Hadithi: Mzaha wa damu

Kigongo iki,Tag muhimu sn mkuu
 
MZAHA WA DAMU 11
By CK Allan
Machozi yalinitoka wakati nikiwa namtazama Janeth akipiga hatua akiwa katika sare maalum za hospitali nilishindwa kujizuia na kusimama kumkimbilia Janeth tayari alishapewa taarifa na daktari wake na sasa nae aliponiona alinikimbilia na kisha tukakumbatiana kwa nguvu, huku kila mmoja machozi yakitoka nilifarijika sana kumuona Janeth akiwa mzima sasa Josephine alikuja kuungana na sisi na kisha tukasogea na kwenda sehemu ya kukaa, baada ya nusu saa Janeth alichangamka kabisa na alikua anauliza habari za baba na mama, na mambo mengine ya hapa na pale, hakika ilikuwa siku nzuri sana dokta matilda alikua bize akirekodi matukio kadhaa kupitia simu yake,

“kaka umekuja kunichukua, tunaondoka hapa bila shaka!” alikuwa akirudia rudia iyo kauli Janeth
“bila shaka mpenzi, leo unaruhusiwa nyumbani” alisema Dokta Matilda akitabasamu,
“sasa turudi ofisini tuangalie taratibu za utawala kisha tumalize zoezi letu” alisema Dokta matilda na kisha tukaenda ofisini ambapo alifungua kabati lake na kutoa faili la Janeth na kisha akaandika andika halafu akabonyeza bonyeza kwenye komputa yake akatutazama akitabasamu
“kwa kawaida huwa hatuna muda maalum wa kukaa na mgonjwa hapa, what matter ni hali ya mgonjwa, wapo wanaokaa wiki, mwezi , miezi, mwaka, miaka lakini tunashukuru kwa janeth yeye amekaa nasi kwa miezi 7 na nusu tu, na kwakweli hali yake imerudi kwa asilimia mia, nimetuma taarifa zake kwa daktari mkuu kwa ajili ya kuthibitisha kuruhusiwa, na muda mfupi faili lake litatumwa hapa na nitaprint kwa ajili ya kutengeneza risiti ya malipo ili muweze kuondoka na Janeth, na wewe pole sana na kwa matatizo yote, Josephine ni rafiki yangu sana na alikua akinieleza changamoto zote anazopitia’ alisema dokta Matilda huku akitazama Komputa yake na kisha akabonyeza bonyeza tena na kisha akasimama kufuata mahali ilipokuwa printa na achukua karatasi kadhaa na kisha akazisaini na kuweka mhuri wake na kuweka kwenye faili, kisha akanyanyua simu na kumuita msaidizi wake na kumpa lile faili,
“tayari sasa tusubiri risiti na kwa muda huu naomba Janeth twende sasa ukaandae mizigo yako mpenzi, mnaweza kuendelea kunisubiri dakika kadhaa” alisema akitoka na Janeth na kisha walirejea baada ya dakika kadhaa Janeth akiwa amebadili nguo za hospitali na kuvaa za kawaida na begi lake dogo mgongoni
“janeth amegoma kabisa kuchukua vitu vyake vyote, kagawa nguo, viatu, mafuta na vitu vingine kwa marafiki zake” alisema Dokta Matilda
“vizuri sana Janeth, utapata vingine mdogo wangu” nilisema nikimpongeza
Baada ya muda mfupi alirejea Yule msaidizi wa dokta Matilda akiwa na faili na kumkabidhi , alilipitia kisha akatabasamu kama ilivyokuwa kawaida yake
“jamani kiukweli kabisa niseme Janeth ameruhusiwa rasmi na kiasi ambacho mlitakiwa kulipa ni tsh 1,880,000 ambacho kimeshalipwa na mtakachofanya mkifika pale mapokezi utampa hii document pale atakupa fomu nyingine ya kujaza , niwatakie kila la kheri” alisema dokta Matilda huku tukitazamana,
“ah Dokta, sijaelewa, nani kalipia matibabu? Au ni wewe Josephine?” niliuliza kwa mshangao
“mimi nilikua nalipia chakula na malazi sio matibabu” alisema Josephine
“ah samahani nilikuwa nafikiri mnajua , chakula na malazi ukitoa ule mwezi wa kwanza ni laki 2 na nusu, na ule mwezi wa kwanza ni laki tatu, ambazo Josephine alilipa zote, matibabu haya ni dawa pamoja na vipimo na psaicho therapy ambazo hizi zinalipwa mwishoni kwakuwa inategemeana na hali ya mgonjwa, kwahiyo sasa juzi ijumaa nilipigiwa simu na mhasibu wa Hospitali kuwa kuna kiasi cha milioni mbili na nusu kimelipwa kwa ajili ya janeth mkifika pale mapokezi na hii document mtapewa mlolongo wote jinsi matibabu yalivyolipiwa na huduma zilizotolewa, kama kutakuwa na chochote tafadhali mrejee hapa” alisema dokta matilda.
Tuliondoka pale ofisini sasa nikiwaza juu ya “deni” ambalo nilikuwa nalo kwa Josephine
Tulifika mapokezi na kumkabidhi ile karatatasi Yule dada, aliisoma na kuandika andika kisha akaipiga mhuri na kunitaka kwenda kwenye chumba kingine kuipeleka hiyo karatasi
“ukinyooosha pale kushoto kama unataka kupanda ngazi kuna chumba kimeandikwa “e-burser” utawapa hiyo karatasi,” nilitoka haraka huku Josephine akiwa amebaki pale mapokezi na janeth
“ooh saini hapa broo, ni kaka yake bila shaka?” aliuliza Yule jamaa huku akiwa ananisogezea karatasi nyingine ya kusaini
“aisee kumbe kuna mlolongo hivi kutoa mgonjwa?” nilisema huku nikiwa nimechoka kidogo na zile nyaraka,
“ndio broo hususani kwa wagonjwa wa watu wakubwa kama hawa kuna usumbufu sana” alisema Yule jamaa huku akionekana nae kuchoshwa

