Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kigongo iki,Tag muhimu sn mkuuMZAHA WA DAMU 10
By CK Allan
Nilimtazama Josephine nae akainua mabega kidogo ikiwa ishara ya kuniambia kuwa nae hajui cha kufanya,
“baba tuachane na hiyo kitu kwanza, kwasasa tujiandae na safari ya Dodoma kwanza tukamcheki Janeth naamini tunaweza kurudi nae akiwa mzima halafu tuone utaratibu wa yeye kurudia mwaka, then mimi nirudi kazini, maisha yaendelee,
Naamini hata mke wangu mtarajiwa atapenda kurejea kazini tena” nilisema nikimshika bega Josephine
“yeah ni kweli sioni haja ya kukimbizana na mkuu wa wilaya na mume wake” alisema mama
“nina wazo” Josephine aliongea kila mmoja alinyamaza ili kumsikilikiza Josephine
“mimi naamini kabisa Janeth akimuona Ephraim atakuwa mzima kabisa na tutarudi nae, na mimi na Ephraim tushughulikie mambo kadhaa ya ofisini kule , mimi nashauri baba ubaki kidogo na mama hapa mimi na Ephraim twende Dodoma”
Alisema Josephine
“yeah hata mimi nashauri hivyo, mama Pumzika mimi mwanao nimerudi mzima kabisa salama salimini”
Baba alikubaliana na mimi na sasa tulitoka mimi na Josephine kutafuta mahitaji mbali mbali ya pale nyumbani
‘twende benki Josephine nikaangalie kilichomo kwenye akaunti” nilisema sasa tukiingia kwenye benki ya NMB pale Ilala,
“habari naitwa Ephraim, nilikuwa naomba statement ya akaunti yangu ya mwaka mzima” nilisema huku nikiwa natingisha vidole vyangu
“tafadhali jaza hapa” alisema akinipa kitabu maalum cha kujaza taarifa sasa niliamini kuwa nimepona asilimia 100 baada ya kukumbuka akaunti zangu zote mbili bila shida yoyote
“zote ni za kwako?” aliuliza Yule mhudumu wa benki huku akinitazama
“ndio, kwani kuna shida?” niliuliza
“hapana, subiri pale kaka yangu” alisema Yule mhudumu sasa nilisogea alipokuwa Josephine na kukaa baada ya dakika chache nilisikia jina langu na kwenda kwa mhudumu kuchukua ile taarifa yangu
“akaunti zako hazijatumika zaidi ya miezi 10 na hivyo haziko active je unahitaji tuziactivate kwa matumizi?” aliniuliza
“aah ndio” nilisema
“tafadhali jaza hii fomu hapa, kisha saini hapa!” alisema Yule mhudumu
“tafadhali naomba uweke kiasi chochote cha pesa kwenye akaunti zako kisha baada ya nusu saa akauanti zako zitakuwa sawa, si unazo kadi zako?” aliniuliza Yule mhudumu
“ah sikumbuki kama ninazo, labda niseme tu sina!” nilisema kwakuwa mara nyingi nilikua natembea na waleti ambayo nilikuwa naweka vitambulisho na kadi zangu
“basi itakupasa kuwa na loss riport ya polisi ili upate kadi nyingine Ephraim, ila kwasasa unaweza kufanya miamala dirishani” nilienda kuweka elfu ishirini yaani elfu kumi kila akaunti pesa ambayo alinipatia Josephine, kisha tukatoka na kuzunguuka kidogo halafu tukarudi tena benki , kulikuwa na kiasi kikubwa cha pesa kwenye akaunti yangu, kwanza ilionekana mshahara wangu ulikua unaingia kama kawaida, halafu nikalipwa pesa ya likizo, lakini nilishangaa pia kuona kiasi cha milioni 6 na laki 4 kimeingizwa kama pesa ya matibabu na pia miliioni kumi na mbili ambayo ilionekana kama mkopo wa elimu kutoka sehemu ambayo sikuifahamu, kisha pesa nyingine ilikua ya mfanyakazi bora mei mosi kutoka mkurugenzi Kongwa, kwa haraka ukijumlisha na mshahara wangu nilikua na zaidi ya milioni 26 kwenye akaunti yangu Ile ya mshahara halafu
akaunti yangu nyingine ambayo ilikuwa kwa ajili ya miradi yangu na “dili” nyingine ilikuwa na milioni mbili na nusu
Niliamua kutoa zile milioni mbili huku nikiacha zile pesa kwenye akaunti yangu ya ajira kwanza kisha tukarudi nyumbani tulikubaliana na Josephine kuwa bila shaka pesa hizi zilikuwa zinatoka kwa Madam Cathe,
“kwanini sasa aweke kwenye akaunti yako na anajua haupo?” alikuwa anauliza Joephine
“ni rahisi tu mpenzi, kama wazazi wangu wangefungua kesi ya mirathi ni kwamba malipo yote yangefanyika kupitia hii akaunti kwahiyo pesa zote zingechanganyika humo ni kama yeye alikuwa ametanguliza mchango wake!” nilisema sasa nikifungua geti kuingia ndani
“vipi tukasema hawa watu leo vipi , mlienda beach?” mama aliuliza
“hapana mama tulienda kutafuta mahitaji kadhaa na vitu vidogo kwa ajili ya Janeth”
“pesa umetoa wapi mwanangu?” mama aliuliza
‘mama mshahara wangu ulikuwa unaingia kwahiyo nimetoa huko” nilisema
“unaweza kuzitoa bila kuleta shida kazini?” baba nae aliingilia kati
“hakuna shida baba ndio maana tutaenda huko Dodoma tujue kinachofuata, inabidi tuondoke kesho asubuhi mapema baba,”nilisema
“ah gari ipo mkwe wangu asipande basi, sisi tupo hatuna safari za mara kwa mara” alisema baba
“sawa itakuwa vizuri tutaongea asubuhi ngoja tuweka mizigo sawa, hivi namba ya hamza si unayo?”
