Hadithi: Nitakupata Tu

Hadithi: Nitakupata Tu

NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 034
******
CHIEF ndio jina lililosomeka juu ya kioo cha simu yake. Hakuipokea kwa wakati ule. Macho yake yaliwatizama wenzake kisha kuitizama tena simu. Sio kwamba alikuwa akiogopa kuipokea simu bali hakuwa na la kumwambia mkuu wake. Akaiacha simu iendelee kuita mpaka ilipokata. Baada ya simu kukatika, kachero yule akauandika ujumbe kwa lugha ya mafumbo na kuutuma kwa Chief. Baada ya kumaliza hilo akamgeukia dereva wa tax. "Utaendelea kuishi hapa kwa Usalama wako mpaka pale hili jambo litakapokwisha." Baada ya kusema hilo makachero wale wakatoka mle ndani tayari kwa safari ya kwenda kuwatafuta Jimmy na Suresh.
*****
Ilikuwa yapata majira ya saa tatu na nusu usiku pale teddy aliposhuka kwenye bajaj pembezoni mwa ufukwe maarufu jijini dar es salaam, ufukwe wa coco beach. Baada ya kushuka hapo akaongoza taratibu mpaka sehemu mmoja iliyojitenga pekee akakaa na kutulia. Hakuwa hapo kwa sababu ya burudani bali alikuwa pale kwa minajili ya kuipa akili yake utulivu. Mambo yaliokuwa yakiendelea yalizidi kumchanganya na kuifanya akili yake ishindwe kufanya maamuzi. Ni mara tatu amenusurika kufa kwa kupigwa risasi, mara ya nne amenusurika kufa baada ya kugeukwa na wenzake kisha kumpoteza fahamu. Mpaka muda ule hakuwa akijua ni vipi ameokolewa katika kisanga kile. Hakujua ni vipi masimba amemtoa katika kifo ambacho kilipangwa kufanywa juu yake. Ni masimba huyu huyu alijitolea kila kitu na uwezo wake kuhakikisha yeye anarudi kwenye uhai. Hakumuacha pale alipowekwa matatani. Hata pale aliposhiriki kuua familia ya Asteria, bado masimba alimpa nafasi ya kubadilika. Licha ya hayo yote bado moyo wake ulikuwa katika mtihani mzito. Aliihitaji pesa na aliuhitaji mzigo wa madawa ya kulevya alionao Masimba. Aliutaka kwa njia yoyote. Hakuhitaji mzigo ule uingie mikononi mwa serikali. Aliutaka na aliuhitaji. Licha ya kuuhitaji huko, lakini hakujua angeweza kuutoaje mikononi mwa mwanaume yule. Hilo ndio lililomfanya afike usiku ule katika fukwe zile za coco beach kujaribu kuwaza hili na lile ili kupata majibu. Kichwa chake alikiinamisha chini huku mikono yake ikiuchezea mchanga. Mawazo yalikuwa yakipishana kichwani. Kuna kipindi katika akili yake alikuwa anawaza na kujilaumu kwa nini akutane na Masimba. Pesa zikaiteka akili yake, pesa zilimfanya aisahau nafasi ya masimba moyoni mwake. Aliihitaji pesa na aliuhitaji mzigo kwa gharama yoyote. Kwa mara ya kwanza akalikumbuka jina la mtu, mtu ambaye angeweza kupanga naye na kupata majibu. Lakini hakujua angewezaje kumpata huyu mtu. Kwani ulipita muda mrefu sana pasipokuonana. Akaichomoa simu yake mfukoni na kubonyeza namba fulani. Baadae simu upande wa pili ikasikika ikiita. Sekunde tatu baadae sauti nzito ikasikika upande wa pili. " Beni Bomphe naonge."
"Teddy killer hapa naongea, nakuhitaji kwenye fukwe za coco beach muda huu kama upo hapa Mjini." Akaingea teddy kisha kukata simu bila kusubiri jibu kutoka upande wa pili. Uso wake ulikuwa kwenye tabasamu matata sana, sasa uhakika wa kuupata mzigo alikuwa nao. Akaendelea kuwaza na kuwazua, baada ya dakika kumi na tano akamuona mtu akitembea taratibu katika fukwe zile. Kijana mweupe mwenye mwili uliojengeka kimazoezi alikuwa akiangaza huku na huko kama mwenye kutafuta mtu. Teddy akainuka na kumsogelea kijana yule. Muda mfupi baadae walikuwa wamesimama wakitizamana. "Habari za masiku Beni?" Akasabahi teddy.
"Nzuri mkuu, naona nchi imetingishwa." Akajibu beni huku akiongeza na maneno kadhaa. "Yeah! Ukiwa mshenzi lazima upate malipo ya kishenzi. Akajibu teddy huku uso wake ukionyesha kujua kila kitu.
"Usiniambie unamjua alietenda hili? Akaongeza ben huku akishindwa kuuficha mshangao.
"Yeah! Namjua! Alijibu kwa kifupi kisha akamuomba Ben waongee kile ambacho amemuitia.
Kwa shingo upande ben akakubali na kufuatana na teddy mpaka sehemu waliokuwa wamekaa mwanzo. "Nipe dili mama nitoweke hapa, watu kama sisi hatuonekani ovyo." Ben akatamka akimuangalia teddy. Teddy akamueleza ben kila kitu huku akificha vichache sana. Ni maelezo ambayo yalichukua dakika kama sita hivi. Baada ya maelezo yote kutoka kwa teddy, beni akatulia huku akimuangalia Ted usoni. Baadhi ya maneno kutoka kwa teddy hayakumuingia akilini. Aliujua uhusiano wao na masimba tokea ndio kwanza wanajiunga na idara ya ujasusi. Lakini haya ambayo yanatoka kinywani kwa teddy yalimuacha na kigugumizi. "Lazima tumuondoe masimba? Hata ikibidi hata familia yake tuitumie katika kuupata huu mzigo? Ni baadhi ya kauli ambazo zilimuacha Ben akiwaza.
"Kwahiyo unataka masimba asafirishwe? Hatimaye akauliza tena.
"Yeah nahitaji kuupata mzigo, kwahiyo ni lazima tumsafirishe. Pakitokea ugumu familia yake itahusika katika kutupa huu mzigo. Sina huruma wala mapenzi katika hili." Akajibu teddy huku kila kitu kikionyesha kuwa hakuwa akitania. Hilo pia halikutegemewa na ben. Lakini kwa kuwa aliitaka pesa Aliamua kukubaliana na teddy kuifanya kazi ile ambayo ilikuwa hatari. Alimjua masimba na aliujua ugumu wake. Kitendo tu cha kusikia kile alichokifanya kwa waziri mkuu ilimthibitishia ni kiasi gani ameingia kwenye vita nzito. Akamuangalia teddy kwa sekunde kadhaa kisha kwa sauti ya kujiamini akasema. "Nitaifanya hii kazi kwa moyo wangu wote. Ikiwa nitamuua masimba ama familia yake, basi damu yao itakuwa juu yako. Ikiwa ataniwahi mimi basi nadhani damu yangu pia itakuwa juu yako." Baada ya kuongea hilo akainuka na kuanza kuondoka huku hofu ikiwa imeutanda moyo wake. Hakupenda kupambana na mtu kama masimba, sio kwa kuogopa lakini alikuwa akimheshimu kama mtu aliyemfanikishia naye kufika pale.
*******
Alikuwa mfano wa simba aliyejeruhiwa, hakutaka kuwapa nafasi maafisa usalama kumtambua kama yeye ndiye aliyehusika na mauaji ya Waziri mkuu. Hilo likimlazimu masimba kutokulala kabisa kabisa akiwasaka Suresh, Jimmy na Mwamvita. Walikuwa watu pekee waliokuwa wakilifahamu hili. Alitaka kumalizana nao kwanza kabla ya kuangalia nini anatakiwa kukifanya. Usiku huu alikuwa maeneo ya sinza afrika sana akitizama kama anaweza kuwaona wabaya wake. Alikuwa ametulia akiendelea kunywa taratibu bia yake. Macho yake yalikuwa yakimtizama kila mmoja ambaye alikuwa akiingia ndani ya bar ile. Muda mwingi alitumia kuitazama saa yake. Muda ulikuwa ukisonga bila kumuona mtu wala kupata chochote kutoka kwa Dee plus. Kazi aliyompa ya kumfuatilia teddy bado haikuzaa matunda. Bado hakumuamini tena teddy. Aliutambua utamani wa teddy na hata mabadiliko yake. Licha ya kumtoa mkononi mwa kifo bado alijua ama kuhisi teddy anaweza kubadilika tena. Hilo likamfanya Masimba mpe dee plus kazi hiyo, kazi ya kuijua mienendo ya teddy. Hilo likampa ugumu wa kuamini kama hakuna chochote. Akauvuta muda akisubiri chochote. Punde mlio wa sms kwenye simu yake ukamgutusha kutoka mawazoni. Mkono ukazama mfukoni na kuibuka na simu. Sekunde moja iliitosha kuufungua ujumbe ule na kuusoma. "Wadudu wawili wamekaa ufukweni wakidonoa chini." Ulisomeka ujumbe. Ilikuwa lugha aliyoielewa, lugha ambayo ilimpa hamu ya kuwajua hao wadudu wawili na kile wanacho kidonoa.
"Ustawi" alijibu kwa neno hilo huku akiirudisha simu mfukoni. Lakini hazikupita hata dakika moja simu yake ikaita. Akaitoa tena mfukoni na kuangalia namba ya mpigaji. "CHIEF" ndio jina lililosomeka. Roho ikapaaa na damu kumsisika. Akapeleka kidole kwenye kitufe cha kijani kisha kuipeleka simu sikioni.
"Nakuhitaji nyumbani muda huu." Baada neno hilo simu ikakatwa. Masimba akaduwaa.hakuamini kupigiwa simu na mkuu wake wa kazi hasa ukiangalia jinsi alivyokuwa akisakwa. Niende? Lilikuwa swali pekee alilojiuliza. Lakini kabla hajapata jibu la swali lake akamuona Dee plus akiingia. Akampa ishara ya kumtaka asogee.. Dee Plus akasogea kisha bila kuongea kitu mfano wa picha na kumkabidhi Masimba
Maelezo ya picha hayapo.

 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 035
Akapewa kitu mfano wa picha,
akaikunjua kutoka kwenye kitu kama
gazeti na kuitupia macho. Akakutana
na picha ya Mpenzi wake akiwa
sambamba na mtu ambaye
alimfahamu sana. Mtu ambaye
alimkuza katika fani hadi kufikia hapo.
Aliitizama picha kwa muda kisha
akairudisha mikononi kwa Dee plus.
"Hakikisha hawakupotei au hakikisha
unakijua kile ambacho
wamekizungumzia." Aliongea masimba
akiunyoosha mkono. Dee plus
aliichukua ile picha na kuondoka
akimuacha masimba akiendelea
kuburudika. Bado alihitaji kujua kile
ambacho teddy na ben
walikuzungumza pale ufukweni. Dee
plus akaondoka safari hii akielekea
katikati ya mji. Alitaka kuanza na ben
kwanza. Kwa kuwa alikuwa na hisia
kuhusu kikao cha pale ufukweni mwa
bahari. Bastola mbili zilikuwa sehemu
tofauti mwilini. Alimjua teddy na pia
ben, licha ya kuwajua huko lakini
hakuhofia kwa kuwa hata yeye alikuwa
mmoja kati yao.
Picha ya teddy na ben wakiwa
ufukweni mwa bahari ni kitu ambacho
kilimjengea maswali masimba katika
kichwa chake. Muonekano wa watu
hawa katika picha aliyoitazama muda
mfupi uliopita hapakuonekana ishara
ya mapenzi juu yao. Ukaaji na jinsi
walivyokuwa wakitizamana ilionyesha
uwepo wa kitu nyeti kilichokuwa
kikijadiliwa na watu hawa wawili. Hisia
kwamba teddy anapanga mipango ovu
juu yake ilikuwa akikigonga kichwa
chake. Haikuwahi kutokea teddy na
ben kuwa na ukaribu huu.. hilo likampa
mashaka na wasiwasi. Hisia kwamba
teddy bado hajabadilika bado
ziliendelea kumsumbua. Akatamani
kumfuata na kwenda kumuuliza kwa
kuwa bado alimpenda sana. Hata
alipokumbuka usaliti aliotendewa na
watu wake, akahisi labda alimtafuta
ben kwa ajili ya kumpa kazi ya
kuwafutilia mbali jimmy na washirika
wake. Vifo vya watu sita katika
nyumba fulani ni ishara kuwa yupo mtu
anayetembea naye kila sehemu. Kwa
mara ya kwanza akawaza
kuitumbukiza risasi kichwani kwa
mwanamke huyu. Ni dhahiri kuwa
mapenzi kwake tayari yalishakwisha.
Akaendekea kuuvuta muda tena na
tena. Wakati wa kuianza hii kazi
hakuwaza kama angefika huku.
Hakuwaza kama yangetokea haya. Kwa
mara ya kwanza akakumbuka wito wa
DG wa idara ya Ujasusi. Wito ambao
kidogo ulionyesha kumtatiza katika
kuukubali. Sekunde hii alikuwa amekaa
akiwaza, sekunde ya pili alikuwa
akiukaribia mlango wa kutokea tayari
kwa safari ya kuelekea kwa Chief.
