Hadithi: Kesi ya Mzee Mnyoka

Hadithi: Kesi ya Mzee Mnyoka

KESI YA MZEE MNYOKA 35

Bwana Johnson aliandaliwa Gari maalum ambalo angepanda pamoja na Tito na walinzi wake wawili, huku Gari nyingine ikiwa na walinzi waliobaki pamoja na Oscar
Na Kisha wageni wengine walifuata kwenye magari mengine, kwa hivyo ilitengeneza msururu mdogo hivi uliokua na magari Kama nane ,


Kutoka uwanja wa Ndege , msururu ulinyoosha Kati Kati ya mji ambapo kulikua na hotel ya Twiga ambapo ndipo Mr Johnson pamoja na watu wake walikua wametafutiwa

Oscar alitulia nyuma kabisa akiwa na walinzi Hawa kadhaa ambao wote hawakujishughulisha nae kila mmoja alikua na hamsini zake, Kuna wakati Gari ilipunguza mwendo kidogo au kusimama kidogo Basi wale walinzi wangehamaki na kuweka silaha zao, kwa hivi wakati mwingine Oscar alitamani kucheka,

Lakini yeye alifahamu kuwa kanuni ya kwanza ya Mambo ya ulinzi Ni kutilia Shaka kila kitu,

Waliendelea na Safari na kufika Hoteli ya Twiga salama.

Tito alimsindikiza mgeni wake mpaka kwenye chumba chake Kisha akarudi nyumbani kwake kupumzika.


************

Bwana Bill nae alikua anapanga mipango yake, akili yake ilimuambia kuwa baada ya kazi hiyo nzito Kwisha anaweza akasahaulika, lakini si kusahaulika tu Bali hata kupotezwa kabisa,

Na hivyo alihakikisha kazi hii anaifanya kwa uwezo mkubwa, asingeweza kutoa jasho lake kwa miaka yote Ile halafu faida wapate wengine,

Sasa mkakati wake uliiva kichwani mwake,

Bwana Bill au Kama walivyokuwa wanamuita "Carlos" wakaimfananisha na jambazi hatari na mlanguzi wa madawa ya kulevya,

Unaweza kusema tofauti yao ilikua rangi tu!

Lakini akili zao zilikua karibu kabisa kufanana,


Mkakati wake aliokua ameundaa aliamini lazima utaawacha mabosi zake Hawa mikono kichwani,

Sasa alikumbuka zoezi ambalo aliambiwa alifanye wiki moja iliyopita alipokutana na Tito,

Zoezi lenyewe ilikuwa kuandaa magari mawili yanayofanana kwa ajili ya kuondoka na mzigo nyumbani kwa Tito kupeleka uwanja wa Ndege,

Ndipo sasa yeye akandaa Magari matatu, huku moja akilificha mahali anapojua yeye,

Kisha magari mawili akayaleta mpaka mgodini Kinjeki kusubiri siku ya tukio,


Tayari mabox ambayo yalitakiwa kupeleka mzigo mpaka nyumbani kwa Tito yalishaandaliwa,

Mzigo huu ulitakiwa kuondoka na Bwana Bill siku chache zijazo mpaka nyumbani kwa Tito ambapo angeunganisha na mizigo mingine Kisha kupakia kwenye ndege,

Kwanza kabisa Bwana Johnson alifanya mazungumzo Rasmi na waziri wa nishati Bwana Tito,

Maongezi haya yalikua mubashara kabisa kupitia vyombo vya habari na Tito alisema kwa niaba ya serikali kuwa baada ya Bwana Johnson kumaliza ziara yake wataalamu wake watatoa taarifa Rasmi kuhusu kupatikana kwa urenium ama la,

Waziri Tito alisisitiza kuwa serikali iko bega kwa bega na kampuni hiyo ili kufanikisha mipango yote kwa ajili ya manufaa ya taifa,


"Kwahiyo Kama nilivyosema, mradi huu utakuwa na mafanikio makubwa endapo kiasi urenium kidogo kitagunduliwa, Dunia inabadilika siku hizi tutapata nishati ya uhakika ya umeme, tutapata mapato , tutapata wawekezaji wengi na mambo mengine kwahiyo Mimi niseme watanzania tuwe watu wa kuvuta subra Mambo mengi mazuri yanakuja"


Alimaliza hotuba yake Bwana Tito huku akipeana mikono na Bwana Johnson kwa ajili ya kumaliza kipindi.

***************


Kati Kati ya jiji la Dar es salaam
Oscar alikua na rafiki yake George wakimalizia kupanga mipango yao ,

Walikubaliana George atangulie kijijini akaandae mazingira ili kwamba Oscar akienda na Tito kazi iwe nyepesi,

Alimpa maelezo yote muhimu na watu wa kufanya nao kazi kwa siku zote atakazokuwa pale Kijijini,


"Tumalize hii inshu Kaka na Bila Shaka baada ya hapa sasa naweza kutulia angalau niangalie maisha mengine"

Alisema Oscar

"Kaka hujawahi kusema hivyo kabisa, tumefanya kazi ngumu, lakini daima hujawahi kutamani kupumzika!"
Alisema George


"Unajua nimewaza Sana na sisi Ni Binadamu pia lazima tuishi Kama wengine , we nenda naamini tutamaliza salama"

Alisema Oscar wakati huo alitoa Simu yake baada ya kutingishika kuashiria ujumbe mfupi uliingia,

Aliifungua na ilikua Ni ujumbe kupitia WhatsApp

"Kesho nakuja bongo"

Ujumbe huo ukitoka kwa Joyce,


Sasa kwa Mara ya kwanza Oscar akahisi kukosa amani,

Bila kujielewa akajikuta anaanza kumfikiria Joyce,

Aliwaza sekunde kadhaa Kisha akamjibu,


"Kwanini? Bado hujamaliza hata mwezi?"


"It's an emergency, we will talk"
Alijibu Joyce akimaanisha Ni dharula, wataongea akija,


"Huyu mtoto anakuja kufanya nini?"

Aliwaza Oscar akiingia kwenye Gari lake na kurudi nyumbani kwa Tito.