“fundi?”
“ndio” nilijibu
“ndio ila gari hii nilifanya service juzi tu hata wiki bado,labda oil tu na vitu vidogo kwakuwa unaenda mbali” alisema baba
_________________________________________-
Kesho yake asubuhi na mapema sasa tulikua tayari kutoka, nilimuachia kiasi kadhaa cha pesa baba huku nikimtania
“ubaki na mrembo wako hapo na mimi naondoka na wangu, mtakodi tax mkiwa mnaenda kanisani’ nilisema huku tukiondoka mimi na Josephine
Nilimpigia hamza kisha tukapitia kwenye gereji yake na kurekebisha vitu muhimu halafu safari ikaanza kuelekea Dodoma,
Safari ilikuwa njema nzuri sana mimi na Josephine tuliongea mengi sana huku tukikumbushana mambo yote mazuri tuliyokuwa tumefanya pamoja kipindi kile tukiwa katika mahaba mazito
“najihisi nimezaliwa upya Ephraim, yaani naona tu tuishi hivi hivi bila ndoa yaani” alisema sasa Josephine wakati tukitoka katika mgahawa mmojawapo uliokuwa kando ya njia tukielekea Dodoma,
Tulifika Dodoma majira ya jioni na kama tulivyopanga hatukutaka kuonekana tulitafuta lodge karibu na Hospitali ya Milembe na kuweka mizigo yetu chumbani
“usiku huu utakuwa mrefu au mfupi sana kwetu?” Josephine aliniuliza akijifunga taulo kuelekea bafuni kuoga
“otea!” nilisema nikijilaza Kitandani
“kwahiyo hutaki kuoga na mimi?” Josephine aliongea kutokea bafuni
“mi sina mpango wa kuoga leo!” nilisema huku nikisimama wima haraka kutoka pale kitandani na kuvua nguo kisha nikavuta taulo na kusukuma mlango wa bafuni.
Saa mbili na nusu tayari tulikuwa tumeshajiandaa na sasa tulikuwa kwenye gari kwenda hospitali , tayari Josephine alikuwa ameshawasiliana na Dokta Matilda ambaye ndie alikuwa daktari wa Janeth na tulifika na kumkuta akiwa tayari mapokezi akitusubiri.
‘hello huyu ni Ephraim bila shaka” alisema Yule daktari kwa uso wa bashasha
“ndio ni yeye na Bila shaka huyu ni Matilda” nami nilisema nikimpa mkono
“hakika, kwakweli Mungu ni mwema sana haya twendeni huku” alisema Matilda huku tukipiga hatua kuelekea ofisini kwake,
“tumechati sana na Josephine na kwakweli Alikuwa anakuja hapa kila mwezi kumtembelea Janeth, tatizo kubwa ambalo linamsumbua Janeth ni depression ambayo inamfanya kuwa na mawazo kupitiliza, na kama ujuavyo hakuna dawa ya moja kwa moja isipokuwa ni kumpa maneno ambayo yatamfanya mgonjwa kukubali hali halisi na kuamua kuanza upya, ama changamoto yenyewe iliyokuwepo kwa mgonjwa kutatuliwa, hii inatokea kwa watu wengi mfano, mtu anapohukumiwa kifungo gerezani , mtu anapofilisika kwa ghafla, mtu kufiwa na mpendwa wake, ama kuvunjika kwa mapenzi n.k” Dokta matilda alikuwa anatupa maelezo yake
“kwahiyo Janeth anaweza kuwa mzima kabisa?” niliuliza
“sio kuwa mzima tu bali hata kurudi shuleni na kuendelea na masomo yake, na nikueleze Tu Janeth anaendelea vizuri sana hebu angalia hapa,
Hapa ni wakati ambapo tunampokea Janeth mwaka jana., angalia hapa na hii ni jana tu wakati natoka kumjazia ripoti yake ya mwisho wa juma” alisema huku sasa akitugeuzia komputa yake kuangalia zile picha mjongeo za Janeth katika matukio mbali mbali,
“ijumaa walikuja hapa walimu wa Janeth na wanafunzi kadhaa huwezi kuamini Janeth aliwatambua wote kwa majina yao, na aliwasindikiza hadi getini akiwa na nesi” alisema sasa dokta akitueleza,
Na sasa tulienda katika eneo maalum kumsubiri Janeth aletwe, baada ya robo saa nilimuona Janeth akiwa pamoja na dokta matilda wakijongea sehemu tulipo
Unapatia sanaMZAHA WA DAMU 11
By CK Allan
Machozi yalinitoka wakati nikiwa namtazama Janeth akipiga hatua akiwa katika sare maalum za hospitali nilishindwa kujizuia na kusimama kumkimbilia Janeth tayari alishapewa taarifa na daktari wake na sasa nae aliponiona alinikimbilia na kisha tukakumbatiana kwa nguvu, huku kila mmoja machozi yakitoka nilifarijika sana kumuona Janeth akiwa mzima sasa Josephine alikuja kuungana na sisi na kisha tukasogea na kwenda sehemu ya kukaa, baada ya nusu saa Janeth alichangamka kabisa na alikua anauliza habari za baba na mama, na mambo mengine ya hapa na pale, hakika ilikuwa siku nzuri sana dokta matilda alikua bize akirekodi matukio kadhaa kupitia simu yake,
“kaka umekuja kunichukua, tunaondoka hapa bila shaka!” alikuwa akirudia rudia iyo kauli Janeth
“bila shaka mpenzi, leo unaruhusiwa nyumbani” alisema Dokta Matilda akitabasamu,
