Hadithi: Kesi ya Mzee Mnyoka

Hadithi: Kesi ya Mzee Mnyoka

KESI YA MZEE MNYOKA 22
Mnyoka Sasa alirudi nyumbani huku akiamini ule utetezi wake kidogo ungesaidia kuwatia Hamasa viongozi ya kuweza kumpa haki yake, kutokana na Hali ngumu ya maisha Mzee Mnyoka Sasa aliamua kuuza baadhi ya vitu vyake pale Ndani ili apate hela ya kujikimu, aliuza baskeli yake Phoenix kwa shilingi elfu 75,

Alimpa mkewe mama Monica elfu 35 na nyingine akabaki nazo,


Mzee Mnyoka Sasa aliacha kabisa kwenda kanisani hata Ile siku moja kwa mwezi, hakuona umuhimu Tena wa kukutana na Padri John,


Mtoto wake James nae aliamua kumsaidia baba yake kwa kufanya vibarua pale mgodini, James Sasa aliweza kurudi na shilingi elfu 15 au 10 kila siku, ambapo alimpa mama yake ahifadhi,

Mzee Mnyoka hakupenda mwanae afanye kazi pale Mgodini, lakini Sasa hakuwa na namna yoyote Ile,


Alijisikia vibaya kuona badala mwanae angekuwa twisheni huko , Sasa yupo na wavuta bangi, na majambazi pale mgodini,...



Hakuwa na namna zaidi ya kumsisitiza tu kuwa Makini,


"Mambo haya yataisha tu,"

Mzee Mnyoka alikua akimwambia mwanae


************

Oscar yeye aliwahi mapema kabisa akajichanganya na wanafunzi pale getini, alijua kuwa lazima Kuna watu watakuja kumchukua Swalehe hivyo alikua makini kutazama mtu ambaye angetoka na Swalehe,


Wakati Pablo na mwenzake wanaingia,


Huku wamevaa vizibao vya Pilika Online TV, Oscar aliwapiga jicho,

Kama mpelelezi mzoefu alihisi Jambo kwenye muonekano wa Pablo, jinsi alivyoongea na jinsi alivyokua Oscar alikataa kuwa huyu Ni mwandishi tu,


Na wakati Pablo anainama kutoa vifaa vyake kwenye begi, ndipo Oscar alifanikiwa kuona bastola kiunoni mwa Pablo,

"Kumbe Ndio wewe!"

Oscar alijisemea Sasa akirudi nyuma Hadi kwenye piki piki yake, aliyokuja nayo,


Alishajua hawawezi kufanya tukio pale, Ni kweli baada ya muda Pablo alitoka na mtu wake kazi ikawa ndogo tu kwa Oscar kuwafuatilia,


Gari haikuelekea ubungo badala yake walinyoosha Kama wanaelekea mwenge, na ilipofika barabara ya shekilango wakasimama kwenye mataa,

Oscar alikua karibu nao kabisa, na kutokana na msongamano jioni idadi ya piki piki na magari ilikua kubwa hivyo Pablo asingeweza kufikiri kufuatiliwa ,

Gari iliendelea ilipofika sinza madukani, wakachukua barabara ya Uzuri
Halafu walipofika kwamtogole Gari wakaingia kulia,

Mwendo wa dakika 6 hivi wakatokea kwenye nyumba moja, Oscar akajifanya kuwapita kidogo Kisha akasimama kwa mbali kidogo, ilishakua saa moja na dakika kadhaa na giza lilikuwepo kwenye sehemu ambazo Hakuna taa, Oscar alijibanza na Kunyata pole pole, hakukua na geti , Oscar alinyata tu kuelekea kwenye Ile nyumba Kisha akatega sikio,

"Ngoja nimpigie, kuwa tushampata dogo"

Alisema Pablo.
"Ndio tunae hapa tunakusikiliza,

Ehh,
Ndio,

Sawa"

Pablo alikua anaongea na Tito,


"Anasema tumalize kazi halafu tuhakikishe Hakuna anayegundua , "


Pablo alimwambia mwezake,

Sasa sikia tunamaliza kazi halafu tutajua pa kumuweka,



Ni wakati huo Sasa Oscar alishusha Kofia yake inayofunika uso Kisha akafungua mlango pole pole,
Kwa kasi ya ajabu aliwatokea na hakuwapa muda wa kutafakari aliachia risasi mbili na sekunde kadhaa Pablo na mwenzake wakawa maiti pale pale,


Sasa alijaribu kumuamsha Swalehe lakini bado alikua amepoteza fahamu, alimbeba na kutoka nae nje begani Kisha akakumbuka kumsachi, alitoa simu yake na bahati mbaya ilikua na nywilla, hivyo akatoa line moja na kuweka kwenye simu yake Kisha akajaribu kukadiria namba moja wapo ya mtu wa karibu Ni wakati anajaribu kupiga Mara simu ikaita,

"Oya Kipanya vipi mbona hurudi Mwana? Si unajua tuna assignment kesho..."

Oscar alimkatisha,


"Sikiliza njooni hapa kwa mtogole mwenye simu Yuko hapa amezimia, njooni mtakuta karibu na mnara hapa kushoto nje ya nyumba,



Yeah, ukishuka sinza madukani unachukua uzuri road, kwamtogole unaingia barabara ya kulia Kama mita 200 hivi kwenye mnara wa simu kushoto Kuna nyumba ya vigae haina geti hapo nje mtamkuta"

Oscar alirudi kwenye piki piki yake akasubiri baada ya nusu saa Sasa zilizifika piki piki zaidi ya 4 wakamchukua Swalehe,.