“haya broo utarudi tena pale mapokezi utawapa hii” alisema sasa akinipa stakabadhi ya malipo niliangalia na kuisoma
“638,000/= refund, discharged for Janeth T, kikulwe”
Niliitazama na kutaka kuuliza swali lakini niliamua kwenda kule kule mapokezi na sasa nilishaanza kukerwa na ile hali yakuzunguuka kwenye zile korido za Milembe, nilimpa Yule dada kile kikaratasi kisha akanipa karatasi nyingine iliyokuwa imeshaandaliwa nikasaini kisha akanitolea bahasha
“unaweza kuhesabu kujiridhisha kaka yangu” alisema akinipa bahasha
Niliangalia na kuona ni pesa
“ah zitakuwa sawa tu , kifuatacho?” niliuliza
“ah wewe tu labda kama unataka kunipa hela ya soda!” alisema akijichetua
“ah hivyo tu?"
, nilitoa waleti yangu na kutoa elf 20 nikampa kisha nikageuka kurudi
“wewe kaka una roho nzuri sana yaani!” alisema Yule dada , sikumjali nilipiga hatua kusogea walipo akina Janeth na kutoka nje ya jengo kuelekea tulipokuwa tumepaki gari yetu
“aah gari ya baba hii!” alisema Janeth akifurahia
“ah kumbe hujaisahahu tu!” nilisema nikifungua mlango na kisha kuwafungulia na wao wakaingia
“ah Janeth hii ni yako” nilisema nikitoa ile bahasha na kumpa
‘hee pesa hii kaka yote yangu?” aliuliza akifurahia
“ndio ni pesa ambayo ulilipiwa matibabu imebaki” nilisema nikifunga mkanda
“sasa nyie watu mkae huko nyuma wote wawili” mpige story
“haha umejuaje” alisema Josephine

Safari ya kwenda Dodoma mjini ilianza na baada ya dakika kadhaa tulikuwa nje ya jengo la halmashauri ya mji, Dodoma.
“Janeth unaweza kutusubiri kwenye gari?” nilisema
Alitingisha kichwa tu kuashiria amekubali huku mimi na Josephine tukishuka na kuingia mjengoni sasa wale waliokuwa wakinifahamu walikuwa kama wanaona mzimu au mzuka ndani ya dakika kadhaa hali ya utulivu ilianza kukosekana pale mjengoni na kupelekea watu kutoka kwenye ofisi zao na baada ya dakika kadhaa nilijikuta nimezunguukwa na kijiji!, hali ilitulia ghafla wakati mkugurenzi alipokuja na kuja kunikumbatia moja kwa moja kisha akanisihi kuongozana nae kuelekea ofisini kwake na sasa na nikamuomba Josephine aendelee kuwasimulia kwa ufupi na kama tulivyokubaliana tulishatengeneza hadithi yetu nzuri ya kuvutia ambayo isingeweza kumhusisha mkuu wa wilaya!