*******************


Mzee Mnyoka akiwa ofisini kwake , sasa wiki hii alipokea wageni wa kutosha, kuanzia waandishi wa redio, magazeti na hata wageni mbali mbali wa serikali,


Hivyo wakati anaelezwa Kuna mgeni mwingine yupo nyumbani kwake anamsubiri, Mzee Mnyoka hakuwa na haraka ya kurudi nyumbani,

Hata hivyo alishapokea wageni wengi nyumbani na ofisini, na tayari cheo Cha mwenyekiti kilianza kumkaa vizuri,


Mzee Mnyoka alirudi nyumbani kwake na kumkuta mgeni wake,

Tofauti na wageni wote mgeni huyu aliomba sehemu ya kujihifadhi kwa muda wa siku tano,

Yeye alidai alitoka shirika lisilo la kiserikali na alikua anafanya shughuli kwa kujitolea na alikua mafunzoni na kazi yake ya kwanza ilikuwa Ni kuripoti matukio hayo ya ziara ya Bwana Johnson na hivyo anaomba msaada wa Kijiji kwa mwenyekiti,

Mzee Mnyoka alitoka kuongea na mkewe Kisha wakakubaliana wampe chumba Cha James kwani hata hivyo siku tano zisingekuwa nyingi.....
Mzee Mnyoka anaweza kujikuta anaingia tena matatizoni kama atamkaribisha huyo mgeni
 
KESI YA MZEE MNYOKA 36

Mzee Mnyoka alitoka chumbani kuelekea sebuleni ambapo mgeni wake alikuwepo...

"Kumbe ulisema unaitwa Bwana Nani vile, "

Mzee Mnyoka alianza...

"George , George Paul Mzee wangu"
Alisema George huku akitoa mkono Tena kumpa Mzee Mnyoka....

"Sawa sasa Kuna chumba Cha mdogo wako hapa bila Shaka utavumilia mazingira yake , si unajua Tena vijana"

Alisema Mzee Mnyoka akichukua begi la George na kutoka nae kuelekea chumbani kwa James,

Alifungua Kisha akamkabidhi ufunguo ...


George alitoa begi lake na kuunganisha baadhi ya vifaa vyake muhimu Kisha vingine akavificha sehemu sehemu mpaka usiku alipoitwa kula chakula Cha jioni alirudi kuendelea na mipango yake kwa ajili ya kesho...


*************

Oscar alikuwa sasa Yuko bize popote alipokuwapo Tito Oscar angekuwa pembeni yake,


Baada ya kuwa na ratiba ya waandishi wa habari Tito alipanga kufanya maandalizi ya kuelekea Mgodini ambapo shughuli kubwa zingefanyika kule ikiwemo makabidhiano....

Waliamini kule kungekuwa na usalama wa kutosha,


Siku hii ya leo Bwana Johnson alialikwa kutembelea makao makuu ya Kanisa la uzima wa milele kwa askofu Majimbi


Askofu Majimbi alimpokea mgeni wake huyo na kusema Ni rafiki wa Kanisa lao na amekuwa hata akifadhili baadhi ya huduma za pale kanisani ikiwemo ujenze wa hosteli kwenye chuo Chao Cha Kanisa pamoja na mradi wa maji...


Tofauti na Tito , Askofu Majimbi alishamtembelea zaidi ya Mara tatu Bwana Johnson akiwa uingereza hivyo walifahamiana vyema ..


Baada ya maongezi ya kawaida walihamia "ofisini" ambapo walifanya mazungumzo yao kuhusu biashara zao....

Kikubwa walijadiliana namna ya kutoa mzigo salama nchini Tanzania na kuondoka nao bila kuathiri uhusiano wa nchi hizi mbili...

Majimbi alimuhakikishia kuwa kupitia Tito Mambo yote yatakaa vizuri ..


***************

Bwana Allan nae hakuwa nyuma aliweka kikosi chake Cha watu kumi ili kusaidiana na Oscar endapo Mambo yatakwama

Hapo nyuma alikua na mjadala mzito pamoja na wenzake kuhusu kumuingiza mtu mwingine katika oparesheni hii, wenzake walisema kuwa mtu huyo asingefaa kutokana na umri wake, lakini pia hata mahusiano yake na mtuhumiwa...

Hata hivyo Bwana Allan alisema mtu huyo bado anaweza kufaa Ni Bora wamtumie ashindwe kuliko kuacha kabisa kumtumia,

Ndipo sasa wakaona wampe taarifa Mhusika mwenyewe....


Jambo la ajabu Ni kuwa mpelelezi wao huyo alisema Yuko tayari kufanya kazi hiyo kwa asilimia 100 na yupo tayari kurudi nchini....


Ndipo sasa akafanyiwa mipango yote ya usafiri kurudi nyumbani Tanzania..


Ni suala Hili lilimfanya Bwana Allan kujaribu kufanya uchunguzi wake kwanini binti yule alikubali kufanya kazi Ile kwa urahisi mkubwa

Jioni hii akiwa ofisini kwake alikua akipitia picha mbali mbali kwenye komputa yake,


Ndipo sasa alijikuta akirudia rudia kuangalia hii picha..


Alitabasamu Kisha akatoa Simu yake ya kazi na kumtafuta Oscar....


***************************

George alitoka asubuhi na mapema alifika mpaka mgodini Kinjeki ambapo alijitambulisha Kama mwandishi mwanafunzi kutoka chuo Cha uandishi wa habari Arusha ..


Baada ya kutoa vitambulisho vyake aliruhusiwa kupita na kuonyeshwa Mambo mbali mbali ya mgodini hapo, ..

Alitoa kamera na notebook yake Kisha akachukua maelezo kidogo na kuungana na waandishi wengine waliokua wanaendelea kuingia mgodini...

Ni tukio kubwa la kihistoria nchini Tanzania na hivyo kwa muda mfupi habari za Kinjeki zilikua zinaandikwa Sana....

**************


Baada ya ratiba zote kukamilika sasa Bwana Johnson alikua amemaliza mizunguuko yote na sasa Safari ya kwenda Kinjeki iliwadia .

****************

Bwana Allan alionana na mpelelezi wake huyo aliyewasili siku hiyo kwa ajili ya kuonana nae ...