Alitembea kwa miguu mpaka maeneo
ya bamaga, hapo akachukua tax tayari
kwa safari ya kuelekea masaki
nyumbani kwa mkurugenzi. Muda
wote alikuwa kimya wakati tax
akisonga kuelekea masaki. Mara moja
moja alikuwa akiangalia kwenye vioo
vya pembeni kuona kama anafuatiliwa,
lakini haikuwa hivyo. Hapakuwa na gari
wala usafiri wa aina yoyote. Wakati tax
inafika kwenye mataa ya Morocco,
akaiona gari nyeupe kupitia kioo cha
pembeni akiwafuatilia. Ingawa gari ile
ilikuwa katikati ya magari mawili, lakini
hilo halikumfanya asigundue kuwa
inamfuatilia yeye kwa kuwa, wakati
anatoka pale afrika sana, -hii gari
aliipita ikiwa imeegeshwa pembezoni
mwa barabara. Hakuongea kitu wala
kuonyesha mabadiliko yoyote, dereva
naye akaendelea kuendesha
pasipokugundua kitu. Wakavuka mataa
sasa wakielekea maeneo ya oysterbey.
Alipoiangalia ile gari, akaiona nayo
ikiendelea kusogea tena ikiwa katikati
ya yale magari matatu . Hapo kengele
za hatari zikaendelea kugonga
kichwani mwake. Hisia kwamba yale
magari matatu yalikuwa katika safari
moja ikamjia. Kwa mara ya kwanza
akajipapasa sehemu alipoihifadhi
bastola yake. Baada ya kuhakikisha ipo
akatabasu huku akimuomba dereva
aelekee ulipo ubalozi wa ufaransa.
Dereva akatii na kuuongeza mwendo,
huku nyuma magari yale nayo
yakaongeza.
Muda mfupi dereva akasimamisha gari
pembeni mwa barabara. Masimba na
dereva wote wakashuka, masimba
akatia mkono wake mfukoni na kutoq
noti mbili za elfu kumi kumi na kumpa
yule dereva. Wakati dereva akijipapasa
kutafuta chenji ya kumrudishia
masimba. Muda ule ule gari zile
zikawapita kwa mwendo ule ule, lakini
kufika mbele kidogo zikaacha barabara
inayokwenda posta, mbili zikaingia
kushoto kwenye barabara
inayokwenda Masaki nyingine moja
ikapita kama inaelekea daraja la
salenda. Kila kitu kilichokuwa
kikitendeka pale kilimsisimua na
kumfurahisha masimba. Kila kitu
kilichokuwa kikitendeka ulikuwa ni
mpango uliosukwa na DG wa Tiss.
Alizijua gari na vile vile alizitambua
mbinu husika. Hakuogopa tena.. dakika
ile ile akaliacha eneo lile akiwa juu ya
usafiri wa pikipiki.
*******
Ukimya ulikuwa umechukua nafasi
yake kama kawaida katika eneo lote la
masaki. Walinzi wa idara zote
walikuwa wakizunguka kila kona
kuwalinda viongozi wote. Makachero
walikuwa kila sehemu wakinusa hiki na
kufanya kile. Masimba alishuka umbali
wa hatua hamsini kutoka yalipo makazi
ya chief. Akatembea taratibu macho
yake ya kitizama kila sehemu. Maafisa
usalama na jeshi maalum la usalama
wa taifa walikuwa wamezagaa kila
upande wakiangalia usalama. Masimba
akatembea kanakwamba hakuwa
akiwaona walinzi na hata maafisa
wengine. Akalikaribia geti, hapo
akasimamishwa huku mitutu ya
bunduki ikielekezwa kwake. Mtu
mmoja alieonekana kama mkuu wa
ulinzi akamsogelea masimba kwa
ukaribu. Alipomfikia na kugundua
alikuwa nani alimpa heshima kisha
kumuongoza kuelekea ndani tayari
kwa kukutana na Chief. Geti
likafunguliwa masimba akaongozwa
mpaka ndani pembeni kukiwa na watu
maalum kutoka kikosi cha walinzi wa
viongozi yaani VIP PROTECTION UNIT.
Kufika ndani akaongozwa mpaka ndani
ya jumba. Kuingia tu akukatana na
macho ya chief mr godliving kimaro
akimtizama. Hayakuwa macho ya
kutisha machoni mwake, yalikuwa
macho ya kawaida na macho ambayo
hayakuwa na chochote. Wakaangaliana
tena na tena, kila mmoja akimtizama
mwenzake. "Shikamoo Mzee."
Hatimaye masimba asabahi. Chief
akaitika kwa kichwa kisha akampa
ishara ya kukaa katika moja ya viti pale
ndani. Masimba akakaa pasipo kubisha.
Macho yake yalikuwa yakimuangalia
Chief. Hata chief naye akawa ana
muangalia usoni. "Bila shaka nadhani
unajua kuhusu hiki kilichotokea hapa
nchini. Mambo yamekuwa magumu
sana, mashinikizo kutoka mamlaka za
juu yamezidi. Mkuu wa nchi anataka
kupata taarifa kuhusu hiki kifo. Lakini
bado wenzako wameshindwa kupata
chanzo cha kilicho nyuma ya hili tukio.
Wote ambao tulidhani wangeweza
kutufumbua katika hili nao huuawa
katika mazingira ambayo nadhani ni
kutaka kuuficha ukweli. Nimekuita
hapa kukupa hii kazi, kushindwa kwa
idara zetu za ujasusi ni aibu kwa nchi
na kwa dunia. Mheshimiwa rais
ametishia kuwaomba CIA NA MOSSAD
katika kumgundua muuaji huyu ama
chanzo mauaji hayo. Fanya ufanyavyo
na kwa njia zako zote ili tufahamu hili.
Unaruhusiwa kutumia chochote katika
hili."aliongea chief akionekana
kukerwa na hiki ambacho kinaendelea
kutokea. "Masimba hakutaka kuongea
kwa muda ule. Kichwa chake kilikuwa
kikiifikiria kazi hii aliyopewa. Kazi ya
kumtafuta muuaji wa waziri mkuu,
muuaji ambaye alikuwa ni yeye
mwenyewe. Akatamani kumjibu
kwamba mimi ndiye muuaji, lakini
akauacha huo mpango.
Angejichunguzaje wakati muuaji
alikuwa yeye? Hapo akauona umuhimu
wa kuwawahi Jimmy, suresh na
mwamvita. Alitambua watu hawa ndio
watakuwa mashahidi juu ya maovu ya
Hayati. "Unadhani mtuhumiwa wa
mauaji aliyenusurika kufa kwa amri
yako anaweza kuifanya kazi nzito kama
hiyo tena akitumwa na watu wale
wale wali0mtuhumu? Akauliza
masimba masimba. . Safari hii
akibadilika.
"Najua kwa nini nimekuita hapa, hayo
mengine achana nayo, nimeunusa
ukweli ndio maana kama mkuu wa
idara nikakuita." Akajibu Chief.
"Sawa nitafanya naomba muda wa wiki
mbili nitarudi hapa nikiwa na ushahidi
ama mtuhumiwa mwenyewe.
Ninachoomba ni ruhusa kutoka
mamlaka za juu kuipekua nyumba zote
zinazomilikiwa na marehemu."
Lilikuwa ombi ambalo lilimduwaza
chief. Hakulitegemea hilo. Akakaa
kimya kama sekunde ishirini kisha kwa
sauti yake akasema. "Sawa nitazingatia
ombi lako." Baaada ya jibu hilo la chief,
masimba akainuka na kutoka tayari
kwa kuondoka huku akicheka
kimoyomoyo.
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1

 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 036
ILIPOISHIA.. alikuwa akicheka
kimoyomoyo. Akicheka baada ya
kupewa kazi ya kumtafuta muuaji,
huku muuaji akiwa ni yeye
mwenyewe. Je nini kitaendelea? Shuka
nayo.
******
Alitembea sasa akitaka kufanya haraka
katiks kulimaliza hili. Suresh, Jimmy na
Mwamvita kisha teddy sambamba na
Beni Bomphe wote lazima waondoke
katika uso wa dunia. Sasa alikuwa huru
kuifanyakazi yake. Sasa alikuwa huru
kufanya kile ambacho alikuwa
akikifanya kwa kificho. Mbinu ya
kuwasafirisha wasichana wale watatu
kilikuwa kitu sawa kabisa. Hii ili saidia
kulificha hili suala mpaka sasa. Idara ya
ujasusi kushindwa kupata fununu za
nani muuaji lilikuwa jambo muhimu
sana katika kazi yake. Rais akitaka
kuyaomba mashirika ya kijasusi kuja
kusaidia katika sakati hili, hilo pia
lilimpa tabasamu, tabasamu la pongezi
kwa kuwa ameifanya kazi hii katika
weledi mkubwa. Kufanikiwa kuizidi
maarifa idara ya kijasusi Tanzania
halikuwa jambo dogo. Kwani hakuna
ambaye hawajui hawa watu. Akaliacha
eneo la masaki katika namna ya
kufurahi. Kwa mara ya kwanza akaona
kuna umuhimu wa kurudi nyumbani
kwake. Nyumba ambayo aliisusa katika
kipindi chote alichokuwa akitafutwa.
Leo alitaka akauangalie mzigo wake,
mzigo ambao ndio unasababisha teddy
kuufanya usaliti. Muda wote alitembea
akiomba Mungu aipate ruhusa ya
kupekua nyumba zote ambazo
zilimilikiwa na waziri mkuu. Kuipata
ruhusa hiyo itamfanya kukamilisha kazi
aliyopewa katika wakati ule alioomba
kupewa.
******
Baada ya kutoka pale coco beach,
teddy alienda moja kwa moja mpaka
nyumbani kwake kinondoni. Aliikuta
nyumba ikiwa kwenye mabadiliko
makubwa. Ilionyesha wana usalama
walipiga kambi hapo na kuipekuwa
nyumba yao nje ndani. Kila kitu
kilikuwa katika mpangili0 wake ule ule
lakini vikionyesha kupekuliwa katika
umakini wa hali ya juu. Teddy
akasimama hapo kwa muda akitizama
hiki na kile. Akili yake ilikuwa
akiufikiria mzigo uliopotea. Licha ya
kujua umechukuliwa na Masimba lakini
hakuwahi kujua ni wapi ambapo
masimba aliuficha mzigo ule wa
mamilioni ya shilingi. Tamaa ya pesa
ikamuingia, akaona ulikuwa ni wakati
wa kuutafuta ule mzigo. Alikuwa na
uhakika wa kuwepo mle ndani ama
kule ambako alipelekwa wakati
alipopoteza fahamu. Akairuhusu miguu
yake kuingia kila chumba na kila
sehemu za siri ambazo huwa
wanatumia kuhifadhi vitu vyao. Tamaa
ya pesa ilikuwa imeshamuingia mtoto
huyu wa kipare. Hakuwaza tena
mapenzi wala pesa, hakuwaza
mipango yao ya baadae alichokiwaza
ni ule mzigo. Mzigo ambao ulimfanya
au na yeye kunusurika kuuawa mara
kadhaa. Alipekuwa na kutafuta kila
sehemu lakini hakupata kitu, hakupata
mzigo wala kitu chochote. Akarudi
chumbani akionyesha kuwaza hili na
lile. Mishipa ya hasira bado
haikuondoka usoni mwake. Chuki dhidi
ya masimba ikaongezeka zaidi na zaidi.
Alitamani kuiruhusu risasi kukipasua
kichwa chake pale ambapo
angefanikiwa kumuona. Baada ya
kuwaza sana akaona ajimwagie maji
kwanza ili akitoka aelekee kule
alipoamkia akaendelee kuutafuta
mzigo. Yote hayo aliyawaza akiwa
anajua masimba bado ni anarafutwa.
Hakujua kile kilichotokea muda mfupi
uliopita. Akayatoa mavazi yake na
kubaki kama alivyozaliwa. Akapiga
hatua mpaka bafuni. Akafungulia maji
na kuyaacha yamwagikie mwilini.
Wakati maji ya kizidi kumpa uhueni
kumbukumbu juu ya kilichotokea usiku
wa jana ikaanza kujirudia. Mauaji ya
mama wa Asteria kwa kutega bomu
kwenye nyumba yake, ulikuwa
mpango ambao ulipangwa afe pamoja
na Masimba. Ni yeye aliyetoa taarifa
kwa Jimmy kuhusu safari ya masimba
nyumbani kwa mama wa Asteria.
Kilichotokea mpaka masimba kupona
hakukijua. Alipowaza tukio la
kusalitiwa na wenzake kisha kupigwa
kichwani na kupoteza fahamu, alihisi
moyo ukizizima. Masimba alimuokoa
na kumtoa mikononi mwa kifo. Lakini
leo alitaka kumuua masimba kwa
sababu ya pesa. Hilo likaonyesha
kumtuliza kwa muda lakini bado
mawazo yake yalikuwa kwenye pesa.