“sasa turudi ofisini tuangalie taratibu za utawala kisha tumalize zoezi letu” alisema Dokta matilda na kisha tukaenda ofisini ambapo alifungua kabati lake na kutoa faili la Janeth na kisha akaandika andika halafu akabonyeza bonyeza kwenye komputa yake akatutazama akitabasamu
“kwa kawaida huwa hatuna muda maalum wa kukaa na mgonjwa hapa, what matter ni hali ya mgonjwa, wapo wanaokaa wiki, mwezi , miezi, mwaka, miaka lakini tunashukuru kwa janeth yeye amekaa nasi kwa miezi 7 na nusu tu, na kwakweli hali yake imerudi kwa asilimia mia, nimetuma taarifa zake kwa daktari mkuu kwa ajili ya kuthibitisha kuruhusiwa, na muda mfupi faili lake litatumwa hapa na nitaprint kwa ajili ya kutengeneza risiti ya malipo ili muweze kuondoka na Janeth, na wewe pole sana na kwa matatizo yote, Josephine ni rafiki yangu sana na alikua akinieleza changamoto zote anazopitia’ alisema dokta Matilda huku akitazama Komputa yake na kisha akabonyeza bonyeza tena na kisha akasimama kufuata mahali ilipokuwa printa na achukua karatasi kadhaa na kisha akazisaini na kuweka mhuri wake na kuweka kwenye faili, kisha akanyanyua simu na kumuita msaidizi wake na kumpa lile faili,
“tayari sasa tusubiri risiti na kwa muda huu naomba Janeth twende sasa ukaandae mizigo yako mpenzi, mnaweza kuendelea kunisubiri dakika kadhaa” alisema akitoka na Janeth na kisha walirejea baada ya dakika kadhaa Janeth akiwa amebadili nguo za hospitali na kuvaa za kawaida na begi lake dogo mgongoni
“janeth amegoma kabisa kuchukua vitu vyake vyote, kagawa nguo, viatu, mafuta na vitu vingine kwa marafiki zake” alisema Dokta Matilda
“vizuri sana Janeth, utapata vingine mdogo wangu” nilisema nikimpongeza
Baada ya muda mfupi alirejea Yule msaidizi wa dokta Matilda akiwa na faili na kumkabidhi , alilipitia kisha akatabasamu kama ilivyokuwa kawaida yake
“jamani kiukweli kabisa niseme Janeth ameruhusiwa rasmi na kiasi ambacho mlitakiwa kulipa ni tsh 1,880,000 ambacho kimeshalipwa na mtakachofanya mkifika pale mapokezi utampa hii document pale atakupa fomu nyingine ya kujaza , niwatakie kila la kheri” alisema dokta Matilda huku tukitazamana,
“ah Dokta, sijaelewa, nani kalipia matibabu? Au ni wewe Josephine?” niliuliza kwa mshangao
“mimi nilikua nalipia chakula na malazi sio matibabu” alisema Josephine
“ah samahani nilikuwa nafikiri mnajua , chakula na malazi ukitoa ule mwezi wa kwanza ni laki 2 na nusu, na ule mwezi wa kwanza ni laki tatu, ambazo Josephine alilipa zote, matibabu haya ni dawa pamoja na vipimo na psaicho therapy ambazo hizi zinalipwa mwishoni kwakuwa inategemeana na hali ya mgonjwa, kwahiyo sasa juzi ijumaa nilipigiwa simu na mhasibu wa Hospitali kuwa kuna kiasi cha milioni mbili na nusu kimelipwa kwa ajili ya janeth mkifika pale mapokezi na hii document mtapewa mlolongo wote jinsi matibabu yalivyolipiwa na huduma zilizotolewa, kama kutakuwa na chochote tafadhali mrejee hapa” alisema dokta matilda.
Tuliondoka pale ofisini sasa nikiwaza juu ya “deni” ambalo nilikuwa nalo kwa Josephine
Tulifika mapokezi na kumkabidhi ile karatatasi Yule dada, aliisoma na kuandika andika kisha akaipiga mhuri na kunitaka kwenda kwenye chumba kingine kuipeleka hiyo karatasi
“ukinyooosha pale kushoto kama unataka kupanda ngazi kuna chumba kimeandikwa “e-burser” utawapa hiyo karatasi,” nilitoka haraka huku Josephine akiwa amebaki pale mapokezi na janeth
“ooh saini hapa broo, ni kaka yake bila shaka?” aliuliza Yule jamaa huku akiwa ananisogezea karatasi nyingine ya kusaini
“aisee kumbe kuna mlolongo hivi kutoa mgonjwa?” nilisema huku nikiwa nimechoka kidogo na zile nyaraka,
“ndio broo hususani kwa wagonjwa wa watu wakubwa kama hawa kuna usumbufu sana” alisema Yule jamaa huku akionekana nae kuchoshwa
“haya broo utarudi tena pale mapokezi utawapa hii” alisema sasa akinipa stakabadhi ya malipo niliangalia na kuisoma
“638,000/= refund, discharged for Janeth T, kikulwe”
Niliitazama na kutaka kuuliza swali lakini niliamua kwenda kule kule mapokezi na sasa nilishaanza kukerwa na ile hali yakuzunguuka kwenye zile korido za Milembe, nilimpa Yule dada kile kikaratasi kisha akanipa karatasi nyingine iliyokuwa imeshaandaliwa nikasaini kisha akanitolea bahasha
“unaweza kuhesabu kujiridhisha kaka yangu” alisema akinipa bahasha
Niliangalia na kuona ni pesa
“ah zitakuwa sawa tu , kifuatacho?” niliuliza
“ah wewe tu labda kama unataka kunipa hela ya soda!” alisema akijichetua
“ah hivyo tu?"