Kesho yake Tito alimuita Oscar


"Yule dogo ameshindikana, Pablo na mwenzake wamekutwa wameuwawa na dogo Yuko hospitali, Sasa sijajua kitu gani kimetokea Ila Sasa nakupa kazi hiyo wewe,
Kammalize huyo mpuuzi pengine akawa amejua kitu fulani "


Alisema Tito


"Yuko hospitali gani kwani"

Oscar alimuuliza Tito

"Sijajua bado lakini tutajua muda si mrefu, shida ni kuwa tayari wanasiasa wameshalichukulia Hili suala tayari, hebu ona,"
Tito aliongea akimkabidhi "tablet" yake aangalie video

"Sisi Kama upinzani tutasimama na Swalehe, tunajua wapo viongozi hawataki kukosolewa, Sasa Bwana mdogo aliuliza swali dogo tu lile tayari wanataka kumuua, tayari nishaongea na Kamanda wa mkoa atoe majibu kuhusu jaribio Hili la mauaji ya mwanafunzi"

Alisema Mheshimiwa Farida, mbunge wa Kawe, wa chama Cha upinzani, huku akiwa amezunguukwa na wanahabari

"Duh Sasa hapa Mzee itakua ngumu kidogo kwa siku hizi maana chochote kibaya kikimtokea dogo itaonekana Kuna mkono wa mtu hebu tufikirie njia nzuri zaidi"

Alisema Oscar akimrudishia simu yake,

"Ngoja nimpigie kamanda Niongee nae"

Alisema Tito Kisha akabonyeza simu yake Tena,

Aliongea kwa dakika tano Kisha akatabasamu,

"Imeisha hii twende zetu Oscar"

Alisema Tito huku wakielekea kwenye Gari

Simu ya Oscar ilitikisika kidogo kuashiria ujumbe mfupi umeingia,

"Leo ni uingereza vs Panama mechi ya kirafiki usikose mechi hii kwenye screen kubwa pale kinondoni Pub saa 1 usiku "

Oscar aliangalia namba iliyotuma iyo sms Kisha akatabasamu!

***********
Iliundwa kamati ndogo ya watu watatu kuchunguza kesi ya Mzee Mnyoka,


Walifika nyumbani kwake asubuh na mapema, walianza kumhoji mkewe Kisha wakahoji na majirani kuhusu tabia na mwenendo wa Mzee Mnyoka, Kisha wakamaliza na Mzee Mnyoka mwenyewe,

"Kiukweli sisi hatujui Kama uliiba au la , sisi tunachuguza tu kujua ukweli, Kisha tutapeleka taarifa yetu kwenye Ofisi ya Kijiji, usijali Mzee Mnyoka kamati itatenda haki, Kama hukuiba Basi usiwe na wasi wasi, Ila tu uelewe itachukua muda sana"

Alisema mwenyekiti wa kamati,

Mzee Mnyoka Sasa aliona huu Ni "uzwazwa" kusubiri kesi isiyo na macho Wala masikio halafu imsubirishe huku watoto wake wakishindwa kwenda shule!

Aliamua Sasa liwalo na liwe aliingia chumbani kwake na kujifungia Kisha akatoa simu yake Ile aliyokua ameificha Kisha akapiga namba fulani aliyoelekezwa,

Namba haikupatikana,

Ni wakati anataka kuirudisha ndipo ikaita,

"Mzee Mnyoka Kuna jipya? "

Ilisikika sauti ya upande wa pili,

Mzee Mnyoka alitambua sauti ya Oscar alimueleza kwa ufupi kuhusu zuio la kuuza kahawa yake kwa kesi ambayo alikua hahusiki nayo

"Nitajie majina ya hao viongozi wa Kijiji"

Alisema Oscar ,
Mzee Mnyoka alimtajia
"Okay Sasa Mzee Niko bize kidogo hawa wote watahusika baadae kwasasa kwa ajili ya mahitaji yako na watoto wako kwenda shule, tutafanya namna, nakushauri jifanye mjinga wasikilize wanachokuambia ili tusiwakurupushe kwa ajili ya Ile inshu yetu, niamini Mzee serikali inatambua mchango wako, sema lazima Kuna Mambo ya kiitifaki yanachelewesha , kesho kutwa utapata msaada wa Pesa unaohitaji

Alisema Oscar Kisha akakata simu,


Mzee Mnyoka aliirudishia sehemu yake Kisha akatoka kwa bahati mkewe hakuwepo,

********
Oscar Sasa alikua amemaliza kuongea na Mzee Mnyoka Kisha akapiga simu mahali fulani huku akitaja jina la Mzee Mnyoka na Kijiji alicho na baadhi ya vitu Kisha akaingia kwenye Gari kwenda Kinondoni Pub,


Alifika Kama saa moja kasoro hivi Kisha akatafuta kiti na kukaa,

Ni baada ya dakika tano alikuja machinga akiwa anauza mikanda ya suruali, na viatu vya kiume, Alikua akipita meza moja baada ya nyingine mpaka alipokua Oscar ,

Alitoa Ile mikanda na viatu na Kisha akatoa kiatu kimoja kumpa Oscar ajaribishe,


Oscar alichukua kile kiatu na kukitazama,.
"Nipe mwenzake"

Alisema Kisha akapewa mwenzake

Na akapeana mkono na yule "muuzaji"

"Asante broo"

"Boya wewe, muone Sasa"

Alijibu Oscar,

Kwani ndani ya viatu vile kulikua na ujumbe ambao Oscar alikua ameomba aletewe kuhusu zile nyaraka alizokua ameiba kwa Tito

Na huyu machinga hakuwa mwingine Bali alikua Ni rafiki yake George..
Well uko vizuri
Unajaribu kupita katika nyayo za Beb Mtobwa ongeza Tashtiti kidogo kwenye Lugha itapendeza zaidi kwakuwa ni mwandishi mpya sio mbaya
Keep it up
 
KESI YA MZEE MNYOKA 23

Oscar alitoka na kuingia kwenye Gari, alitoa karatasi iliyokua kwenye vile viatu, Kisha akaanza kuisoma,

maelezo yalikua wazi wazi, kuwa taarifa zile zilihusu mapato na matumizi kwa mwezi wa 5 mwaka 2016, katika mgodi wa Kinjeki, ambapo Sasa taarifa hizi zilikua zinaenda kwa Bwana Johnson, ambaye ndie CEO wa UreFact,


Kwahiyo Oscar alipata kuelewa kuwa mtu wa tatu katika kampuni Ile alikua huyu Jamaa,

"Oh kumbe,"

Oscar aliwaza huku akienda kwa Tito,

Alimkuta Tito anasubiri taarifa ya habari ya SAA mbili, usiku,.

