GT
Leo tarehe 1 Dec watu wanashusha nodo kama hawana akili nzuri yote haya ni kufanya counter attack ya hotuba ya kesho.
Nadhani waandaaji wa hotuba ya Samia wanakazi ya kufanya maana matamko ni mengi mno watakuwa wana edit kila mara. Kitima ndo kawamaliza kabisa.
================
Gen-Z tumepokea taarifa hizi tumeona tuwambie yafuatayo wazee wetu.
1. Kwanza tunafahamu hawa sio Wazee wa Dar ifahamike kuwa hawa ni Wazee wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar na wanakwenda kukutana na Mwenyekiti wao wa Taifa CCM lakini pamoja na hayo Wazee wa Dar watusaidie kumwambia Samia Suluhu kwamba yeye sio Rais wetu - hatujamchagua, hakuna uchaguzi uliofanyika kwani Gen Z walifanikiwa kuonyesha dunia kuwa hakukuwa na uchaguzi.
2. Wazee Wa Dar watumie fursa hii kumshinikiza Samia Suluhu kujiondoa Madarakani na wamwambie Samia arudi Kizimkazi akalee wajukuu huku akisubiri kuwajibika iwe ndani au Mahakama za Kimataifa kwa mauaji aliyoyafanya tarehe 29-30 October.
3. Wazee Wa Dar wamambie Samia Suluhu aturudishie mateka wote aliowateka kwenye utawala wake, akiwemo mwanachama wake Humphrey Polepole, Mdude Nyagali, Soka na wengine wengi.
4. Wazee wa Dar wamwambie Samia kwamba, atupatie miili ya ndugu zetu tukazike. Kwani kuna familia nyingi hajawapata miili ya Nindugu zao ili wakaizike kwa heshima.
5. Wazee wa Dar wamwambie Samia yeye ni Rais haramu, wabunge ni haramu, madiwani ni haramu na wenyeviti wa mitaa, vijiji na vitongoji ni haramu.
6. Hakuna neno jipya ambalo atalizungumza Samia Sukuhu zaidi ya maneno aliyoyazungumza ya kuwatisha vijana wasiandamane, tunamwambia Maandamano ya Tarehe 9 Disemba yatakuwa maandamano makubwa ajabu ambayo hayajawahi kutokea katika historia ya maandamano Afrika na duniani, yatakuwa maandamano ya amani na waandamanaji tutakuwa na mabango tu.
Mwisho, wazee watumie busara zao kumsihi Samia Suluhu kujiulu mapema, kuunga mkono kuundwa kwa Serikali ya Mpito itakayoandaa katiba mpya na baadaye Uchaguzi huru na wa haki chini ya katiba Mpya,na tuwakumbushe Wazee kuwa wao hawawezi kuwa wasemaji wa vijana na hiyo haitazuia vijana kufanya maandamano ya amani kushinikiza Samia Suluhu ajiuzulu ili taifa lifungue ukurasa mpya.
1 DESEMBA 2025
View attachment 3510067