, nilitoa waleti yangu na kutoa elf 20 nikampa kisha nikageuka kurudi
“wewe kaka una roho nzuri sana yaani!” alisema Yule dada , sikumjali nilipiga hatua kusogea walipo akina Janeth na kutoka nje ya jengo kuelekea tulipokuwa tumepaki gari yetu
“aah gari ya baba hii!” alisema Janeth akifurahia
“ah kumbe hujaisahahu tu!” nilisema nikifungua mlango na kisha kuwafungulia na wao wakaingia
“ah Janeth hii ni yako” nilisema nikitoa ile bahasha na kumpa
‘hee pesa hii kaka yote yangu?” aliuliza akifurahia
“ndio ni pesa ambayo ulilipiwa matibabu imebaki” nilisema nikifunga mkanda
“sasa nyie watu mkae huko nyuma wote wawili” mpige story
“haha umejuaje” alisema Josephine
Safari ya kwenda Dodoma mjini ilianza na baada ya dakika kadhaa tulikuwa nje ya jengo la halmashauri ya mji, Dodoma.
“Janeth unaweza kutusubiri kwenye gari?” nilisema
Alitingisha kichwa tu kuashiria amekubali huku mimi na Josephine tukishuka na kuingia mjengoni sasa wale waliokuwa wakinifahamu walikuwa kama wanaona mzimu au mzuka ndani ya dakika kadhaa hali ya utulivu ilianza kukosekana pale mjengoni na kupelekea watu kutoka kwenye ofisi zao na baada ya dakika kadhaa nilijikuta nimezunguukwa na kijiji!, hali ilitulia ghafla wakati mkugurenzi alipokuja na kuja kunikumbatia moja kwa moja kisha akanisihi kuongozana nae kuelekea ofisini kwake na sasa na nikamuomba Josephine aendelee kuwasimulia kwa ufupi na kama tulivyokubaliana tulishatengeneza hadithi yetu nzuri ya kuvutia ambayo isingeweza kumhusisha mkuu wa wilaya!
Tuliamua kufanaya hivi kwasababu nyingi
Kwanza tuliona ndio njia nzuri ya kupunguza uzito wa jambo hili kulimaliza kwa haraka lakini pia tayari kulikua na dalili kuwa mkuu wilaya na mumewe walishawajibika katika hili na sasa ingetosha na sisi kuwaheshimu katika hilo, pili sikutaka kabisa kuingia kwenye "bifu" lolote
moyoni nilikuwa najisikia hatia kabisa kudanganya wazi wazi lakini tayari nilishafanya maamuzi
“kwahiyo ilikuwa hivyo wakati nafuata ile flash nilipigiwa simu na ndio nikatekwa na watu ambao walikuwa wanataka niwafungulie komputa ambayo walidai ilikuwa na nyaraka muhimu sana, kwanza nilijua ni komputa ya mtu binafsi lakini wakati najaribu kufungua nikaona ni komputa mojawapo ya zile za tume ya taifa ya uchaguzi maana ile logo yao ilikuwa pale, kwakuwa sasa mimi ni mtumishi wa serikali nikaona bora kukataa nikawaambia siwezi zile komputa zimefungwa kwa namba maalum na nisingeweza kufungua, wakasema wanajua ninazo password nikagoma wakanipiga sana na kunitesa na walinipeleka mpaka porini huko morogoro, na kwasababu nilishaona sura zao baadhi wakaona ni bora wanipoteze!
siku hiyo wakaniweka kwenye gunia na kunipiga sana, na kisha walinitupa porini wakidhani nimeshakufa kwa bahati niliokolewa na mkulima mmoja ambaye alinitibu mpaka nikarejea katika hali ya kawaida”
nilimaliza kutoa hadithi yangu ya uongo nusu na ukweli nusu, kisha tukaongea mambo kadhaa na mkurugenzi akanielekeza kwenda kwa afisa utumishi kuripoti. Nilimkuta tayari akinisubiri na akaniuliza kama nilikua tayari kurudi kazini
“sikia nakupa siku 14 broo,ni kama ajira mpya vile haha!” alisema kisha akanisihi kupitia barua yangu kesho yake.
“kuhusu nyumba yako, vitu vyako tuliweka kwa Adolf huyu ni Afisa Tehama mpya ambaye tulimpata kwenye hizi ajira mpya, kwahiyo vile vitu vyako vidogo vidogo nyaraka, vitambulisho n.k vyote tumeviweka kwenye sanduku moja la chuma, vitu vingine vya ndani tulimpa dogo atumie wakati akijipanga naamini hilo liko sawa kwa upande wako
Kazi nzuri master. Keep it up 👊👊
Shusha ya kulalia mkuuAs usual tunaenda Hadi mwisho hakuna arosto
Mbona kama story imeganda, au simu yangu mbovu?
As usual tunaenda Hadi mwisho hakuna arosto
MZAHA WA DAMU 01
by CK Allan 0746 266 267
“Baba njoo uone amefumbua macho yake! Ameamka! Baba Njoo!” ilikua ni sauti ya mtoto mdogo wa kike ambaye alikuwa akikimbia kutoka nje
Nilijaribu kukaa lakini sikuweza kabisa, mwili wangu ulikua unauma kila sehemu, kila kiungo nilihisi maumivu makubwa sana, nilijaribu kufungua mdomo lakini sikuweza, na sasa nilijaribu kunyanyua mkono, nilijikuta nikiishiwa nguvu!, mikono yangu yote ilikuwa imefungwa vitu vizito na sikuweza hata kujigeuza,
Wakati nikiendelea kujigeuza ghafla niliona mwanaume mmoja akiingia kwa haraka
“ohh Asante Mungu,nilisema mimi hakufa huyu! Nilisema mimi ataamka!” alisema yule mzee kwa haraka akimkumbatia Yule mtoto wake,
“Zawadi, kimbia haraka kamuite mama mwambie unko amezinduka!” alisema sasa Yule mzee huku Yule binti akitoka mbio, niliendelea kuduwaa sana!