Ndipo akamkaribisha,


"Aisee karibu , kamanda kaniambia kamaliza kazi ngoja tuone kwenye habari watasemaje"


Tito aliongea akijiweka sawa,

"Karibu kwenye taarifa yetu ya habari usiku huu, na tunaanzia hapa jijini Dar es salaam

Kamanda wa polisi Kanda maalum amesema kwamba wanamshikilia kijana Swalehe Issa Mganga, mwanafunzi wa chuo kikuu Cha Dar es salaam kwa kile wanachodai kusema kuwa kijana huyo ALIJITEKA, hebu tumsikilize kamanda,"

"Ni kweli tunamshikiria kijana huyo kwa mahojiano maarum, vijana siku hizi wanatafuta popularity tu, na sisi porisi tumesema tutakua makini na mtu yoyote anayejaribu kureta taharuki kwa jamii, haiwezekan utekwe, harafu upige simu kuwa njooni mnichukue nimetekwa, huu Ni ujinga, hatutakubari jeshi ra porisi riingie doa"

Alimalizia kamanda yule kwa lafudhi yake ya "Kikuria"


Huku Sasa Tito machozi yalikuwa yanamtoka kwa kicheko,.

Oscar nae akajikuta anacheka tu


**************

Kijijini Kinjeki siku hiyo asubuh na mapema walikuja wageni wakijtambulisha kuwa Ni shirika lisilo la kiserikali wanahamasisha ujenzi wa vyoo na usafi, walisema watatoa zawadi kwa wanaume na watoto baada ya kuachia mziki kidogo Sasa uwanja wa Kijiji ulifurika,


Mzee Mnyoka nae alikuwepo, hakujua Hili Wala lile hivyo watoto walikua wakicheza na wale wageni walitoa zawadi mbali mbali, Kisha wakaita wazee kumi kumi pale mbele na kuwapa maswali ya kawaida kuhusu usafi n.k..
Huku wakichukua majina yao,

Baada ya kumaliza walisema watatoa zawadi kubwa zaidi kwa washindi na watakaopata bahati,


Hivyo mzee Mnyoka, Mzee Omari, Bwana Heri, Mzee mbega na wengine wakaingia fainali,


"Sasa kwa bahati nzuri washindi wetu wamegawana points kwahiyo tutatoa vikaratasi vyenye namba, na atakayepata namba ndogo zaidi Basi ndie mshindi wetu ambaye atapata shilingi milioni moja"

Alisema dada mmoja ambaye ndie aliyekua mshereheshaji,


Walitwa majina na kupewa namba Mzee Mnyoka nae akapewa namba yake, Kisha wakaambiwa wafungue vile vikaratasi,

"Naam, mshindi wetu Ni Mzee Mnyokaaaaaa! Makofi kwake jamani!"

Alisema mshereheshaji na Mzee Mnyoka akakabidhiwa Pesa zake!


Wanakijiji walimpongeza Mzee Mnyoka kwa bahati yake hiyo aliyokua nayo,

"Kweli Mungu katusaidia, wamezuia laki 3 za kahawa tumepata milioni moja"

Alisema mama Monica kwa Furaha,

Ni wakati anaingia chumbani Mzee Mnyoka Sasa alielewa , aliahidiwa kupewa msaada wa Pesa!

"Bila shaka ndio hizi! Wamenipa kwa staili hii ili watu wasielewe!"

Mzee Mnyoka akitabasamu Sasa alielewa hii ilikua kazi ya Oscar!

Hakumueleza chohote mke wake kuhusu Pesa zile zilipotoka, alihifadhi vizuri na pasipo sababu za msingi alizigawanya akaweka shilingi laki mbili chini ya godoro, na shilingi laki 4 juu ya dari na zilizobaki akaweka mezani,


siku hiyo Mzee Mnyoka alikua na furaha tele, alishasahau mambo ya kesi na hakuona Tena umuhimu wa kuumiza kichwa,

"Watanitafuta wao"

Alijisemea,

Mzee Mnyoka alikua amejenga nyumba yake kwa tofali za kuchoma na alifanikiwa kuezeka kwa bati ,ingawa lilikua limechakaa lakini nyumba ya Mzee Mnyoka ilikua ni moja Kati ya nyumba nzuri pale Kijijini,


Mzee Mnyoka pia alifanikiwa kuwa na televisheni pamoja na kisimbuzi Cha Azam,


Na hivyo Mara kadhaa vijana wangefika pale kwa Mzee Mnyoka kutazama mechi mbali mbali haswa zile zilizohusu Simba au Yanga,

Na hivyo halikua Jambo la ajabu kusikia makelele kutokea pale Nyumbani kwa Mzee Mnyoka,

Taarifa za Mzee Mnyoka kupata milioni moja zilisambaa pale kijijini na vijiji vya karibu Kama Moto wa mabua,


Na Sasa Wenye roho mbaya wakaanza kutafuta namna ya kugawana au kuzichukua zote....