Akayaondoa mawazo yale kwa
kuichukua sabuni na kuanza kujipaka
mwilini. Ni wakati akilifanya hilo
akausikia mlango ukifunguliwa kisha
nyayo za mtu zikasikika kuingia pale
ndani. Akayafunga maji kisha kutulia
mle mle bafuni. Miguu bado iliendelea
kutembea pale chumbani. Akaangalia
pembeni kidogo sehemu ya kuwekea
vifaa vyake, lakini hakuiona bastola
yake, alikuwa ameisahau pale
chumbani sambamba na mavazi yake.
Akaendelea kutulia huku bado mtu
yule akionekana kuhangaika hapo
chumbani. Akatamani kutoka mle
bafuni lakini hakuweza kwa kuwa
kulikuwa na ugumu, pia alikuwa uchi
na bastola yake ilikuwa chumbani.
WakAti akifikiria nini cha kufanya, mtu
yule akasikika akitoka mle chumbani
kisha kupotelea. Teddy akaufungua
mlango na kuchungulia kwa nje,
macho yake yakamuona mtu
akimalizikia kwenye kiza. Kwa kuwa
alikuwa uchi huku akiwa bado na povu
la sabuni, teddy alitoka mpaka ndani
na kuingia chumbani. Cha kwanza
kukiangalia ilikuwa bastola yake.
Akaiona ikiwa pale pale alipoiacha.
Akaangalia na vitu vingine. kitu
alikikuta kikiwa kipo pale pale. Yule ni
nani? Na alikuja hapa kufanya nini?
Yalikuwa maswali ambayo hayakuwa
na majibu.
******
Wana usalama walikuwa mtaani
wakiendelea kuwafuatilia Jimmy na
Suresh. Kila sehemu walikuwepo na
hata kwenye makazi yake ya siri
yalikuwa yakichunguzwa kwa umakini
wa hali ya juu. Muda wote walioanza
kumchunguza bado hapakuwa na
chochote walichokipata kutoka
kwenye uchunguzi wao. Mawasiliano
yao yalikuwa yameingiliwa na
kufuatiliwa kwa kila hatua. Hakukuwa
na mawasiliano ya kutia shaka. Licha ya
hilo wanausalama bado walikuwa
wakiendelea kufuatilia. Katika
kufuatilia huko wakagundua kuwa
Jimmy huwasiliana na namba karibu
tano kwa kila siku. Namba hizo huwa
haipiti dakika mbili mpaka tano
pasipokuwasiliana. Hilo likawatia shaka
wana usalama wale. Kwani hata
walipoifuatilia mawasiliano ya Suresh
walikutana na namba zile zile na
mawasiliano yale yale na muda ni ule
ule kama yale ambayo hufanyika kwa
Jimmy. Wote wakahisi uwepo wa
mawasiliano yasiofaa kati ya watu
wale... leo hii vijana wawili walikuwa
wamekaa maeneo buguruni kwa
mnyamani wakibishana sambamba na
vijana kuhusu sakata linaloendelea
hapa nchini kuhusu kutekwa kwa watu
na kupotea kwa mwanaharakati na
mkosoaji mkuu wa serikali ya Tanzania
Ben John Saatisa. Wakati wengine
wakiilaumu serikali hasa Idara ya
Ujasusi, wengine walikuwa wakikihoji
chama chake kwa kukaa kimya muda
wote mpaka pale mitandao ya kijamii
kuibua suala hilo. Licha ya ubishi huo,
lakini walikuwa hapo kwa kazi
maalum. Kazi aliowaleta hapo ilitokana
na kugundua kuwa mmoja kati ya watu
wanaowasiliana na Jimmy pamoja na
Suresh alikuwa akiishia katika viunga
hivyo vya buguruni. Walibishana hapo
lakini macho na mawazo yao yalikuws
mbele ya jumba fulani kubwa. Hapo
ndipo anapoishi mtu wao waliokuwa
wakimfuatilia. Wakati mabishano
yakiendelea, wakaiona ikiingia taratibu
katika eneo la jumba hilo. Punde lango
likafunguliwa na ile gari kupita ndani
moja kwa moja. Vijana wale
hawakuonyesha chochote bado
waliendelea kubishana. Ikiwa
hazikupita hata sekunde kumi tokea
kuingia kwa hari hilo. Wakamuona
mwanadada mrefu na mrembo sana
akichungulia kutoka ndani kisha
kuufunga mlango. Haukupita muda
tena wakamuona muokota makopo
akipita akielekea pale kwenye lango la
jumba lile. Macho yao yakahamia kwa
muokota makopo yule. Muokota
makopo ambaye aliwashangaza na
kuwaduwaza. Hakuwa muokota
makopo kama anavyoonekama.. bali
huyu alikuwa mtu kama wao.. Yaani
hata yeye alikuwa ni kachero, lakini
hawakujua kwa nini yuko pale na
imekuaje Akajibadili na kuwa muokota
makopo.
ITAENDELEA
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1

 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 037
Alikuwa muokota makopo, muokota
makopo ambaye hakuonekana
kufanana na kazi hiyo. Bado
wakaendelea kumtizama. Hata wakati
analifikia geti na kuligonga bado
walikuwa wametulia wakimtizama.
Suruali iliyochanika, kofia chakavu na
fulana ya hovyo haikuwafanya
wapelelezi hawa waamini kile
walichotakiwa kuaminishwa.
Kuaminishwa kuwa huyu alikuwa
mchafu tena muokota makopo. Kila
mmoja akaendelea kumtizama safari
hii kwa umakini. Wakataka
kuaminishwa kuwa hakuwa mtu kama
wao, lakini hilo halikutokea kwao
kuamini. Kuamini kuwa yule ni
mwenda wazimu. Walijua na
kutambua kuwa yule alikuwa
mwenzao. Geti likafunguliwa na
mwanadada yule yule aliyelifunga
mwanzo, hakuna aliyetegemea
kutokea kwa kilichotokea. Kwani muda
mfupi walikuwa wakimuangalia yule
mtu kama muuza machupa. Hata
wakati akiliendea geti walilijua hilo.
Lakini kitendo cha geti kufunguliwa na
kushuhudia ule upigaji wa muokota
makopo yule, wakabaki wameduwaa.
Mwanadada aliyefungua geti alikuwa
chini nje kidogo ya geti akiwa hana
fahamu. Mtu yule muokota makopo
akageuka na kuwapa ishara ya
kumchukua mwanamke yule. Hapo
ndipo walipomtambua na kumjua
muokota makopo. Huyu alikuwa Dee
plus, huyu alikuwa kijana wao. Baada
ya kuitoa ile ishara Dee plus
akalifungua geti taaratibu na kuzama
ndani. Macho yake yakakumbana na
giza, giza ambalo ilikuwa ishara kuwa
jumba lile halikuwa linaishi watu wa
kawaida. Kingine kilichomstaajabisha
ulikuwa ni ukimya. Ukimya ambao
hapo mwanzo haukuwepo. Bastola
ilikuwa mkononi wakati akiuendea
mlango wa jumba lile kwa kupitia chini
ya magari ambayo yalikuwa pale
ndani. Bado ukimya uliendelea kutanda
na kumfanya Dee plus a0ngeze
umakini. Alipoufingia mlango kwa
upande wa nyuma akasimama kwanza
kusikiliza kama atasikia kitu chochote.
Lakini bado hakuisikia sauti ya tv wala
sauti ya redio. Jumba lilikuwa kimya
kabisaa. Akaendelea kusonga mbele.
Baada ya kutembea hatua kadhaa,
akaukuta mlango ukiwa wazi, hapo
akasita kwanza. Akasimama upenuni
mwa jumba lile. Mbele yake
akiutizama mlango ambao ulikuwa
wazi. Licha ya kusubiri kwa muda wa
dakika moja, lakini hakuweza kumuona
mtu yoyote akitoka ama kuingia. Hapo
akaamua kusogea mbele zaidi
kuufuata mlango. Alipoufikia
akatembeza macho yake ndani kwa
sekunde moja akitegemea kuona
chochote lakini hakuliona hilo. Sasa
akaamua kuingia ndani kabisa. Bado
ukimya na giza viliendelea kuwepo
hata ndani. Bastola mkononi, macho
yakitembea huku na huko akafanikiwa
kuingia mpaka sitting room. Bado
ukimya haukuondoka hapa. Akatulia
hapo akiangalia kama mtu wake
atakuwepo hapo, lakini bado
hakumuona mwenyeji wake. Sebule
haikuonyesha dalili ya uwepo wa watu
hapo. Hilo pia likamshangaza kama sio
kumduwaza.
Akainuka akipanga kuitafuta switch ili
awashe taa aangalie. Wakati anafika
karibu na swichi akaisikia sauti ya mtu
akigugumia kwa maumivu. Akaacha
kwanza alichotaka kukifanya alatulia
ilikusikiliza kwa makini. Bado sauti
dhaifu ya mtu aliye0nyesha yupo
kwenye hatua za mwisho aliendelea
kuisikia safari hii kwa karibu. Dee plus
asogea mdomo wa bastola ukiwa
mbele. Mbele kidogo akakanyaga kitu
mfano wa maji. Kabla hajajua ni kitu
gani, harufu ya damu ikasikika puani.
Akatambua kuwa ilikuwa damu tena
inawezekana ni damu ya mtu yule
anayegumia kwa maumivu. Hapo
akaliacha hilo la damu na kuanza
kumsaka majeruhi. Kengele za
tahadhari zikilia kichwani kwake.
Haikuwa sawa na hapukuwa na
usalama tena. Alishawahiwa na mtu.
Kitendo cha kuukuta mlango uko wazi
kisha kulikuta hili la dimbwi la damu
ilikuwa ishara kuwa tayari kuna mtu
amemuwahi katika hili. Hii ilikuwa ile
ile staili ya fumbana midomo. Hata
huyu naye alikuwa amezibwa mdomo
kutotakiwa kuongea chochote. Nani
atakuwa amelifanya hili wakati hii
ilikuwa ni siri ya idara ya ujasusi? Nani
anavujisha hili kutoka ndani ya idara ya
usalama wa Taifa? Tuna wanaotusaliti?
Tuna wanaovujisha hili? Nani amejua
nani atakuja huku ndani? Yalikuwa
mawazo yaliyomsogeza mpaka chini ya
sakafu alipolala mtu yule. Bado alikuwa
akiugulia maumivu. Akainama
kumuangalia mtu huyu kama anaweza
kupata lolote, lakini haikuwa hivyo,
mtu yule akampa ishara ya kuwasha
taa.. Dee plus akainuka huku bado
bastola iko usawa wa mtu huyu.
Akarudi nyuma na kuiwasha taa..
sebule yote ikawa nyeupe. Hapo
akashtuka baada ya kukutana na watu
watatu wakimtizama. Teddy, Ben na
Mwamvita. Wote walikuwa
wakitabasamu huku teddy akipiga
makofi. Dee plus hakushtuka na
hukuwajali, bado macho yake yalikuwa
yakiutizama mwili wa mtu yule
aliyelala katikati ya dimbwi la damu.
Akili yake ikafanya kazi kwa haraka.
Akageuka kuwaangalia watu wale
watatu, hakuamini macho yake pale
alipokutana na midomo mitatu ya
bastola ikimtizama huku sakafuni
kukiwa na miili ya wale vijana wawili
ikiwa haina uhai. Hakuacha
kuuonyesha mshangao wake. Watu
watatu ambao alikuwa akiwatizama
hawakuuonyesha utani wala masihara.
Hata pale walipokuwa wakimsogelea
hakujua nini cha kufanya. Ilikuwa
miujiza tu kutoka mikononi mwa
viumbe hawa watatu. Viumbe ambao
hawakuwahi kuwa na roho
kibinadamu. Akasimama akimuangalia
zaidi teddy. Kwa mara ya kwanza
alikuwa akiushuhudia unyama wa
teddy. Hakuonyesha kama hata yeye ni
kachero. Hapa aliubeba unyama
unyama. Wote wakamfikia katika
muda ule ule. Midomo ya bastola zao
iliugusa mwili wa Dee plus.
Wakimtizama katika kila aina ya
vitendo na ishara. Nadhani hawakuwa
wakimjua vizuri dee plus, nadhani
hawakuwa wakimjua kwa kuwa
hawakuweza kusimama kwa muda ule.
Mapigo fulani ya kijapani yalisababisha
bastola zao kuanguka chini pasipo wao
kutaraji. Sasa walikuwa wakitizamana,
wakiangaliana na hata kusogeleana.
Dee plus alikuwa akiwatizama jinsi
walivyokuwa wanakuja. Ni wakati hilo
likifanyika mlango ukafunguliwa kwa
kasi huku risasi zikivurumishwa ndani
ya sebule. Hakuna aliyesimama hapo
bali kila mmoja akachupa kwa upande
wake. Moshi wa baruti pekee ndio
uliyesikika ndani ya chumba kile. Dee
plus alikuwa amebana nyuma ya meza
kubwa macho yake yakitizama kila
upande. Ukimya ulikuwa umechukua
nafasi kubwa ndani ya jumba. Hakuna
hata mmoja ambaye alikuwa
akipumua. Pale alipojibanza Dee plus
nyuma yake kulikuwa na mlango
mdogo ambao mwanzo hakuwa
ameuona. Hata mtu ambaye alikuwa
akimimina risasi naye alikuwa
amejibanza kimya. Sebule bado ilikuwa
giza kutokana na risasi zilizokuwa
zikivurumishwa kuipasua taa. Dee
akaufungua mlango taraatibu na
kuingia ndani ya Chumba kile kisha
kuufunga tena. Wakati akitaka
kugeuka nyuma aondoke, akamuona
mtu mle ndani. Huyu alikuwa
mwanadada. Alikuwa akitetemeka
huku akiwa hana hata vazi maungoni
mwake. Alikuwa akitetemeka sana na
licha ya kutetemeka huko pia alikuwa
akivuja damu maeneo mbali mbali ya
Mwili wake. DEE PLUS AKATULIA
AKIMTIZAMA HUKU MDOMO WA
BASTOLA UKIMLENGA MWANAMKE YULE.