Yule mzee alinisogelea huku akitabasamu na kisha akaniinua na kunigeuza upande wa pili ambapo sasa nilijisikia afadhali kidogo na ndipo nikashuhudia majeraha kadhaa mwilini mwangu, kwa ufupi ni kama mtu aligongwa na gari, ama kupondwa pondwa na mawe
Nilijikuta naishiwa nguvu na kufumba macho yangu kujaribu kukumbuka chochote
Nilijikuta sikumbuki chochote na kadri nilivyojilazimisha kufikiri ndivyo maumivu yalizidi
“ah usijali utapona kabisa kijana wangu, utapona kabisa, utapona kabisa!” alisema Yule mzee huku akifungua chupa moja iliyokuwa mkononi mwake na kuweka kwenye kijiko huku akinilisha mdomoni,
Ndipo sasa nikahisi maajabu mengine mwilini mwangu, ndioo
Ladha!, sikusikia ladha yoyote mdomoni mwangu na hivyo sikuweza kujua ni aina gani ya kitu nalishwa!
“loh!” nimekuwaje?
“imekuwaje?’ nilijiuliza maswali mengi bila majibu
Ni wakati huo huo sasa Yule mzee alitoka nje ya kile chumba na kisha baada ya muda aliingia akiwa na mwanamke pamoja na yule mtoto, nilijaribu kukadiria umri wao ulikuwa kama miaka 55 au 60 hivi,
“oooh jamani, Mungu ni mwema! Ooh jamani, kijana wa watu jamani, jamani, jamani!” Yule mama sasa aliongea akinishika nywele zangu kichwani huku machozi yakimtoka
“ah kwa.. kwa… kwa… ni… ah” nilijaribu kuongea lakini mdomo hakuweza kabisa kunyanyuka
Ni kama taya zangu hazikuwa sawa, ni kama taya ya juu ilirudi chini na ya juu ikarudi chini..
“ooh umesemaje! Umeongea!” Yule mzee alishikwa na mshangao mpaka akaangusha chupa yake huku mke wake nae akisimama kwa mshangao!
“ameongea!, ameongea!” walijikuta wakisema kwa pamoja huku wakikumbatiana kwa furaha!
Sasa nilielewa kumbe kuna tatizo kubwa zaidi ya hata hili nililokuwa nafikiria,
Kwa maana hiyo hata kuongea kwangu kumewashangaza sana kama sio kuwafurahisha!
“sasa pumzika kijana! Utapona tu!” alisema Yule mama huku akitoka
“mimi nabaki na anko, mama!” alisema Yule mtoto huku akisogeza kiti na kukaa pale kitandani
“mama yangu alisema umekufa! Lakini baba akasema hujafa, utaamka, baba yangu ndie aliyekuleta ….’
“zawadiii muache anko alale kwanza utamuongelesha baadae!” aliita Yule mama na yule mtoto akaondoka zake
Baada ya wiki moja sasa maumivu yalipungua kwa baadhi ya sehemu za mwili na niliweza hata kujigeuza kitandani pasi na kuwa na msaada, ingawa bado mdomo ulikua hauwezi kunyanyuka na sikuweza kutamka maneno yaliyonyooka,
“tutaangalia namna ya kukufungua huu mkono mmoja kwanza wa kulia maana ni kama umeanza kupona hivi” alisema Yule mzee akinyanyua mkono wangu na kweli maumivu yalikua yamepungua kabisa.
Kesho yake Yule mzee alinifungua vile vipande vya miti ambavyo vilikuwa vimewekwa kwe mkono wangu kwa uangalifu mkubwa kisha akatoa kama mafuta Fulani hivi akaweka kwenye mikono yake na kisha akaanza kuuvuta kunyoosha pole pole,
Nilisikia maumivu makali sana , na kuhisi kama mkono unataka kunyofolewa, lakini Yule mzee aliendelea tu huku nikizidi kupiga kelele Yule mama alishindwa kujizuia alitoka nje, Yule mzee aliendelea tu kana kwamba alikua kiziwi, alipaka yale mafuta na kuendelea kuunyoosha na kadri alivyokuwa akiendelea sasa maumivu yalipungua, na hatimaye yakakaacha kabisa
“loh, huyu mzee mchawi nini!”
niliwaza sasa nikimkodolea macho
Aliniachia ule mkono kisha akanitaka kujaribu kukunja vidole
Vidole vvyote vilikua vinajikunja isipokuwa kidole cha mwisho kidogo
Ambacho kiligoma kabisa
“sasa fanya mazoezi, kumbuka unapona haraka, lakini utapona haraka zaidi kama utaendelea kufanya mazoezi” alisema Yule mzee akifunga zile chupa zake akatoka nje.
Hata mimi nilitaka kupona haraka ili nijue hasa kitu gani kilinitokea, kwa uhalisia sikukumbuka chochote, hata jina langu pia! Hakika sikuelewa kitu gani kinatokea katika maisha yangu, je nilipata ajali? Nilivamiwa na majambazi? Au nilikuwa mwanajeshi nimetoka vitani? Nilishambuliwa kwa bomu? Je hapa nipo wapi? Hawa wanaonihudumia ni akina nani?