***************


Oscar Mara nyingi alikua analala pale, na siku zote alizokaa , Sasa alizoeana na Joyce,

Mara nyingi usiku wangebaki wenyewe wakicheza michezo ya Komputa,

Kisha kila mmoja angeenda kulala,


Oscar alimchukulia Joyce Kama mdogo wake tu, kwanza Joyce alikua mdogo kiumri miaka 21 tu! Wakati Yeye Oscar kwenye vitambulisha vyake baadhi vilionyesha yeye ana miaka 35, vingine vingeonyesha yeye ana miaka 32 na pengine vingeonyesha ana miaka 29,

Wakati kwa uhalisa Oscar alikua na miaka 30,


Joyce alikua mwaka wa kwanza chuo kikuu nchini Uturuki, akisomea mambo ya mifumo ya Komputa, Oscar alipenda Sana kuwa karibu na Joyce katika muda wa ziada Kama huu maana Kuna vitu vingi alijifunza ,


Baada ya kutoka kwa Tito Sasa Oscar alipitiliza sebuleni ambako alimkuta Joyce akiwa anamsubiri,


Leo tunacheza FIFA 15,

Nimeshaapdate"


Alisema Joyce

Haya bhana,

Walianza kucheza na huku story zikinoga,

"Eti Kaka Oscar mkeo Yuko wapi kwani"

Alianza Joyce,


"Yupo tu ila sijui wapi,"
Oscar nae alijibu kibaharia

"Mh, na Mimi utanifundisha kupigana?"

Joyce aliongea sasa...

"Hahaha wewe, pigana na keypads na keyboard ya komputa tu!

Oscar aliongea Kisha akanyanyuka na kufungua mlango kuelekea kwenye chumba chake Cha siku zote,

Mazingira ya chumba chake ilibidi atoke nje Kwanza ndipo azunguuke kwenye korido kuelekea kwenye chumba chake ambacho tunaweza kusema hivyo,

Ni wakati anaingia ndipo geti likafunguliwa kuashiria ugeni,

Oscar alijificha kidogo kuangalia watu hao na hatimaye alimuona Mr Bill akiwa na Frank wakielekea ndani,

"Mh hawa jamaa usiku huu vipi?

Na mbona Tito asinijulishe?"

Oscar aliwaza huku akitafuta namna ya kusikiliza hayo maongezi yao,

***********

Mzee Mnyoka alimaliza kuangalia marudio ya kipindi Cha Bunge, Kisha akazima TV yake na kuelekea chumbani kwake, nyumba ya Mzee Mnyoka ilikua na vyumba vitatu vyumba viwili vikiwa ndani na chumba kingine ambacho mtoto wake James alilala mlango wake ulijitegemea kwa nje,


Mary alilala chumba Cha ndani karibu na sebule huku Mzee Mnyoka na mkewe wakitumia chumba kingine,


Wakati Mzee Mnyoka anapanda kitandani Mara taa zikazimika,

"Ooh umeme umeisha huo "

Mama Monica alidakia,

"Hapana nimeangalia kulikua na uniti 12 Jana tu, haziwezi Kwisha labda umekatika kwa muda au Kuna shoti mahali,"

Mzee Mnyoka alimjibu mkewe huku akipapasa papasa anapoweka tochi yake,


Ni wakati anahangaika ndipo sauti Ya Mary ikasikika akipiga kelele,

Ndani ya dakika mbili waliingia watu waliojifunika nyuso zao wakiwa na mapanga na marungu,

Walimtoa Mzee Mnyoka na mkewe mpaka sebuleni
Walikua wanne,

"Mzee tunataka pesa, lete pesa hapa kabla hatujafanya mambo mengine"

Alisema mmoja alionekana Kama kiongozi wao,

Mzee Mnyoka sasa alichanganyikiwa, mke wake sasa alikua analia huku akiomba wasiwadhuru

Hata hivyo Mzee Mnyoka alikuwa sasa akijiuliza alipo mwanae James kwa wakati ule,

Mzee Mnyoka aliwaangalia wale vijana huku akitamani enzi zake zijirudie,

Mzee Mnyoka wakati anatoroka kutoka jeshini alikua haswa kijana aliyekua na nguvu,


Vijana kama wale angeweza kuwanyamazisha dakika mbili tu!


Hata hivyo sasa hapa hakuwa peke yake, asingeweza kujitetea yeye pamoja na familia yake ,

Lakini je akiwapa hizo pesa watamuacha salama?

Alijua wazi vijana wale hawakutoka mbali, kwahiyo walijua uwepo wa millioni moja pale ndani,

Mzee Mnyoka sasa akawa na mawazo awape au asiwape...
 
KESI YA MZEE MNYOKA 24

Mnyoka alisimama,

"Sasa Kuna Giza pesa ziko ndani"

Mzee Mnyoka alisema,

"Oi nenda nae"

Alisema yule kiongozi akimueleza mwenzake,


Mpaka hapo Mzee Mnyoka alihisi hao walikua vibaka tu wa mtaani na sio majambazi, Kwanza hata kutumia silaha walikua wanatetemeka,


Lakini mtoto wake James Yuko wapi?


Alikua sasa anajiuliza maswali

Aliingia chumbani

Aliangalia laki 4 alizoweka mezani akazikosa, hivyo akanyanyua godoro na kutoa laki mbili ,

"We Mzee acha utani ,au unataka tukuue"

Alisema yule mwizi,

"Zimebaki hizo tu"

Mzee Mnyoka alisema sasa,

Wakati wanajaribu kubishana kwa ghafla kelele zilisikika nje,


"Wezi, majambazi, wezi!, Wauwawe! "

Kundi la watu walikuwa nje ya nyumba ya Mzee mnyoka ,


Ni wakati yule mwizi anashangaa ndipo Mzee Mnyoka akampiga kichwa akaanguka chini na panga likamtoka, Mzee Mnyoka aliliwahi panga Kisha akapiga kelele nje,

"Ingieni mtusaidie"

Sekunde kadhaa James aliingia ndani akiwa na kundi la vijana na kuwaweka chini ya ulinzi, Mzee Mnyoka nae alitoka na yule mwingine akiwa amemuweka chini ya ulinzi,


