, kila siku mnamuimbia misifa na mapambio hata kwenye mambo ya kutisha kama haya ya sasa. Utakuta wataalam wenu wote kimyaaaa!!!
 
Ok.
Kenya oyeeeeeeee..
 
Wakenya hebu mtuache kwanza fanyeni mambo yenu na sisi tufanye yetu kwenye kipindi hiki corona ikiisha tutajua nani alipita njia sahihi

Mtuhubiri mpaka kwenye makanisa halafu tusiwaseme.
 
Hi
Kanisa sio majengo, ila ipo ndani ya mioyo yetu, rais wetu alishatuagiza tuendelee kuomba ila tukiwa kwenye nyumba zetu, nyie mumeambiwa muombe ila mkikusanyika huko huko kansani na kupumuliana.
Kama wewe ni Mkristo kasome Hosea 4:6
Hiyo ndio maana halisia ya kanisa. La kuhuzunisha ni pale watu wanakongamana kwa ajili ya maombi halafu wanapageuza kikao cha kukejeli na kusabasi. Bali na kero, ni kufuru kiaina mbele ya mwenyezi mungu!..
 
Rais kusemwa akikaidi mbona inasemwa kote, Trump alikaidi na kupuuza maoni ya wataalam, kirusi kimeipiga Marekani mpaka wigi zimemsimama, leo anasemwa sana.
Hilo sio tusi ukiangalia kwa mtazamo wa Kikenya, maana huku tumezoea kumsema rais wetu akiboronga, matamko ya rais wenu kuruhusu muendelee na mibanano kwenye makanisa, hapo ni wazi alikadi na kupuuza ushauri wa kitaalam na ingetamkwa na rais wetu Uhuru aisei angetafuta pakutokea maana angesemwa na Wakenya hadi achoke.
Tatizo kwenu mumesahau urais ni taasisi ya umma mpaka mumekua too personal, hamtaki kumshauri, kila siku mnamuimbia misifa na mapambio hata kwenye mambo ya kutisha kama haya ya sasa. Utakuta wataalam wenu wote kimyaaaa!!!
Mmezoea kukosolewa ila mhubiri tu huyu kawatoa povu..
 
Mhubiri hajakosoa, ingekua amekosoa wala hatungeona kama issue maana huku tumezoea kukosoana na kuambiana kweli, lakini huyo mhubiri anapotosha na mnamshabikia utadhani mchezaji wa Simba kafunga bao.
 
Na bado, nabii tito anakuja na nyingine ya kenya.

Kwa sasa sidhani kama wahubiri wenu hao watakua na ujasiri wa kuibeza Kenya tena maana namba zenu zinanapandisha kwenye kirusi, uzembe wa kutokuchukua tahadhari utawaweka wahubiri wenu kuwa busy kidogo, kesho msongamane kwenye hayo makanisa muone shughuli yake, mfahamu hekima tumepewa na Mungu tuitumie.
 
Kenya namba zashuka licha ya kuchukua tahadhari TOKA MWANZO? Cases ni ngapi na fatalities ni ngapi?
Mkuu, hii sio ligi.
 
Back
Top Bottom