My soulmate .Mwenzi wa roho yangu
Sehemu ya 26.
Ndani ya ofisi ya Sambeke inc:
Braiton alitoka nje kuongea na simu ya Anitha.
Anitha : Mambo Braiton? , Mpenzi wangu!.
Braiton : Poa mambo Anitha mzima?.
Anitha : Mimi mzima lakini kwanzia juzi jumamosi sijaku ona!.
Braiton : Kwa hiyo umeanza kunichunga si ndio?.
Anitha : Hap…. ( Anitha alikatishwa na Braiton.)
Braiton : We sikia nikuambie kitu sio kila kitu ujue mimi nina shida afu unaanza kuniuliza maswali maswali kama mtoto wa secondary mie!. (Alisema kwa hasira kiasi)
Anitha : Samahani Braiton nakujulia hali tu jamani!!!.. .
Braiton :Wewe unanijulia hali au unanichunguza?. We si nshakwambia mimi mzima mambo ya kuto kuniona juzi sijui jana mimi inanihusu nini?.
Anitha : Eeeeh Basi yasiwe mambo makubwa umesema una shida!??? .
Braiton : Ndio nina shida ya pesa.
Anitha : Duh Braiton juzi juzi si nlikupa laki umepeleka wapi jamani wewe unatumia hela hovyo!.
Braiton : Kwani pesa haziiiishagi!? , au ulidhani ukinipa hiyo pesa ndo itakaaa milele. Aisee mimi nitakata simu! Unajua?.
Anitha : Basi mpenzi nakutania jamani mpenzi wangu Braiton!.
Braiton :Mimi nina shida ya elfu hamsini. Nimepata kazi mpya.. (Kabla hajaendelea alikatishwa.)
Anitha : Jaaaamani Braiton mpenzi hongera sana Jamani.. (Anitha alisema kwa furaha baada ya kusikia habari nzuri.)
Braiton : Ndo hivyo nataka nipate hela ya nauli , na hela ya kula ambayo itanisaidia mwezi huu.
Anitha : Je utani rudishia mshahara ukitoka!?.
Braiton : Yani hata sijamaliza siku mbili ushaanza kuongelea mshahara utanitia gundu sasa!.
Anitha : Haya Mpenzi wangu ntakutumia muda sio mrefu.. (Kabla Anitha hajamaliza kuongea simu ilikatwa bila hata kuagwa.)
Anitha : Helo Braiton. (Aliangalia simu akagundua imekatwa.)
Anitha : Aaaah amekata simu!.(Alisema kwa hasira!)
Baada ya kuongea na simu Anitha alianzisha maongezi na rafiki yake Rose.
Nyumbani kwao Anitha:
Rose : Nini Shida tena? . (Rose aliuliza baada ya kuona rafiki yake akikunja uso.)
Anitha : Amekata simu huyu Braiton huyu! .
Rose : Mhhh pole!. Shoga yangu!.
Anitha : Ah hiyo isiwe tabu!. Amenipa habari njema.
Rose : Habari gani shooo embu nipashe!.
Anitha : Kabla sijakwambia twende ukanisindikize kwa wakala wa kutuma hela kwenye simu!.
Rose : Twende lakini unipe huo ubuyu! Shoooo mimi tena na wewe!.
Anitha : Hahahahaahahahah We unaonekanaga mpole mtu hawezi dhania ety unapenda umbea.
Rose : We kwani upole na habari za muhimu wapi na wapi ?.
Anitha : Hahahahahahah Haaaaaallllloooooooo!. (Anitha alisema hivyo akinyanyuka kwenda kujiandaa kwa ajili ya safari yao fupi!.)
Baaada ya Dakika kadhaa Rose na Anitha walitoka nje kuelekea kwa wakala wa kutuma pesa Anitha alio ombwa na Braiton.
Anitha : Aiiiisee Shoga yangu Braiton si kapata kazi mpya.
Rose : Khaaa sasa hiyo ndo inakufanya ushobooooke!!?.
Anitha :Ndio jamani mpenzi wangu kapata kazi . Kaniomba hela ya mwezi wa kwanza elfu 50 nataka nimtumie 80 kabisa ili asiwe na shida!.