Kwa muda mfupi tayari mgambo wa Kijiji walifika na kuwachukua wale wezi,


Sasa umati wa watu ukahamia ofisi ya Kijiji,


"Nilienda kuangalia video kule kwa Isa , wakati nakaribia hapa nikaona watu wakiwa wameshika mapanga halafu wanaongea chini chini, Mimi kuona hivyo ndio nikarudi haraka kule kwenye Banda la video, na kwa bahati kulikua na muvi inaendelea watu walikua wengi ndio nikawaambia tumevamiwa, tukaja haraka"

James alitoa maelezo yake

"Afadhali tumepona inabidi kuwa makini na hizi pesa"
Mama Monica alisema,


***************

Oscar aliambaa ambaa na ukuta lakini hakuweza kusikia chochote alifanikiwa ,

Baada ya muda Frank alitoka akiwa amebeba box moja hivi akaliweka kwenye gari, Kisha akatoka akarudi na kuchukua box lingine, halafu akafungua mlango wa nyuma wa gari na kutoa mabox kadhaa na kuyaweka chini,

Yalikua Kama sita hivi,


Baadae aliyaingiza mabox hayo sebuleni kwa Tito,


Kisha baada ya dakika kadhaa wakarudi kwenye gari na kuondoka

Kwa mahesabu ya haraka haraka Ni kuwa Akina Frank walileta mzigo na kuchukua mzigo!

Oscar alishindwa kujua Aina ya mzigo ambao umeletwa na ule ambao umechukuliwa,


************

Kama alivyosema Kamanda, kijana Swalehe alifuguliwa kesi ya kujaribu kujiteka,


Polisi walidai Swalehe alijitengenezea mazingira hayo ili kujiletea umaarufu, kwamfano walisema Simu ya Swalehe ilikua "on" muda wote na ndio yeye aliwapigia Simu marafiki zake waende kumchukua,


Kitu pekee ambacho baadhi ya watu na polisi hawakujua

Baada ya Pablo kumueleza Tito mahali walipo ,

Tito alipiga tena Simu, kwa Pablo, alitaka kumueleza Jambo la kufanya, na ndipo Simu haikujibiwa, ndipo sasa Tito alituma vijana wake wengine ambao walifika na kukuta mwili wa Pablo na mwenzake huku wakimkosa Swalehe,


Ndipo sasa Tito aliwaambia watoe iyo miili na kwenda kuitupa mbali,

Hivyo ile hoja ya Swalehe kujiteka ilichukua nafasi,

Swalehe alipata mawakili ambao walijitokeza kumtetea na kesi yake ikaahirishwa na alinyimwa dhamana kutokana na kile kilichosemwa Ni kwa ajili ya usalama wake


*************

Oscar alikutana na Boss wake Allan kuangalia walipofikia na mambo yaliyohitajika,

"Sio mbaya, Kuna kila dalili Tito anaweza akawa ndio anahifadhi bidhaa pale, halafu yeye ndio anasafirisha, maana yeye Kama waziri Ni rahisi kwenda nje na mzigo bila kukaguliwa, hivyo Nina wasi wasi siku hiyo watakua walileta mzigo, wao wameondoka na mzigo gani, jibu la haraka haraka hiyo itakua pesa Oscar"

Alisema Mr Allan,..

Hakika huyu Mzee alikua na akili ya ziada katika kuelewa mambo, Oscar alimkubali Sana, na hata mafanikio yake mengi yalitokana na akili za huyu Mzee,

"Wewe endelea kujiatach kwa Tito mpaka ifikie akuamini kabisa, ili siku watakayokwenda kule mgodini uongozane nae, na ndio siku ya kumaliza hii biashara"

Alisema Mr Allan
Wakiagana,

*************************************"

"Sasa kaka Oscar unaona hii program! Unaweza kuhack, CCTV camera yoyote ukiwa ndani ya mita 100, halafu ukivaa na hizi earphones unasikia kabisa Hadi sauti!"

Joyce alikua anampa maelezo Oscar kuhusu programu hivi

"Aisee we Noma, kwahiyo hii inahack Camera tu?"

Oscar aliuliza huku sasa akiwa ametoa tabasamu,

"Yeah, "
Alisema Joyce,


Oscar sasa alificha furaha yake, ile program ingemsaidia kwenye mambo yake hapo baadae,


**********

BAADA YA WIKI MOJA

Mzee Mnyoka aliitwa tena kuhojiwa na kamati ya uchunguzi, Kisha kesi yake ikaahirishwa tena na zaidi Sana Mzee Mnyoka akazuiwa kutoka nje ya Kijiji mpaka kesi yake itakapoisha, Mzee Mnyoka alijiona Kama mkimbizi kwenye Kijiji chake mwenyewe,


Mwanae James alisharudi shule na hakika Mzee Mnyoka asingeweza kusahau msaada wa Oscar,

Maisha kidogo yalikua nafuu kwa Mzee Mnyoka, kwani pesa zile zilimsaidia kulipa madeni ya shuleni na kuendelea na maisha yake Kama kawaida,


**************

Siku hiyo
Oscar alitumwa na Tito kuchukua baadhi ya Nyaraka za kiofisi pale nyumbani kwake, Tito alikua anajiandaa kwenda Dodoma kwenye vikao vya Bunge,

Oscar alifika nyumbani na kwa bahati nzuri mke wa Tito hakuwepo,


Oscar alifika sebuleni na Kisha akachukua vifaa alivyoagizwa alitoka huku akihakikisha Camera zinamrekodi vizuri kila sehemu anazopita, Kisha akaingia kwenye gari na kutoa komputa mpakato ya Joyce,
Alifungua ile programu Kisha akabonyeza bonyeza batani,

Halafu akaiacha ikiwa wazi halafu akashuka kwenye gari, alitembea haraka na mlinzi hakuwa na Shida alijua kuna kitu amesahau,


Oscar sasa alipitiliza mpaka sebuleni halafu akaingia chumbani kwa Tito, alitoa funguo zake anazojua yeye Kisha akaingia ndani,