Bwana Allan alitaka kumuona ili ajihakishe Kama kweli Ni yeye aliamua mwenyewe kuwemo kwenye misheni hii,


Bwana Allan alikumbuka sasa jinsi alivyomshawishi msichana yule alivyokuwa mdogo kabisa pale Saint Rock international School Kenya, mwaka 98 wakati ambapo Bwana Allan alipewa jukumu la kutafuta watoto wa viongozi ambao wangekuwa tayari kuwa wapelelezi baadae, kwa faida ya nchi,


Siku hiyo akiwa Kenya alikua amemfuata mtoto wa waziri mkuu mstaafu ambaye alikua shuleni hapo,


Na baada ya kufika shuleni, na kuuliza habari zake aliambiwa tayari alishahamishwa siku mbili zilizopita kwenda uingereza,

Kwakua lilikuwa Ni Jambo la Siri hakukua na sababu ya kulaumu mtu na ndipo wakati anataka kutoka hapo shuleni akatambulishwa mtoto wa waziri Tito,

Joyce ambaye alikua na miaka 10 wakati huo nae akisoma shuleni hapo,


Ni wakati anaongea nae na kumuuliza masomo anayopenda na kupitia ripoti zake ndipo sasa Bwana Allan akaanza kumuhusudu binti huyo aliyekuwa mahiri katika masomo ya tehama

Na ndipo alifanikiwa kumueleza taratibu na hatimaye alipofikisha miaka 15 serikali ikamchukua moja kwa moja!

Na ndipo sasa kila Mara akawa anapata udhamini wa masomo nje ya nchi , baba yake Mzee Tito kutokana na kuwa mtu wa shughuli nyingi alijua tu mwanae yupo masomoni nje ya nchi akisomea Mambo ya komputa mengine alijua serikali inagharamia,


Bwana Allan alikuwa anawaza yote haya akiegesha Gari yake pembeni mwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere...


Ni wakati muafaka ndipo alipomuona mtu wake akitoka alimpungia mkono na Kisha akamkumbatia..


"Oh my daughter"

Alisema huku akimpokea begi kuelekea kwenye Gari...
 
KESI YA MZEE MNYOKA 37

"So how was your studies"

Alianza Bwana Allan,

"Wonderful, it's stage Four, final now, I know I can make it"

Aliongea Joyce huku akionyesha huzuni kiasi,

"Yaa najua utamaliza vizuri, najua uwezo wako, you see, doing great jobs to your country makes you great and unforgettable too"


Alisema Bwana Allan,

"Task yako Ni kuongoza camera zote , na mifumo yote ya ulinzi, and giving location, and way out, I hope Ni simple job, utakaa ndani tu ,no physical battle hahahaha"

Alisema Mr Allan akimpa majukumu yake hayo Joyce ambaye alikua mtulivu tu, akitingisha kichwa,

"Kapumzike , but take care, no one knows, L2 wako Ni George, na L1 Ni Oscar, vifaa utapata kesho"


Aliongea sasa akiondoa Gari pale airport ,alimtaja Oscar makusudi Kisha akaongeza sentensi nyingine haraka haraka kana kwamba Ile "Oscar" ilitoka bahati mbaya ...

Na sasa alipata jibu kuwa Hawa wawili walikua kwenye mahaba, Kama sio mahusiano,


***************

Bwana Bill aliwaita watu wake na kujipanga kwa ajili ya kupokea ugeni , aliwaita vijana wake wa kazi Frank na Jacob akiwapa nasaha kuhusu ugeni mzito uliokuwa unatarajiwa kuwasili kuanzia kesho jioni,

"Hii Ni dili yetu ya mwisho, nilikua nataka kuwaficha lakini sijaona sababu ya kufanya hivyo,..

Tumepambana siku zote na sasa mzigo umetoka,

Kama kawaida watakuja hao vitumbo hapa kesho na watafanya mikutano miwili,

Mkutano wa kwanza Ni kule nje, mkutano wa kuangalia angalia Mambo na Kisha watasoma ripoti yao feki, halafu watasema ujinga wao hapo, halafu mkutano utaisha na wataingia vyumba vya nje huko na waandishi wao,


Halafu baadae watamaliza na kuaga na kutoka, kwahiyo waandishi wa habari na wadudu wote wanatakiwa nao waondoke,


Halafu sasa usiku watakuja tena kufanya mkutano wao vyumba vile vya chini pamoja kuingia kule maabara,

Sasa huu mkutano wa kwanza hauna Shida, lakini mkutano wa pili huu wa usiku ndio wa muhimu,


Kwanza hakuna mjusi yoyote asiyehusika kuingia,

Hata hao wenyewe Akina Tito wataingia na walinzi wao mmoja mmoja tu, hatutaki ujinga Kama ule wa kuvamiwa na boya mmoja,...

Baada ya huo mkutano wao,

Tutaondoka nao kwa ajili ya kwenda kupakia mzigo dar kwenye Yale magari mawili , ambayo moja utaendesha wewe na jingine ataendesha huyu,


Kuna swali mpaka hapo?


Aliuliza Bwana Bill akiwaangalia watu wake...


**************

George sasa alikuwa tayari chumba Cha mkutano ambapo kazi yake kubwa ilikua kuangalia mazingira na mahali pa kupita baadae wakati wa kazi, alipiga jicho camera mbali mbali za ulinzi pamoja na Mambo mengine ya Msingi Kama mpelelezi,


Alitegemea kupokea Timu nyingine ambayo wangekuja na Gari maalum lenye vifaa vyote ambavyo vingetumika kuwaongoza

Hakika sasa walikua wanatamani kazi ianze muda wowote ..