Nilijiuliza maswali mengi sana yasiyokuwa na majibu nikajikuta machozi yakinitiririka tu, kila nilivyokuwa nawaza ndivyo ambavyo machozi yalikuwa yanatoka hata hivyo jambo moja ambalo nilikua na uhakika nalo ni kuwa hawa watu walikuwa wamejitolea kunisaidia kwa hali zao na mali zao pengine na kila kitu walichokuwa nacho, je nimekuwapo hapo kwa muda gani? Wiki, miezi, miaka? Nilitamani sana kujua
Nilikumbuka mzee alinihakikishia kuwa ningepona kabisa na kurudi katika hali yangunya kawaida sasa nilisubiri kwa hamu siku hiyo, siku ambayo ningesimama kwa miguu yangu siku ambayo nitaongea kwa kinywa changu, siku ambayo nitaongea kila kitu, siku ambayo nitasimulia kila kitu kilichonikuta na kila kitu kuwa hadharani.."
“ooh usiwaze sana kijana wangu, nakuhakikishia umeshapona, kesho tunafungua mkono mwingine na mguu mmoja” alinikatisha Yule mzee katika mawazo yangu
Nilitingisha kichwa tu kukubaliana nae huku moyoni mwangu nikitoa shukrani za dhati kwa mzee huyu.
Kesho yake asubuhi na mapema mzee alinifungua mkono wa kushoto pamoja na mguu wa kulia, na sasa mikono yangu ilikuwa huru na niliweza kuikutanisha tena pamoja kwa mara kwanza , pamoja na maumivu makali niliyosikia lakini niliona ni bora kuwa katika hali ile kuliko kurudishiwa ile mizigo ya miti, na hivyo nilijikaza kweli kweli, wakati mwingine nilijifanya kutabasamu wakati mzee alipokuwa akinihudumia lakini ningeugulia maumivu makali wakati mzee akiwa ametoka, hata hivyo ilikua afadhali nilikua naweza kuona mguu wangu, pamoja na mikono yangu ikiwa huru, nakumbuka siku ile nililala nikiwa na furaha sana, usiku ule niliota ndoto za ajabu ajabu na mara kadhaa nilistuka na kuamka, sikukumbuka kama niliwahi kuota ndoto kadhaa kwa muda wote nikiwa pale kitandani kama siku Ile!
hata hivyo maumivu yalikua yakipungua kabisa na kesho yake asubuhi niliweza kujigeuza na kukaa kitandani mwenyewe huku nikifanya mazoezi ya kukutanisha mikono na kuinyoosha, bado mdomo haukuweza kutoa maneno ya kueleweka ingawa nilijitahidi kabisa kuhakikisha yanatoka
Baada ya mwezi mmoja hivi ....
niliweza kusimama na kuchechemea na kutoka nje kutazama jua na kurudi ndani, sio hivyo tu bali niliweza kushika kikombe cha uji na kunywa mwenyewe, sasa ningeweza kutoka kwa kuchechemea kuzunguuka nyumba kisha ningerudi ndani bila kuwa na msaada wowote, na nilikuwa naelewa mazingira yale niliyokuwepo yalikua maeneo ya porini kabisa na sikuweza kuona nyumba yoyote zaidi ya shamba kubwa ambalo limezunguuka ile nyumba, pamoja na hayo kulikua na uzio wa seng’eng’e ambao ulizunguushiwa nyumba yote, pamoja na kuwa nyumba hii ilikua porini lakini ilikua imejengwa kisasa kwa mbao imara na kwa namna ya ujenzi wa Kijerumani hivi, na kisha kulikua na umeme wa jua ambao ulileta mwangaza katika nyumba hii, mzee huyu pia alikua na piki piki yake aina ya watco ambayo alitumia mara kadhaa kwenda kuchukua mahitaji mbali mbali...
Siku hiyo alikuja Yule mzee akiwa na furaha sana alikuja na kiboksi kidogo hivi na kukifungua kilikuwa na vidude vya plastiki hivi na kisha akanitaka niweke mdomoni na kingine nikafunga kwa juu kwenye kidevu,
Aliniambia natakiwa kuvaa kila siku labda nivitoe tu wakati wa kula tu!
, ni kweli vifaa vile vilikua vinavuta taya zangu na kuweka mdomo katika hali ya kawaida na nikaanza kutoa maneno mawili , matatu, sentensi na hatimaye ndani ya mwezi mmoja mwingine nikaweza kabisa kuongea ingawa kwa pole pole hatua kwa hatua lakini niliweza kufanya mazungumzo kabisa na kueleweka, hakika Mungu ni mwema sana na hatimaye nilikua naelekea kupona kabisa na sasa niliweza kutambua jina la wenyeji wangu hawa yaani mzee Tito na mkewe Imelda, hakika walikuwa ni watu wema sana hawa watu,
Hata kama walikuwa wameshiriki kwa namna yoyote kunifanya hivi nilivyo bado ningeweza kuwasamehe kabisa makosa yao kwa jinsi walivyonihudumia kwa namna ya pekee na kunijali kabisa bila shaka kuna mengi zaidi nataka kujua kuhusu watu hawa, hata hivyo kwasasa nilikuwa na jambo moja tu,
Mimi ni nani na nimetokea wapi? Na kwanini niko hivi nilivyo leo? Wakati mwingine nilikuwa naogopa hata kumuuliza mzee Tito kuhusu asili yangu
“isije kuwa Mzee Tito na mama Imelda ndio wazazi wangu mimi! , halafu nikawauliza kuhusu hili jambo nikazidi kuwatia simanzi” yalikuwa ni mawazo katika hisia zangu,
Hata hivyo sikuwa na namna nyingine zaidi waswahili walisema njia rahisi ya kujua jambo ni kuuliza, na mimi sikuwa na njia nyingine isipokuwa kuuliza, kwahiyo nilisubiri mpaka kuhakikisha mwili wangu umeimarika kabisa ili niweze kuanzisha safari nyingine ya kujitambua!
