Hadithi: My Soulmate

Naona Chuo Unazungumzia Arusha Tech Kijanaa
 
My Soulmate Sehemu ya 16.
Imedhaminiwa na EquatorSpecials
######### ILIPOISHIA ###########
Eric alikutana na Rita akampa wazo la kumsaliti Nickson kwa ajili ya kupata hela nyingi zaidi lakini pia awe na rita pamoja na kwamba Eric ni pendapenda kampenda kwa kweli Rita au kamtamani? Yote sawa kwake alikaa akawaza cha kufanya akiwa kwenye dilema amwambie rafiki yake ama akubali?.
*** Twende Nayo sasa *******
Eric alikaa akiwaza akajua ikitokea amekataaa kwa sababu RIta ndo kama ameshikilia mpini wa kisu hiki wanaeza kosa hela kabisa . Akasema liwe na liwalo.Eric alichukua simu yake ya mkononi aka andika ujumbe.
Eric : "Sawa Nimekubali...." akitaka kutuma kwa Rita . Roho ikasita akaifuta aka andika ujumbe mwingine "Nickson wale watu wa chuo wanataka kutugeuka kaka.". alipo taka kutuma aliwaza akakumbuka mwalimu john aliwa ambia urafiki wa nyanya kwenye tenga kumaanisha kuwa kila moja lazima aende na maisha yake. Aka andika ujumbe mwingine "Sawa nimekubali lakini hakikisha hiyo hela naipata. Na pia nafanya hivi kwa sababu nakupenda Rita.".Eric alifanya maamuzi ya kumgeuka rafiki yake kwa ajili ya sababu zake.
Rita alimjibu akamwambia "Sawa tuta zungumza zaidi. Nakupenda pia wewe ni mwanaume shupavu Mwaaaaaah.". Rita alifurahia maaana anajua ana malengo yake.
**********************************************************************************
Ilipofika mida ya asubuhi Rita alimpigia Eric ili wakutane na Boss Sambeke ambaye alikuwa Boss wa zamani wa Nickson.
Boss : "Za sa hizi jamani?"
Eric na Rita : "Salama!".Wote wali itikia kwa pamoja.
Rita : "Boss huyu ndo mpenzi wangu hendsam wangu anaitwa Eric!.". Rita alisema kwa mapozi.
Boss : "Za saa hizi yeroo?"
Nickson : "Salama boss!"
Boss : "Huyo ndo yule ulisema yupo Uganda? "
Rita : "Hapana huyu ni hendsam wa hapa hapa nimeamua kuachia ngazi kule mi nimempenda huyu zaidi."
Eric : "Asante mpenzi."
Boss : "Sawa karibu sana usimchezee huyu mdada tu."
Eric : "Hapana mkuu hapa nimekwama hamna kuchezeana."
Boss : "Sasa umekubali alicho kuambia Rita ili upate hela zaidi?"
Eric : "Ndio lakini msini tapeli tu!."
Boss : "Hahahaha nani akutapeli?. Mi siezi nikakutapeli wala usiogope."
Eric : "Sawa hapo umesema la maana!"
Boss : "Sasa mimi nahitaji ufanye kimoja ili tuwe sawa."
Eric : "Chochote tu mkuu nieleze.".Wakati huo Rita alikua ana ondoka kwa hiyo aliaga na kuwa acha hapo.
Rita : "Kwa herini jamani!. Mpenzi kwaheri."
Eric :"Sawa mrembo wangu mwaaah.".
Boss : "Haya kwa heri mamy!."
Eric : "Niambie Boss."
Boss : "Kwanza tukubaliane amekuambia kiasi gani?."
Eric : "Alisema nitapatiwa millioni mia."
Boss : "Aaaaah hapana nlimwambia millioni 95 lakini kuongeza millioni tano mbona ni kidogo tu.Hakuna neno yerro millioni mia lazima upate!"
Eric : "Sawa haina shida!."