**************************

Msafara wa Bwana Johnson pamoja na viongozi wengine wa serikali akiwemo waziri Tito sasa ulikua unakaribia kabisa Kinjeki kulikua na Gari nyingi za watu Binafsi, serikali na waandishi wa habari,


Katika msafara huu pia kulikua na Gari lililofanana na Gari ya kubebea wagonjwa likiwa na alama ya Msalaba mwekundu, pembeni,


Ndani ya Gari hii Joyce alikua pamoja na wenzake wanne yaani watatu walikua wamekaa sehemu ya nyuma na Dereva akiwa mbele, walikua sambamba kabisa na Gari la mheshimiwa waziri ,


Ndani ya Gari hili walikua na vifaa vyote vya mawasiliano kwa ajili ya kuwasaidia George na Oscar huku wawili Kati yao wakiwa tayari kwa mapambano pia Kama italazimika,


Kama wapelelezi waliendelea kupiga hadithi za hapa na pale mpaka pale walipofika Kinjeki sasa walifunga mitambo yao, na Kisha sasa wakajaribu kuwasiliana na George,


"L2, L2! Tupo karibu yako tafadhali hakiki, ova"

Alisema Joyce kupita kifaa chake kidogo alichokua ameweka kwenye Shati,


"Control, L2 hakiki!"

Alisema George nae akiwa anajiweka sawa pale kwenye kiti, alitabasamu huku akifurahia kuona wenzake wakiwa wamefika kwa wakati,

Aliwasikia vyema kupitia kidude kidogo alichokiweka masikioni mwake...

Kwa haraka unadhani kuhisi George alikua ameweka Vispika vidogo vya masikioni kwa ajili ya kusikiliza muziki...


Msafara Sasa uliingia kijijini Kinjeki mgodini na ziara Rasmi ikaanza,


Oscar alikua karibu na walinzi wa Bwana Johnson huku kila mmoja akiwa bize na kumlinda mtu wake,

Oscar alijaribu kuangaza macho huko na huko na hatimaye alimuona George akiwa amening'iniza kamera yake huku akiwa bize kuchukua matukio,

Sasa Oscar alitamani kucheka lakini alijikaza

Mkutano ulikwenda vizuri tu na hotuba ikaandaliwa Kama ilivyopangwa.


"Kwahiyo serikali itaendelea kushirikiana na kampuni ya ureFact kwa mkataba mwingine wa miaka 7 na tunaamini Kama Mambo yakienda vizuri, serikali Hii itaanza kunufaika na mradi huu ndani ya muda mfupi ujao"

Alihitimisha Tito..

Waandishi waliruhusiwa kuondoka na sasa Bwana Tito na mgeni wake walihamia ndani kwa ajili ya kutembea tembea kuangalia maeneo ya ule mgodi.. Kisha wakapanda Magari na kurudi mjini huku waandishi wakishuhudia!
Waandishi walianza kuondoka maeneo hayo huku kila mmoja akiamini kazi imeisha,.
Ni wale watu wanne na wengine wawili ambao kwao kazi ndio kwanza ilikua inaanza usiku ule,
Baada ya kuona kila mmoja ameondoka hatimaye Ile "ambulance" nayo ilijikongoja taratibu kutoka kwenye maeneo hayo ya mgodi kwa ajili ya kazi nyingine kubwa usiku huo...
 
KESI YA MZEE MNYOKA 38 (episodes hizi za mwisho ni kwa udhamini wa ndugu Gily )

SAA 4: 00 MGODINI KINJEKI
Tayari Waziri Tito na rafiki yake Bwana Johnson walikua ndani ya mgodi huku wakipita maabara na kukagua mali zao
“umefanya vizuri sana Bwana Tito hakika tunakwenda kuitawala dunia na nataka nikuambie kitu ndugu yangu.. wewe ni Raisi ajaye wa nchi hii!” alisema bwana Johnson huku akimhakikishia rafiki yake huyo kuwa atafanya awezavyo ili Tito awe Raisi , Tito aliduwaa huku akimkonyeza Oscar kwa jicho la kumuambia “unaona! Nilikuambia”

Hakika kulikua na mzigo wa kutosha na zoezi liliobaki likikua kupanga vizuri mizigo hiyo ili kuunganisha na mzigo wa nyumbani kwa Tito kisha kuupakia kwenye ndege maalum aliyokuja nayo Bwana Johnson tayari kupeleka Ulaya

Akili ya Oscar iliwaza huko na huko na tayari alishaona jambo la kufanya..

Mpango wa kwanza ilikua kuzuia mzigo huo usitoke nje ya mgodi na kuwakamata Bwana Tito na genge lake bila kutumia nguvu nyingi, lakini pia bila kumwaga damu ikibidi , mpango huu ulikua namba moja kutoka kwa Bwana Allan kwani alitaka kuona Tito akikamatwa na ngozi moja kwa moja,
Mpango wa pili ulikuwa kumuacha Tito amalize mambo yake na kisha akamatwe njiani kwenda uwanja wa ndege ambapo msafara wake ungeavamiwa na kisha yeye na wenzake kutiwa mbaroni, hata hivyo Oscar alipinga mpango huu akidai Tito ni mjanja anaweza kufanya jambo asiende uwanja wa ndege au hata kuwageuka
Mpango wa tatu ilikuwa kumvamia Tito nyumbani kwake wakati akiwa na mzigo wake kisha Johnson akamatwe akiwa hotelini hata hivyo mpango huu ulipingwa vikali kwani tayari ingezuia matatizo ya kidiplomasia endapo Bwana Johnson angekanusha kuwa hajui chochote na hivyo zigo la lawama lingeangukia serikali ya Tanzania hivyo namna bora ilikuwa kuwakamata Tito na genge lake wakiwa mzigoni!


George alirudi kwenye ile ambulance na kisha wakafanya mipangilio mbali mbali kwenye komputa zao huku kukiwa na screen kubwa mbele yao walisogeza ambulance yao karibu kabisa na mgodi na kisha wakaanza kusoma mazingira ya jengo kupitia kamera mbali mbali mbali

“ shit, ecyripted!’ alitoa sauti ya kukasirika Tom
“ nini kwani unashindwa?” aliuliza George nae akisogea karibu
“washenzi wameweka mfumo namba 9 plus ambao hatuna namna ya kuingilia camera za ndani, hapa tunaweza kuona nje tu!” alisema Tom

“ so tunafanyaje? Kwani hamkujua litatokea hili? Acheni ujinga Oscar yuko ndani , Oscar yuko ndani !!, do something!” George alifoka

‘ Tom, nipishe,” aliongea Joyce akivua vile vifaa vyake masikioni kisha akakaa pale kwenye komputa,
Alibonyeza komputa kwa dakika kadhaa huku maandishi mengi yakijitokeza katika ile screeni kubwa mbele yao hatimaye Joyce alipiga kelele za furaha..
“bingoooo!”