Inaendelea kunoga!!!MZAHA WA DAMU 02
By CK Allan
Nilikuwa nimeshatimiza zaidi ya miezi miwili na nilikua natembea bila fimbo ya kuegemea na wakati mwingine ningeweza hata kufanya kazi ndogo ndogo vidonda vikubwa vilishapona na hata vile vidude vya kuweka mdomoni nilikuwa siweki tena, niliweza kunyoosha mikono yote na miguu isipokuwa sikuweza kuinama walau kugusa miguu, mgongo ulikataa kabisa,
Na hata wakati najitazama kwenye kioo niliweza kuona makovu makubwa usoni,
“nilipatwa na nini!”
nilikua nikijisemea kila wakati nilipokuwa najitazama kwenye kioo
Siku hiyo baada ya chakula cha usiku sasa nilivunja ukimya na kuomba mzee Tito anisimulie kila kitu kuhusu mambo yote yaliyonitokea nakumbuka mzee Tito alistuka hivi na kisha akamtazama mkewe ambaye alitingisha kichwa tu kuashiria kuwa mzee Tito aendelee kunisimulia kila kitu, na bila kusita mzee Tito akaanza,
Kunielelezea kama ifuatavyo
OCKOBA 15, 2019
Siku hiyo nilitoka hapa nyumbani kuelekea sokoni kuchuka mahitaji ya hapa ndani, wakati huo nilipanga pia kupitia dukani kuuliza baadhi ya dawa kwa ajili ya mazao yangu hapa shambani, kwa kawaida huwa natoka alfajiri sana na huwa naendesha piki piki kwa masaa zaidi ya matatu mpaka kufika barabara kuu ya lami ambapo ni mji mkubwa tu wa Manyoro, nikifika Manyoro kuna rafiki yangu mmoja ambae naacha piki piki yangu pale kwake kisha nasubiri basi ambalo linatoka Gairo kwenda Morogoro ambapo nafanya manunuzi na mahitaji yangu mengine kisha nalala asubuhi yake nageuza nalo mpaka Manyoro nachukua piki piki yangu narudi nyumbani, na kama nitakuwa na mizigo mingi basi naiacha kwa Yule rafiki yangu kisha nabeba kidogo kidogo kwa piki piki kama ujuavyo hapa hakuna usafiri wowote zaidi ya piki piki yangu,
Sasa kwanini tunaishi huku porini na kwanini tupo wenyewe na mambo mengine kuhusu sisi haya tutazungumza baadae!
Kwasasa nikueleze namna tulivyokutana!
Basi siku hiyo ya tarehe 15 mtoto wetu zawadi alikua hajisikii vizuri sana kama ujuavyo watoto wanakuwa na magonjwa mbali mbali, nilienda mjini kutafuta mahitaji na ilinibidi kufanya niwezavyo nirejee siku ile ile, niliwahi kufika Manyoro na kupata usafiri na majira ya saa 9 mchana nikawa nisharejea Manyoro tayari kabisa kurudi huku porini kwetu
Bahati mbaya siku hiyo sikumweleza mwenyeji wangu kuwa nitarudi siku ile ile hivyo akatumia usafiri wangu kwenda kijiji cha jirani na akakawia kurudi, bahati mbaya tena wakati anarejea tu kukawa na pancha ndogo kwenye tairi ya nyuma,
Mwenyeji wangu alinisihi sana kulala siku ile maana mpaka tunamaliza kutengeneza piki piki ilikua ni saa moja kasoro usiku, hata hivyo ilibidi kumueleza hali halisi ya mgonjwa wangu niliyemuacha nyumbani na hivyo baada ya kumshinikiza sana na kumsihi akaomba nipunguze mizigo na niondoke na kijana wake wa kiume ili anisindikize na kesho asubuhi nimrudishe na nirejee na mizigo mingine,
Nisingeweza kukataa, ukilinganisha kutembea katika msitu mnene na chombo cha moto usiku ukiwa mzee kama mimi halafu tena usiku, isingekuwa busara, hivyo nikakubali kuondoka na Yule kijana na nikamuachia jukumu la kuendesha piki piki na tukaianza safari yetu saa moja huku giza likiwa limeingia, na kwakuwa tulikua na mizigo hatukwenda kasi sana, tulikua tunafuata barabara ya vumbi ambayo haikutumika sana na iliishia kwenye shamba la mkonge na mara nyingi magari yaliyopita huko ni yale ya kampuni tu kubeba mkonge, baada ya hapo tunaingia kwenye njia ya kawaida ambayo ni hii inayokuja hapa nyumbani, hata hivyo wakati tunakaribia kumaliza lile shamba la mkonge tulipishana na gari ambalo lilikua na mwendo mkali, nakumbuka ilibidi kusogea pembeni ili kulipisha, na kisha tukaendelea na safari tararibu huku tukipiga hadithi za hapa na pale, ni wakati tumepita kabisa lile shamba mara ghafla mbele yetu tukaona gunia lililoonyesha kufungwa vizuri sana!
kwa kuwa barabara ilikua nyembamba sana hatukuwa na namna isipokuwa kusimama na kulisogeza pembeni ili tupite, wakati tunafika na kulikagua sasa tuliona damu zikiwa zinachuruzika pembeni,
“babu itakua mboga hii wale jamaa wameangusha labda ni wawindaji” alisema Yule kijana kwa maana ya kushawishi tufungue lile gunia, hivyo tukapaki pembeni na kufungua,
Lahaulaaa wakati tunakata zile kamba sasa wote tulipigwa na bumbuwazi baada ya kushuhudia mwili wa binadamu ukiwa katika hali ile,
Mzee Tito sasa alitulia kidogo kama anayetafuta maneno ya kusema, huku akiniangalia usoni na kisha akamtazama mkewe kana kwamba anauliza aendelee ama la,na kisha akaendelea
Kwahiyo tukatoa lile gunia na kujaribu kusikiliza mapigo ya moyo na tukashangaa sana kuona bado kulikua na uhai!