Tuliamua kufanaya hivi kwasababu nyingi

Kwanza tuliona ndio njia nzuri ya kupunguza uzito wa jambo hili kulimaliza kwa haraka lakini pia tayari kulikua na dalili kuwa mkuu wilaya na mumewe walishawajibika katika hili na sasa ingetosha na sisi kuwaheshimu katika hilo, pili sikutaka kabisa kuingia kwenye "bifu" lolote
moyoni nilikuwa najisikia hatia kabisa kudanganya wazi wazi lakini tayari nilishafanya maamuzi
“kwahiyo ilikuwa hivyo wakati nafuata ile flash nilipigiwa simu na ndio nikatekwa na watu ambao walikuwa wanataka niwafungulie komputa ambayo walidai ilikuwa na nyaraka muhimu sana, kwanza nilijua ni komputa ya mtu binafsi lakini wakati najaribu kufungua nikaona ni komputa mojawapo ya zile za tume ya taifa ya uchaguzi maana ile logo yao ilikuwa pale, kwakuwa sasa mimi ni mtumishi wa serikali nikaona bora kukataa nikawaambia siwezi zile komputa zimefungwa kwa namba maalum na nisingeweza kufungua, wakasema wanajua ninazo password nikagoma wakanipiga sana na kunitesa na walinipeleka mpaka porini huko morogoro, na kwasababu nilishaona sura zao baadhi wakaona ni bora wanipoteze!
siku hiyo wakaniweka kwenye gunia na kunipiga sana, na kisha walinitupa porini wakidhani nimeshakufa kwa bahati niliokolewa na mkulima mmoja ambaye alinitibu mpaka nikarejea katika hali ya kawaida”

nilimaliza kutoa hadithi yangu ya uongo nusu na ukweli nusu, kisha tukaongea mambo kadhaa na mkurugenzi akanielekeza kwenda kwa afisa utumishi kuripoti. Nilimkuta tayari akinisubiri na akaniuliza kama nilikua tayari kurudi kazini
“sikia nakupa siku 14 broo,ni kama ajira mpya vile haha!” alisema kisha akanisihi kupitia barua yangu kesho yake.
“kuhusu nyumba yako, vitu vyako tuliweka kwa Adolf huyu ni Afisa Tehama mpya ambaye tulimpata kwenye hizi ajira mpya, kwahiyo vile vitu vyako vidogo vidogo nyaraka, vitambulisho n.k vyote tumeviweka kwenye sanduku moja la chuma, vitu vingine vya ndani tulimpa dogo atumie wakati akijipanga naamini hilo liko sawa kwa upande wako
 
MZAHA WA DAMU 12

By CK Allan
“Vile vile naamini ulicheki kuna miamala imepita pita kwenye akaunti yako, kiuhalisia tulipata maagizo kuwa upo kwenye matibabu kwakuwa hakuna aliyeweza kuprove kwamba umefariki na kama tulivyohisi kumbe imekuwa sawa, kwasasa kuna nyumba mpya nadhani ambayo tulipata ufadhili wa AMREF wa nyumba moja ya mtumishi iko nyuma tu hapo kama unaenda idara ya maji, kama hutajali utakaa hiyo kwa maana ndani ya wiki mbili uwe umeshafanya maandalizi, kuhusu kazi yako mpya na vitu vingine tutajua hapo ukirudi kazini” alisema afisa utumishi huku sasa akinipa mkono wa kwaheri
Nilitoka nje na kuwakuta watu kadhaa wakiwa bado wamemzunguuka Josephine na sasa walipenda kusikia kutoka kwangu
“wakuu ninarudi kazini baada ya wiki mbili, nawashukuru sana kwa maombi yenu la sivyo nisingerudi salama , tutaonana na jamani, michango ya harusi iko pale pale wale ambao bado hawajachanga!” nilisema sasa huku nikicheka!
niliwaacha watu wakiwa wamefurahi na kumshika mkono Josephine na kurudi kwenye Gari.
Tulienda mpaka mjini na kutafuta mgahawa na kuagiza chakula kisha nikampigia simu mama na baba kuwajulisha kuwa Janeth alikuwa mzima kabisa na nilikuwa narudi nae hakika ilikuwa ni siku ya furaha sana kwetu sote,
“unasemaje kuhusu Madam Cathe? Kurudi Dar bila kutoa shukrani kwake sio jambo jema!” nilisema nikimtazama Josephine
“yeah ni kweli, vile vile amuone Janeth, nadhani tumsalimie kisha kesho turudi Dar”
alisema Josephine, na baada ya kula tulitoka na kurudi tena kwenye gari tuliamua kuwasiliana nae kwanza kwakuwa tusingejua alipo kwa wakati huo na simu iliita tu bila kupokelewa, kwakuwa tayari ilikuwa mchana tuliamua kubahatisha kwenda nyumbani kwake kumsubiri