Wote walikodoa macho mbele kwenye Tv kubwa kisha wakaanza kufuatilia chumba kimoja baada ya kingine!

Kule ndani zoezi lilikuwa linakaribia mwisho kabisa kwani maboksi mengi tayari yalipangwa vizuri kabisa na ilibaki kuyatoa nje tu kuyapakia kwenye gari..
Tito na wenzake sasa walirudi kwenye chumba cha mikutano kwa ajili ya kuhitimisha mambo machache

“kuna kazi nataka unifanyie “
Tito alimnong’oneza Oscar
“ndio boss!”
“kuna mende watatu nataka uwaue tukitoka hapa tu!” Tito alimwambia Oscar huku akitabasamu kana kwamba anamaanisha mende kweli..

“wako wapi Bos” alisema Oscar huku akisogea pembeni

“watakuwa hapa….” Tito alikatishwa na sauti ya Bili aliyekuwa anaingia kwa kasi pale chumba cha mikutano akihema

“ kuna watu wanatufuatilia mkuu,’’ alisema Bili huku akitoka na Tito nae alitoka nje akifuatiwa na Oscar ambaye alishahisi akina George wameshtukiwa..
“wanafanyaje kazi kiboya hivi?” Oscar alijisemea akipiga hatua kuelekea chumba cha mawasiliano

“kuna upuuzi gani hapa unafanyika?” tito alifoka

“angalia hapa Bosi inaamaanisha kuna watu wameingilia Camera zetu na wanaweza kutazama kinachoendelea hapa!” alisema jamaa mmoja aliykuwa amekaa kwenye kiti cha kuzunguuka..

“ sio kutazama tu mpaka kurekodiwa mnarekodiwa mbwa nyiee!” alisema Tito kwa ukali..
“ Yaani wewe mpuuzi badala uwe nje sasa hivi kuwakamata hao wahuni uko hapa unanitazama?” alisema Tito akimgeukia Bili ambaye alichukua bunduki yake na kuwachukua vijana wake kukimbilia nje
********************"
Ni wakati wanaendelea kupekua pekua kamera za mle ndani ndipo wakafanikiwa kuwaona akina Oscar na Tito pamoja na genge lao lote, pamoja na kwamba hawakusikia sauti lakini wote walitambua kuwa wamegundulika na kama walivyotarajia basi waliona akina Bili wakitoka nje kwa haraka wakiwa na Bunduki..
‘haya show inaanza jamani’ alisema George akivaa kikoti chake kinachozuia risasi kisha akachukua bunduki yake..

“ mimi na Tom tutawazuia kwa nje, na wewe na mwenzako mtakuwa mnaendelea kufuatilia na kutuelekeza sawa?’ alisema George akimuelekeza Joyce na hatimaye yeye na Tom wakaruka nje ya gari na kusogelea vichaka kuelekea mgodini..

Bili alitoka nje kabisa pamoja vijana wake sita huku mmojawapo akiwa na kifaa kidogo kufuatilia ni wapi walitakiwa kwenda, walikua wakikimbia kwa kasi sana

Gerorge na Tom walijibanza kama mita 80 hivi kutoka ilipokuwepo gari na sasa waliona wazi wazi akina bili wakija kwa kasi kuelekea pale walipo,

“tunawamaliza hawa” alisema Tom
Waliweka bunduki zao sawa kwa ajili ya kuanza kushambulia, lakini kinyume na matarajio yao waliona akina Bili wakilala chini na kuanza kutambaa kwa tumbo kama nyoka kuelekea ilipo Ambulance


Oscar hakuwa akiwaza sana huko nje akili yake ilikua inawaza haraka namna ya kupambana na walinzi wa Johnson pale ndani, ama kuwazimisha ili awaweke chini ya ulinzi
Wakati akitafakari jambo la kufanya Tito alipiga simu kuita chopa, hakutaka mgeni wake ajue kinachoendelea hivyo alitaka kumtoa haraka haraka pale mgodini kabla mambo hayajaharibika..

“ooh shit” Oscar alijisemea aliwakodolea macho walinzi wa Bwana Johnson ambao hakuna hata moja aliyeonyesha kucheka wala kununa

Walitoka na kuingia chumba kingine ambapo Tito alimueleza Johnson kuwa itabidi arejee Dar kwa chopa ili wafanye haraka kuondoka ikibidi usiku huo huo..

“is there any problem mr Minister?’ alimuuliza kama kulikua na shida yoyote, Tito alidai ni kwasababu za kiusalama tu lakini hakuna chochote,
**************************
Kule nje mapambano yalikua yanaanza tom aliamua kushambulia ili wasikaribie kabisa ile ambulance na ndipo akina Bili wakajibu mashambulizi

“wazuge niwafuate” alisema George akikimbia kwa kasi kuwazunguuka pale walipokuwepo wakati wao waliendelea kumsogelea Tom pale alipokuwepo, Tom alifanikiwa kuwaua wawili kati yao, wakati George anakaribia kuwamaliza ghafla taa za gari zilimulika na kwa spidi kali ikatokea gari ndogo Bili na wenzake watatu wakakimbilia huko na kuingia kwenye gari na kutokomea!

“hii maana yake nini” alisema George akimsogelea Tom wakati akikagua zile maiti mbili pale chini,
 
KESI YA MZEE MNYOKA 39
(episode hizi za mwisho ni kwa udhamini wa Gily Asante brother)

Hakukua na muda wa kupoteza na hivyo Tito akaamuru mizigo ianze kutolewa nje kwa ajili ya kupakiwa kwenye yale magari mawili,
Tito alitaka kumaliza mambo yake bila kufanya kosa lolote lile na kwa mahesabu yake usiku ule ulikua wa muhimu sana kuliko usiku wowote katika maisha yake,

Hata hivyo Tito alishangaa kuona vijana wake akina Bili hawajamletea mrejesho wowote ule kutoka huko nje..