Hakutaka kumuamini kwa asilimia
zote. Hata katika kazi zao za kijasusi
hakutakiwa kumuamini mtu yoyote.
Kitendo cha teddy kutaka kumuua ni
kuonyesha ni jinsi gani binadamu
hawaaminiki. Akaichukua khanga
ambayo ilikuwa juu ya meza
akamtupia na kumtaka watoke mle
ndani. Kwa kuwa mwanamke yule
alikuwa mwenyeji wa jumba lile
akamuongoza Dee plus kutoka katika
jumba lile wakiacha milindimo ya risasi
ikiendelea.
*******
Alihitaji kuupata ujumbe kutoka kwa
Dee plus kutoka sehemu fulani
aliyomtuma. Lakini muda ulikuwa
umekwenda sana na bado hakuwa
amepata ujumbe huo pia Dee plus
hakuwa amefika. Hilo likampa
wasiwasi kidogo. Akaamua kumpigia,
lakini simu yake ilikuwa ikiita tu
pasipokupokelewa. Hata hilo
hakulitegemea. Akili yake ikamwambia
dee plus alikuwa msambweni. Wakati
akitaka kuinuka tayari kwa safari ya
kumfuatilia.. mlango ukafunguliwa
akaingia dee plus, hakuwa mwenyewe
bali alikuwa na mwanamke
aliyeonyesha kulowa damu. Hapo
akagundua kuwa mawazo yake
kwamba Dee alikuwa msambweni
yalikuwa sahihi. Akawaangalia wote
kwa pamoja, lakini kabla
hajazungumza chochote simu ya
Masimba ikaita. Akaichomoa simu
mfukoni na kuangalia Jina la mpigaji.
Alikuta simu inatoka kwa mama yake
mzazi. Machale yakamcheza.. akahisi
hatari kwa mzazi wake sambamba na
wanawe France na Yaseer. "Hallow
Mamaaa!!!!! Akaita masimba..
"Tunahitaji mzigo wetu!! La sivyo
utakuta maiti za wanao na mama yako
mzazi." Haikuwa sauti ya mama yake,
bali ilikuwa sauti ya mtu mwingine
ambaye hakuweza kumgundua.
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1

 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 038
ILIPOISHIA
Tunaomba mzigo wetu la sivyo utakuta
maiti za wanao pamoja na mama yako
mzazi.
ENDELEA NAYO.
Kwa muda masimba akapigwa na
bumbuwazi, butwaa la kutokuamini
alichokisikia. Simu ilishakatwa na
haikuwa ikipatikana tena. Mama yake
na watoto wake Yaseer na France
walikuwa chini ya himaya ya watu asio
wajua. Hasira zikaendelea kuchemka
ndani kwa ndani. Aliwapenda sana
wanawe na hata mama yake.
Hakupenda waguswe na kubughuziwa
na mtu yoyote. Lakini leo kuna watu
ambao wamekwenda kuugusa moyo
wake na roho yake. Walikwenda
kumtingisha na kumtia hofu.
Walikwenda kuonyesha kuutaka mzigo
kwa njia nyingine. Ni nani hawa
wanacheza na watoto wangu? Ni nani
hawa wanacheza na mama yangu?
Yalikuwa mawazo yaliyomuondoa pale
ndani. Alitaka kuondoka katika muda
ule kuelekea kwao Handeni. Alitaka
kuwahi kukabiliana na watu hawa.
Mzigo ni wa nini kwangu? Watu wangu
wanathamani kuliko hata huu mzigo.
Wakati anaukaribia mlango wa
kutokea akaisikia sauti ya Dee plus
ikimuita. Hapo ndipo alipogutuka na
kugundua kuwa Dee plus alikuwa pale
ndani tena akiwa na mwanamke
aliyeliwana damu. Akageuka na
kumtizama Dee plus, macho yao
yakaongea kwa sekunde mbili,
sekunde ya tatu masimba alikuwa
akiufungua mlango akiondoka pale
kwa safari ya Tanga. Safari ya
kuupeleka mzigo sababu ya kuwaokoa
watu wake. Alitembea hasira
ikichemka, alitembea kana kwamba ni
kichaa. Bastola mbili zikiwa mwilini
katika sehemu tofauti. Alikuwa
ameingiq vitani rasmi, alikuwa
ameingia kwenye mapambano. Teddy,
mwamvita, suresh na jimmy ilikuwa ni
lazima wafe. Ilikuwa ni lazima
waondoke. Muda mfupi alikuwa
sehemu moja katika nyumba yake ya
Siri maeneo ya kijitonyama. Alikuwa
ndani ya chumba akiuchukua ule mzigo
tayari kwa kuupeleka sehemu husika.
Alikuwa tayari kufanya kila kitu kwa
sababu ya watoto na mama yake.
Baada ya kuweka kila kitu katika hali
nzuri, safari ya kuelekea Handeni
ikaanza. Alikuwa katika kiwango
kikubwa cha hasira, alimtoa teddy
moyoni na hata rohoni. Alikuwa tayari
kumuua kwa mikono yake mwenyewe.
Alikuwa tayari kuufumua ubongo wa
mwanamke huyu mpuuzi. Alitambua ni
yeye ambaye alikuwa nyuma ya hili
suala la kushikiliwa mateka kwa wazazi
wake. Hakutaka kumwambia mtu
yoyote zaidi ya Dee plus. Hata Chief
hakutaka kumwambia kwa kuwa
anaweza kuongea na wasaidizi wake
wakaivujisha. Alitaka kupambana
mwenyewe, alitaka hili suala liishe
mikononi mwake. Suala la kifo cha
waziri mkuu akaliweka pembeni
kwanza. Mawazo yalikuwa kwa watoto
wake na bibi yao. Wakati akipita
kwenye daraja la wami akaliona gari
likimpita kwa kasi sana. Mwendo wa
gari lile ulimshangaza sana lakini kwa
kuwa halikumhudu akaamua kuachana
na mawazo kuhusu hilo. Akaendelea
kuendesha gari kwa mwendo wa
wastani. Wakati anafika mkata ili
aingie kwenye barabara iendayo
Handeni, mlio wa sms ukaingia kwenye
simu yake. Akaitoa simu mfukoni,
akakutana na Jina la My love juu ya
kioo cha simu. Sms kutoka kwa Teddy
hiyo ilimshtua. Akaufungua ujumbe ule
huku moyo wake ukiwa na wasiwasi
mkubwa. "Najua ushajua mpaka sasa
mimi ni nani. Naomba upeleke mzigo
ukiwa pekee yako, ujanja wowote
utakaoufanya utakuja kuokota maiti za
hawa vifaranga vyako." Ulisomeka
ujumbe ule. Akaurudia kuusoma tena
na tena. Hakutaka kuamini kama
ulikuwa ukitoka kwa teddy mwanamke
aliyekuwa akiimba mapenzi kila siku.
Mwanamke aliyekuwa akimwambia
Nakupenda kila siku. Akaurudia tena na
Tena ulitumwa kweli na Teddy.
"Nitakupata tu na Nitakuua kwa mkono
wangu." Akajisemea mwenyewe huku
akiirudisha simu mfukoni. Teddy
alikuwa ameonyesha yeye ni nani
katika hili. Aliamua kujiweka wazi.
Akaipita mazingara na kuitafuta SUA.
Gari ikatembea na kutembea katika
mwendo wa kawaida.
******
Mji wa Vibaoni ulikuwa umepoa kwa
ukimya, wakazi karibia wote walikuwa
wamelala huku mbwa tu wakisikika
wakibweka. Alitembea kwa miguu
baada ya kuiacha gari sehemu ya mbali
kidogo. Alitembea usiku ule akiwa na
mavazi maalum ya kutembelea usiku.
Kutoka kijiji cha kwambwembwele
alipoiacha gari, akapitia barabara
iendayo arusha eneo maarufu liitwalo
kwa kadenge. Akatembea usiku ule
pasipokukutana na kitu chochote
mpaka alipotokea maeneo ya Shule ya
Msingi mlimani (zamani alijulikana
kama vibaoni) baada ya kufika hapo
akatulia kwanza akiangalia nyumba
yao. Macho yake yakawaona watu
wawili ambao walikuwa wamesimama
Nje ya nyumba yao. Aliendelea
kuangalia mara akauona mwanga wa
taa za gari ukisogea taratibu. Masimba
akaendelea kidogo akitizama kwa
makini. Akamuona mtu mwingine
akitokea nyuma ya nyumba ya mzee
Mauya. Baba mzazi wa Rukia Mauya.
Baada ya kutoka mtu yule akaonekana
akiisogelea gari ambayo ilikuwa tayari
imesimama karibu na nyumba yao.
Akaondoka pale na kupitia nyuma
nyuma mpaka pembeni mwa uwanja
wa shule ya msingi. Wakati huo watu
wale bado walikuwa wamesimama
huku mmoja wao akiongea na simu.
Punde akauona mlango wa gari ile
ukifunguliwa, wakashuka watu wawili
ambao aliwatambua kwa haraka.
Alikuwa mwamvita na Ben. Hata
alipoiangalia gari ile vizuri aliitambua
kuwa ni ile gari iliyompita kule wami.
Baada ya watu wale kushuka
akawaona wakiingia ndani ya nyumba
yao kisha wakatoka wakiwa
wanawasukuma watoto wake na
mama yake. Wakati hilo likifanyika
mlango mwingine wa gari ile
ukafunguliwa. Safari hii alishuka teddy
mkononi akiwa ameshikilia bastola.
Kwa kuwa watoto na hata mama wa
masimba walikuwa
wakimjua,wakamkimbilia na kutaka
kumkunbatia. Haikuwa hivyo, haikuwa
hivyo kwa kuwa Teddy hakulitaka hilo.
Akashudia wanawe wakipaa angani
baada kupokea mapigo kutoka kwa
teddy. Hakuvumilia hilo, muda huo huo
alikuwa amechupa hewani na
kuwadaka watoto wake kabla ya kufika
chini. Akatua nao chini katikati ya watu
wale huku mdomo wa bastola ukiwa
kichwani kwa Teddy. Kilikuwa kitendo
ambacho hakikutarajiwa na watu wale,
kitendo ambacho kiliwaacha kwenye
hamaniko. Wakati hilo likiendelea
mama yake masimba akachoropoka na
kutaka kukimbilia pale alipokuwa
mwanawe. Hakumfikia wala kusogea..
Bastola ya Mwamvita Ikakohoa na
wakati ule ule Masimba akamshuhudia
mama yake akipaa juu na kuanguka
chini. Damu zilikuwa zikivuja kifuani.
Masimba hakuamini hilo, hakuamini
kama chini pale amelala mama yake.
Akakurupuka kukimbilia ulipolala mwili
wa mama yake mzazi. Wakati huo huo
wanakujiji nao walikuwa wakiinuka
kutokana na kuusikia mlio wa bunduki.
Baada ya kuona watu wameanza
kuamka majumbani mwao,
wakambeba mtoto mmoja na kuingia
naye kwenye gari kisha kui0ndosha
gari kwa mwendo wa kasi wakimuacha
masimba akilia juu ya mwili wa mama
yake.
Alikuwa haamini kama mama yake
ndiyo yule aliyekuwa amelala pale
chini damu ikivuja kama maji. "Mnala
inuka chilonge. Usekunasa mnala wezi
ukuluwo na walonge na yuhi? Inuka
mnala." ( inuka mama tuongee,
usiniache mama, wajukuu zako
wataongea na nani? Inuka mama)
alilalamika masimba huku akimtingisha
mama yake. Lakini haikusaidia kitu,
mama yake hakuwa na kauli tena.
Alikuwa katika hatua za mwisho za
uhai wake. Pale pale akashuhudia
mama yake akikata kauli na kugeuza
shingo. Muda mfupi akaacha kupumua.
Mama yake alikuwa amekufa mikononi
mwake. Mama yake alikuwa amekufa
kwa ajili yake. Mwamvita alikuwa
amemuua mama yake. Akashindwa
kuongea kwa muda. Mama yake
alikuwa amenyamaza kimya. Akainuka
na kusimama pembeni akiuangalia
mwili wa mama yake. Lakini
alipoangalia pembeni hata mwanawe
Yaseer alikuwa ameanguka akitokwa
na damu puani, mdomoni na masikioni.
Alikuwa amepoteza fahamu. Muda ule
ule difenda ya polisi yenye askari kumi
wenye silaha nzito ikawasili.
