Hadi leo najiuliza, ilikuwaje tukajenga SGR kwenda Burundi na kuacha kuboresha TAZARA kuwa SGR ambapo tungefika Congo kirahisi sana

Hadi leo najiuliza, ilikuwaje tukajenga SGR kwenda Burundi na kuacha kuboresha TAZARA kuwa SGR ambapo tungefika Congo kirahisi sana

Reli ya TAZARA alijenga kihistoria, Mkopo wa ujenzi wa Reli hii ulikamilika kulipwa awamu ya 5 ila hatujui mikataba iliyokaingiwa huko nyuma maana mchina nae mjanja lazima alichungulia fursa ya miaka 100 mbele.

Reli ya kati mkakati wake ni mizigo pamoja na abiria, ni Rahisi sana kupata abiri kwa reli ya kati kuliko Tazara japo sisemi kuwa si bora. Reli ya kati itaenda kutuunganisha na kuboresha biashara kati ya Tanzania na Uganda, Tanzania na Rwanda, Tanzania na Burunduni pamoja na Congo

Kuna inchi kama 4 hapo ambazo zitarahusisha biashara na ndiyo maana awamu iliyopita iliwekeza sana kwenye miundombinu na usafirisha mpaka kwenye maji na ndiyo maana uliona MV Victoria kule Ziwa Victoria inaanza na nyingine inaendelea kuundwa, Ziwa Nyasa pia na Tanganyika.

Issue ni Strategic Plan tu
Hakuna nchi ambayo ina mzigo wa kuleta bandari ya dar
Burundi ,Rwanda hazina cha ku export ambacho kitakuwa na significant effect.

Tazara ndo ilikuwa reli ya kuitegemea kwa ajili ya kuiweka busy dar port.

Congo wakiamua kisafirisha magogo tu,. Wanaeza kuiweka busy Tazara railway
 
Afrika mtu akiwa cheti anafanya kazi na kujituma sana.Akipata Diploma anaongeza juhudi na ubunifu na kufanya kazi Kwa uaminifu . Akipata digrii Moja anafanya kazi Kwa majivuno. Akipata mastars anafanya kazi Kwa majivuno na dharau. Akipata PhD anafanya kazi Kwa mikataba,vikao na kuangalia maslahi tuu. Bila posho hafanyi kazi. Yaani PhD yake ni ya kupata mshahara mkubwa na marupurupu basi na anafanya kazi Kwa muda kidogo huku akisema kuwa afadhali Sasa napata mshahara mkubwa Kwa kazi kidogo,Tena ya kufanyiwa na walioko chini yake.
Akiwa Professor anaingia Jalalani na kuanza upya kama ombaomba mitaani ,tofauti yake ni kuwa ombaomba Kwa wakuu wenye kuweza kumtoa Jalalani na kumpa neema ya maisha Bora.
Mchezo unaishia hapo anakua ni mtu wa kusifu na kuabudu wanadamu wenzake Tena wenye Elimu ndogo kuliko yeye.

Usitegemee wasomi na watawala wa afrika wafanye jambo lenye maslahi mapana Kwa Taifa zaidi ya kuangalia matumbo yao. Miradi mikubwa Ina pesa nyingi sana za wizi. Kila mtawala anawaza miradi mipya na kutelekeza miradi iliyoko tayari na inayozalisha. Mfano Mradi wa gesi.Wapya walikuja wakautelekeza mradi wa gesi na kuturudisha wanakotaka wao kisa walituaminisha kuwa mradi wa gesi una ifisadi lakini hawawachukulii hatua hao waliofanya ifisadi.

Reli ya TAZARA ni standard G Railwas imekosa umeme tu kuendesha train ya umeme.
Duh
 
Hakuna nchi ambayo ina mzigo wa kuleta bandari ya dar
Burundi ,Rwanda hazina cha ku export ambacho kitakuwa na significant effect.

Tazara ndo ilikuwa reli ya kuitegemea kwa ajili ya kuiweka busy dar port.

Congo wakiamua kisafirisha magogo tu,. Wanaeza kuiweka busy Tazara railway
Hadi Leo nashindwa kuelewa kwa Kweli ilikuwaje tukaamua kujenga SGR kwenda Burundi?

Hata hao Burundi sijui kama wana uwezo wa kiuchumi wa kuifikisha Congo kwa haraka reli ile!
 
SGR haiendi Uganda! Inaishia Mwanza!

Kama target ni Congo , kulikuwa na haja gani kuipeleka Burundi na Rwanda tena kwa gharama kubwa sana? Kwa nini tusingeboresha TAZARA na kufika Congo kirahisi sana?
Ni kujipendekeza tu, ilipaswa priority iwe sgr kwenda kigoma.

Kaliua-mpanda-kalema (kisha unajenga kalema kuwa bandari).

TAZARA mnaijenga pia tawi kutokea tunduma kwenda kasanga na mnajenga bandari ya kasanga.