Rose : Mhhhh aisee huyu jamaaa kaku shika moyo angalia asikuchezeee.
Anitha : Hamna alini ahidi kuwa ata tulia na ata wacha uhuni wake!. Nakuhakikishia muda sio mrefu ataanza mipango ya ndoa yetu!. Ndio maana nafurahi.
Rose : Mhhh ndio alivyo kuambia?.
Anitha : Hapana lakini nilimuuliza kuhusu ndoa akasema hana kazi mahari atapata wapI?.
Rose : Ni kweli Dear na mapenzi hayaliwi! . Hivi alikuambia anataka kujipanga kwanza ama?.
Anitha : Ndio ajipange mie niolewe!.
Rose : Eeeh hongera shoga!.
Anitha : “Asante jameni!.”
Walifika dukani kwa wakala wa kutuma simu na kuzituma hela hizo kwa Braiton.Anitha alivyo ituma akamtumia ujumbe Braiton kudhibitisha kama simu imefika.
Braiton : “Imefika.”. Bariton alijibu tu hivyo na hakusema asante.
Njiani wakirudi nyumbani kwa Anitha :
Anitha : Shoga yangu unajua huyu mtu na wasiwasi nae kiasi.
Rose : Wasiwasi gani?.
Anitha : Nahisi kama Braiton sio mwaminifu sana!.
Rose : We usijipe presha bure shoga yangu. Yani wewe ngoja akuoe ndo utajua baadae!.
Anitha : Hapana Rose huyu sio mwaminifu kuna kisauti kichwani mwangu inaniambia nimwache atanitenda sema ndo hivyo nampenda.
Rose : Mhhh mpendwa we fuata moyo wako unavyosema.
Anitha : Kweli au tufanye hivi kama utakubali!.
Rose : Kufanya nini mwaya?.
Anitha : Inabidi ukubali kwanza .
Rose : Heheheheh Anitha rafiki yangu tokea utotoni ndio ulivyo . Lakini unajua wewe ndo wa ubani wangu kwayo mi ntakusaidia na lolote utakalo!.
Anitha : Enhee hapo sawa!.
Rose : Haya niambie sasa!.
Anitha : Nataka umpe majaribu Braiton.
Rose : Majaribu!!?. (Alioneshwa akishtuka na kutokuelewa!)
Anitha : Ndio majaribu ili ni pate kufahamu uaminifu wake!.
Rose : Kivipi sasa kwani mimi shetani!?
Anitha : Wewe nae haujua jua tu ni majaribu gani?.
Rose : Ndio !!!!. Mi sijajua shogaaa!.
Anitha : Wewe jifanye umempenda afu unataka kulala nae kama mpenzi wake!.
Rose : Anhaaaaa Duh! Rafki yangu mbona kazi unayo nipa ngumu hivyo?.
Anitha : Sio ngumu wewe muweke kwenye mtego afu akiangukia si unaniambia namwacha huto hitaji kulala nae ukiona anakutaka kweli una muumbua!!.
Rose : Mhh hapo ndugu yangu utakuwa umemkamata vyema hapo nakupa pongezi kwa hilo wazo!.
Anitha :Mwenzangu huyu mtu nina mjua alikuwa na tabia ya kutaka kulala na mdada yeyeote anae pita mbele yake!.
Rose : Kweli mpendwa nita kusaidia kumshika japo sio kazi ndogo au rahisi!.
Ofisi ya Sambeke:
Braiton alikuwa ana swali la kwenda kumu uliza bosi wake Bwana sambeke.
Bration aligonga mlango akaona maaajabu. Duuh Stela alikuwa amepakatwa na bwana Sambeke aki mpa mabusu ya mdomoni wakati huo Braiton anaingia hawakumsikia.
Braiton alishtuka sana asiweze kuamini macho yake ali baki aki duwa asiweze kuamini .Kuwa Stela ana uhusiano na boss wake na isitoshe alimjibu vibaya mara mwisho yamkini ana uwezo wa kuweza kumuondosha kazini ndani ya sekunde mbili tu. Ali nyata mpaka nje alifunga mlango taratibu asisikike.
Itaendelea………….