CK Allan
JF-Expert Member
- Aug 14, 2013
- 2,781
- 6,139
- Thread starter
- #101
MADAM PRESIDENT 15
Anaendelea Allan,
Niliamua kuelekea Kigamboni kwasababu kuu mbili,
Kwanza sikumuamini Tena Jesca,
Hivyo nikaona niwe nae mbali Kama kumpoteza,
Lakini sababu ya pili nilitaka sehemu ya utulivu ili niandae mkakakati wangu imara kwa ajili ya kutatua suala lilijojitokeza,
Nisingetaka kukimbizana na polisi kwa siku hizi kabla sijaweka mpango mkakati,
Eneo hili kwa baba mchungaji maeneo ya vijibweni lilikua mbali na mji kiasi hivyo niliamini itakuwa hatua nzuri kwangu kupanga mashambulizi.
***************
Taarifa zilianza kusambaa kwa Kasi ya umeme kuwa nimetoroka Mahabusu kwa kumjeruhi Askari mmoja, polisi walisema Kuna iwezekano mkubwa nilipata msaada wa kufanikisha kutoroka,
Polisi waliahidi zawadi ya milioni 10 kwa yoyote ambaye angefanikisha kunikamata,
Sambamba na Hilo Niliongezewa mashtaka mengine mawili
Kujaribu kuua na kutoroka huku nikiwa chini ya ulinzi,
Baada ya Jose kurudi Sasa nilikamilisha mpango wangu.
****************
Saa tatu usiku nilivaa mavazi yangu ya kazi huku nikiwa na begi langu mkononi, moja kwa moja nilipanda pantoni kuelekea posta,
Nilishuka na kutembea haraka Kisha nikavaa kofia yangu na kuziba uso kiasi,.
Nilifika Hadi zilipo ofisi za Mbongo na kusimama nje getini,
Nilisimama pale huku nikiaangalia saa yangu,
Muda kidogo ilitokea Gari nyeupe taratibu nikatoka pale nilipoegamia kuifuata Ile Gari,
Ni Kama dereva alijua nina Jambo maana wakati nasogea alilisimamisha kabisa Lile Gari kunisubiria..
"Habari , dada"
Nilisalimia
"Salama Kaka, karibu nikusaidie"
Alijibu .
"Bila shaka Ni mwandishi Christabela?"
Niliuliza nikiiweka sawa kofia Yangu.
"Ndio Ni yeye, samahani sijui tunaweza kurudi ndani Kama Ni suala la kiofisi?"
Alisema Christabela.
"Hakuna haja, nimefurahi jinsi ulivyoandika kuhusu kesi ya Allan,..
Sasa chukua hii bahasha Ina kila kitu"
Nilimpa Ile bahasha Kisha nikaondoka zangu kwa haraka kurudi Kigamboni.
Nilirudi nikiamini Christabela atafanya kazi yake vizuri,
Nilimpa Ile bahasha makusudi nikijua fika kesho yake Raisi alikua anafanya mkutano na vyombo vya habari na Kama alivyokuwa akijinasibu alitaka kuulizwa swali lolote kuhusu yeye Binafsi na Siasa,
"Janet na Siasa"
Ndio jina lililopewa mkutano huo..
Katika bahasha yangu kwa Christabela nilimwambia namna ya kuuliza maswali na ikiwemo barua za Janet na picha moja Kama ushahidi hivyo nilitegemea Christabela "aue"
Kesho yake saa 4 asubuhi nilikua chumbani kwangu Kigamboni nikiwa nakodolea macho mkutano wa Raisi na vyombo vya habari,
Janet alianza kwa kutoa historia yake kuzaliwa , maisha yake ya utotoni na jinsi alivyoingia kwenye Siasa,
Vyakula anavyopenda na Mambo mengine, mengi yakiwa ya uongo ,
Baada ya hotuba alikaribisha maswali na waandishi wakauliza maswali mengineyo hatimaye nikamuona Christabela akisogea mbele na kushika maiki..
"Come on baby!,"
Nilijisemea nikiomba Christabela amalize game....
