Hadi leo najiuliza, ilikuwaje tukajenga SGR kwenda Burundi na kuacha kuboresha TAZARA kuwa SGR ambapo tungefika Congo kirahisi sana

Hadi leo najiuliza, ilikuwaje tukajenga SGR kwenda Burundi na kuacha kuboresha TAZARA kuwa SGR ambapo tungefika Congo kirahisi sana

Ishu ni kuwa alitaka tulipe sawa , gari za Tanzania na Rwanda , 160 usd , return
Trick is Rwanda umbali mkubwa utakaotembea kutoka rusumo ni kwenda bugarama ambapo ni 400 plus kms, kwa rate ya 160 usd ni kiwango sahihi cha roadtoll kwa nchi nyingi Africa .
Rwanda analipa hiyo 160 usd halafu anakwenda Dar na Ruvuma , 1200 plus kms
ndiyo maana huwa anatuona mafa.la
 
kwa nini umepoteza nguvu as if nimesema sgr ni kwa ajili ya kuwahudumia wananchi tu?...nimesema "ni kuwahudumia wananchi pia". kwamba such a direct clause umeshindwa kuelewa inamaanisha nini?

Hata hivyo jukumu la serikali ni nini? hivi unadhani kujenga sgr kwenda kigoma. kisha kaliua-mpanda ni hasara?

TRC mpaka sasa wanasurvive kwa sababu ya train na mizigo inayosafirishwa kwenda njia hizo tu.
jaribu kustudy geopolitic ya tz mkuu
Kwa upande wa mizigo tungeboresha Tazara kuiwekea umeme na kuwa Kiwango cha SGR hali ingekuwaje?

Kulifanyika hata comparison kulinganisha hayo mambo mawili?

Kwenda Hadi Mpanda naweza kwambia kuwa ni hasara kwa sababu Bado sioni faida za kiuchumi za haraka maana still faida zinategemea effectiveness ya Bandari ya Kalema
 
Siku Saba zilizopita shirika la habari la Ujerumani DW wametoa makala nzuri sana kuelezea upekee wa Reli ya Tazara inayotoka Tanzania hadi Ndola nchini Zambia.

Wameelezea upekee wa reli hii na namna inavyopita kwenye mbuga maarufu za Selous na Mikumi na inavyopita mwenye milima ya Iringa hadi kuingia Zambia.

Waandaaji wa Makala hii wamehoji sana uchakavu wa reli hii na namna ambavyo serikali za nchi zetu zimeipuuza na kiufanya ichakae sana na kutoleta matunda yaliyokusudiwa!

Baada ya kuiona Makala hii nimegundua kuwa Reli ya Tazara inafika hadi Zambia ambapo Kuna urefu wa kilomita chache sana Kwenda Congo ambazo Pia zimeunganishwa na reli nyingine Kwenda Congo , Mji wa Lubumbashi ambao ni mji Mkuu wa kibiashara.

Kwa ninavyojua reli ya kati kwa Kiwango cha SGR mpaka mwanza na Kigoma itagharimu kiasi cha Trilioni si chini ya 25 kwa ujumla wa vipande vyote.

Jambo lililonishangaza ni kuwa tayari Reli ya Tazara inafika hadi Ndola Zambia na kuna Reli nyingine inafika hadi Lubumbashi , Congo kutoka Zambia.

Je haikuwa sahihi kwetu kuboresha Reli ya Tazara kwa Kiwango cha SGR na kuiwekea umeme na kuongea na Zambia kidiplomasia tukawakopesha hela za kuboresha reli kutoka Zambia hadi Lubumbashi Congo kwa Kiwango cha SGR?

Kwa mtazamo wangu naona gharama za kuboresha Reli ya Tazara kwenda Congo kwa Kiwango cha SGR ingekuwa ndogo sana kuliko kuijenga upya hadi Burundi na kuanza kuongea na Burundi ili waifikishe Congo jambo ambalo sidhani kama litakamilika hivi karibuni kutokana na hali ya kiuchumi ya Burundi! Na uhohehae wao kutokana na vita!

Nauliza swali hili kwenu wadau! Je kulikuwa na haja Kweli ya kujenga Reli ya SGR kwenda Kigoma na Mwanza? Au Tungeboresha tu TAZARA kuwa Kiwango cha SGR ambapo tungetumia gharama ndogo na kufika Congo kirahisi sana?

Hii ndo ramani ya Zambia inavyoonesha ukaribu wa Zambia na Lubumbashi Congo na urahisi wa kufika Congo kupitia reli ya TAZARA

View attachment 2160243

Waulize mataga na chawa wa Mwendazake 😄😄.

Utasikia itadumu miaka 100 😬😬
 
Kwa upande wa mizigo tungeboresha Tazara kuiwekea umeme na kuwa Kiwango cha SGR hali ingekuwaje?
Kulifanyika hata comparison kulinganisha hayo mambo mawili?

