ndiyo maana huwa anatuona mafa.laIshu ni kuwa alitaka tulipe sawa , gari za Tanzania na Rwanda , 160 usd , return
Trick is Rwanda umbali mkubwa utakaotembea kutoka rusumo ni kwenda bugarama ambapo ni 400 plus kms, kwa rate ya 160 usd ni kiwango sahihi cha roadtoll kwa nchi nyingi Africa .
Rwanda analipa hiyo 160 usd halafu anakwenda Dar na Ruvuma , 1200 plus kms
Kwa upande wa mizigo tungeboresha Tazara kuiwekea umeme na kuwa Kiwango cha SGR hali ingekuwaje?kwa nini umepoteza nguvu as if nimesema sgr ni kwa ajili ya kuwahudumia wananchi tu?...nimesema "ni kuwahudumia wananchi pia". kwamba such a direct clause umeshindwa kuelewa inamaanisha nini?
Hata hivyo jukumu la serikali ni nini? hivi unadhani kujenga sgr kwenda kigoma. kisha kaliua-mpanda ni hasara?
TRC mpaka sasa wanasurvive kwa sababu ya train na mizigo inayosafirishwa kwenda njia hizo tu.
jaribu kustudy geopolitic ya tz mkuu
Waulize mataga na chawa wa Mwendazake 😄😄.Siku Saba zilizopita shirika la habari la Ujerumani DW wametoa makala nzuri sana kuelezea upekee wa Reli ya Tazara inayotoka Tanzania hadi Ndola nchini Zambia.
Wameelezea upekee wa reli hii na namna inavyopita kwenye mbuga maarufu za Selous na Mikumi na inavyopita mwenye milima ya Iringa hadi kuingia Zambia.
Waandaaji wa Makala hii wamehoji sana uchakavu wa reli hii na namna ambavyo serikali za nchi zetu zimeipuuza na kiufanya ichakae sana na kutoleta matunda yaliyokusudiwa!
Baada ya kuiona Makala hii nimegundua kuwa Reli ya Tazara inafika hadi Zambia ambapo Kuna urefu wa kilomita chache sana Kwenda Congo ambazo Pia zimeunganishwa na reli nyingine Kwenda Congo , Mji wa Lubumbashi ambao ni mji Mkuu wa kibiashara.
Kwa ninavyojua reli ya kati kwa Kiwango cha SGR mpaka mwanza na Kigoma itagharimu kiasi cha Trilioni si chini ya 25 kwa ujumla wa vipande vyote.
Jambo lililonishangaza ni kuwa tayari Reli ya Tazara inafika hadi Ndola Zambia na kuna Reli nyingine inafika hadi Lubumbashi , Congo kutoka Zambia.
Je haikuwa sahihi kwetu kuboresha Reli ya Tazara kwa Kiwango cha SGR na kuiwekea umeme na kuongea na Zambia kidiplomasia tukawakopesha hela za kuboresha reli kutoka Zambia hadi Lubumbashi Congo kwa Kiwango cha SGR?
Kwa mtazamo wangu naona gharama za kuboresha Reli ya Tazara kwenda Congo kwa Kiwango cha SGR ingekuwa ndogo sana kuliko kuijenga upya hadi Burundi na kuanza kuongea na Burundi ili waifikishe Congo jambo ambalo sidhani kama litakamilika hivi karibuni kutokana na hali ya kiuchumi ya Burundi! Na uhohehae wao kutokana na vita!
Nauliza swali hili kwenu wadau! Je kulikuwa na haja Kweli ya kujenga Reli ya SGR kwenda Kigoma na Mwanza? Au Tungeboresha tu TAZARA kuwa Kiwango cha SGR ambapo tungetumia gharama ndogo na kufika Congo kirahisi sana?
Hii ndo ramani ya Zambia inavyoonesha ukaribu wa Zambia na Lubumbashi Congo na urahisi wa kufika Congo kupitia reli ya TAZARA
View attachment 2160243
TAZARA ni sgrIzo Protokali ndo zimezuia kuboresha reli ya Tazara kuwa SGR?
Mbona hoja zako nyepesi sana?
Reli ya Kati inalenga Congo mashariki,Burundi,rwanda,ugandaKwa upande wa mizigo tungeboresha Tazara kuiwekea umeme na kuwa Kiwango cha SGR hali ingekuwaje?
Kulifanyika hata comparison kulinganisha hayo mambo mawili?
Kwenda Hadi Mpanda naweza kwambia kuwa ni hasara kwa sababu Bado sioni faida za kiuchumi za haraka maana still faida zinategemea effectiveness ya Bandari ya Kalema
Cartoon zako zilikuwa zinanifurahisha sana nyakati za mwenda zake😆😆😆😆🤣🤣🤣🤣
Congo ni kubwa sana,SGR haiendi Uganda! Inaishia Mwanza!