“twende Oscar!” alisema Tito akitoka na kumuacha Johnson na walinzi wake

Walitoka na kurudi kwenye chumba cha mawasiliano hawakukuta mtu yoyote hali ambayo ilimtisha sana Tito ni wakati wanatoka ndipo wakajikuta wanatazamana uso kwa uso na bunduki za watu wawili…

“uko chini ya ulinzi mheshimiwa waziri!” alisema George huku akimnyooshea bunduki yake Tito ambaye alimkodolea macho Oscar yalioashiria afanye kitu..

“tupe bastola yako yako Ocar’ Alisema Tom huku akimsogelea Oscar

Oscar kwa upole alitoa bastola yake na kunyoosha mikono juu, Tito hakuamini macho yake
“Magimbi nitakuua!” alijikuta akisema kwa sauti Tito, kwa akili yake alijua ni Askofu Magimbi ndie aliyemuuza kwa serikali..

“wako wapi hawa mbwa?” Tito aliwaza akiangaza macho huku na huko wakati akitoka nje ya mgodi mikono yake ikiwa juu

Sasa kwa mbali mlio wa chopa ulisikika ni wazi kuwa lile agizo la Tito lilitekelezwa haraka sana
Bili hakwenda mbali pamoja na wale wenzake watatu
“kama nilivyowaambia leo ndio siku yetu!’ alisema Bili

‘una mpango gani Bosi?” aliuliza Frank
“ ni wazi kuwa wakina Tito watakamatwa sisi tujibane pale na kufuatilia mzigo pole pole na kuhakikisha kuwa sisi ndio tunabaki na mzigo tutauza wapi mimi hiyo kazi niachieni” alisema Bili ama Carlos kama walivyopenda kumuita wenyewe,

Ni wakati wanaendelea kujadili ndipo wakasikia mlio wa chopa
‘haiwezekani!” alisema Bili,
Wote walitoka nje ya gari na kushuhudia mwanga mkali wa chopa kuelekea kule mgodini,

“nina wazo Boss, kwanini tusiende pale mgodini na kujua kitu gani kinaendelea ili kama vipi tuvamie?” alisema Jacob,
‘hatujajua hawa watu ni kina nani na wana silaha kiasi gani, maana tusije kukamatwa kiboya, kumbukeni tumeingoja hii siku kwa miaka mingi!” alisema Bill

‘ingieni kwenye Gari endesha bila kuwasha taa!” alisema Bill na safari ya kwenda Mgodini tena ikaanza

_____________________________________________

Joyce aliendelea kuangalia picha mbali mbali alimuona Oscar akiwa chini ya Ulinzi pamoja na Tito,
Alijikuta akitabasamu tu na sasa walikaribia kumaliza zoezi hili na alitaka kumfanyia sapraizi kwa kuonana nae baada ya kazi ile ngumu,

Bwana Johnson baada ya kuona kimya aliwaamuru walinzi wake watoke nje ya mgodi kwani hakujua kitu gani kimetokea

************************
‘C Room, L2 hapa!” alisema George akibana kifaa chake masikioni

“yes , tunakupata” aliitikia Joyce
“ niunge” alisema George
“okay dakika mbili! Alisema joyce huku akibonyeza vifaaa vyake na kisha Bwana Allan akaonekana kwenye Tv kubwa pale mbele yao
“jiwe mkononi,” alisema Oscar baada ya kusikia sauti ya Bwana Allan upande wa pili

“mchanga na maji?” aliuliza Allan
‘huu unafuata mawe yalipo mkuu!” alisema George
“kwahyo vifaa vya kutosha si ndio?”
“haraka iwezekanavyo maana kuna kokote zimezagaa sana hapa!” alimalizia George
Ni wakati George na Tom wanazubaa kuangalia chopa iliyokuwa inatua milio ya risasi ilisikika kutokea vichakani ambapo Bili na watu wake walijitokeza na kumfanya Tito kutabasamu
Oscar alimvuta Tito na kurudi nae ndani kwa spidi kali
“acha!” George alimfokea Tom ambaye alitaka kuwashambulia akina Oscar
Wakati wanashuka haraka haraka walikutana na Bwana Johnson na walinzi wake wawili, bila kuuliza nao waligeuza na kuingia kwenye chumba kimojawapo na kujifungia
“samahan bwana Johnson Tumekwisha!!’ alisema Bwana Tito huku akikaa chini
Ilibidi kumueleza kila kitu huku akisisitiza kuwa huko nje wamezunguukwa


‘twende tukasadie ‘ joyce aliongea na dereva wake kisha wakaongeza mwendo kuwawahi akina George,
Risasi ziliendelea kurindima na sasa Mgodi uligeuka kuwa uwanja wa damu na machozi tom na George walikua wakipambana ana kwa ana na Bili na watu wake, na wote wakajikuta wameishiwa risasi na mapambano ya mwili yakashika kasi,

Rubani wa chopa baada ya kukosa mawasiliano na bosi wake Tito pamoja na hali ya vita aliamua kunyanyua tena chopa yake na kupotelea angani,
“haya mko chini ya ulinzi sitisheni mapigano!” alisema Joyce akiwaamrisha akina Bili ambao tayari walikua wanaendelea kutoa kipigo kwa akina Tom,
Walikubali kujisalimisha na Haraka George na Tom waliwaweka chini ya ulinzi na kuwafunga kamba maalum na kuwalaza chini,
Walikusanya na wafanyakazi wengine kadhaa na kuwaunganisha na sasa wakaingia kuwafuatilia akina Tito na Johnson,

“ joyce twende, Tom na mwenzako bakini hapa backup inakuja muda sio mrefu” alisema George akiwahi kufungua mlango na kutokomea ndani.