Kwenda Hadi Mpanda naweza kwambia kuwa ni hasara kwa sababu Bado sioni faida za kiuchumi za haraka maana still faida zinategemea effectiveness ya Bandari ya Kalema
Reli ya Kati inalenga Congo mashariki,Burundi,rwanda,uganda
 
SGR haiendi Uganda! Inaishia Mwanza!

Kama target ni Congo , kulikuwa na haja gani kuipeleka Burundi na Rwanda tena kwa gharama kubwa sana? Kwa nini tusingeboresha TAZARA na kufika Congo kirahisi sana?
Congo ni kubwa sana,

Tazara inaweza kupokea mizigo ya Lubumbashi, Burundi na Rwanda zinaweza kupokea mizigo ya Bukavu na Kisangani.

Kwahivyo kazi iendelee ya kuifungua nchi
 
Kwa upande wa mizigo tungeboresha Tazara kuiwekea umeme na kuwa Kiwango cha SGR hali ingekuwaje?
Kulifanyika hata comparison kulinganisha hayo mambo mawili?

Kwenda Hadi Mpanda naweza kwambia kuwa ni hasara kwa sababu Bado sioni faida za kiuchumi za haraka maana still faida zinategemea effectiveness ya Bandari ya Kalema

..nini hasara za Tazara kuwa Cape Gauge Rail?

..reli zote za nchi za SADC ni Cape Gauge Rail.

..unanichanganya hapo kwenye Standard Gauge vs Cape Gauge.
 
..nini hasara za Tazara kuwa Cape Gauge Rail?

..reli zote za nchi za SADC ni Cape Gauge Rail.

..unanichanganya hapo kwenye Standard Gauge vs Cape Gauge.
Hajui kama Tazara ilishakuwa na project ya ku-update reli yake ilianza kuunganishwa Dar mpaka Zambia miaka ya 90's kama sikosei, kuna jamaa zangu walipata ajira kwenye project hiyo na mpaka sasa bado wapo wanafanyakazi Tazara.

Labda tu kuna kitu hakijui, hapo Tazara sasa hivi kuna treni ya mizigo ya kampuni ya makaburu ambayo inatumia tu miundombinu ya Tazara lakini ina wafanyakazi wake na treni zake.

Washambenga wengi hawana habari hata media zetu nina hakika hawajui kinachoendelea Tazara ya leo.
 
Kitu ambacho huwa sielewi ni ili swala.

Tungeamua kuboresha njia reli ya kati tukajenga depot mfano dodoma na morogoro malori yote yanayofanyw transit yanachukulia mzigo hapo na kusambaza.

Kiasi cha pesa tungeweza kujenga highway zinazosogea hadi mipakani kurahisha usafirishaji wa mizigo na abiria.

Reli ingesaidia kupungua mrundikano wa mizigo bandarini maana ni kutoa na kupeleka depot kwa ajili ya other transit.

Hakuna lori ambalo lingeruhusiwa kufika ukanda wa bandari
 
Kitu ambacho huwa sielewi ni ili swala. Tungeamua kuboresha njia reli ya kati tukajenga depot mfano dodoma na morogoro malori yote yanayofanyw transit yanachukulia mzigo hapo na kusambaza.

Kiasi cha pesa tungeweza kujenga highway zinazosogea hadi mipakani kurahisha usafirishaji wa mizigo na abiria.

Reli ingesaidia kupungua mrundikano wa mizigo bandarini maana ni kutoa na kupeleka depot kwa ajili ya other transit. Hakuna lori ambalo lingeruhusiwa kufika ukanda wa bandari
Si ndio plan ya bandari kavu ya Kwala?
 
Jambo lililonishangaza ni kuwa tayari Reli ya Tazara inafika hadi Ndola Zambia na kuna Reli nyingine inafika hadi Lubumbashi , Congo kutoka Zambia.

Je haikuwa sahihi kwetu kuboresha Reli ya Tazara kwa Kiwango cha SGR na kuiwekea umeme na kuongea na Zambia kidiplomasia tukawakopesha hela za kuboresha reli kutoka Zambia hadi Lubumbashi Congo kwa Kiwango cha SGR?
Wewe 'Jamaa' huwa sikuelewi kabisa katika 'thought process'yako ikoje?

Sasa kama umesema TAZARA imetelekezwa na nchi hizo mbili, licha ya kuwepo uhitaji wake mkubwa sana, ni kipi kinachokufanya udhani kwamba SGR na yenyewe itapitia matatizo hayo hayo?

Wala huna muda wa kjiuliza ni sababu zipi hasa zinafanya TAZARA isithaminiwe sana na mmojawapo wa hawa washirika wawiwli?

Umejiuliza kama mshirika mmoja anaona anazo njia mbadala za kufikisha mizigo anayotaka, na kutokuwa na haja ya kushughulikia TAZARA?

Au umejiuliza ufanisi wa bandari inayohudumiwa na TAZARA, pengine ndiyo inayochangia TAZARA isiwe na ufanisi?