"Mheshimiwa Raisi Kuna huyu Mtu ambaye ametoroka hivi karibuni , tuliona Mara ya kwanza ulisisitiza akamatwe ndani ya siku kadhaa je Ni kwanini umelichukulia suala lake Kama so special hivi na Kuna wahalifu wengi tu tunaona walifanya matukio na hujawahi kutoa tamko?"
Aliuliza Christabela
"Ooh no Christabela unachemka mama, swali gani Hilo?"
Nilijikuta napandwa na hasira nikitamani kuzima TV,
"No wengi walininukuu vibaya, wakati naongea na mapolisi Kanda maalum ya Dar es salaam , siku Ile ndio kesi ya Allan ilikua Kama Ina trend hivi ndio nikatoa Kama reference Wala hakukua na kitu cha ziada, "
Alisema Janet,
"Mheshimiwa Kuna swali la nyongeza kwenye kitu hicho hicho,"
Alinyoosha mkono mwandishi mwingine
"Naitwa Mazinge kutoka Powerful media, mheshimiwa hili suala la Allan, Kuna maneno huko mtaani kuwa huyu Ndugu mlishawahi kuwa na mahusiano enzi hizo na Sasa ikaundwa hii kesi ili kupoteza ushahidi Kama Raisi anadate na Raia wa kawaida"
Ukumbi mzima waliangua kicheko na minong'ono ikaanza mpaka ikabidi muongoza mkutano atulize kelele...
"Ni kweli hata Mimi nimesikia hayo maneno, Ila Sasa Kama Raisi siwezi kujibia maneno ya mtaani , Binafsi natamani nimuone maana hata Mimi mwenyewe simjui,
Hahahahaha"
Janet alimalizia kujibu swali huku akiangua kicheko,
Maswali mengine yaliendelea Kisha mkutano ukafungwa...
Nilizima TV Kisha nikatabasamu,.
Hatua ya kwanza ilishaisha bado hatua ya pili,
Hatua iliyofuata ilikua Ni kuchapisha picha yangu tukiwa na Janet , siku ambayo alikuja kunitembelea shuleni na tulipiga karibu na kibao Cha shule,
Lakini pia nilimpa Christabela majina ya watu ambao walijua mahusiano yetu na Janet wengi wakiwa wanafunzi wenzangu mombo sekondari,
Ni kweli kesho gazeti la MBONGO
Lilipambwa na Habari
"KUMBE JAMBAZI NA RAISI WANAJUANA"
huku picha yangu na Janet ikiwa imewekwa na kipande Cha barua,
Habari hiyo ilikua gumzo siku hiyo na jina Langu likiwa midomoni mwa Watu,
Uzuri Ni kwamba wale wote tuliosoma mombo sekondari ambao niliwaandika walihojiwa na wakakiri,
Baadhi ya waandishi walifika Mpaka shule niliyosoma huku wakifananisha mazingira tuliyopiga Ile picha,
Wengine walidiriki kurusha kwenye Televisheni,
Hakika Sasa nchi nzima ilisimama, na wanaharakati wakaanza kufuatilia undani wa kesi yangu ya wizi,
Wapo waliodiriki kusema nijitokeze hadharani watanilinda,
Hatimaye Raisi alijitokeza Tena hadharani baada ya siku chache,
Alisema wapo watu waliokusudia kumchafua kupitia tukio Hilo na kwamba kujuana nae ama kutojuana nae hakuondoi uhalifu wake,
"Kumbukeni Raisi hakutokea mbinguni, Sasa kusema kuwa najuana na Allan ndio afanye uhalifu na asichukuliwe hatua?, Bado nawasihi Jeshi la polisi kumtia Nguvuni ili ajibu mashataka anayokabiliwa nayo"
Janet alisema
Baada ya kauli hii Sasa hoja mbali mbali ziliibuka na kila mmoja akaanza kuongea kwa kadri anavyoona inafaa...
"Raisi anapaswa kujiuzulu, kwanza alidanganya kuwa hamjui, lakini baadae alivyopewa ushahidi anasema anamjua, Sisi Kama ATC tunamtaka Raisi ajiuzulu kulinda heshima ya kiti Cha Uraisi"
Alisema mama Devota