Yaani ziwa Tanganyika kunakuwa bandari tatu ambazo zinafeed drc kuanzia kalemie mpaka katanga lubumbashi.

Kusema unajenga sgr kwenda rwanda ili upeleke mizigo drc ni kujidanganya tu.

Northern drc inatumia mombasa route sana.
 
Very bold
Siasa inapeleka sgr kwenda Rwanda na burundi nchi ambazo hazina zinacho exoprt
Sgr. Hata ikifika huko itakuwa inarudi na mabehewa empy kama maroli ya rwanda, burundi ,shinyanga na mwanza yanavyorudi Dar.
huwa sielewi kagame amewaroga kwa uchawi gani ccm....malori yanayokwenda rwanda ndiyo hayo unayakuta manyoni yamepaki yanasubiri mnada wa kuku walete dar.
 
Hadi Leo nashindwa kuelewa kwa Kweli ilikuwaje tukaamua kujenga SGR kwenda Burundi? Hata hao Burundi sijui kama wana uwezo wa kiuchumi wa kuifikisha Congo kwa haraka reli ile!
Politics mkuu

Burundi hata kama akijenga hiyo reli kwenda kongo bado haifiki kwenye sehemu potential za copper cobalt's n.k

Kiufupi its not worth it kwa burundi kujenga reli hiyo
 
huwa sielewi kagame amewaroga kwa uchawi gani ccm....malori yanayokwenda rwanda ndiyo hayo unayakuta manyoni yamepaki yanasubiri mnada wa kuku walete dar.
Halafu wana hati punguzo ya roadtoll!
 
Ni kujipendekeza tu, ilipaswa priority iwe sgr kwenda kigoma. Kaliua-mpanda-kalema (kisha unajenga kalema kuwa bandari). TAZARA mnaijenga pia tawi kutokea tunduma kwenda kasanga na mnajenga bandari ya kasanga. Yaani ziwa Tanganyika kunakuwa bandari tatu ambazo zinafeed drc kuanzia kalemie mpaka katanga lubumbashi. Kusema unajenga sgr kwenda rwanda ili upeleke mizigo drc ni kujidanganya tu. Northern drc inatumia mombasa route sana.
Kwa nini kipaumbele kikubwa kikawekwa kwenda Kigoma badala ya ya kwenda Zambia na Zambia tayari Kuna mfumo wa Reli hadi kwenda mji mkubwa kibiashara wa Lubumbashi?

Huoni kuwa kuna shida?

Kwa nini basi tusingepeleka hadi Kigoma tu na Kalema then izo Bandari ziboreshwe ili mizigo ifike Congo kwa meli though ni njia ndefu sana!

Kwa nini tumetumia hela nyingi kupeleka hadi Mwanza?
 
Afrika mtu akiwa cheti anafanya kazi na kujituma sana.Akipata Diploma anaongeza juhudi na ubunifu na kufanya kazi Kwa uaminifu . Akipata digrii Moja anafanya kazi Kwa majivuno.

Akipata mastars anafanya kazi Kwa majivuno na dharau. Akipata PhD anafanya kazi Kwa mikataba,vikao na kuangalia maslahi tuu. Bila posho hafanyi kazi. Yaani PhD yake ni ya kupata mshahara mkubwa na marupurupu basi na anafanya kazi Kwa muda kidogo huku akisema kuwa afadhali Sasa napata mshahara mkubwa Kwa kazi kidogo,Tena ya kufanyiwa na walioko chini yake.

Akiwa Professor anaingia Jalalani na kuanza upya kama ombaomba mitaani ,tofauti yake ni kuwa ombaomba Kwa wakuu wenye kuweza kumtoa Jalalani na kumpa neema ya maisha Bora. Mchezo unaishia hapo anakua ni mtu wa kusifu na kuabudu wanadamu wenzake Tena wenye Elimu ndogo kuliko yeye.

Usitegemee wasomi na watawala wa afrika wafanye jambo lenye maslahi mapana Kwa Taifa zaidi ya kuangalia matumbo yao. Miradi mikubwa Ina pesa nyingi sana za wizi. Kila mtawala anawaza miradi mipya na kutelekeza miradi iliyoko tayari na inayozalisha. Mfano Mradi wa gesi.Wapya walikuja wakautelekeza mradi wa gesi na kuturudisha wanakotaka wao kisa walituaminisha kuwa mradi wa gesi una ifisadi lakini hawawachukulii hatua hao waliofanya ifisadi.

Reli ya TAZARA ni standard G Railwas imekosa umeme tu kuendesha train ya umeme.
well said mkuu.

Lakini TAZARA ni cape gauge si standard gauge.

But cape gauge bado iko kwenye chat sana.

Kuitelekeza ni uzuzu tu umetamalaki
 
Politics mkuu
Burundi hata kama akijenga hiyo reli kwenda kongo bado haifiki kwenye sehemu potential za copper cobalt's n.k
Kiufupi its not worth it kwa burundi kujenga reli hiyo
Hili swali inabidi kupelekwa Bungeni.
 