Kwa dakika kadhaa tulikaa kimya tusijue tufanyaje na mwisho tukaona tuuache ule mwili pale pale,
Tulikua na sababu kadhaa za kuacha ule mwili pale,
kwanza hakukua na uhakika wa kupona kwa hali ile, lakini pia hatukujua ni kitu kilifanya ule mwili kuwa pale,
Lakini pia tulikuwa na mizigo kadhaa na sisi wawili vipi tuchukue na huyu mtu ambaye ni nusu mfu?
na hivyo tukawasha piki piki na kuondoka,
Baada ya kwenda kama nusu kilometa hivi sasa nilipaza sauti kumtaka yule kijana asimamishe piki piki,
“tunarudi kuuchukua ule mwili!” nilisema na Bila kubisha yule kijana akasimamisha piki piki tukageuza!
na kwa bahati tukaukuta ukiwa pale pale,
Ilibidi mimi niendeshe piki piki kisha Yule kijana akaushikilia ule mwili pale kati kati yetu na safari ikaanza nakumbuka tulifika saa 6 usiku huku tukiwa tumechoka sana,
Na kila kitu kikaanzia pale hadi siku ile ulipozinduka! Alisema mzee Tito huku akifuta machozi
‘mke wangu hakuamini kama wewe ulikua hai mpaka baadae nilipomuaminisha kuwa unaweza kupona ndipo akaanza kuniunga mkono na kunisaidia kutengeneza dawa na kukutunza mpaka leo hii” alimalizia mzee Tito huku akinisihi sasa nikalale kwani kwa siku ile mazungumzo yalikuwa yametosha,
“kwa leo inatosha mwanangu, Mungu akipenda na wewe ipo siku utatusimulia hadithi yako, tuna imani kisa chako kinasisimua sana, jambo moja tu tunakuhakikishia tuko pamoja na wewe, haya kalale baba” alisema mama Zawadi!
Nilisimama na kurudi zangu chumbani kwangu huku nikitafakari maneno ya Yule mzee
“kwahiyo kumbe nilitupwa msituni kwenye gunia, je nani alifanya hivyo?” nilijaribu kuwaza huku nikiwa najaribu kufumba macho kuutafuta usingizi,
Ni wakati nikiwa nimelala ghafla niliota ndoto nilijiona Nipo kwenye ukumbi kama wa mikutano hivi nikiwa mmojawapo wa watu wengine wengi wanaume kwa wanawake, ilikua ni kama semina hivi na sikuweza kuelewa mara moja ilikua inahusu nini, kulikuwa na makelele ya watu kupita pita na kufanya kukosekana kwa utulivu pale ndani,
Mara aliingia mwanamke mmoja akiwa na walinzi huku na huku kisha sisi sote tukasimama na kumpigia makofi, Yule mama akatupungia mikono na kisha akatuashiria kukaa, mara akaanza kupita kwa mtu mmoja mmoja kumuuliza jina lake na sehemu anayotokea alipofika kwenye meza yangu nikasimama na kumpa mkono huku nikitetemeka na kisha akaniuliza jina langu
“naitwa Ephraim” nilisema huku nikitoa mkono wangu na kumpa alitabasamu kisha akasema
“mume wangu pia anaitwa Ephraim” alisema Yule mwanamke huku watu wakiangua kicheko
Mara ghafla wakaingia watu waliovaa nguo za jeshi na kuanza kurusha risasi huku na huko tukaanza kukimbia huku na huko nilijikokota na na kutafuta mlango wa kutokea na kufanikiwa kutoka nje mara ghafla mbele yangu alikua Yule mwanamke akitabasamu huku akiwa amenielekezea bastola usoni
“nakuuaaaa” alisema huku akiachia risasi, niliiona ile risasi ikiwa inakuja pole pole kama kwenye filamu ,
“hapanaaaaaaaaaaaa!” nilisema kwa sauti huku nikisimama kitandani na kukaa, jasho lilikuwa linanitoka na kwa hivi Mzee Tito na mkewe tayari walikuwa mlangoni wakibisha!
“vipi kuna shida ? tafadhali fungua!” ilikua sauti yam zee Tito
‘hakuna Shida mzee tutaongea asubuhi naombeni mkapumzike,
Niliamka sasa kisha nikachukua kidaftari kidogo ambacho nilikuwa naandika baadhi ya kumbu kumbu ambazo zilikua zinanijia na ndoto nilizokuwa naota katika siku za karibuni nikaandika ile ndoto kisha nikapanda kitandani kulala.
Kesho yake asubuhi sasa niliwasimulia mzee Tito ile ndoto pamoja na lile jina ambalo nilitamka katika ile ndoto sasa mama Tito alikuwa ameshika mdomo tu akishangaa
“inawezekana jina lako ni hilo la Ephraim, sasa je Yule mwanamke ni nani na ile semina ilihusu nini?” mzee Tito alisema
“ehee nina wazo” sasa nilisema huku macho yakiwa yamenitoka
“ndio tunakusikiliza” alisema mzee Tito na mkewe kwa pamoja
“nahitaji kupata simu ambayo inaweza kuingia mtandaoni” nilisema huku nikiwa na uhakika na wazo langu
“ngoja tulifanyie kazi kesho tutafute simu pamoja na line ya fastel nadhani huku msituni inaweza kuwa inashika nimeona kwenye matangazo yao” alisema mzee Tito.
Ni kweli kesho yake alikuja akiwa na simu nzuri ya HTC pamoja na kadi ya Fastel na kama tuliovyotegemea ilikua na mtandao mzuri kabisa…