Alizunguusha mlango wa kabati Kisha akaona mlango mwingine ambao ulikuwa unafunguka kwa nywila,

Alitoa kidude fulani hivi Kama pafyumu akapuliza pale kwenye zile batani na sasa tarakimu nne zikawa zimekolea rangi ya buluu kuliko zingine, Oscar alijaribu kuotea tarakimu nne hizo lakini zikagoma,

Sasa Oscar aliumiza kichwa,


Baadae alijaribu kuwaza,

"Mwaka aliochaguliwa kuwa waziri huyu "

Alijisemea huku akiweka 2015 ,
Na hatimaye mlango ukafunguka,

Oscar aliingia ndani na hakuamini macho yake,

Chumba kilikua kimegawanywa Mara mbili,

Upande mmoja ulikua na mabox, na upande mwingine ulikua na shelfu zilizopangiliwa noti za kimarekani na noti za kitanzania,


"Aisee,"

Alijisemea
alipiga picha kadhaa Kisha akatoka na kufunga mlango
Na kutoka nje,

Alifika kwenye gari na kubonyeza bonyeza Tena ile laptop Kisha akaondoka ,


Alifika na kumkabidhi Tito ambaye aliondoka zake kuelekea Dodoma,


Oscar alipitiliza mpaka kwa Bosi wake na kumpa zile picha,


"Tito Ni mwanaharamu,amehamishia benki nyumbani kwake?"

Mr Allan alifoka sasa akizunguusha tai yake..
 
KESI YA MZEE MNYOKA 25

"Hawa viongozi wakijiji hawanijui, sasa nimewavumilia , inatosha, wananifanya Mimi mhalifu lakini sio mhalifu kweli, sasa ngoja niwafanyie tukio ambalo hawatalisahau"

Mzee Mnyoka aliwaza ,

Msomaji Kama utakumbuka tuliona kuwa zao la biashara ambalo wananchi wa Kinjeki walilitegemea Ni kahawa, na kahawa hii ilinunuliwa kwa mwaka Mara moja,

Utaratibu Ni kuwa baada ya mwananchi kupewa vielelezo vyote Basi kahawa yake ingepimwa Kisha angeandikishwa kwenye daftari la mwezi husika, na kupewa namba, kutokana na namba ya uandikishwaji wake kwenye daftari, halafu viongozi wa kamati ya kahawa wanajumlisha idadi ya kilo zote na kutuma ripoti wilayani ambapo malipo yalifanyika kwa awamu mbili,



Siku ya kulipwa pesa pale Kijijini ilikua Ni sherehe,


Serikali ya Kijiji ambapo ndipo palikua na Nyaraka za kahawa hapakuwa na ulinzi wowote palifungwa tu na kufuli,



Siku hiyo usiku Mzee Mnyoka alivizia kisha kwa tahadhari kubwa akalazimisha kufungua lile kufuli kwa ufunguo wake aliochonga, alienda mpaka kwenye kabati Kisha akatafuta daftari la kahawa la mwezi ule, alipohakikisha ndio lenyewe akalitia kwapani Kisha akatoka na kufunga mlango kwa kufuli Kama kawaida,


Ilikua imebaki siku moja ili kufanya uhakiki wa wale waliouza kahawa, halafu kesho kutwa ingekuwa awamu ya Kwanza ya malipo,

Kesho yake, wananchi walikusanyika Kama ilivyo ada na kutokana na Hali ya uchumi kila mmoja alitamani awe wa Kwanza kuitwa jina lake ili awepo kwenye malipo ya awamu ya Kwanza,


Walikaa nje zaidi ya masaa matatu bila mwenyekiti au mtendaji kutoka nje
Wananchi sasa wakaanza kukosa uvumilivu....



*************


Oscar alikua anaenda Mara Moja moja kwa Tito hivyo aliendelea na mipango yake taratibu, Joyce alikua ameenda Serengeti kwenye utalii wa ndani pamoja na rafiki yake wa uturuki aliyemtembelea, hivyo Tangu Oscar atumie komputa yake hakuwa amepata muda wa kuishika,



Sasa siku hii Oscar akiwa ametulia kwake akiweka mipango yake sawa ndipo sasa Joyce akatuma sms,

"Nimerudi uko wapi ?"

"Nipo kitaa, vipi una jipya mtoto mzuri?"

Oscar alijibu,


"Ninalo, njoo home"

Alijibu Joyce,

"Okay poa, nakuja jioni, "

Oscar alijibu Kisha akaendelea na mishe zake,

Jioni Oscar alienda Kwa Tito, alipenda kuwa karibu na Joyce kwani kwa muda alikua anasahau "Shida" zake na kujikuta a akuwa Kama mtu wa kawaida , Oscar kila Mara alipokua na Joyce alimkumbuka mdogo wake Dorcas,

Alifika ndani na kumkuta Joyce akimsubiri,


Tofauti na zile siku zote leo hii Joyce alikua amevaa nguo fupi laini ya kulalia,

Iliyoonyesha mpaka ndani ya mwili wake,


"Ooh Leo mbona umewahi kulala!?"
Oscar aliongea huku akijifanya hajaona chochote,


"Nilikua nakusubiri leo tulale wote"

Joyce alisema huku akionyesha Hana wasi wasi,

"We mtoto Leo umevuta bangi?"

Oscar alisema sasa akimtazama Joyce,


Joyce sasa alimsogelea Oscar pale kwenye sofa,


"Nakupenda Sana kaka Oscar naomba Sana uwe mpenzi wangu"

Joyce alisema huku machozi yakitaka kumtoka,

Oscar sasa alistuka na kuona Joyce alikua Hana utani,

Ni wakati anatafuta namna ya kujinasua sasa Joyce akaongea

"Ukinikatalia ujue namuambia baba, umeingia chumbani kwake na ushahidi ninao!"
Alisema Joyce sasa macho yakimtoka,


"Unashangaa? We si umeingia ndani? Na Tena sio hivyo tu najua mpaka kazi yako unayofanya, vyote namuambia!"