Kama target ni Congo , kulikuwa na haja gani kuipeleka Burundi na Rwanda tena kwa gharama kubwa sana? Kwa nini tusingeboresha TAZARA na kufika Congo kirahisi sana?
Bunge hilihili la kina Babu Tale na MwanaFa?Hili swali inabidi kupelekwa Bungeni.
Kwa upande wa mizigo tungeboresha Tazara kuiwekea umeme na kuwa Kiwango cha SGR hali ingekuwaje?
Kulifanyika hata comparison kulinganisha hayo mambo mawili?
Kwenda Hadi Mpanda naweza kwambia kuwa ni hasara kwa sababu Bado sioni faida za kiuchumi za haraka maana still faida zinategemea effectiveness ya Bandari ya Kalema
Hajui kama Tazara ilishakuwa na project ya ku-update reli yake ilianza kuunganishwa Dar mpaka Zambia miaka ya 90's kama sikosei, kuna jamaa zangu walipata ajira kwenye project hiyo na mpaka sasa bado wapo wanafanyakazi Tazara...nini hasara za Tazara kuwa Cape Gauge Rail?
..reli zote za nchi za SADC ni Cape Gauge Rail.
..unanichanganya hapo kwenye Standard Gauge vs Cape Gauge.
Si ndio plan ya bandari kavu ya Kwala?Kitu ambacho huwa sielewi ni ili swala. Tungeamua kuboresha njia reli ya kati tukajenga depot mfano dodoma na morogoro malori yote yanayofanyw transit yanachukulia mzigo hapo na kusambaza.
Kiasi cha pesa tungeweza kujenga highway zinazosogea hadi mipakani kurahisha usafirishaji wa mizigo na abiria.
Reli ingesaidia kupungua mrundikano wa mizigo bandarini maana ni kutoa na kupeleka depot kwa ajili ya other transit. Hakuna lori ambalo lingeruhusiwa kufika ukanda wa bandari
Wewe 'Jamaa' huwa sikuelewi kabisa katika 'thought process'yako ikoje?Jambo lililonishangaza ni kuwa tayari Reli ya Tazara inafika hadi Ndola Zambia na kuna Reli nyingine inafika hadi Lubumbashi , Congo kutoka Zambia.
Je haikuwa sahihi kwetu kuboresha Reli ya Tazara kwa Kiwango cha SGR na kuiwekea umeme na kuongea na Zambia kidiplomasia tukawakopesha hela za kuboresha reli kutoka Zambia hadi Lubumbashi Congo kwa Kiwango cha SGR?
Hizi 'Depot' zimezungumziwa mara nyingi sana, lakini naona kuna maslahi ya watu yanayozuia mpango huo kufanyika.Kitu ambacho huwa sielewi ni ili swala. Tungeamua kuboresha njia reli ya kati tukajenga depot mfano dodoma na morogoro malori yote yanayofanyw transit yanachukulia mzigo hapo na kusambaza.
Kiasi cha pesa tungeweza kujenga highway zinazosogea hadi mipakani kurahisha usafirishaji wa mizigo na abiria.
Reli ingesaidia kupungua mrundikano wa mizigo bandarini maana ni kutoa na kupeleka depot kwa ajili ya other transit. Hakuna lori ambalo lingeruhusiwa kufika ukanda wa bandari
Kumbe hata huna ufahamu wa jambo unalolizungumzia; unaweka tu mada mradi umesikia habari ya TAZARA ikizungumziwa?Reli ya Kati haifiki Kagera inaenda Mwanza ambapo kufika Uganda lazima upande tena meli na kusafiri si chini ya masaa 24!
Reli ya kati SGR imeenda Mwanza na Kigoma na hapo hakuna tena Reli kwenda Burundi!
Kulikuwa na haja gani kujenga Reli ya kati kwa Kiwango cha SGR?
Reli zetu hatujengi kuwanufaisha majirani, tunajenga kwa manufaa yetu wenyewe kwanza, halafu majirani wanapata makombo yetu. SGR haikujengwa kwenda Rwanda, bali ilijengwa kwenda Mwanza, na Kigoma baadaye. Rwanda, Uganda, Burundi na DRC watajiunganisha kwenye SGR yetu kwa kushirikiana nasi siyo kuwa tumawajengea.Bado hata tazara haihitaji kujengwa kuwa SGR.
TAZARA ni cape gauge ambayo bado ni modest sana. tatizo ni siasa zetu za kiafrica.
Siasa ya ccm imeisusa tazara ambayo inafeed nchi kama zambia na southern drc na imeikumbatia rwanda yenye ukubwa wa 26,000kmsq kama mkoa wa Tanga.
Ni aibu sana.