“ni wageni wake unaweza kumwambia Josephine wa Ephraim yupo kwako” nilimwambia Yule mlinzi
“na huyo kwenye gari ni nani?” aliuliza akikagua kagua gari
“ huyu ni dada Yangu” nilisema sasa nikiwa nataka kubadili mawazo
“ah msijali ndio wakati wake huu anakuja kupata chakula muda sio mrefu, ila msubiri tu hapo hapo kwenye gari” alisema Yule askari akizunguka zunguka na bunduki mkononi
Wakati tukirudi kwenye gari mimi na Josephine kwa mbali gari ya mkuu wa wilaya iilikuwa inajongea mahali tulipo na sasa tulisimama mimi na Josephine kutazama wakati gari hiyo ikiingia kwenye geti, baada ya muda mfupi tuliruhusiwa kuingiza gari ndani na sasa tukashuka na kupiga hatua ambapo madam Cathe alikuwa amepigwa na ganzi kana kwamba alikuwa ameona mzimu
‘aah ooh, we-we, ni- ni Ephraim!” alisema madam Cathe akiwa ameweka mkono mdomoni, sasa Dereva wake alipigwa na mshangao tu ,
‘ni mimi madam na huyu ni Janeth, na Josephine’ nilisema Madam Cathe akinipa mkono na kisha akasalimiana na Josephine na sasa akatukaribisha ndani kwenye jumba lake
“eeh naomba ufunguo broo” ilikua ni sauti ya mlinzi ambapo nilimrushia ule ufunguo ili apaki gari sehemu sahihi wakati sisi tukiingia ndani ya ile nyumba ya mkuu wa wilaya
‘karibu sana jamani ninyi ni wenyeji hapa!’ alisema Madam Cathe, tayari walishafika wasaidizi na kutuelekeza sehemu ya kukaa kwenye sebule kubwa iliyokuwa na samani za kisasa. Yeye alipitiliza kwenye vyumba vingine ambapo alirejea baada ya nusu saa akiwa amebadili nguo
“aah niliwaacha kidogo jamani” alisema akitutaka radhi
‘ah hakuna shida’ niliitikia kwa aibu kidogo
“haya Janeth umepona mama!? Mungu ni mwema sana” alianza madam Cathe akijechetua
“Janeth huyu ni madam Cathe, ndio amelipia matibabu yako na ile bahasha niliyokupa imetoka kwake!” nilisema sasa nikimtambulisha Janeth alisimama kwa furaha na kwenda kumpa mkono
“karibu shosti! Karibu sana” alisema madam Cathe kisha akabonyeza bonyeza simu yake na kuweka sikioni
“Njoo huku sebuleni kwa wageni” alisema kisha akakata simu
“najua leo mnataka kurudi Dar, lakini jamani naomba sana leo mlale hapa!” alisema madam Cathe akitutazama
‘Bila shaka shosti sisi leo usingizi ni hapa!” alisema Josephine wakati huo aliingia msichana mwingine rika la akina Janeth
“haya mchukue huyu Shoga yako hapa muonyeshe mazingira afurahie ila kama mtataka kutoka muombe ruhusa yangu” alisema huku Janeth akisimama kwa unyonge kidogo akimfuata Yule msichana


“huyu ni mdogo wetu wa mwisho anaitwa Angel yupo kidato cha sita nahisi wanaweza kuzoeana kwa muda” alisema Cathe akitutazama
“haya niambie Ephraim naona mzuka au mzimu?, ujue Fredi alinipigia asubuhi kuwa umefika halmashauri na nilivyoona simu ya Josephine nilijua tu mpo hapa mjini sikuweza kupokea muda ule tulikua kwenye kikao cha wilaya” alisema madam Cathe
“vipi broo hajambo?” nilisema nikitabasamu lakini madam Cathe alionyesha kustuka hivi
“ah ameondoka kurudi Dar juzi afya yake sio nzuri sana hivi mnafahamiana kwani?” aliuliza madam Cathe
“ah nilimuona kwenye picha tu ila sijawahi kukutana nae, Josephine yeye ndio anafahamiana nae!’ nilisema kwa kujiamini bila kupepesa macho
“haya sasa Ilikuwaje mume, ukapotea hivi hivi majanga gani yalikukuta” aliuliza , na bila kusita nilimhadithia ile hadithi ya uongo nusu na ukweli nusu
“ah kwahiyo unasema hao watu unawajua sura zao kabisa?” aliuliza tena
“yeah nikiwaona hivi naweza kuwatambua kwakuwa tulikaa sana kwenye gari, na hata sauti zao nazitambua wazi, lakini kwakweli kwasasa nimeamua kuendelea na maisha yangu sitaki kukumbuka yaliyopita” nilisema nikimimina Juisi nyingine kwenye glasi yangu, huku mkuu wa wilaya akiwa anashusha pumzi na kuangalia huku na huko kama anayetafuta maneno ya kuongea
“kwakweli kwa niaba ya familia yangu, Natoa shukrani za pekee kwako madam,umenisaidia sana kipindi chote na umesaidia matibabu ya Janeth lakini pia umeisadia sana familia yangu, kwa hali na mali, na hata Josephine umemsaidia sana, ndio maana tumeonasio busara kupita hapa bila kukuona” nilisema Tuliendelea na hadithi za hapa na pale na madam aliahidi kututembelea Dar akiwa na mume wake.
_____________________________________________________________
Majira ya saa tatu siku asubuhi siku iliyofuata tayari nilikuwa jengo la halmashauri kuchukua barua yangu ya kurudi kazini na kisha tulipitia kwenye kituo cha kujaza mafuta na safari ya Dar ikaanza tukiwa na Janeth na Josephine, safari ilikuwa nzuri sana na majira ya
Jioni tayari tulikuwa jijini Dar,