Boss : "Sasa nataka twende ofisin kwangu ukakutane na vijana wangu wa kazi uwaelekeze vitu vya kubadilisha nataka hii tuibadilishe ifanane na kile mlicho onyesha kule ili iwe rahisi kuiuza maana si mfanano tu?"
Eric : "Ndio haina neno."
Eric na Boss Sambeke waliondoka hapo na kuelekea kwenye ofisi ya boss huyo wakakaa na hao vijana wa boss huyo waka anza ku iga kila kitu na kwa sababu kulikua na hela na vijana watano wali iboresha zaidi.
**********************************************************************************
Nickson aliendelea ku pambana na maisha japo kuwa ame ahidiwa millioni 150 bado hajapewa na lazima maisha yaendelee . Nickson aliendelea kwenda kubeba zege na kazi zingine za mikono ambazo rafiki yake Dulla alikuwa akimuitia. Dulla alimsifia sana Nickson kw akuwa mpambanaji japo kuwa amesoma kama hamna kazi yeye ana mbinu ali mradi maisha yasonge.
Nickson aka piga simu kwa RIta yule secretary wa chuoni kwao kufatilia majibu.
Rita : "Halo!".
Nickson : "Habari za masiku dada!."Nickson aliongea kwa sauti ya heshima.
Rita : "Salama nani?"
Nickson : "Mimi Nickson ambae nilikuja huko chuoni kwa ajili ya aplikesheni ya makala za masomo."
Rita : "Aaaaaah nimekukumbuka. Sasaaaa."
Nickson : "Ndio."
Rita : "Mkuu wa chuo alipata udhuru kwa hiyo kikao tulichokuwa tumepanga kufanya kimeghairishwa labda aki rudi tutafanya mwezi huu mwishoni ama mwezi ujao mwanzoni."
Nickson : "Ahhaa sawa dada yangu!."
Rita : "Haya karibu kaka wala usiwe na shaka nitakujulisha!."
Nickson : "Sawa asante."
Rita : "Haya kwa heri."
Nickson bila kujua kuwa rafiki yake ameshamgeuka alimpigia na kumueleza kuhusiana na simu aliopiga kwa ajili ya kumpa rafiki yake moyo. Na Eric alijifanya kama hajui kitu!.
Nickson pia alimkumbuka mpenzi wake Stela akampigia lakini alikata simu na kumtumia ujumbe mfupi na kusema "Nipo kwenye kikao nitakupigia!.". Siku hiyo ilipita na wala Stela hakumtumia ujumbe wowote wala kupiga kama alivyo ahidi Nickson alisikitshwa sana na hicho kitendo lakin hakua na mbinu alijua yamkini Stela anachapa kazi sana.
**********************************
Upande mwingine mandoto yupo na mpenzi wake mpya ambae ni mke wa mtu lakini mume wake amesafiri.
Mandoto : "Ah mpenzi una niweza jamani leo nalala na huku!. Nataka kubaki na Sara wangu".
Sara : "Mh we acha kujishaua uyu mtu akirudi atakuvunja meno."
Mandoto : "We acha kunitisha mimi mwanaume eti."
Sara : "Haya mi ntawaacha nimwone kidume wangu. Wewe ama yeye."
Mandoto : "Kwa hyo huingilii?"
Sara : "Ah wewe mimi ndo kombe mshindi ndo atanichukua si uta kuwa wewe mpenzi?"
Mandoto : "Ndio mpenzi kwa ajili yako nitakua shujaa."
Sara : "Wacha wee!"
Mandoto : "Mimi hatari. Nlienda judo mimi."
Sara alisema hivyo akitoa nguo zake kwa ajili ya kwenda kuoga aka muita Manoto wakaoge.
Walikula waka angalia muvi na kucheza kushoto na kulia. Na waka lala . Ilipofika saa nane usiku Sara aliamshwa kwa sauti ya mtu aliekuwa akitembea mule ndani akifungua kama ni kwake.
Sara : "Mpenzi mpenziiii amka......"
Mandoto : "Mhh....... ". Bado alikuwa kwenye usingizi mzito.
Sara : "Amka wewe kuna mtu anatembea ndani amka bhana.". Moyo wa Sara ulikuwa unaenda mbio kwa uoga.