Wakashuka na kuanza kupiga picha za
tukio lile. Muda ule ule gari aina ya
wagonjwa ikafika na kumchukua
yaseer. Kila kitu kilitokea kwenye
kipindi kifupi sana. Muda ambao
ulibadilisha maisha ya masimba.
Hakujua kama mwanawe atapona
kutokana na pigo la Tedd na pia hata
france naye hakujua kama atakuwa
salama. Watu walikuwa wengi
wameuzunguka mwili wa mama wa
masimba. Mama ambaye alikuwa ni
maarufu sana pale vibaoni na Handeni
yote kwa ujumla. Vilio vikatawala huku
watoto wa kike wa marehemu wa
kipoteza fahamu kwa taarifa hiyo.
Muda wote Masimba hakuwa akiongea
taswira ya mwamvita akimshuti mama
yake ilikuwa ikijirudia. Matundu
matano ya risasi kifuani yaliuondoa
uhai wa mama yake. Akaitamani iwe
ndoto, aliitamani iwe kama hadithi ya
kusadikika. Lakini mwamvita aliutoa
uhai wa mama yake. Mbele ya macho
yake ulilala mwili wa mwanamke
mwenye thamani kuliko mwanamke
yoyote duniani. Akainuka akipiga hatua
kwa mara nyingine akielekea ulipolala
mwili wa mama yake. Hakuufikia kama
mwanzo, kizunguzungu kikali
kikamfanya aanguke chini, macho
yakaingiwa na Giza na hakuona
kilichoendelea.
******
Alijifungia chumbani akilia kwa
uchungu. Pembeni aliuweka mzinga
wa pombe kali. Macho yake yalikuwa
yamevimba kwa kilio na majuto. Mbele
kidogo kwenye kitanda kidogo alikuwa
amelala france mtoto wa masimba
akitibiwa na Daktari binafsi. Taswira
yake ikalikumbuka tukio la mwamvita
kuruhusu risasi kumuua mama wa
masimba. Akakumbuka kumuona
mama yule akiinguka. Chozi likashuka
na kushuka Zaidi. "Hukustahili Kufa
mama yangu. Umenitendea mema
sana tokea nilipokujua . Nisamehe
mama yangu ni samehe kwa ujinga
wangu. Aliongea Teddy akilia. Kichwani
akavuta taswira ni hali gani alionayo
masimba kwa muda ule. Akainuka na
kutoka nje ya kile chumba. Safari yake
ikaishia chumba kingine mle ndani.
Akaichomoa bastola yake na
kuinyanyua juu mdomo wa bastola
ukagusa kichwani mwake. Teddy
alitaka kujiua. Hakuweza kulivumilia
lile. Kidole kikashuka mpaka kwenye
kitufe cha kufyatulia risasi.
Maelezo ya picha hayapo.

 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 039
Kid0le kikashuka mpaka kwenye kitufe
cha kufyatulia risasi. Akaivuta pumzi
kwa muda. Akili yake ilikuwa ikikinzana
na moyo wake. Moyo ulihitaji atende
kile, lakini akili ikakataa kutii matakwa
ya moyo. Bado akatulia kidole kikiwa
kwenye kitufe. Alikuwa ametulia
akiusikilizia uamuzi wa vitu viwili.
Uamuzi wa kukatisha maisha yake ama
kufuata kingine. Ni katika kuwaza huko
akapata maamuzi mapya. Maamuzi
ambayo yalimfanya aishushe bastola
yake. Akatulia akiufikiria uamuzi mpya
alioupata. Akili yake ilimwambia
aondoke hapa Tanzania aende nchi
yoyote akatafute sehemu ya kuishi
akiwa sambamba na France. Huo
ulikuwa uamuzi wake, maamuzi
ambayo hakutaka kumshirikisha mtu.
Akatoka ndani ya chumba kile na
kurudi kule alipomuacha Daktari
akimtibia France. Akaufungua mlango
na kuingia macho yake yakakutana na
macho ya france yakimtizama kwa
wasiwasi. Teddy akatabasamu tayari
kwa kuuondoa wasiwasi ule. Akapiga
hatua mpaka pale alipokuwa amelala.
Akapiga magoti na kuushika mkono
wake. Akayapeleka macho yake usoni
kwa france. Akahisi kama alikuwa
akitizamana na Masimba kutokana na
kufanana kwao. France alikuwa ni
Masimba mtupu. Alimuangalia sana
mwisho wake akashindwa kuyazuia
machozi yake yasishuke. Bado mwili
wa mama yake masimba ulipopaa
angani baada ya kupigwa risasi na
Rukia ulikuwa ukijirudia. Roho
ikamuuma na kumuuma. Ule ushujaa
wote ukapotea kabisa. Sasa alikuwa
ameivaa hofu na kuuvaa woga.
Alikuwa aki0gopa kukutana na
masimba. Hapo ndipo alipozidi kuona
umuhimu wa kuondoka hapa nchini.
"Nakupenda sana mwanangu Frances.
Wewe ndio pekee furaha yangu pekee
iliyobaki. Najua baba yako atanitafuta
na hata kuniua. Lakini kabla hajaniua
nataka nikwambie kuwa Nakupenda
mwanangu na ninataka tuondoke hapa
tukaishi Ulaya. Nia yangu nikukufanya
uishi kwa furaha." Baada ya kuongea
hayo akainuka na kuondoka pale
nyumbani. Alitaka kuipanga mipango
kimya kimya pasipo ku0ngea na mtu
yoyote. Hata kupokea simu ya
Mwamvita hakuwa akifanya hivyo ndio
maana leo hii hakuwa katika makazi
yake yanayojulikana.
****
Bado hakuwa na fahamu na hakuwa
akijua kile kilichokuwa kinaendelea.
Handeni ikazizima kwa majonzi na
vilio. Kila mmoja aliyesikia kifo cha
mama huyu alisikitika sana. Watu
wakaendelea kumiminika kutoka
maeneo mbalimbali. Muda mfupi
nyumbani ulijaa umati wa watu. Kila
mmoja alikuwa akisikitika na kulaani
kile kilichotokea. Vijana wenye
uchungu wakataka kuleta fujo kwa
kuwalaumu polisi. Lakini hawakujua,
hawakujua kuwa Polisi hawakuwa na
kosa lolote. Masimba bado hakuwa na
fahamu, ndio kwanza madrip ya maji
yalikuwa yakimiminika kwenye
mishipa. Habari zikasambaa kama moto
wa kifuu. Idara ya ujasusi ikaipata
taarifa hiyo. Ilikuwa taarifa
iliyowashtua wengi. Katika wote hao
Dee plus pekee ndiye aliyeumia sana.
Alimjua mama wa Masimba kwa kuwa
waliishi jirani kabisa nyumba zao
zipakana kwa hatua tano tu. Hakutaka
kuliamini hilo katu. Akaona kulikuwa
na umuhimu wa kumpigia masimba.
Licha ya kupiga sana na simu kuita,
lakini simu haikupokelewa. Dee plus
akaamua kuipanga safari katika muda
ule kuelekea Handeni. Hakutaka
kuchelewa.. muda mfupi baadaye
alikuwa barabarani akielekea handeni.
Asingeweza kubaki Dar wakati Vibaoni
imepatwa na msiba. Aliitembeza gari
kwa mwendo wa kutisha, trafiki walio
jaribu kumsimamisha njiani walikutana
na kitanbulisho. Wakamuacha
aendelee kwenye safari yake. Saa tano
na nusu asubuhi alikuwa akiingia katika
viunga vya vibaoni. Alipokelewa na
umati wa watu sambamba na vilio.
Aliufungua mlango na kushuka.
Hakuongea na mtu zaidi ya kuongoza
mpaka nyumbani kwa kina masimba.
Alipokuwa akikaribia macho yake
yakakiona kitu ambacho kilitafanya
machozi ya mdondoke. Chini ya ardhi
ya nyumba ya Wanamchiwa mbele
kidogo ya uwanja wa nyumba, damu
nyingi ilikuwa imetuwama chini.
Akasogea mbele huku miguu
ikimtetemeka. Akaiangalia ile damu
kwa muda wa dakika mbili bila
kuongea kitu. Baada ya kuangalia
akageuka na kurudi ndani ya gari.
Akaliwasha gari na kuliondoa gari
kuelekea hospital ya Wilaya ya
Handeni. Moyo ulikuwa ukibubujikwa
na damu, hakuwahi kufikiria kama
Teddy angekuwa mnyama kiasi kile.
Moyoni mwake hata yeye akaapa
kumuondoa katika uso wa dunia hii.
Teddy lazima uilipe hii damu ya mama.
Lazima uilipe kwa gharama yote. Muda
mfupi alikuwa kwenye maegesho ya
magari hospital pale. Alishuka na
kukutana na makachero wengine
ambao walitoka Dar es salaam.
Akawasalimia, kisha akawapita na
kuelekea chumba cha kuhifadhia maiti.
Wakati anausukuma mlango kuingia
ndani.. macho yake yakatua juu ya
mwili wa mama wa masimba. Matundu
matano ya risasi yalikuwa
yamekiharibu kifua. Dee plus
akashikwa na butwaa.. miguu ikawa
mizito kupiga hatua. Akasimama
akiutizama mwili wa mwanamke yule
asiye na hatia. Punde mlango
ukafunguliwa akahisi kilio cha kwikwi
kikitokea kwa nyuma yake. Akageuka
taratibu kumtizama huyu anayelia.
Macho yake yakamuona masimba
akiwa ameshikiliwa huku na huko.
Alikuwa akitia huruma sana.. machozi
yalikuwa yakishuka kama maji.
Akamuangalia huku akisogea. Kufika
karibu yake akasimama mbele yake.
"Don.!!! Aliita Dee..
"Teddy amenilazimisha nimuue. Teddy
amekitafuta kifo ambacho nilikuwa
tayari kukighairisha. Wameniulia mama
yangu na kuwaumiza wanangu. Yaseer
yupo mahututi amesafirishwa leo na
makao, lakini france wameondoka
naye na sijui hali yake." Aliongea
masimba akiendelea kulia akitembea
kuelekea pale ulipo mwili wa mama
yake
******
Ulikuwa muda wa mazishi ya mama
yake. Alikuwa amesimama pembeni
akilia wakati masheikh walipokuwa
wakiuombea mwili wa mama yake.
Dada zake na kaka zake hawakuwa na
hali, kila mmoja alikuwa akigalagala
kwa vilio. Wajukuu na ndugu wengine
hawakukamatika. Kwa masimba
alikuwa bado haamini. Haamini kama
ndio mwisho wa mama yake. Taswira
ya mwamvita akimshuti mama yake
iliendelea kujirudia kichwani kwake.
Bado alikuwa akikunbuka risasi zili
zilivyomtupa chini mama yake.
"Mwamvita nitakuua kwa mikono
yangu." Akanong'ona taratibu. Swala
ya kuuswalia mwili wa marehemu
ikaendelea kama kawaida na mwisho
watu wakaubeba mwili ma marehemu
kuupeleka katika nyumba yake ya
milele. Umati uliohudhuria
ulimshangaza kila mmoja hasa wale
majasusi waliokuja kumpa msaada
masimba. Kila alipokuwa akitembea
taswira ya mwamvita haikuondoka
usoni mwake. Mazishi yakafanyika na
watu wote wakarudi nyumbani. Lakini
cha ajabu alipotafutwa masimba
hakuonekana. Hata kaka yake
samwebondo alipotumwa akamtizame
makaburini hakumuona. Na hakuwa
masimba pekee bali hata Dee plus
hakuwepo. Hilo likawashangaza wana
ndugu wote simu yake haikupatikana
na hata sehemu zote alizotafutwa
hakuonekana. Kila mmoja akaongea
anachokijua ili mradi tu. Masimba
hakuonekana hata usiku ulipoingia.
******
Upepo ulikuwa ukivuma mithiri ya
milipuko. Ndio kwanza Masimba
alikuwa akiingia katika jiji la dar es
salaam. Safari hii aliamua kuendesha
gari mpaka Bunju nje kidogo ya jiji la
dar es salaam. Kuelekea huko
kulitokana na kuogopa kundulika
mapema na watu wanaomtafuta.
Kingine kilichomsogeza Huko ni
ukaribu wa sehemu anapoishi
mwamvita. Aliendesha gari mpaka
bunju A nyumbani kwa Neema
Mtobwa. Aliipaki gari umbali mfupi
kutoka nyumba alioishi neema.
Akatembea kwa miguu mpaka usawa
wa jumba analoishi Neema. Hakutaka
kupitia mlangoni, alichupa na
kudondokea kwa ndani. Hapo
akatembea tena na kuufungua mlango
wa nyuma. Mlango ukamtiii!! Hapo
akaingia ndani bila wasiwasi.
Akatembea mpaka sebuleni. Hapi
akakutana na Neema mtobwa akiwa
amejilaza kwenye kiti. Akamsogelea na
kumtingisha. Neema akafumbua
macho yake, akajikuta akitizamana na
masimba. Akainuka na kumkumbatia
kwa nguvu. "Pole sana Masimba.
Nimesikia kutoka ndani kilichotokea.
Lakini kwa nini uko hapa wakati ndio
kwanza mama amezikwa leo!!!!@
aliongea neema aki0nyesha
kushangaa.