ilikuwa ni furaha sana kuweza kufika nikiwa na Janeth salama salimini nakumbuka baba na mama walifurahi sana na mama aliondoka na Janeth Jioni ile ile kwenda kanisani ambapo alisema Mchungaji wake alimwambia kuwa alitakiwa kwenda nae mara tu anaporejea kutoka kwenye matibabu,

Hatimaye baada ya wiki moja mimi na Josephine tulirejea Dodoma ambapo baada ya kupata nyumba ya kukaa alinisaidia kupanga vitu sawa , ilikuwa ni nyumba ya kawaida ya vyumba viwili, sebule , jiko pamoja na stoo na ilijengwa maalum kwa ajili ya mfanyakazi ambaye hakuwa na familia kubwa.
Josephine alirudi Mbeya kwa ajili ya kujiandaa kurudi kazini pamoja na kuongea na familia yake kwani kwa kipindi chote aliwasiliana nao kwa simu tu

Kwa hivi tulikubaliana yeye aende masomoni chuo kikuu cha Dodoma, na hivyo ingekuwa rahisi ya sisi kuonana na hata kukaa pamoja ikibidi, kwani hatukuwa tayari kutengana tena!
Nakumbuka siku hiyo nikiwa kazini madam Cathe alinitumia ujumbe kuwa angependa kuonana na mimi nyumbani kwake, sikuona umuhimu wa kumjulisha Josephine kuwa ningeenda kwa mkuu wa wilaya, hivyo baada ya kurudi nyumbani kwangu nilijiandaa na kutoka kuelekea yalipokuwa makazi ya mkuu wa wilaya na nilifika getini na kujitambulisha na baada ya dakika kadhaa niliruhusiwa kuingia ndani,

Tayari mkuu wa wilaya alikuwa ameshatoka akiwa amevalia suruali yake kama kawaida na tisheti juu iliyokuwa na maandishi makubwa yaliyosomeka “VISIT TANZANIA” nilimsalimia na sasa akanikaribisha kwenye bustani yake iliyokuwa pembeni ya nyumba na kisha akaagiza vinywaji baada ya maongezi mafupi aliniambia sababu ya yeye kuniita pale
“Ephraim, kwanza pole sana na matatizo yaliyokupata lakini naomba kujua jambo moja?” alisema huku akinitazama
“hao watu waliokushambulia unaweza kuwakumbuka ukiwaona?” aliuliza
“baadhi kwa wale wote waliokuwa kwenye gari naweza kuwakumbuka walikuwa wanne, wawili walikaa mbele na wawili nilikua nao siti ya nyuma,” nilisema huku nikishushia juisi taratibu, tayari nilikuwa nimeshajiapiza kuwa sitaibua hili suala tena na hivyo nilitaka kulimaliza juu kwa juu na sikupenda kamwe kumtaja mume wa madam, na hivyo kwa macho makavu kabisa nilipindisha ile hadithi yangu, “naamini hili suala limeisha kwasasa tusonge mbele!” nilisema
 
Unapatia sana
Aisee
 
MZAHA WA DAMU 13
Madam Cathe alinitazama tu huku akitoa kitambaa chake na kuanza kujifuta machozi yaliyokuwa yakimtoka,
“nisamehe kwa hili Ephraim, najua unajaribu kunificha lakini najua kila kitu, najua mume wangu ndie ambaye alikushambulia na kujaribu kukuua akidhani kuwa tulikua katika mahusiano, alisema sasa huku akitoa simu yake na kunionyesha kipande kidogo cha video kikionyesha mtu aliyekuwa katika kipigo kikali na kisha akiwa anaingizwa katika gunia
“huyu ni wewe Ephraim, alisema huku akijifuta machozi ambayo yalikua yakimtirikika, nilitumiwa hii video na usiku ule ule nilifika hadi pale ambapo walikua wamekutupa, lakini tulikuta gunia tupu! Na hata mume wangu baada ya kujua ukweli alikua anajaribu kuomba msamaha lakini akapatwa na ugonjwa ambao madaktari wanasema unasababishwa na mtu kujisikia hatia, na mbaya zaisi alikua na presha kwahiyo daktari anasema kupona itategemea miujiza ya Mungu alisema Madam Cathe huku akizidi kulia, na mimi nilijikuta machozi yakinitoka na kwa jinsi nilivyokumbuka yale mateso…
“madam yameisha! Na mimi naamini alifanya kwa ajili ya kulinda upendo wake, tafadhali tulimalize hili na mimi sina kinyongo kabisa!” nilisema
Tuliendelea na maongezi na hatimaye nikaondoka zangu kurudi kwangu.