Mandoto : "Unasema...? ."
Sara : "Kuna mtu ndani nimemsikia."
Mandoto "Majambazi ama? Mume wako amerudi? ".
Sara : "Hapana sio mume wangu alisema atarudi mwezi ujao."
Mandoto alivaa koti na ndala akaenda mpaka sebuleni huku Sara akimfuata kwa nyuma kimachale machale.Kuhamaki ni mume wake na Sara amerudi kakaa kwenye sofa la sebuleni akiwa tazama tu. Sara alianza kulia kama mtoto. Afande Stanleyalikua ameweka silaha zake kwenye meza ya kahawa.
Afande Stanley: "Sara huyu ni nani?".
Sara : "Mume wangu nisamehe." Sara alisema akiendelea kulia na kupiga magoti.
Afande Stanley : "Kijana naona hupendi maisha yako."
Mandoto : "Samahani mkuu ni shetani."Mandoto alisema huku akilia utasema sio yule aliekuwa akijitamba ni mwanaume!.
Sara : "Mume wangu huyu alini laghai mume wangu nisamehe.."
Mandoto : "Mkuu mwone huruma mkeo mimi ndo nime mlagai msamehee mkuu."
Alisema akisogelea mlango akatoka mbio mpaka nje akakuta mlango umefungwa aka panda juu ya geti haraka sijui nguvu alipatia wapi. Alipanda mpaka juu suruali ika chanika kwenye ncha ya geti akashukia upande mwingine akiwa na suruali nusu. Aliponea chupuchupu lakini alimsikia Afande Stanley akisema "Nikikikumata nitakuua."
Mandoto alikimbia mpaka kwake akakumbuka kaacha simu na wallet yake kwa Afande Stanley. Ali pata wasiwasi kila saa ana kuwa na wasiwasi kuwa Afande anaweza mtokea mda wowote.
******************************************
Upande mwingine Nickson ametoka kwenye mihangaiko yake ya ku hakikisha mkono unaweza kwenda kinywani. Akiwa na rafiki yake Dulla.
Nickson : "We jamaa inabidi ukaoe!."
Dulla : "Ah mi siamini wanawake kabisa!."
Nickson : "Wamefanyaje?"
Dulla : "Ah ndugu yangu acha na wanawake bhana".
Nickson : "Unawaogopa nini tuka kutetee kwa wadada?."
Dulla : "Bora hata ninge kua nawaogopa sio huyo mdada anaitwa Josephina ali fanya niwajue wanawake vizuri."
Nickson : "Josephina! ana jina zuri kwa hiyo alikufanyaje?."
Dulla : "Mkuu yule mdada alikua hana chochote wala lolote bhana mimi nika mpenda hivyo hivyo."
Nickson : "Ah jamaa huyo alikudtisha huyo!."
Dulla : "Nakwambia nilimpendea alikua anapenda kuchakarika yani mara zingine nilikuwa naskia ana fanya zege!"
Nickson : "Wacha wewe mwanamke huyo?."
Dulla : "Yani we acha tu. Sasa alipata marafiki wa china wakawa wanamletea mizigo mpaka huku mimi nikajichanga nikampa hela. Yani nakwambia nilijinyima kwa sababu nilimpenda na nikajua akifanikiwa lazima na mimi nifanikiwe."
Nickson : "Enhee. Aka pata na bwana china nini?".
DUlla : "Hapana mkuu"
Nickson : "Leta hadithi baba..."
Dulla :"Aliniambia kuwa akipata tutakuwa tuna gawana faida."
Nickson : "Enhee ikawaje?".
Dulla : "Bhana wewe aka anza mwezi wa kwanza hapati faida yani faida akipata anarudisha kwenye mzunguko wa biashara kwa hiyo akawa hana kitu cha kutumia nikawa nampa hela ya matumizi na bado namlisha nikijua akifanikwa mambo yatakua poa!."
Nickson : "Dulla wewe au umetunga!."
Dulla : "Mimi huyu huyu mbona kama huamini?".