"Neema, mama yangu ameuawa na
hatarudi tena. Nitabaki vipi handeni
wakati waliomuua mama yangu
wanafurahi? Nimekuja kuwapeleka
kuzimu wakaungane na Mama
Yangu.""....
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1

 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 040
Neema alimuangalia masimba kwa
muda bila kuongea kitu. Alikuwa
akikiangalia kile ambacho kipo ndani
yake. Maumivu, majonzi na hata
machozi ni kitu ambacho alikisoma
ndani ya macho ya Masimba. Kingine
alichokiona ni hasira na utayari wa
kufanya chochote. Hakuwa na
lakuongea. Maneno yalimuishia
mdomoni. Akashuhudia masimba
akitoweka machoni mwake mithili ya
mzimu. Akitembea akionyesha
hakutaka mashauriano na mtu. Alikuwa
katika safari ya kumfuata Mwamvita
nyumbani kwake mbezi beach. Moyo
wake ulijaa uchungu, alikuwa
akitembea huku akibubujikwa na
machozi. Alikuwa akilia hasa pale
alipouona mwili wa mama yake
ukifukiwa. Akajua hatamuona tena.
Akajua hata muona mwanamke huyu
aliyemjali sana. Bastola zake bado
zilikuwa mahali tulivu. Akatembea
mpaka kituo cha daladala. Akajivuta
machozi kisha akatulia akisubiria
daladala. Muda mfupi akaiona daladala
ikija huku konda akipiganikiza vituo.
Ilipodimama alikuwa wa kwanza
kupanda. Baada ya kupanda akatulia
kwenye siti akitizama nje kupitia
dirishani. Kwa kuwa ulikuwa usiku ,
barabara haikuwa na foleni. Wakajikuta
wakitumia dakika saba kufika mbezi
Africana. Baada ya gari kusimama,
masimba akashuka taratibu na kuanza
kutembea taratibu kuelekea nyumba
anayoishi Mwamvita. Alitembea kama
mtu wakawaida na mwenye shughuli
zake akipishana na watu na hata polisi
wa Doria. Bado hakuwajali na bado
hakuwatizama. Akaingia uchochoro
fulani na kwenda kutokea mtaa wa pili
sehemu ambayo alikuta panabar.
Baada ya kutokea hapo kwenye bar,
akasogea hapo na kutafuta kiti. Kwa
kuwa ilikuwa sehemu kimya sana licha
ya kuwa na bar, lakini pia aliiona kuwa
ilikuwa sehemu nzuri yakutulia
kuuvuta muda akiwasubiri watu
wapungue aweze kuingia kwa
Mwamvita kwa Urahisi. Baada ya
kuvuta kiti akamuita mhudumu na
kumuomba ampelekee mzinga wa
Whisky. Mhudumu akafanya hivyo na
muda mfupi baadae Masimba alikuwa
akimimina kinywaji mdomoni huku
macho yake yakicheza kila kona. Kwa
kuwa sehemu aliyokaa ilikuwa na giza
aliweza kuwaona wote waliokuwa
wakiingia. Alitulia akiendelea kunywa
taratibu mpaka saa saba kasoro usiku
ndipo alipoondoka hapo akiifuata
barabara inayoelekea nyumbani kwa
Mwamvita. Alitembea kwa kufuata giza
mpaka nyumba ya pili kutoka nyumba
anayoishi Mwamvita. Akasimama hapo
akiitizama vizuri nyumba anayoishi
mwamvita. Nyumba yote ilikuwa giza
kasoro taa moja tu ya chumba ndio
ilionyesha kuwaka tu. Hilo alilitegemea
kwa kuwa alijua baada ya tukio lile
lazima mwamvita angejidhatiti.
Akaondoka hapo sasa akipiga hatua
kuelekea kule. Akauvuka uzia wa
nyumba ile, akajikuta sasa akitazamana
na nyumba ya mbaya wake.
Akatulia hapo kwa muda bila hata
kufanya chochote. Alikuwa akifikiria ni
nini afanye ili kuingia mle ndani.
Kuwaka kwa taa moja katika jumba lile
haikumfanya masimba ategeke. Siku
zote aliamini kuwa chumba
kilichowashwa taa hakikuwa na watu.
Watu walikuwa katika chumba kingine
kabisa. Hilo akaliamini na ndio
lililomfanya asimame. Aliamini
mwamvita alikuwa sehemu ndani ya
nyumba na sio katika chumba kile
kinachowaka Taa. Hilo likamfanya
umakini uongezeke. Safari hii bastola
aliishikiria mkononi. Akasogea mpaka
kwenye ukuta wa Jengo lile. Akauangia
ukuta ule kama atauweza. Baada ya
kujiridhisha sasa alikuwa akiuparamia
ukuta mfano wa nyani, muda mfupi
akaangukiwa ndani pasipokutoa sauti.
Baada ya kuanguka pale alijiinua
haraka mpaka upande mwingine.
Wakati akitembea alijikuta akijikwaa
kwenye ndoo za bati. Ukelele
ukatokea. Hilo likamuongoza masimba
mpaka chini ya mti. Akajibanza hapo
kuona kama kelele zile zingemleta mtu
pale. Ni kweli hakuwa mbali na
mawazo yake. Punde akawaona watu
watatu wenye silaha wakitokea pande
tofauti. Kila mmoja alikuwa akitokea
upande wake. Katika kitu ambacho
hakukitarajia ni kuwaona walinzi hao.
Kwa mara ya kwanza Hili
likamshangaza. Mwamvita kulindwa na
watu wenye silaha nzito. Hata
alipowaangalia watu hawa kwa uzuri
aliwatambua kwa karibu. Kuwatambua
huko kulampa picha ya
kinachoendelea. Walinzi waliokuwepo
pale walikuwa walinzi wanaomlinda
Chief. Hilo lilimaanisha chief alikuwa
hapo ndani. Hilo likamuongezea
umakini. Wazo kuwa Chief alikuwa
upande huu lilikigonga kichwa chake.
Lakini akalitupilia mbali baada ya
kuwaona watu wawili wakiufungua
mlango na kuchungulia Alikuwa Chief
akiwa sambamba na Mwamvita. Chief
alikuwa kwenye Bajama huku
Mwamvita akiwa kwenye mtandio
mwepesi uliofungwa kihasarahasara.
Bado macho ya masimba hayakutulia.
Yalicheza na walinzi wote na hata
wakati mwingine yakiwaangalia chief
na mwamvita. Mpango wa kumuua
mwamvita ulikuwa umekuwa mgumu
kutokana na uwepo wa Chief. Akaaona
haukuwa muda muafaka kwa siku ile.
Hakutaka kumfanya chief aelewe
kinachoendelea. Aliamua kuighairisha
hukumu ya mwamvita akiipanga
kufanyika siku inayofuata. Baada ya
walinzi wale kuangalia na kutokuona
kitu, wakaturudi kila mmoja katika
nafasi yake. Ni muda huo masimba
alipochupa na kutua nje kisha
kutokomea gizani.
*****
Alimbeba France mikononi akiondoka
katika nyumba ile ya siri. Ulikuwa usiku
wa saa saba Teddy alipoamua
kuondoka katika Jiji la dar es salaam
akielekea arusha kabla ya kuvuka
mpaka na mkuingia kenya. Alitembea
usiku ule kuogopa kugundulika mpaka
alipofika maeneo ya barabarani.
Akasimamisha pikipiki na kujipakia
kisha safari ya kibamba. Alitaka
kwenda kulala chalinze iwe rahisi
kuondoka pasipokujulikana. Hakujali
kazini kwani aliomba likizo ya miezi
miwili akisingizia kwenda kukaa
matanga kwenye msiba wa mama
mzazi wa mpenzi wake. Baada ya
dakika kumi na tano alikuwa kibamba.
Akashuka na kumlipa dereva wa
pikipiki kabla ya kusogea mbele kidogo
sehemu ambayo ilipaki gari aina ya
Noah. Baada ya kuifikia ile gari mlango
ukafunguliwa. Akampakia France kisha
yeye na baada ya hapo gari ikang'oa na
kuianza safari. Safari ya kuuhama mji
kwa muda. Alijua hasira za masimba
zingeisha mwilini mwake. Moyo wake
ulikuwa ukivuja kwa maumivu.
Machozi yalikuwa bado yakishuka.
Hakujua mwisho kama ingekuwa vile.
Tamaa ya pesa imeondoa utu wake.
Sasa alikuwa akiukimbia mji
alioupenda. Akimuacha mpenzi
kwasababu ya tamaa. Hakutegemea
hilo kabisa kichwani kwake.
*********
Ni asubuhi tulivu na yenye mawingu ya
hapa na pale. Masimba alikuwa
ametulia mahali akiitizama barabara na
watu wake. Alikuwa hapo baada ya
kuhaha usiku mzima akimtafuta Teddy
pasipokumuona. Alikuwa hapo
akiituliza akili yake akiwaza wapi
ambapo teddy alikuwa amekwenda.
Alijaribu kuwasiliana na Dee plus
kumuuliza kama alikuwa na fununu
kuhusu teddy na hata mtoto, lakini jibu
alilopewa halikumridhisha. Kwamba
teddy hakuonekana tokea mchana wa
jana. Hilo likampa shaka kuhusu
mwanawe france. Hakujua wapi teddy
alikuwa amempeleka. Hilo likaendelea
kumuumiza kichwa. Alichokifanya ni
kuondoka pale na kuingia mtaani
kunusa kama atapata chochote. Cha
kwanza alichoamua ni kuelekea
kijitonyama kuonana na Chief. Aliamua
kufanya hivyo ili kujua alipo mwanawe
na kuhusu kuweka angalizo katika
watu kujua kuhusu mwanawe. Kuhusu
france aliamua kumsaka kimya kimya.
Aliwasili kijitonyama pale na kulakiwa
kwa mshangao na baadhi ya
wanausalama waliomtizama. Kila
mmoja alikuwa na taarifa ya kuuawa
kwa mama yake mzazi. Kwa nini yuko
hapa? Yalikuwa maswali bila majibu.
Salaam na pile zikachukua sehemu
yake. Akawajibu kwa kichwa kisha
kuingia ndani. Baada ya hapo
akaongoza mpaka ofisini kwa Chief.
Hapo akakutana na pole nyingine
kutoka kwa sekretari wa Chief.
"Pole Masimba! !!...
"Nitapoa pale waliomuua mama yangu
nitakapo tumbukuza risasi zangu
kwenye vichwa vyao." alijibu masimba
alimuacha Dada yule akishangaa.
"Mzee yupo ama katoka? Akauliza
masimba. Kabla yule dada hajajibu
mlango wa ofisi ya Chief Ukafunguliwa.
Akatoka Mwamvita na Jimmy. Macho
yao yakakutana na macho ya Masimba.
MSHTUKO alioupata Mwamvita
Ulishuhudiwa na kila mmoja pale. Chief
ndiye aliyepigwa zaidi na butwaa.
Macho ya Masimba yalikuwa
yakimtizama Mwamvita. Alitamani
kumuua mbele ya watu. Alitamani
kumtafuna mbichi. Mikono yake
ilikuwa ikitetemeka kwa hasira. Hilo
Chief alilishuhudia hakuwahi kumuona
kijana wake akiwa vile. Alihisi lolote
litatokea, ni kweli mkono wa masimba
ulikuwa ukishuka mahali alipohifadhi
bastola yake. Tukio la kuuawa kwa
mama yake likajirudia tena na tena
kichwani kwake. Lakini chief
alimuwahi na kumshika mkono
akimtaka waingie ndani ya ofisi.
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1

 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 041
Chief hakukitegemea kile kilichotokea
pale. Mshtuko wa mwamvita na
mikono ya masimba kutetemeka kisha
kushuka chini ilikuchomoa bastola,
vilikuwa vitu vilivyomchanga. Yeye ni
jasusi mwandamizi. Kilichotokea pale
alihisi uwepo wa kitu kikubwa nyuma
yao. Akamuangalia Masimba kwa
makini sana. Alimuangalia akimsoma
uso wake. Alichokutana nacho
kikaitengeneza hofu, hofu ambayo
hakujua ilipotoka. Ni vipi amuogope na
kumjengea hofu kijana wake. Hilo
likampa ujasiri wa kutaka kumuuliza
Masimba. Wakati akitaka kuuliza,
masimba akainua uso wake na
kumtizama Chief. "machozi" ya
machozi yalikuwa machoni kwa
masimba yakishuka taratibu
mashavuni. Chief akaendelea kupigwa
butwaa. Masimba alikuwa akilia?
Masimba anadondosha machozi? Ni
kutokana na kifo cha mama yake au
nikule kukutana kwao na Mwamvita?
Kabla ya kupata majibu ya maswali
yake. Masimba akainuka na kutoka
ofisini huku nyuma akiubamiza mlango
wa ofisi ya chifu kwa nguvu. Hata hili
likikuwa Jipya kabisa kwake. Akauona
uhasama kati ya Masimba na
Mwamvita. Hilo likamfanya ahisi kuwa
mwamvita na masimba wanajuana
ama mwamvita anahusika na kifo cha
mama wa Masimba. Akatamani kuuliza,
alitamani kupata majibu kutoka kwa
watu hawa wawili. Lakini sana sana
kutoka kwa masimba ambaye alikuwa
ni kijana wake. Hata yeye alianza kuhisi
kitu kwenye kukutana kwake na
Mwamvita kabla hawajawa wapenzi.