BAADA YA MWAKA MMOJA
Tayari tulikuwa tumetoka kumpumzisha mume wa madam Cathe kwenye makazi yake ya milele, nilikumbuka maneno yake ya mwisho kwangu huku sauti yake ikiwa inakata kata, akiomba msamaha kwa kila kitu, pamoja na ubaya wote alionifanyia lakini nilijikuta machozi yakinitoka kwa hivyo niliondoka haraka pale hospitali na kesho yake asubuhi nilipata taarifa za kifo chake.

Siku hiyo nilikuwa nyumbani wakati nikiwa najaribu kumshawishi Mzee Tito wa kule porini kuwa niende kumchukua zawadi ili nikae nae Dodoma nimpeleke shule, Mzee Tito alikuwa anaelekea kukubali tatizo lilikua kwa mke wake, ambaye alikataa kata ,
Nilijaribu kuongea na Josephine akasema alikua na wazo na akirudi chuo tutalifanyia kazi.
Sikujua ni wazo gani lakini niliamini angeweza kufanya namna ili tumtoe zawadi kule kijijini kwanza tulikua tumefanikiwa kutengeneza urafiki na Zawadi na isingekuwa shida kuambatana nasi.
“sasa tunaenda wapi tena ulisema una wazo?” nilikuwa namuuliza Josephine wakati tukiwa tunakatisha mitaa kuelekea gereza kuu la Dodoma,
“tulia baba wewe si umeomba ushauri?” alisema Josephine huku akitabasamu
Sikua na jinsi zaidi ya kuendesha gari kisha tukapaki sehemu maalum na baada ya ukaguzi Josephine akaomba tuongee na mkuu wa Gereza.
“tunaomba kama kuna mfungwa mwanamke umri kati ya miaka 25 mpaka 35 hivi ambaye labda amekosa mtu wa kumlipia faini, ama mfungwa ambaye anatoka hivi karibuni na hana ndugu au rafiki yoyote akitoka hapa!” Josephine alisema baada ya salamu na mkuu wa gereza baada ya kusikia dhamira yetu alipiga simu na kumuita askari mmoja wa kike kisha baada ya kumpa maelezo aliondoka na kurudi baadae akiwa na msichana mmoja wa umri kati ya miaka 27 hivi
“kwakweli wengi ni vijana na kwa kesi yao hawa nadhani huyu anaweza kuwafaa
“ana kosa gani huyu” aliuliza mkuu wa gereza
“huyu anashtaka la kumuibia mpenzi wake shilingi laki 8” alisema Yule askari
“amehukumiwa miezi mitatu gerezani na anamaliza kifungo wiki ijayo lakini anawaambia wenzake kuwa atarudi tena gerezani maana hana sehemu ya kwenda na ni kweli maisha yake yamekuwa ya kwenda gerezani na kutoka” alisema Yule afande
“je tunaweza kuongea nae peke yetu tafadhali?” nilidakia huku nikimtazama Josephine ambaye alikubaliana na mimi kisha tukapelekwa chumba kingine Yule askari akabaki nje
“Mimi naitwa Ephraim, na huyu ni mke wangu mtarajiwa anaitwa Josephine! Sijui unaitwa nani mwenzetu!” nilisema huku nikitabasamu na kumpa mkono
“mi naitwa Furaha Jackson Mtaita” alisema
“okay Jina zuri sana”alisema Josephine nae akimpa mkono
“sasa Furaha tunaomba utusikilize, kwa makini na kisha ufanye uamuzi” alisema Josephine huku akimsogelea Yule msichana
‘tafadhali sana tunaomba tukutoe hapa! Ukaishi na sisi, kwakweli sio moja kwa moja na sisi lakini iko hivi, tuna wazazi wetu ambao kiasi ni wazee wanaishi huko morogoro kijijini