Kwa nini kipaumbele kikubwa kikawekwa kwenda Kigoma badala ya ya kwenda Zambia na Zambia tayari Kuna mfumo wa Reli hadi kwenda mji mkubwa kibiashara wa Lubumbashi? Huoni kuwa kuna shida?

Kwa nini basi tusingepeleka hadi Kigoma tu na Kalema then izo Bandari ziboreshwe ili mizigo ifike Congo kwa meli though ni njia ndefu sana! Kwa nini tumetumia hela nyingi kupeleka hadi Mwanza?
Kupeleka kigoma pia ni kuhudumia watz wengi wa magharibi mwa nchi.

Watu wa magharibi wanafurahia na wanapenda usafiri wa treni kuliko mabasi.

kwa sababu usafiri wa train salama zaidi kuliko mabasi

Tatizo la TAZARA ni ownership. hebu fikiria, zaidi ya 70% ya reli ya tazara iko tanzania lakini dg wa tazara kimkataba anatakiwa atoke zambia.

Hivyo tz inaona kama tazara ni kwa ajili na ni ya zambia.

Upande wa zambia, siasa za ccm hawazielewi na hivyo huona bora wasijikite sana katika kuwekeza tazara badala yake wanatumia hata reli za kushuka kwenda south maana tazara imeungana na reli inayoshuka kwenda south africa mpaka cape town
 
Kupeleka kigoma pia ni kuhudumia watz wengi wa magharibi mwa nchi. Watu wa magharibi wanafurahia na wanapenda usafiri wa treni kuliko mabasi. kwa sababu usafiri wa train salama zaidi kuliko mabasi

Tatizo la TAZARA ni ownership. hebu fikiria, zaidi ya 70% ya reli ya tazara iko tanzania lakini dg wa tazara kimkataba anatakiwa atoke zambia. Hivyo tz inaona kama tazara ni kwa ajili na ni ya zambia.

Upande wa zambia, siasa za ccm hawazielewi na hivyo huona bora wasijikite sana katika kuwekeza tazara badala yake wanatumia hata reli za kushuka kwenda south maana tazara imeungana na reli inayoshuka kwenda south africa mpaka cape town
Kumbuka SGR inajengwa kwa fedha za mkopo na gharama zake ni zaidi ya Trilion 25 kufika hapo kigoma tu!

Kama target ya Serikali ni kuhudumia wananchi basi huo utakuwa wehu wa Kiwango cha rami maana kama inajengwa kwa fedha za mkopo inaweza kuchukua hata miaka 200 kurudisha hilo deni na haitakuwa na faida yoyote kwa Taifa.

Hoja yako kuhusu siasa za CCM na Zambia hazina mashiko kwa sababu hata Kenya siasa zake na CCM haziendani Ila Mbona tunatumia diplomasia vizuri sana kuweka maslahi yetu ya kiuchumi vizuri na Kenya!
 
Lol...kwani kagame ameweka hati punguzo kwa malori ya tz yanayokatisha rwanda kwenda drc?.....witchcraft is real
Ishu ni kuwa alitaka tulipe sawa , gari za Tanzania na Rwanda , 160 usd , return
Trick is Rwanda umbali mkubwa utakaotembea kutoka rusumo ni kwenda bugarama ambapo ni 400 plus kms, kwa rate ya 160 usd ni kiwango sahihi cha roadtoll kwa nchi nyingi Africa .

Rwanda analipa hiyo 160 usd halafu anakwenda Dar na Ruvuma , 1200 plus kms
 
Kumbuka SGR inajengwa kwa fedha za mkopo na gharama zake ni zaidi ya Trilion 25 kufika hapo kigoma tu!

Kama target ya Serikali ni kuhudumia wananchi basi huo utakuwa wehu wa Kiwango cha rami maana kama inajengwa kwa fedha za mkopo inaweza kuchukua hata miaka 200 kurudisha hilo deni na haitakuwa na faida yoyote kwa Taifa.

Hoja yako kuhusu siasa za CCM na Zambia hazina mashiko kwa sababu hata Kenya siasa zake na CCM haziendani Ila Mbona tunatumia diplomasia vizuri sana kuweka maslahi yetu ya kiuchumi vizuri na Kenya!
kwa nini umepoteza nguvu as if nimesema sgr ni kwa ajili ya kuwahudumia wananchi tu?...nimesema "ni kuwahudumia wananchi pia". kwamba such a direct clause umeshindwa kuelewa inamaanisha nini?

Hata hivyo jukumu la serikali ni nini? hivi unadhani kujenga sgr kwenda kigoma. kisha kaliua-mpanda ni hasara?

TRC mpaka sasa wanasurvive kwa sababu ya train na mizigo inayosafirishwa kwenda njia hizo tu.
jaribu kustudy geopolitic ya tz mkuu
 
Back
Top Bottom