Alijua ulikuwa mkutanishano wa
kimipango. Ulikuwa ni mpango
uliosukwa. Wazo hilo likamfanya
atamani kuchukua simu yake ili
kumpigia Mwamvita, lakini kabla
hajafanya hivyo mlango ukafunguliwa..
akamuona Masimba akirudi mle ndani.
Akamuangalia mkuu wake kwa muda
kisha kwa sauti yenye Hasira akanena.
"Ningejua Jana ningewaua pale mbezi.
Nilikuwa na uwezo wa kuwaua wote
kwa Risasi, lakini nilighairisha kutokana
na uwepo wako. Watu waliotoka humu
ndani ni wahusika katika mauaji ya
waziri mkuu. Na hata mama yangu
ameuawa kwa sababu ya hili suala.
Wameuchukua uhai wa mama yangu
kwa sababu ya hili suala. Nakamilisha
ushahidi ili nimlete Jimmy hapa. Cha
ajabu hata idara yetu inamtafuta lakini
leo unamleta. Sasa sikia leo nakuletea
kichwa cha Mpenzi wako mwamvita.
Nitamuua kwa mkono wangu. Yeye
ndiye aliyemshuti mama yangu mbele
ya macho yangu. Nitamuuua. Hili
nakwambia wewe na ukimwambia na
kusababisha apotee nitakuua wewe.
Nitakuua Chief Kama nilivyomuua
Waziri mkuu kutoka na ujinga aliokuea
akiufanya. Nimekwambia ili ujue kuwa
sishindwi chochote." Aliongea
masimba huku akilia. Aliondoka ndani
ya ofisi akiwamuacha Chief katika
mshangao. Mdomo uko wazi mshangao
ukitawala usoni kwake. Kwamba
Masimba ndio kamuua waziri, kwamba
waziri alikuwa akifanya upuuzi, ni
kweli ndio amefanya. Kwamba
Mwamvita ndiye amemuua mama wa
masimba mbele ya masimba? Lina
ukweli kiasi gani hili? Jimmy anahusika
na kifo cha waziri? Kwamba Masimba
Jana Aliingia nyumbani kwa
mwamvita? Yamekuwaje Haya?
Masimba amechanganyikiwa? Yalikuwa
maswali lukuki kichwani mwake.
Katika maswali hayo kile cha mwisho
ndicho kilichomtisha. Aliwalea vijana
wake lakini kuna kipindi walimtia hofu.
Akainua simu na kupiga sehemu tatu
tofauti. Baada ya hapo akatulia.
Hazikupita dakika tano mlango
ukafunguliwa. Aliyeingia ndani alikuwa
mwanamke. Tena mwanamke ambaye
hakuwahi kumjua. Huyu alikuwa
amevalia buibui liliuficha mpaka uso
wake. Mkonono alionyesha kushika
kitu mfano wa CD. Chief akamuangalia
mtu huyu kwa muda bila kuongea na
mgeni wake. Mgeni huyu aliyemvamia
ofisini kwake pasipo na taarifa.
"Chukua hii cd.. kuna vingi vitakusaidia
ikiwa ni pamoja na kumjua aliyemuua
waziri mkuu." Aliongea mwanadada
yule akiunyoosha mkono wake kumpa
chief ile CD. Chief akamuangalia yule
mwanamke kabla ya kuipokea CD na
kuiweka kwenye Droo. Alikuwa katika
kipindi kigumu sana. Imekuaje mtu
huyu amepata ruhusa ya kuingia humu
bila kuzuiwa.
*****
Wakati mwanamke yule mwenye
baibui akiingia ofisini kwa mkurugenzi,
masimba alikuwa amekaa ndani ya
jengo lile Akitizama mlango wa ofisi ya
Chief. Uingiaji wa mwanamke yule
ulimtia wasiwasi kutokana vazi lake.
Mwanzo alidhani labda ni kachero wa
hapo, lakini alipotoka mara hii mawazo
akayaondoa baada ya kuuona wasiwasi
machoni kwa mgeni huyu wa Chief.
Akamuacha amtangulie kwa mbele
kisha yeye kufuata nyuma. Mtu yule
alikuwa akitembea akigeuka kila
wakati hofu yake akiona kama
anatafutwa. Masimba bado alikuwa
akimuangalia kwa umbali wa hatua
kama Hamsini. Wakati mtu yule
akiuendea mlango wa mwisho kabla
hajalifikia geti, masimba alishapita kwa
njia nyingine na kutokea sehemu
tofauti kabisa na Eneo lile. Akatulia
katikati ya watu wakiongea huku
macho yake akitizima pale pale
kwenye mlango. Alikuwa amemlia
mashaka mwanamke yule. Alitambua
alikuwa ametoka mahala na alikuja
pale ofisini kwa Chief kuleta kitu fulani.
Mashaka hayo yalitokana na
mwanamke yule kuonekana ni
mwenye wasiwasi wakati wa kuingia
na hata kutoka. Muda mfupi akamuona
yule mwanadada akitoka pake nje,
akaanga angaza huku na huko. Baada
ya muda akaonekana ikisimamisha tax
kisha kuondoka eneo lile. Masimba
akaendelea kutulia. Alijua na kuhisi
kuwa mwanamke yule hakuwa peke
yake. Alijua lazima kuna watu mahali
fulani wakitimzama na kumfuatilia kwa
kila kitu anachofanya. Aliendele kutulia
akiangalia hilo. Ni kweli alichokuwa
akikiwaza kwani baada ya dakika mbili
kupita tokea mwanamama yule
aondoke, akawaona watu watatu
wakiondoka kutokana katika sehemu
fulani na kuongoza wakitembea kama
watu ambao hawakuwa wakijuana.
Aliwaangalia watu wale akiwa bado
amekaa hap0. Alikuwa amehisi uwepo
wa mtu ama watu wengine eneo hilo.
Ni kweli kama mwanzo wanaume
wawili wengine wakasimama na
kuanza kuondoka lakini hawa
wakienda uelekeo tofauti na watu
waliowatangulia. Hilo sasa likampa
uhakika kwamba kina Jimmy ni wengi,
licha ya wingi huo lakini aliamini Siku
ilikuwa siku ya mwisho yaMwamvita
kuivuta hewa ya mwenyezi Mungu.
Alipohakikisha hapakuwa na watu
wengine wakuwatilia shaka, masimba
aliinuka na kusogea barabarani nia
ikiwa ni kuisubiria tax iliyoondoka na
yule mwanamke. Alisubiri kwa dakika
kumi nzima lakini hakuiona ile tax
ikirudi. Hilo likampa wasiwasi kuwa
huwenda dereva yule ameshauawa
mpaka wakati huo. Wakati akiliwaza
hilo akaiona ile tax ikitokea kwa mbali.
Kwa kuwa alikuwa amekalili namba za
gari haikuwa shida. Alisimama
barabarani na kupunga mkono. Baada
ya hapo tax ikasimama. Masimba
akaisogelea na kuufungua mlango wa
nyuma. "Nipeleke ulipompeleka yule
mwanamke. " aliongea masimba bila
kuongeza neno lolote. Dereva akitii
akawasha gari na safari ikaanza. Kila
mmoja alikuwa kimya, dereva akiwaza
pesa masimba alikuwa akiwaza kuhusu
mwanamke aliyeingia na kutoka Ofisini
kwa Chief. Kitu kwamba Chief
amepelekewa kitu na kupewa
shinikizo ni kitu pekee ambacho
kiligonga kichwa chake. Hakuwahi
kumuona wala kumjua mwanamke
yule. Hilo likampa uhakika kuwa Jimmy
alikuwa ameongeza watu
wakumsaidia. Wakati wamefika Sinza
kumekucha Masimba akamuona
mwanamke akitembea pembezoni
mwa barabara. Huyu alivaa suruali ya
Jeans na Tishirt yake nyeupe. Chini
alikuwa amevalia raba nyeupe
sambamba na miwani ya juu ilionekana
kwa watu wengine lakini kwa Masimba
ikionekana ni miwani maalum
inayovaliwa na majasusi. Licha ya
mwanamke huyu kujibadilisha
kimavazi lakini hakuweza kumpoteza
masimba. Alikuwa ni mwanamke
aliyetoka ofisini kwa chief muda mfupi
uliopita. Akamwambia dereva yule wa
Tax aisimamishe gari pembeni mwa
kituo fulani cha tax. Dereva akatii kwa
kusimamisha gari. Masimba akalipa
kisha kushuka bila kuongea kitu. Muda
wote macho yake yalikuwa kule kwa
yule mwanamke. Alitembea kwa
umakini akikwepa kuonekana. Safari ya
mwanamke yule ikaishia kwenye
saloon moja ya kike pale pale
kumekucha. Masimba akatulia
pembeni umbali wa hatua mia
akiangalia kule kwenye saloon ile ya
kike. Akasubiri kwa dakika kumi nzima
lakini hakumuona mwanamke yule
akitoka. Hilo likampa wasiwasi
mkubwa sana, muda mfupi alikuwa
akimuita kijana mmoja ambaye
alikuwa anapiga Debe pale kituoni.
"Mambo vipi mzee!!? Akasalimu
masimba baada ya kumuita mpiga
debe.
"Fresh mkuu, nipe dili mwana." Akajibu
mpiga debe yule.
"Kuna kitu nataka nikuulize lakini kabla
sijakuuliza kamata hii."alisema
masimba huku akumkabizi kijana yule
noti ya Elfu kumi. Kijana yule
akaipokea huku akimuangalia Masimba
usoni.
"Duh respect mwana niulize tu
nitakujibu kama nitakuwa najua
chochote. Aliongea yule mpiga debe
akionyesha kutabasamu kwa noti ile.
"Nahitaji kuhusu ile saloon pale.
Akaongeza masimba huku
akimuonyeshea kidole kuelekea ilipo
saloon.
"Wewe ni Njagu au ni mwana
usalama?" Akauliza yule teja huku
akionyesha hofu kwa mbali. Hilo
likamvutia Masimba. Akakiona kitu cha
kufanya.
"Hapana mimi sio njagu wala Usalama
wa Taifa. Mimi ni mtu wa kawaida.
Nimekuja hapa na dada mmoja muda
mfupi uliopita. Ameingia pale ndani
lakini mpaka sasa simuoni akitoka."
Alijieleza masimba akimtoa hofu. "Ooh
wewe ndio umekuja na Dada V...? Aaah
kwani hujui kinachoendelea mle
ndani? Pale ni saloon kwa nje lakini
palepale kuna mlango wa kutokea
nyuma anbapo hapo kuna vigogo
wengi wa serikali. Akajibu teja.
"Wanafanya nini Hao Vigogo? Au kuna
danguro? Akauliza Masimba akijifanya
hajui chochote kinachoendelea.
"Wewe kweli mgen.... akakatisha
maongezi baada ya kumuona
mwanamke mmoja akitoka. Hilo
likamvutia Masimba kutizama kule.
Macho yake yakavutiwa na mwanamke
aliyetoka mle ndani. Hakuvutiwa
kimapenzi bali alivutiwa kwa kuwa
alikuwa ni mwanamke yule yule
aliyeingia muda mfupi uliopita.
Alionekana akuangaza huku na huko
kama ni mwenyekutafutq kitu, punde
akarudi tena ndani. Haikupita hata
dakika, akawaona vijana wengine
watatu tena wa kiume wakitoka. Hawa
walionekana ni kama wale wakongo
wanaokaa kwenye masaloon hapa
mjini. Lakini muonekano wao
haukufanana na watu hao. Masimba
akaiona hatari ya kuendelea kuwa
pale. Akamuomba Yule mpiga debe
amuelekeze anapoishi ili aweze kurudi
usiku kuongea naye chochote. Mpiga
debe yule alimtajia Masimba mtaa na
sehemu anayoishi. Baada ya hapo
akatoa Noti mbili za elfu kumi kumi na
kumpa huku akimuachia onyo la
kutokumwambia yoyote kile
walichoongea. Baada ya hapo Masimba
akaondoka pale kurudi anapoishi kwa
maandalizi ya kurudi usiku kwa
maswali zaidi pia na kazi zaidi.
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1

 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 042
Hakutaka kugundulika mapema
kwamba alikuwa katika viunga vile.
Kutazama kwa mwanamke yule
kulimpa mashaka kwamba kuna kitu
atakuwa anakitafuta. Akamuaga teja
yule na kuondoka katika eneo lile la
Sinza. Safari hii akaamua kuelekea
nyumbani ili aanze kwanza kumtafuta
Teddy na kujua wapi alipo mwanawe
France. Muda wote alikuwa
akiikumbuka sura ya mama yake. Alijua
mama yake angeamka siku yoyote na
kuwa hai tena. Hakujua kuwa mama
hakuamka na kamwe hataamka. Kwa
mara ya kwanza tokea asubuhi
akamkumbuka Dee plus. Alitaka kujua
wapi alipofikia kuhusu wapi teddy
alipo. Lakini hakutaka kufanya pale
pale, alitaka kusubiri afike nyumbani
kwanza ndipo angemtafuta. Alifika
nyumbani kinondoni kigiza kikiwa ndio
kwanza kinaimeza nuru ya mchana na
kuukaribisha usiku huu tulivu kwa
wengine. Nyumba yake ilikuwa kimya
kuonyesha kutokutembelewa na mtu,
achilia mbali kuishi watu. Aliiongoza
mpaka getini bila wasiwasi, akajaribu
kulisukuma geti la kuingilia,
akashangaa likufunguka "mtego"
lilikuwa neno la kwanza kutamkwa
katika kinywa chake. Akafungua geti
taratibu na kuingia ndani. Hapo
akakutana na mwanga hafifu kutokana
na kumezwa na kugiza kile cha saa
moja usiku. Bado ukimya ulitawala na
bado kengele za hatari ziliendelea
kukigonga kichwa chake. Akatembea
safari hiii bastola ikiwa mkononi.