Na mwisho, hivi unajuwa kusoma ramani kweli ikiwekwa mbele yako, ili kujuwa ni sehemu zipi hasa za DRC ambazo zinahitaji kuhudumiwa zaidi ya hiyo Lubumbashi?

Unajuwa DRC ilivyo kubwa, toka kusini hadi Kaskazini? Hata kama leo sehemu za Kaskazini zitakuwa zina matatizo, wewe unadhani hali itakuwa hivyo hivyo daima?

Ndiyo, TAZARA inahitaji kukarabatiwa ili ifanye kazi zake kwa ufanisi zaidi, na bandari yetu nayo inahitajika kufanya kazi kwa weledi zaidi ili mizigo ya nchi hizo zote iweze kuongezeka; na kama kutakuwepo na ulazima wa kuifanya iwe ya SGR, basi iwe hivyo kwa wakati maalum tukiwa na uwezo wa kufanya hivyo.

Lakini kwa sasa, huwezi kudharau umuhimu wa SGR inayopitia katikati mwa Tanzania, si kwa manufaa ya nchi yetu pekee, bali hata kwa majirani zetu pia, kibiashara.
 
Kitu ambacho huwa sielewi ni ili swala. Tungeamua kuboresha njia reli ya kati tukajenga depot mfano dodoma na morogoro malori yote yanayofanyw transit yanachukulia mzigo hapo na kusambaza.

Kiasi cha pesa tungeweza kujenga highway zinazosogea hadi mipakani kurahisha usafirishaji wa mizigo na abiria.

Reli ingesaidia kupungua mrundikano wa mizigo bandarini maana ni kutoa na kupeleka depot kwa ajili ya other transit. Hakuna lori ambalo lingeruhusiwa kufika ukanda wa bandari
Hizi 'Depot' zimezungumziwa mara nyingi sana, lakini naona kuna maslahi ya watu yanayozuia mpango huo kufanyika.

Ni maswala ya "Kamba ndefu tu" yanayozuia mambo mengi ya maana yasifanyike hapa nchini. Maneno mengi matamu matamu, lakini inapokuja kwenye utendaji, ni tofauti kabisa!
 
Reli ya Kati haifiki Kagera inaenda Mwanza ambapo kufika Uganda lazima upande tena meli na kusafiri si chini ya masaa 24!

Reli ya kati SGR imeenda Mwanza na Kigoma na hapo hakuna tena Reli kwenda Burundi!

Kulikuwa na haja gani kujenga Reli ya kati kwa Kiwango cha SGR?
Kumbe hata huna ufahamu wa jambo unalolizungumzia; unaweka tu mada mradi umesikia habari ya TAZARA ikizungumziwa?
 
Bado hata tazara haihitaji kujengwa kuwa SGR.

TAZARA ni cape gauge ambayo bado ni modest sana. tatizo ni siasa zetu za kiafrica.

Siasa ya ccm imeisusa tazara ambayo inafeed nchi kama zambia na southern drc na imeikumbatia rwanda yenye ukubwa wa 26,000kmsq kama mkoa wa Tanga.

Ni aibu sana.
Reli zetu hatujengi kuwanufaisha majirani, tunajenga kwa manufaa yetu wenyewe kwanza, halafu majirani wanapata makombo yetu. SGR haikujengwa kwenda Rwanda, bali ilijengwa kwenda Mwanza, na Kigoma baadaye. Rwanda, Uganda, Burundi na DRC watajiunganisha kwenye SGR yetu kwa kushirikiana nasi siyo kuwa tumawajengea.

TAZARA ilijengwa mwaka 1970 kwa ajili ya kuifanya Zambia isiwe tegemezi kwa nchi za Rhodesia, Mozambique, and South Africa ambazo zilikuwa hazijapata uhuru wakati huo. Baada nchi zote tatu hizxo kupata Uhuru, Zambia imekuwa haiitegemi TAZARA sana kwani inaweza kutumia bandari za Beira, Maputo, Richards Bay na Durban. TAZARA ilikuwa ni ubia kati ya Tanzania na Zambia kwa mkopo kutoka China; kwa hiyo uamuzi wowote wa kuboresha TAZARA siyo wa serikali ya Tanzania tu, ni lazima Serikali ya Zambia ihusike pia. Uamuzi wa kuboresha reli za TRC ni wa serikali ya Tanzania tu; tutaamua kwa wakati tunaoona unatufaa
 
Kiongozi wa watu vs kiongozi wa Mapaka😁😁😁
 
Muhimu reli zetu ziungane na majirani, mfano reli ya Kilimanjaro Tanga ifike Mombasa, ya Kati ifike Kongo, ya Mwanza ikunje Bukoba hadi Uganda, tutafutiwe Mv Liemba mpya kwenda Congo, Mv Mbeya ifike Malawi. Huko ndio kufungua nchi
 
Back
Top Bottom