Nickson : "Dah mi najuaga we muhuni tu kumbe una roho nzuri hivi sasa ikawaje?".
Dulla : "Mwezi kama wa nne hivi aka anza kupata faida inayo eleweka wateja anao kwa hiyo mambo yakawa shwari. Lakini tatizo likaja moja!"
Nickson : "Tatizo gani hilo alikufa au?".
Dulla : "Bora kufa nakwambia mkali! we acha niliapata pigo la maisha bhana."
Nickson : "Enhee leta mambo mkuu!."
Dulla alitoa sigara mfukoni akaiweka kinywani akaiwasha akavuta kama pafu mbili hivi akaendelea kuongea.
Dulla : "Yule mdada aka anza kubadilika hapokei simu mara ananijibu ovyo tu alimradi."
Nickson : "Yupi huyo Josephina! Ama?"
Dulla :"Huyo huyo jamaa yangu."
Nickson : "Weweee.."
Dulla : "Mimi nilikaa kimya nikidhani labda ni biashara inamchanganya labda imekuwa ngumu kwake."
Nickson : "Enheee."
Dulla aliendelea kwanza akuvuta sigara yake aka malizia funda la mwisho akaitupa chini na kuikanyagia ili kuizima.
Dulla : "Hata shilingi moja ya hela zake sijawai kuzila pamoja na kwamba alisema ata gawana na mimi sikuona hata kila nikimwambia anasema bado lakini ana nunua simu mpya ma wigi mengi tu mara nguo za gharama vito na bado tu anasema hamna faida. Baada ya miezi aka acha kuja kwangu tena akahamia kupanga nyumba kubwa zaidi mara nisikie ana gari jipya ana wafanyakazi kwenye kampuni yake."
Nickson : "Daaah hatari"
Dulla : "Nikamfuata nikamwambia vipi mbona umebadilika akasema oooh unajua mimi saivi nimekuwa sio kama kiwango chako mimi nabaki na wewe kufanyaje?."
Nickson : "Dah maisha bhana si ulimpa mtaji huyo wakati alikuwa akibeba zege saivi ana kigari anasema wewe sio level zake?"
Dulla : "Inaniuma sana kaka!. Akasema bhana we usinitafute bhana marafiki zangu wenye hela watanishangaa kukaa na mtu anae kaa gheto kama wewe. Nikwamwambia usisahau lakini mimi nilikupa mtaji jamani."
Nickson : "Hapo bora umemkumbusha."
Dulla : "Heee ujasikia alichokifanya sasa."
Nickson : "Enhee akafanyaje?"
Dulla : "Akaenda kwenye pochi yake akatoa laki nne aka nipa kwa madharau akisema na upotee usinisumbue na hela zako. Hela ndogo hivi unani ganda?."
Nickson :"Ulichukua hela?"
Dulla : "Hapana mimi madharau sipendi kabisa. Nilimuachia hela zake bhana nasikia alipata ka bwana ka sharobaro akamlia hela zote akamzalisha na akapotea na hela zake saivi Josephina yupo mtaani na watoto wake ni wanaomba omba alirudi kwangu nikampa 10,000 nikamwambia potea."
Nickson : "Kweli man hujafa hujaumbika duh!."
**********************************************************
Upande mwingine Mandoto hatoki nyumbani kwake mchana anatoka usiku tu kukwepa kuonekana na Afande Stanley. Usiku mmoja alikwenda bar usiku alivyo enda chooni alishtukia kuona Afande stanley akiwa nae ndani ya choo hicho. Alibaki akimtumbulia macho ha amini kama ni amebambwa kirahisi hivyo.
Afande Stanley : "Mimi ni mwindaji Mandoto huwezi nikimbia nikakuacha...".
Itaendelea...............
 
Reactions: Sax
My Soulmate Sehemu ya 17.
Produced by; Equator Special.