Alisema Joyce

"Ooh shit"

Oscar alijisemea huku akivuta pumzi,


******************************************"
Baada ya zogo kuanza sasa mwenyekiti alitoka akiwa na mtendaji pamoja na wajumbe kadhaa,


"Jamani Kuna Jambo limetokea, daftari la majina limepotea"

Alianza mwenyekiti,

"Aah haiwezekani! Haiwezekani!

Huo Ni ujanja mnataka kitudhulumu pesa zetu!"

Sasa kulikua hakuna masikilizano Tena, tayari kikao kilivunjika na watu wakaanza kuondoka!

Mwenyekiti alijaribu kuwatuliza wanakijiji lakini haikusaidia,

Viongozi wa kata walifika jioni kidogo akiwemo na mheshimiwa diwani Bwana Mapunda,

Alikaa na viongozi kwa masaa mawili lakini hakukuwa na namna isipokuwa daftari lipatikane!


Ilibidi sasa kuitisha mkutano wa dharula jioni ile ile Tena, kwenye ukumbi wa shule,

Ambapo kwa kauli moja wananchi walisema hawataki kusikia kitu zaidi ya daftari kurudi,


Hii ilichagizwa na ukweli kuwa wanakijiji wengi walikua wanapoteza risiti wanazopewa na hivyo "mkombozi" wao pekee ilikua Ni lile daftari,

Hivyo kwa mantiki iyo kikao kilivunjika rasmi hakukuwa na maelewano Tena,


Mzee Mnyoka alikua ametulia tuli kwenye kiti chake hakuongea Wala kujadili chochote,


Alisimama Kisha akaondoka zake kurudi nyumbani.

*************

"We mtoto mbona unaongea vitu vya ajabu hivyo"

Oscar sasa alimgeukia Joyce katika Hali ya kugutuka,


"Nishakuambia hivyo sasa Ni juu yako kuamua"
Joyce alisema huku akibetua midomo,

"Sikiliza Joyce, kwa sasa Ni mapema mno kujua kila kitu ila nitakuambia ukweli..


Mimi Ni mlinzi Binafsi wa baba yako nimetumwa na serikali, unajua nchi yetu ipo katika Vita ya kiuchumi na mawaziri wote wamewekewa walinzi Hawa, "

Oscar alianza kumueleza Joyce uongo uliofanana na ukweli,


"Mimi mwenyewe nakupenda Joyce ila umri wako, na kazi yangu hii hairuhusu, ila sasa naomba Kwanza uniambie umejuaje"

Oscar aliongea sasa akijifanya kuwa mpole,


"Sikiliza ulitumia ila app ya droneHack, sasa unapofuta footage bila kuclear data, halafu Mimi nikaongia nikarestore previous data naona kila kitu"

Alisema Joyce

"Okay, na umesema unajua kazi yangu Ni kazi ipi?"

Oscar aliuliza,

"Kile kidude ulichotumia kupata password za mlangoni kwa baba, niliingia mtandaoni na kuona kuwa vinatengenezwa kwa Oda maalumu kwa watu wa usalama, hususani wanaomlinda Raisi,

Lakini pia ulikuwepo kwenye msafara wa wanajeshi 6 walionda Israel mwaka 2001, kupata mafunzo, na ulivyorudi hukuajiriwa popote, kwahiyo Mimi nilihisi tu"

Alisema Joyce,

"Aisee Joyce usipende kujua mambo mengi utapata tabu Sana,

Kiukweli nipo hapa tu kwa ajili ya kumlinda baba yako na familia yake kwa ujumla wake"

Oscar alisema sasa kichwa kikimjaa..


"Kwahiyo unasemaje sasa"

Joyce aliuliza...


"We piga kitabu Kwanza ukirudi uturuki tutakuwa tunawasiliana ila sasa mambo haya usije kumuambia mtu, na ndio nitajua Kama umekua au bado"

Oscar alisema Kisha akamkumbatia Joyce,


"Usiwe na wasi Kama unanipenda Basi utanisaidia kuficha hizi Siri, narudia Tena usije kumuambia mtu"

Oscar alisema huku akimparaza paraza nywele zake


Alimuachia Kisha akarudi zake ndani kwenda kulala

**********

Mr Johnson aliendelea na shughuli zake uingereza Kama kawaida huku akipokea kamisheni zake Kama kawaida, sasa kampuni yake iliendelea kuwika Kama kawaida,

Na sasa alikua akiandaa timu yake kwa ajili ya kuja Tanzania, ili kuangalia mgodi wake,

Aliendelea kuwasiliana na Mr Bill na Tito Kama kawaida huku wakiweka mipango yao ,

Hata hivyo Oscar alikua anawafuatilia kwa karibu...
 
Nikae hapa au patanipa arosto bure[emoji848]
FB_IMG_1681054960376.jpg
 
KESI YA MZEE MNYOKA 26

Kama ilivyo kijijini habari zilikua zikisambaa haraka, lakini kadri zinavyosambaa ndivyo zilivyokua zinazidi kupotoshwa,


Hivyo wengine walikua wakitangaza kuwa tayari pesa za malipo zilishakuja na mtendaji na mwenyekiti wake wamezitafuna, na hivyo wameficha daftari kupoteza ushahidi,


Wengine walisema pesa bado hazijatafunwa ila mpango huo upo, ndio maana daftari limepotea ili mradi kila mmoja aliongea la kwake,


Wale waliokuwa na Visa vyao na uongozi walitumia nafasi hii vizuri kutoa maneno yao mabaya,



Kesho asubuhi wanakijiji walifurika nje ya ofisi ya Kijiji, Safari hii hata wale ambao Jana hawakuwepo leo walifika, hata wale ambao hawakua na biashara yoyote ya kahawa nao walifika,