Na walikaa muda mrefu sana bila kuwa na mtoto sasa wakampata mtoto mwaka juzi juzi ana kama miaka mitano hivi sasa hivi, sasa kwakweli tunataka tumchukue Yule mtoto ili aende shule, lakini ni ngumu sana kwa wale wazee kumruhusu kwasababu wanaona kama anawapa kampani hivi, lakini pamoja na hayo mimi ndio nilikua naishi nao pale sasa nimepata kazi huku mjini hawana mtu wa kuwasaidia angalau hata kupika chakula” alisema Josephine
“kwahiyo unataka nikawe Housegirl huko kijijini kwa baba yako?” aliuliza Furaha
“Hapana,
aliongea Josephine akitabasamu!

tungetaka housegirl tungempata tu! Sisi tunataka ndugu yetu wa kukaa na sisi awe ndugu yetu kabisa! Na kila tulicho nacho kiwe chake, awe sehemu ya familia yetu, ndio maana tumekuja hapa ili kupata mtu ambaye akitoka hapa hana ndugu wala rafiki wa kumpokea huko mtaani, sisi tunahitaji mtu kama huyo!” kwa siku zote ambazo nilimfahamu Josephine sikuwahi kuona akiongea kwa hisia kama vile, na pasipo kutarajia Furaha alisimama na kumkumbatia Josephine huku machozi yakimtoka
“sijawahi kuona upendo kama huu, niko tayari!” alisema Furaha huku akizidi kumkumbatia tena Josephine
Tulitoka na kurudi tena kule kwa mkuu wa Gereza na kisha kumueleza kuwa tulikuwa tayari kuondoka na Furaha
“Hakuna shida mtajaza fomu hapa na kuacha nakala ya kitambulisho cha taifa ama leseni ama kadi ya mpiga kura na tutawaruhusu kuondoka nae kwakuwa amebakisha siku chache tu ambalo ni ndani ya wiki moja” alisema kisha Furaha akaruhusiwa kuwaaga wenzake na kisha tukamaliza taratibu zote na kutoka na Furaha,
Tulipita sokoni na kununua vyakula ambavyo tulihisi Furaha angependelea kula na kumnunulia nguo za kutosha ambapo tulipanga baada ya siku kadhaa twende kwa mzee Tito tufanye “mabadilishano” tuliendelea na maandalizi na kisha niliomba ruhusa kazini na kwakuwa Josephine alikuwa ameshamaliza mitihani yake ya chuo tuliongozana pamoja kwenda kwa mzee Tito, tukiwa njiani sasa kuelekea kwa mzee Tito baada ya kupita mjini Manyoro nilijaribu kumuuliza Furaha kuhusu historia yake

mimi na Josephine hatukuweka umakini mpaka pale Furaha alipokuwa ameendelea na stori yake
“ mama Yangu alikuwa naitwa Imelda na baba yangu aliitwa Jackson kwahiyo tulikua tunaenda Likizo Mwanza kwa Meli Ile ya mv bukoba
nilikua na miaka 13 wakati ule wakati meli ikiendelea na safari nilipotea vyumba na kuanza kuzurula huko na huko na wakati ajali inatokea niliwahi kuokolewa na mzee mmoja ambaye alinitupia kwenye mbao moja iliyokua inaelea na nikabahatika kuokolewa mwanzoni kabisa na wavuvi, baadae nilitoka nchi kavu na sikuwahi kukutana na ndugu zangu tena, na hapo ndipo maisha yangu yakaanzia mtaani, nimeishi hivyo hivyo nikitoka mji mmoja hadi mwingine na mpaka nikaenda Dodoma baada ya kushauriwa na rafiki yangu na kazi zetu zilikua ni hizo za kujiuza na kuibia wanaume” alisema Furaha kana kwamba alikua anaongea stori za kufurahisha tu,
“subiri kwanza!”, nilisema huku nikisimamisha gari , walibaki kushangaa huku mapigo yangu ya moyo yakienda kwa kasi nilipaki gari pembeni kidogo na kisha nikafungua mlango na kutoka nje
Sasa Josephine na Furaha walinifuata huku wakiniuliza sababu
“umesema kuwa mama yako aliitwa Imelda?” niliuliza nikiwa nimemshika bega
“ndio, unamjua kwani?” aliuliza Furaha
“wewe ukimuona unaweza kumkumbuka?” na mimi nilimtandika swali Furaha
“Siwezi kumsahau mama yangu, kwanza alikuwa ananitokea hadi kwenye ndoto yaani” alisema furaha, sikumjibu kitu nilielekea kwenye gari huku wakiwa bado hawaelewi na kisha nikatoa simu yangu na kumuonyesha baadhi ya picha za Imelda niliyekuwa namhisi mimi
“mama yangu yuko hai!!!!” alipiga kelele furaha, huku akilia kwa sauti