#############Tulipoishia ######################
Mandoto alikuwa hatoki nyumbani kwake mchana anatoka usiku tu kukwepa kuonekana na Afande Stanley. Usiku mmoja alikwenda bar usiku alivyo enda chooni alishtukia kuona Afande stanley akiwa nae ndani ya choo hicho. Alibaki akimtumbulia macho ha amini kama ni amebambwa kirahisi hivyo.
Afande Stanley : "Mimi ni mwindaji Mandoto huwezi nikimbia nikakuacha...".
**** Endelea *******************
Ni kwenye club moja ilio changamka sana mida ya saa nane usiku. Mandoto anaelekea kwenye uwani kwa ajili ya kujisaidia. Mara Afande Stanley anaingia ndani ya choo hicho.
Afande Stanley : "Mimi ni mwindaji Mandoto huwezi nikimbia nikakuacha...".
Mandoto : “Umenipataje?”. Aliuliza akiwa ana tumbua macho.
Mara ghafla kuna mkaka na mdada wali ingia kwenye choo hicho na wakipiga kelele za shangwe wakiwa na dalili zote za kulewa. Mandoto alipo ona nafasi hiyo alitoka anakimbia mpaka nje.Mandoto anakimbia huku kichwa kikiwa na pombe tayari kwahiyo ana yumba yumba wakati huo Afande anamfatilia taratibu.
Afande : “Wewe una lala na mke wangu wewe?”.
Mandoto : “Nisamehe kaka..”. Mandoto alisema huku akikimbia kwa yumba yumba na kizungu zungu kiki msumbuwa anatamani kukimbia sana lakini mwili hauwezi.
Afande : “Huwezi nikimbia.” Huku akimfuata Mandoto taratibu kama mtu anaewinda sungura alie umia mguu!.
Mandoto : “Nisamehe ndugu sisi sote bina damu.”
Afande : “Hapana wewe unajua ninavyompenda Sara mimi?”
Mandoto : “Kuwa mpole haya mambo ya kawaida!”
Afande : “Mambo ya kawaida ?”.
Mandoto : “Ndio mkuuu kuwa mpole.”
Afande : “Niwe mpole na mtu nlie mkuta analala na mwanamke wangu? Mwanamke anae nifanya nijitoe vingi kwa ajili yake?. We ulikua wapi wakati anaumwa na saratani miezi sita?”
Mandoto: “Kaka kuwa mpole.”
Waliendelea kuongea mpaka kutoka nje ya club hiyo . Mandoto bado ana hangaika kutembea lakin hawezi kwa sababu ya pombe.
Afande : “Unajua nina vyo mpenda? Sara umelala nae kwenye kitanda changu kama ndio nyumba yako unadhani nimekufa ama?”.
Wakati huo wanapigana mke wa afande alifika maeneo hayo alikua akimfwata mumewe nyuma nyuma bila ya mumewe kujua anafuatiliwa.
Mandoto alisamama akasema hapa ama zangu ama zako siwezi kubali uni aibishe kisa ya mwanamke ninaye mpenda alianza nakurusha ngumi kumuelekea afande Stanley. Wakati huo sara ali ingia ndani ya pub akijua mumewe alingia humo muda sio mrefu akiwa ana angaza angaza kumtafuta mumewe.
Afande Stanley : “Hahahah inaoneka umeamua tuyamalize kiume sio?”.
Afande alisema huku akirusha ngumi za tumbo mfululizo kwa Mandoto . Mandoto alimkuatia wakawa wana garagara chini wakirushiana makonde ya kila maeneo. Mara ghafla sauti ya bunduki kufyatuliwa ilisikika . Sara alikuwa nje wakati huo na aliona sauti ilipotokea alimwona mumewe na mandoto wakiwa wamelaliana hakuna aliekuwa akisogea.
Sara alipiga ukunga kwa uoga aka anza kutetemeka akamkimbilia eneo la tukio ili ajionee kilichotokea. Akiwa akizidi kusogea aliona eneo hilo likiwa limejaa damu alishindwa kuamini kile alichokiona mbele ya macho yake.