Baada ya kufungua mkutano diwani aliwaeleza wazi wazi kuwa daftari lao lilikua limepotea na hivyo watakaohudumiwa kwa kuanzia Ni wale tu wenye risiti wakati wakifanya "namna" nyingine,


Diwani hakumaliza maelezo yake wanakijiji wakaanza kupiga makelele ya kusema mwenyekiti na Mtendaji watolewe kwenye nafasi zao,



"Hatumtaki mwenyekiti na Mtendaji!"
Wanakijiji walipiga kelele,

"Sasa huko mnafika mbali, ila mnajua wazi, hatuwezi kumtoa mtendaji wa Kijiji, ila mwenyekiti kwakua mmemchagua ninyi tunaweza kumbadilisha"

Diwani alisema na sasa diwani akashauri uchaguzi wa mwenyekiti ufanyike pale pale,


Kamati ya siasa waliingia ofisini kujadiliana kwa muda wa dakika kumi Kisha hatimaye wakatoka na jina la mwenyekiti wa muda,


"Haya kamati yenu ya siasa imewachagulia jina la muda la mwenyekiti na si mwingine Ni Bwana Ndugai Msoka Mnyoka !,"


Wanakijiji walilipuka kwa vifijo na nderemo na kumbeba Mzee Mnyoka juu juu kumpeleka pale mbele,


**************

Oscar alijitahidi kumkwepa Joyce huku akiamini wiki ijayo ataondoka zake kurudi chuoni uturuki hivyo alimuhesabia siku tu,

Jioni hiyo alikutana na Bosi wake mr Allan kwa ajili ya kupewa sasa misheni nzima,

"Kwahiyo tunatarajia Tito akitoka Dodoma wiki hii, aje Dar, akishafika Dar Kuna uwezekano mkubwa akakutana na majimbi, na lazima tujue wataongea nini, maana wanaweza kupanga siku ya kwenda kule au hata siku ya kumpokea Mr Johnson, lakini vile vile Hawa ndio watatupa muelekeo,
Au wewe unafikiri nini Oscar
Alisema Mr Allan,


"Boss, Mimi nahisi hata mzigo wa urenium upo pale kwa Tito, Kama umesafirishwa Basi Ni kidogo Sana, nahisi Jambo moja, kuwa mipango yao Ni kukusanya mzigo wa kutosha halafu Mr Johnson akija na naamini anaweza kuja na ndege Binafsi, Basi atarudi na mzigo, kwa maana hiyo Johnson anamtumia pesa Majimbi, Kama msaada wa Kanisa,..

Halafu Majimbi anampa Tito Pesa,..

Halafu Mr Bill analeta mzigo kutokea kule mgodini, Tito anawapa pesa za posho na pesa za kulipa vibarua na wafanyakazi kule..."

Oscar alitoa maoni yake,

"Yeah ipo hivyo, sasa kwa sasa suala la Msingi Ni kujua huyu Tito na Majimbi watakutana lini na wataongea nini, naamini kesho kutwa Tito anamaliza vikao vya Bunge, namjua hawezi kukaa Dodoma wiki mbili yule"

Alisema Mr Allan..

***************************************

Mzee Mnyoka sasa alifika pale mbele,

Alimtazama mwenyekiti aliyefururushwa kwa jicho la kumuambia "utakoma"

Mzee Mnyoka hakuongea maneno mengi alisema atashirikiana na wajumbe wa kamati kuhakikisha kila mmoja analipwa stahiki zake,


"Naamini tutashirikiana kabisa kuhakikisha mambo yanakaa sawa, ila naomba tusaidiane kwa yoyote atakayepata dondoo au kujua daftari lilipo tunaomba asaidie,

Binafsi nitatumia kila ninavyoweza kupata daftari Hilo, "
Mzee Mnyoka aliongea huku akipigiwa makofi na wanakijiji


***********

Siku hiyo ilikua Mapumziko Bungeni kutokana na Bonanza la michezo la wabunge kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kuchangia damu,


Tito akiwa anakaribia uwanjani ndipo waziri mwenzake wa miundo mbinu Bwana Anthony shija akamtumia sms
"Tito tuonane"
"Okay poa Broo"

Tito alijibu,

Hawakuwa na mazoea Sana au tuseme hawakua marafiki Sana, inasadikika wawili hao walishakuwa katika mahusiano na mwigizaji wa filamu Jesca,


Hivyo Tito alistuka Sana na ujumbe huu wa Shija,

Baada ya Bonanza Tito alimtaarifu Shija Kisha wakakutana nje ya mgahawa wa Royal Palm

"Nina Jambo moja tu Bwana Tito"

Alianza Bwana Shija,

"You can fool some people some time but you can not fool all the people all the time"

Alisema Shija,
"What do you mean"

Tito alistuka,

"Unachofanya kinjeki, kule kwenye Mgodi usidhani kila mtu hajui"
Alisema Shija huku akipiga funda moja la bia yake kwenye glasi,


"Kitu gani, kinachofanyika? Najua uliitaka Sana hii wizara, na hata nilipotoka na Jesca uliumia Sana! Kwanini lakini unapenda kunifuatilia?"..



Tito alisema huku hasira zikianza kumpanda

"Huyu Ngedere katoka wapi kwenye shamba langu la mahindi?"

Tito aliwaza..

"Sikiliza Bwana Mdogo Tito,


Mimi Niko kwenye system miaka minne zaidi yako, najua pale Kuna urenium na wewe na mwenzako Johnson mnapiga hela nyingi, sasa sikiliza,

Nataka kila mwezi unipe mgao wa million 500 , la sivyo unajua mziki wangu"

Alisema Bwana Shija huku akisimama..

"Loh, huyu bwege kajuaje?"


Tito aliwaza huku akitoa Simu yake ...
 
Back
Top Bottom