“Tito alishindwa kufanya maamuzi yoyote Bwna Johnson alijilaumu sana kwa kufanya ujinga wake wote huo lakini sasa hakukua na namna wakati wakiwa bado wametulia
Sauti ya George iliwataka kujitokeza na kujisalimisha
“mheshimiwa waziri tunakuomba ujisalimishe pamoja na watu wako, tunakupa dakika mbili uwe umetoka hapa nje!” alisema George

“mkuu twendeni” alisema Oscar huku akimuongoza Tito kutoka nje

Walitoka nje na kutokea kwenye Korido kubwa Tito alishikwa na mshangao mkubwa kumuona binti yake Joyce akiwa ameshika bunduki na mavazi ya kijeshi
 
KESI YA MZEE MNYOKA 40 (Gily anatudhamini)

Tito aliongea hayo akijaribu kumsogelea Joyce
“usisogee!” alisema George huku akimkonyeza Joyce ambaye alienda kuchukua silaha za walinzi wa Johnson kisha wakaanza kutembea kutoka nje,
‘MY DAUGHTER ! ‘’ alisema Tito, Oscar alijitahidi kumeza mate huku akipigwa na butwaa,
“kumbe! Sikujua, kwanini nimekuwa mzembe kiasi hiki kutomjua Joyce tangu mwanzo’ Oscar aliwaza,
Na hatimaye walifika nje na kuanza kuwafunga kamba Tito na walinzi wa Bwana Johnson kisha wakamfunga Bwana Johnson mwenyewe,

Wakati Tito anazidi kushangaa Joyce alienda kwenye ile gari yao na kutoka na kijikoti cha kijeshi pamoja na bastola mbili kisha akapiga saluti kwa Oscar
‘naitwa Joyce, NSA level 4 ! alisema huku akijitambulisha kwa Oscar na kumkabidhi Oscar kile kikoti ambacho alikivaa huku Tito akizidi kuchanganyikiwa..

“kwahiyo kumbe wewe Oscar ulikua mpelelezi .. hahahahahaha dah! Mimi ni mpumbavu! Mimi ni mjinga!’ alisema Tito kwa uchungu!

Oscar alivaa vidude vya mawasiliano na kisha akachukua jukumu lake kama kiongozi..

“nendeni kule chini mkafunge milango yote vizuri na kuhakikisha ulinzi upo kila sehemu” aliongea Oscar huku jicho lake likimtazama Joyce


Baada ya saa moja Bwana Allan alifika pamoja na kikosi chake na kuwachukua akina Tito na genge lake na kuwaondoa chini ya ulinzi mkali..
Oscar walirudi kwenye ambulace yao na kuanza safari pole pole hakuna aliyeongea chochote..

>>>>>>>>>>>>>
BAADA YA SIKU CHACHE

Tito alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani pamoja kufilisiwa mali zake zote, alimtaja Askofu Mjimbi ambaye alikutwa akiwa amejipiga risasi ya kichwa na kufariki. Bwana Johnson alirudishwa na kufunguliwa kesi upya nchini uingereza,

Oscar alikua amefanya mpango wa kuonana na Joyce kabla hajaondoka lakini kwa sababu ambazo hakuzielewa Joyce hakupatikana tena kwenye simu yake

Siku hiyo aliamua liwalo na liwe na hivyo akajitosa kwenda kumvaa Bwana Allan..

‘oscar, ni wewe tu hujafika hapa ofisini tangu tukio lile, nikajua bado umepumzika! Hata hivyo afadhali umekuja maana ni wewe ulibakia tu, ili na mimi nikapumzike!” alisema allan akimkaribisha Oscar,

“kwani kuna nini!” aliuliza Oscar hata akasahau jambo lililomleta
“ Namba moja ametoa zawadi kwenu na ofa, na kwa kazi kubwa mliyofanya, zipo nyingi ila tuanze na hii kwanza, “ alisema akitoa kwenye droo yake picha moja ya nyumba nzuri sana yenye uzio mpana,
‘Ipo hapa mjini maelezo yapo nyuma ya hiyo picha,’ alisema halafu
Na hii hapa.. alisema huku akitoa hundi ya pesa dola za kimarekani elfu 50,

“hayo ndio yametoka kwa namba moja , mimi zawadi yangu kwako Binafsi ni hii hapa!” alisema akitoa bahasha nyingine akimkabidhi Oscar,
Oscar aliichukua na kutaka kuifungua..
“hapana hii utafungua nyumbani, haya sasa niambie kitu gani kimekuleta”

aliuliza Allan akimtazama Oscar machoni..
Oscar hakujua anzie wapi

“mkuu ni kuhusu Joyce!” alisema Oscar.
‘ana nini!” aliuliza Allan kwa ufupi
“aah hapatikani na sijawahi kumuona tena tangu siku ile, na kwao hayupo, na George pia hapatikani!’ alisema Oscar kwa aibu kidogo..

‘nilikuambia umebaki mwenyewe,” sijui kama ulielewa, anyway nenda zako nyumbani ,kumbuka hiyo bahasha ukafungue kwako..

Alisema Allan akinyoosha mkono wake,

Oscar alimjua vyema bosi wake huyo hivyo akatoka kwa upole na kushika mlango tayari kutoka

‘take care!” alisema Allana akimuaga.

Oscar alifika nyumbani kwake na kutazama ile picha ya nyumba hakika ilikua nzuri sana na zaidi sana ilikua eneo zuri sana kama mlimani hivi,

Aligeuza ile picha na kuona namba ya simu, alikua anataka kupiga ndipo akakumbuka kuwa hajafungua ile bahasha!
Haraka alichukua ile bahasha na kuifungua..

Ndani yake kulikua na passport mpya ya kusafiria yenye picha yake pamoja yenye jina JACOB LAURENCE ISAYA ikimtambulisha kama mfanyabiashara pamoja na kitambulisho cha kupigia kura na kadi ya benki vyote vikiwa na jina hilo hilo!

“Asante Mungu!” Oscar aliruka kwa furaha kwani tayari hii ilimaanisha anapata likizo ndefu ,
‘Joyce uko wapi?’ aliwaza huku akichukua vitu vyake alivyoona kuwa ni muhimu na kuondoka tayari kuhamia nyumba yake hiyo mpya!
Alitoka nje na kuitazama nyumba yake hii aliyokaa karibia miaka mitatu, kisha akatoa simu yake na kupiga ile namba
“njoo tegeta kwa ndevu , hapa uliza kwa Waroma halafu kuna njia inashuka kama unaenda mji mpya utaona kama mlima hivi nipo hapo” sauti ya mwanaume upande wa pili ilisikika

Oscar aliendesha gari lake kwa kasi na baada ya masaa mawili alifika na kweli alikuta nyumba kama vile vile alivyoiona kweny picha ilikua nzuri sana,

‘bila shaka ni bwana Jacob eeh?’ alisema Yule mzee
“ndio hujakosea kabisa’ alisema oscar akimsalimia Yule mzee,

Alimtembeza nyumba nzima na kisha akamkabidhi funguo na kuaga..