Sara alifika pale akausogeza mwili wa mumewe uliokuwa ukimlalia mandoto. Kutahamaki ni Mandoto alikuwa akilala pale akiwa marehemu kutokana na risasi aliopgwa kifuani alianza kulia kwa uchungu kipindi hicho mumewe akiwa haamini kilichotokea alikuwa akitoa macho tu alipo rudi kwenye fahamu zake alimshika mkono wake aka anza kumburuta waondoke.
Sara : “Niache we muuwaji niache mimi.”.Alisema akiwa anahangaika kutoka kwenye mikono ya mumewe.
Afande : “Twende huku wewe na wewe nitakumalizia.”. Alisema akimburuza alipo ona haondoki almnyanyua na kumuweka begani na kutokomea nae pasipo julikana na mtu mmoja mmoja akianza kufika kwenye eneo la tukio.Ma askari hawakukawia kufika baada ya wasamaria kupiga simu polisi.
Mandoto alichukuliwa na gari ya hospitalini na kuwahishwa hospitalini kama jitahada za kuokoa maisha yake.
Rose dada yake na Mandoto alikuwa amelala wakati huo aliamshwa na simu kutoka hospitali akiombwa afike kwa ajili ya kumwona kaka yake aliekuwa amevamiwa . Wakati huo hakuna aliejuwa ukweli nini kilichotokea. Rose alipofika alijitambulisha akasema yeye ni nani.
Docta : “Rose nina habari mbaya kaka yako amekutwa akiwa amepigwa risasi ya kifuani na sidhani kama ni majambazi maana alikutwa na wallet yake na kila kitu.”
Rose : “Unaongea nini? Kaka yangu mimi hapa. Yuko wapi.” Rose aliongea akiwa anatoa macho bila kuamini amini anachosikia.
Docta : “Tafadhali kuwa mpole rose.”.Docta alisema kwa njia ya kiustarabu.
Rose : “Sio niwe mpollllee kaka yangu yukowapiiii….??”Rose alitoa sauti kali na kwa uwoga.
Docta : “Bahati mbaya tumejaribu kumuokoa lakini imeshindikana.”Docta aliendelea kuongea kwa huruma na upole.
Rose : “Una maaana gani imeshindikana nataka kumwona kaka yangu.”Rose alisema kwa sauti akianza kutoa machozi.
Docta : “Nataka uniahidi kuwa utakuwa mpole nikakuoneshe kaka yako.”Docta alisema kwa upole aki inuka tayari kwa ajili ya kuanza safari ya kwenda kumuona Bwana mandoto.
Rose : “Sawa.”Rose wakati huu alishindwa hata kutoa sauti.
Rose alifuatana mpaka mochwari na dactari pamoja na mfanya kazi wa mochuari. Docta alimwomba afungue kabati namba nne . Droo ilifunguliwa na mfuko wa kufunukia ulifunuliwa .
Rose : “Kakaaaa kaka jamani umeniacha kaka …”.Rose aliangua kilio baada ya kuona mwili katika droo hiyo ni kaka yake kweli aliona kama ndoto moja inayo tisha na kutesa sana alilia kwa uchungu ambao hata hauwezi kuandikika.
Upande mwingine Nickson akiwa anajiandaa kwenda kwenye mizunguko yake alikuwa pia ana sikiliza habari za asubuhi hakuamini alichokiona alimfuata Bertha moja kwa moja akamlazimisha aamke kabla ya taarifa hizo kuisha Bertha alipo ona hivyo hakuamini kuwa anaona kifo cha mumewe.
Bertha : “Mume wanguu jamani mume wangu jamani umeniacha nitabaki na nani mimi.”.Bertha alilia visivyo mfano aki mkumbatia Nickson aliekuwa akimpa matumaini kuwa yote ni maisha na ni mpango wa Mungu .Bertha hakuamini kuwa amampoteza mumewe tena aliekufa kikatili pamoja na kuwa alikuwa ni mkatili sana kwa bertha bado alimpenda hivyo hivyo .
Bertha aliamua kwenda alipo tokea kwa ajili ya kumzika aliekuwa mumewe.
Itaendelea…..
 
Well waiting next episode
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…