SASA
Wote tulikuwa tukilia na niliamini kabisa kila jambo lilipangwa na mwenyezi Mungu
“what a coicedence!”
alisema Josephine wakati tukirudi kwenye gari, ilibidi tumueleze wazi wazi Furaha kuwa sasa anaenda kukutana na mama yake mzazi baada ya miaka mingi!
Tulifika majira ya jioni na tuliamua kumbakisha kwenye gari kidogo Furaha na baada ya salamu ilibidi tuwaeleze ukweli kabisa na kabla hatujamaliza kuongea tayari mama Imelda alikua nje kwenye gari na sisi tukatoka haraka kumfuata kule nje na tayari Furaha nae alikuwa ametoka nje na sasa walikua wametazamana tu kama mafahali waliokuwa wamechoka kupigana!
sasa tulikuwa tunatazama tu mtanange huo na kisha kama wote walikuwa wameamrishwa walikumbatiana kwa nguvu, na kilio kilitawala huku Josephine akiwaunga mkono, Zawadi nae alikuwa analia bila kuelewa chochote!
 
MZAHA WA DAMU FINAL (sehemu ya mwisho)
Ilikuwa ni furaha isiyokuwa na kifani baada ya mama kumpata binti yake, na binti kumpata mama yake, Ilikua kama ndoto na nilikumbuka masaibu yote yaliyokuwa yamenikuta kumbe kila jambo lilikua na makusudi yake, ona sasa Kumbe tumeweza kumpata mtoto wa mama Imelda
Baada ya siku mbili tulifanikiwa kuondoka na zawadi huku tukiwaachia binti yao Furaha na hakika Furaha ilikuwa imerejea,
Hata hivyo jambo lingine la kufurahisha mzee Tito alikubali kuondoka kule kijijini na kuhamia Manyoro mjini ambapo alisema alikua na kiwanja na angeanza ujenzi muda mfupi ujao, na sisi tuliahidi kumpa ushirikiano katika ujenzi
“hapa unaweza kuweka ranchi kubwa ya wanyama na kuweka wafanyakazi kisha kuweka miradi mikubwa ya kilimo kisha wewe ukawa kule Manyoro , maisha ndio haya haya mzee Tito, na akina Zawadi hakuna ulazima waishi maisha unayoishi wewe!” nilikumbuka maongezi yetu sasa nikikanyanga mafuta kuelekea Dodoma.

Hatimaye tulipata shule nzuri kwa ajili ya Zawadi na baada ya hatua zote alianza elimu yake ya awali.

Maisha yaliendelea na hatimaye Josephine alikuwa amemaliza masomo yake na Mdogo wangu Janeth alikuwa mwaka wa pili chuo kikuu cha Dodoma katika sayansi ya komputa.
Tulikuwa tumepanga kufanya safari ya kwenda kufanya sherehe ndogo ya kufungua nyumba ya kuishi kule Mjini Manyoro kwa Mzee Tito pamoja na kuwatambulisha ndugu, kwa muda wote huo sio familia yetu wala ya akina Josephine ambaye alikua anafahamiana na mzee Tito zaidi ya kuwasiliana kwenye simu tu na siku hii tuliipanga rasmi ili waweze kukutana,
Tulifika tayari mzee Tito alikuwa ameshaandaa sehemu nzuri ya ya kutupokea, nyumba ilikuwa imekamilika kabisa,

Furaha alikuwa amebadilika kabisa, tayari alikuwa na duka lake la kuuza vipodozi pale manyoro mjini na kwa miezi sita aliyokuwa ameanza tayari alikuwa na muelekeo mzuri, hakika ilikuwa ni furaha na kila mmoja alikuwa akimshukuru Mungu kwa ajili ya wema aliokuwa amenifanyia mzee Tito ambao ulipelekea kupata binti yake na kubadili kabisa maisha yake! Na Labda maisha yangu pia!
__MWISHO

Niwashukuru watu wote kwa kufuatilia mkasa huu na uwe dedication kwa wote na hususani mpendwa wetu leadermore aliyetangulia..

Nawapenda wote na tutakuja na story ndefu zaidi ya episodes 100
ambayo sitaitaja..
Kwa yeyote anayetaka kunipa udhamini nichape kitabu angalau kimoja tu,
Ama kuwezesha hiki kipaji kiendelee kusogea basi
tunaweza kuwasiliana+255 746 266 267 (WhatsApp,call &sms)
CK Allan

"Mwisho wa mwisho jambo la msingi sio Miaka tuliyoishi kwenye maisha yetu Bali ni maisha tuliyoishi kwenye miaka yetu!!
Wabilah towfiq
 

Ndio Rasmi sasa!!
🙇🙇
 
Inaendelea kunoga!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…