“mzee sasa mbona haraka!’ alisema oscar
“nimeambiwa nikupe ufunguo halafu niende kazi yangu ilikua kulinda tu hapa!” alisema Yule mzee
Na huku akitoka kwa haraka Oscar alitabasamu tu huku akijiachia kwenye nyumba yake hiyo,
Akili yake sasa ilikua kwa Joyce alijaribu kutuma emails, na meseji za whatsap lakini hazikujibiwa na Joyce hakuwa online kabisa

Simu yake iliita na kwa haraka aliipokea bila kuangalia mpigaji
“joyce !?” alijikuta akiuliza
“ utakuwa mwehu, umeacha hati yako ya nyumba Mr Jacob, nakutumia mtu akuletee, huyo mwenzako nae kawa chizi kama wewe!” alisema Bwana Allan, kisha akakata simu!

“huyo mwenzako nae kawa chizi kama wewe!’ oscar aliirudia hii kauli kichwani mwake
“kwa maana hiyo anajua alipo si ndio!?” alijiuliza akikaa vizuri kwenye kochi lake

Aliletewa ile hati na Paulo mfanyakazi mwenzake pale ofisini ambaye nae alisema hajui chochote kuhusu Joyce alipo,

“kila mmoja alikuja kivyake pale kama wewe na kisha akaondoka na bahasha yake akasepa” alisema Paulo huku akirudi zake ofisini..
 
KESI YA MZEE MNYOKA- MWISHO WA MWISHO (
Kwa udhamini wa mkuu Gily )

Baada ya wiki moja
Oscar alikua amejilaza kwenye sofa huku akiangalia vipindi mbali mbali kwenye televisheni yalikua ni matangazo ya moja kwa moja kutoka chuo kikuu cha dar es salaam ambapo waziri mkuu alikua akiwatunukia shahada ya uzamivu wanafunzi waliohitimu mafunzo maalum ya mifumo ya komputa , hawakuwa wengi sana, na kutokana na kozi yenyewe,
Na wanafunzi hao kuitwa mmoja mmoja,
‘Na huyu ni mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi na kupata GPA 4.9 anaitwa JOYCE TITUS KILIBIKA!
Alisema mc wa shughuli hiyo
“whaaaaat!” alisema oscar akiruka pale kwenye kochi na kuvaa haraka haraka kisha akawasha gari na kuwahi mwenge. Mlimani..

Kama bahati alikuta sherehe bado hazijakamilika na wahitimu bado walikua ndani

Ndugu jamaa na marafiki walikua wamezunguuka nje na zawadi zao huku wakisubiri kwa hamu wapendwa wao watoke nje!

Naam hatimaye walianza kutoka mmoja baada ya mwingine wakiwa na majoho yao,

Oscar alijitahidi kujipenyeza hadi akafanikiwa kuwa karibu na mlangoni kabisa, kwanza hakua na zawadi yoyote! Hivyo ilikua ni rahisi kufika mbele kabisa,

Hatimaye mtu wake alitoka! Oscar kama mshale alichomoka na kwenda kumkumbatia Joyce! Joyce nae hakuamini macho yake, machozi yalimtoka kwa furaha,

Bila kujali macho ya watu oscar alimbeba Joyce na kutokomea nae kwenye gari…..

‘oscar tunaenda wapi? Ujue ndugu zangu nimewaacha na mshangao wa haja” alisema Joyce huku akivua joho la kubaki na suruali na tisheti nyepesi , oscar hakujibu chochote alizidi kukanyaga mafuta kuelekea Tegeta,

Baada ya safari ya kutokuamini hatimaye walifika , oscar alishuka na kwenda kufungua geti na kuingiza gari ndani kisha akafunga tena geti na kumbeba tena joyce hadi ndani na kumtua kwenye sofa!

“oscar. Oscar..”
“shhhhh!” oscar aliweka kidole mdomoni kumuashiria asiseme kitu Joyce kisha akamsogeza karibu na kuanza kumtomasa na kumvua nguo moja baada ya nyingine mwishowe walijikuta katika mapenzi mazito hapo hapo sebuleni, na hivyo kuamua kuhamia chumbani na shughuli ikaanza upya,


Saa mbili Usiku walirudi sebuleni na joyce alikimbilia simu yake,
“yaani wamepiga mpaka wamekoma, nimetafutwa sana!’ alisema Joyce
“vipi nikupeleke !” aliluliza Oscar
“ah keshoo njaa inauma hatari’ alisema Joyce akitafuta jiko lilipo oscar nae alimfuata akiwa na bukta .

Kesho yake walienda hadi gereza la keko kumtembelea mzee Tito,

oscar alibeba kitabu cha hadithi kilichoitwa “MPANGAJI” ili kumpa mzee Tito asome akiwa lupango..

“hakika maisha ni hadithi ndefu sana” alisema Joyce wakiwa njiani kurudi,


“nakuachia binti yangu, muangalie, nakuamini Oscar, asije kulia machozi yanayotokana na wewe!” oscar alikumbuka maneno ya mzee Tito muda mfupi uliopita na kujikuta machozi yakimtoka,
Hakupendezwa na hali hii ya kuishi na Joyce wakti baba yake akiwa gerezani lakini hakuwa na namna yoyote,
Maisha lazima yaendelee

Aliwaza akikanyaga mafuta kurudi tegeta.

MWISHO.

Namba zangu ni 0746 mia mbili sitini na sita mia mbili sitini na Saba


Niwashukuru sana wadau,
Asanteni kwa support yenu!
Mpaka wakati mwingine kwenye "MPANGAJI AU MZAHA WA DAMU"
 
Back
Top Bottom