The Icebreaker
JF-Expert Member
- Feb 11, 2018
- 22,278
- 65,817
Umeamua kumtumia huyo Mama ili kutangaza biashara yako bila kua na mkataba nae wala kumlipa?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nilifikiri hujui wajibu wa mfanyabiashara kutunza habari za wateja kwa faragha.Habari zetu kupitia JF zinafika mbali sana.
Ishukuriwe platform hii kwa kutusaidia kuonekana kupitia mijadala yenye tija hasa kwa sisi eneo letu la ujenzi na hamasa tunazopeana humu.
Tunapenda kuwajuza tu kuwa Mama Dangote ni miongoni mwa wateja wetu waliofika #MbaoTanzania kuchukua mzigo wa kutosha hivi karibuni. Tunaamini bila shaka taarifa zetu alikutana nazo humu na kuamua kutufungia safari. Siku akirudi tutamuuliza zaidi.
UMBEA KIDOGO
Sasa, kama inavyofahamika si kawaida kumdadisi mteja na ni vyema kutunza siri za wateja (na tunazitunza), lakini kiukweli imetufurahisha kuona Mama huyu amechukua mzigo wa kutosha kiasi cha kujiuliza anajenga ghorofa?
Yes, tunajua mama ni bosslady hapa mjini na tulishawahi kutambulishwa ni moja wa MDs wa Kampuni ya Wasafi. Je, kwa mzigo huu unadhani atakuwa anashusha mjengo wa aina gani, maeneo yapi?
JF ni jungu kuu. Tunasubiri ukoko!
Nilifikiri hujui wajibu wa mfanyabiashara kutunza habari za wateja kwa faragha.
Kumbe unajua, umeamua kuvunja faragha ya mteja kwa makusudi tu.
Umeamua kumtumia huyo Mama ili kutangaza biashara yako bila kua na mkataba nae wala kumlipa?
Umaarufu wa Kuliwa na Vijana?
Taarifa kwamba Mama Dangote anajenga na kaja kununua mbao kwako ni nyeti. Hata wewe umejua hilo, ndiyo maana ukajihami kuongelea habari za siri za wateja.Hapa kuna faragha gani imevunjwa? Hakuna taarifa nyeti tulizotoa. Isitoshe uzi kama huu ungeweza kuanzishwa na yeyote ambaye amemuona hapo barabarani kwa sababu huyu ni celeb.
Ni kutangaza indirect coz huyo Mama ni maarufu,mbona wateja wengine huleti habari zao?Kumsifia mteja ni kutangaza biashara?
Mkuu kubashiwa ndio kufanyaje?Kuna thread ya kubashiwa huko ndio tinaconcetrate.
Kununua vifaa vya ujenzi anunue tu ila kashabashiwa.
Kweli hujui,njoo nikufundishe mammy🤗Mkuu kubashiwa ndio kufanyaje?
Nimeomba maana acha ungeseKweli hujui,njoo nikufundishe mammy🤗
Ndio kubashiwa huko kumbe unajuaNimeomba maana acha ungese
Taarifa kwamba Mama Dangote anajenga na kaja kununua mbao kwako ni nyeti. Hata wewe umejua hilo, ndiyo maana ukajihami kuongelea habari za siri za wateja.
Habari ya kujitetea kwa kusema "uzi kama huu ungeweza kuanzishwa na yeyote" ni sawa na mwizi aliyeiba, halafu anajitetea kwa kusema "mtu yeyote angeweza kuiba".
Huo si utetezi, hapo umekubali umefanya kitu.
Hujui kama huyo mama, ambaye ni mwingi wa habari, anajenga hiyo nyumba kinyemela hataki watu fulani wajue. Umemuanikia habari zake hapa umma ushajua. Kama kuna watu wanamdai washajua, kama kuna wezi wanatafuta mtu wa kumuibia washajua, kama kuna ndugu kupe wanapanga kufuata watu kuwa ombaomba washajua. Ushamuharibia.
Ni hivi, kwa mfanyabiashara wa level yako, ile list tu ya nani ni mteja wako ni list inayotakiwa kulindwa.
Siyo kwa kulinda faragha ya mteja tu. Hata kwa kuilinda biashara yako.
Kwa sababu mpinzani wako wa kibiashara anaweza kuisoma thread hii, akamtafuta huyo mama, akamtongoza kibiashara, akamchukua asiwe mteja wako tena.
Kwa hii familia ilivyo wala sitostaajabu wakienda buguruni na kupiga picha pale wauza mbao wanapashusha mizigo yao na kuja kuaminisha watu vinginevyo.
Na haitokuwa ajabu pia uzi huu ukawa umeandikwa na mmoja wa machawa wao. Maana upande mmoja mtu anakwambia anatunza siri ya mteja, upande mwingine anamuanika bibi wa watu na bahama yake.
Ni kutangaza indirect coz huyo Mama ni maarufu,mbona wateja wengine huleti habari zao?
Kama hamjakubaliana umrekodi kwa sababu fulani fulani basi unastahili cheti cha mfanyabiashara ambaye hajatumia akili 2022.
Tuna tofauti kubwa ya kifalsafa na hatuwezi kuelewana. Labda makosa yangu nakupa kanuni katika ulimwengu wako usio na kanuni.Huu mtazamo hatukubaliani nao, japo tunauheshimu.
1. Mantiki ya kusema uzi ungeweza kuanzishwa na yeyote ni kutokana na muktadha wa mteja, hadhi yake na jambo lenyewe. Isitoshe, kuja kununua mbao hakufanya siri ndio maana unaona hata video imerekodiwa akiwa comfortable hivyo kwake si tatizo.
2. Sera yetu haina uoga na washindani, sana sana tunashirikiana nao japo kwa tahadhari. Hivyo kutaja orodha ya wateja au mtu mwenye ushawishi kama Mama Dangote kwetu ni fahari kwa sababu inadhihirisha kuwa tunaaminika na hatuna ubabaishaji kama wauza mbao wengine.
Mwisho kabisa, tunaamini kwenye kutangaza mazuri ya wateja badala ya mabaya yao. Hatuoni tatizo wala athari ya kibiashara kwetu wala kwa mteja wetu kwa kuonesha kufurahia mafanikio yake.
Karibu Ujenge Nasi. Mbao zipo za kutosha.
Umekatika, publicity is publicity😄.Publicity is Publicity