Alitembea taratibu akiufuata mlango
wa kuingilia ndani ya nyumba. Akili
yake ilikuwa ikimwambia kuna hatari.
Mawazo yake yalikuwa yakimwambia
kuhusu hatari. Hakutaka kupuuza
katika hilo. Umakini ukaongezeka zaidi
na zaidi. Alipoufikia mlango akajaribu
kuufungua. Cha ajabu mlango
ulifunguka kuonyesha kuwa haukuwa
umefungwa. Akaingiza kichwa na
kuchungulia ndani. Hapo akapokewa
na giza tototo ambalo halikumsaidia
kuona chochote. Akaufungua mlango
zaidi akaingia mwili wote. Akatembea
mpaka kwenye swichi na kuwasha taa
zote mle ndani. Baada ya kuwashataa
akajikuta akidhangaa baada ya kuona
matone ya damu sakafuni. Hilo lilikuwa
jambo ambalo hakulitegemea.
Akaendelea kuangalia kwa umakini
huku Bastola mkononi. Alitembea
kufuata matone yale ya damu. Bastola
ilikuwa ikitangulia. Kila alipokuwa
akigeuka hata bastola iliangalia huko.
Matone ya damu bado yaliendelea.
Moyo wake ulikuwa ukidunda akihisi
labda mwanawe France alikuwa
ameuliwa na Teddy. Akahisi jasho
likimvuja pale alipoyaona matone yale
yakiishia nje ya mlango wa chumba
chake. Hapo akasimama na kuivuta
pumzi. Punde akausukuma mlango na
kuangukia ndani. Macho yake yakatua
Juu ya mwili wa mtu. Ukelele wa Hofu
na uchungu ukamtoka. Dee plus
alikuwa amelala kifudi fudi sakafuni,
mwili wake ukiwa hautananiki kwa
kuchakazwa na risasi. Akahisi bastola
ikimponyoka na kudondoka chini.
Hakuamini macho yake. Akausogelea
mwili wa Dee Plus na kupiga magoti
mbele yake. Mikono yake ikatamani
kuushika mwili ule lakini mikono
haikumruhusu. Alikuwa akitetemeka
kwa hasira. Alikuwa akitetemeka kwa
hofu ya kuuawa hata kwa wanawe.
Alimtegemea Dee plus katika vita hii.
Alimtegemea Dee plus katika
kumsaidia hili. Leo alikuwa amepiga
magoti mbele ya mwili wake. Ni jana
tu walikuwa wakimzika mama yake,
lakini leo na yeye alikuwa marehemu
tena akiwa ameuliwa kinyama.
Masimba akautizama mwili wa Dee
plus zaidi na zaidi. Wakati akiutizama
mwili wa Dee, akakiona kitu mfano wa
picha pembeni kwa mwili wa Dee.
Huku mikono ikimtetemeka
akanyoosha na kuichukua ile picha.
Kuitizama tu, akahisi machozi
yakimdondoka. Ilikuwa picha yake
akiwa pamoja na watoto wake na
mama yake pamoja na Tedy.
Kilichomchanganya ni kukuta katika
picha ile kuna sura za watu wawili
zimepigiwa alama ya X. Sura ya
kwanza ilikuwa ya mama yake mzazi.
Picha ya pili ilikuwa ya mwanawe
France. Ina maana France wamemuua?
Lilikuwa swali lililomuasha masimba.
Lilimuamsha kutoka kwenye kulia
mpaka kwenye umasimba wake.
Masimba yule ambaye hajawahi
kukiogopa kifo. Akaitizama ile picha
kwa muda, kisha achovya kidole chake
kwenye Damu ya Dee plus na kuchora
alama ya X kwenye picha ya Teddy.
"Nitakuua Teddy, Nitakuua kabla ya jua
la kesho." Alitamka masimba huku
akiinuka akiutizama mwili wa Dee plus.
Hakuwa akiamini mpaka muda ule.
Mama kisha Dee plus harafu mwanawe
France ndani ya siku mbili. Akaona huu
ni wakati wakuacha kuutafuta ushahidi
wa waziri mkuu katika uhusika wake
katika biashara ya madawa ya kulevya.
Alitaka kudili na uandaaji wa tiketi kwa
sababu ya kuwasafirisha watu watano.
Alikuwa ni lazima aandae tiketi hizo
katika muda unaotakiwa. Ni lazima
Mwamvita aondoke, ni lazima Jimmy
apotee, Teddy lazima afutike katika
uso huu wa Dunia. SURESH NA BEN nao
wanatakiwa kwenye safari hiyo. Sasa
hakutaka kwenda kwa yule teja,
aliamua kumtafuta Mwamvita. Hawezi
kumuacha aendelee kuivuta hewa
wakati mama yake alikuwa amelala
kaburini. Atamuachaje Teddy wakati
alishaufumba mdomo wa france na
Dee plus? Hakuwa tayari kuutafuta
ushahidi. Alitaka kuua kwanza kisha
ndio afanye alichotakiwa kufanya.
Akaona amuarifu chief juu ya kifo cha
Dee Plus. Akafanya hivyo katika muda
ule, kisha akaongeza na kusisitiza
kuhusu kile alichomwambia kuhusu
Mwamvita. Chief akaitikia kanakwamba
yeye ndiye alikuwa mfanyakazi wa
chini. Akiitikia huku akihisi kuvurugwa
kwa kile alichokisikia. Akauona
umuhimu wa kuwaweka walinzi
kadhaa katika chumba alichokazwa
Mtoto wa Masimba. Sasa hakuwa
akiwaamini hata watu wa chini yake.
Alijikuta kila kitu akitaka kukifanya
yeye. Hakutaka hili suala lifike popote.
Aliamua kuuufumba mdomo wake
huku akifuata angalizo alilopewa na
Masimba la kutomwambia Mwamvita
chochote. Sasa alikuwa amekaa kimya
na kushika tama.
*****
Moyo wake haukuwa tayari kuwaacha
watu hawa wakiwa hai. Alijaribu
kumtafuta Mwamvita kila sehemu
lakini hakufanikiwa kumuona popote
pale. Hapo akaamua kumshirikisha
Chief katika hili. Alitambua lazima
kutakuwa na mawasiliano kati yao.
Safari hii hakutaka kumpigia simu,
alitaka kumfuata nyumbani kwake kwa
kuwa alitaka kupata taarifa kwa kina.
Akaondoka kule mafichoni kwake na
kuelekea mpaka masaki. Kufika hapo
akaambiwa Chief hayupo ameelekea
ikulu kuitikia wito. Hilo likamfanya
atulie kwa muda akitafakari nini cha
kufanya. Alihitaji kujua alipo mwamvita
na Hata Teddy. Lakini mpaka muda huo
hapakuwa na fununu ya wapi walipo
watu hawa. Hapo ndipo alipoona
umuhimu wa kumfuata yule Teja kule
Tandale kwa mtogole mtaa maarufu
uitwao Yemen. Alihisi kama kwenda
huko kunaweza kumpa taarifa ama
kunusa chochote kinachohusiana na
Mwamvita na Hata Teddy. Alipenya
chochoro hii na Chochoro ile. Punde
alikuwa amefika katika eneo hilo
ambalo kwa hapa Dar es salaam
liliogopeka sana Hasa kutokana na
kuwa na wapiga kabali wenye uzoefu
mkubwa kuliko sehemu yoyote hapa
Tanzania. Akapita kwenye chochoro
nyingine mpaka kuibukia kwenye
nyumba ambayo alikuwa akiishi Teja
yule. Ilikuwa nyumba nzuri ambayo
kama ungewahi kuiona usingeamini
Teja yule alikuwa akiishi katika
nyumba ile. Ukimya ulikuwa
umetawala huku kukionyesha kuwa
Watu walikuwa wamelala mle ndani.
Akaugonga mlango mara ya kwanza
kisha mara ya pili. Akaisikia sauti
kutoka ndani ikiuliza.
"Nani huyo?
Hakujibu bado alikuwa akuugonga
mlango. Punde akasikia nyayo za mtu
zikisogea mlangoni. Harafu komeo
likasikika likifunguliwa kwa ndani. Sura
ya mwanaume wa makamo ikatokea.
"Shikamoo mzee wangu!! Alisalimia
Masimba.
"Marahaba, karibu ndani. Aliitikia mzee
na kukaribisha. "Nilikuwa namuuliza
Vickita Visenti kama yupo. Alisaili
Masimba akimuangalia yule mzee
usoni.
"Huyu kijana leo naona ameuliziwa
sana. Muda sio mrefu walikuja
mwanaume na mwanamke
kumuuliziA, Sasa nakuona na wewe!!!.
Nenda kule mwisho upande wa kulia
ndio chumba chake kulipo." Alitoa
maelezo yule mzee huku
akimuonyesha masimba kwa kidole.
Masimba akaingia ndani na kuongoza
mpaka kule alipoelekezwa. Kufika
mlangoni akasimama na kuchungulia
ndani kupitia tundu la ufunguo. Jicho
lake likatua kwenye mwili wa Yule teja
akionyesha kulala. Baada ya kuona
hivyo akaushika mlango na kuufunguq
taratibu na kuingia. Kuingia
kulikofuatana na Kutupa maji pale
Kitandani. "MICHIRIZI YA DAMU" Ndicho
kitu peker kilichoonekana pembeni
mwa Vickita.
MASIMBA AKACHOKA
Maelezo ya picha hayapo.

 
Mwendelezo lini? Maana kila wakati tunachungulia mpaka tunaanza kufikiri kuwa mwandishi kapatwa na jambo baya.
 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 043
Mwili wa tejayule ulikuwa umelala
kanakwamba alikuwa kwenye usingizi
wakawaida, ukimuangalia juu juu
unaweza kudhani alikuwa usingizini
lakini michirizi YA damu pembeni mwa
ule Mwili ndio kitu kilichomwambia
masimba kuwa mtu yule alikuwa
ameshasafirishwa kwenda kuzimu.
akaufungua mlango akaingia ndani
nakuurudisha mlango akabaki ndani
akiutizama Mwili wa kijana yule. kisu
kidogo kikiwa kifuani kwa kijana huyu.
kwa mara nyingine alikuwa
amewahiwa na watu wale. watu
ambao walianza kumtia hofu nakujua
kuwa alikuwa akionekana kila mahala
alipokuwa akipita . akasogea mpaka
kitandani alipo mwili wa kijana yule.
wakati akitembea taratibu ndani ya
chumba, macho yakagota kwenye
pazia la dirisha. hapo akauona uwazi
ambao aliutilia mashaka. uwazi
uliokuwepo ulikuwa na uwezo wa
kupitisha mdomo wa bastola .
akasimama kwanza akikitizama hicho.
baada ya kutizama sana akageuza
macho kuuangalia tena mwili wa
kijana. hapo akakiona kitu kilichofanya
kengele za hatari kugonga kichwani
Kwake. usawa wa kusimamia mtu
endapo atataka kuuchunguza mwili
ndio usawa ambao uliachwa uwazi.
masimba hakuwa mjinga kiasi hicho.
aliujua mtego, aliujua kwa kuwa kama
angesogea mbele zaidi basi risasi
kutoka kwa mtu ambaye alihisi
kuwepo kwake kwa nje ya chumba
kile. alichokifanya nI kurudi nyuma
nakuizima taa kisha kuondoka taratibu
bila kupiga kelele. akatokea sebuleni
na kuondoka kwa kutokea mlango wa
mbele. hiyo ilikuwa mbinu ya kijasusi,
siku zote unapoingia sehemu ukakuta
kuna tukio la kutisha kisha ukaiona hila
fulani ndani yake, unachotakiwa
kufanya ni kutoka hapo kwa kutokea
mlango ulioingilia kwanI kwa
mazingira ya kifo kilichotokea watu
wanaweza kukutengenezea "mlango"
wa kifo kwa kutumia kifo kilekile
kilichotokea. aliujua akipita mlango wa
uani unaweza kuwa mtego kwake kwa
kuwekewa mazingira ya kupigwa
Risasi. Alitembea taratibu safari hii
akiamua kuwatafuta Teddy Harry na
mwamvita kwa sabab ya kuwaondoa
hapa chinI ya jua. bado tukio la
kupigwa risasi kwa mama yake na
kuuawa kwa Dee Plus lilikuwa
likikisumbua kichwa chake. alitembea
usiku ule akihitaji kuelekea mbezi
beach anapoishi mwamvita alitambua
kuwa Angeweza kumpata kwa wakati
ule. alikuwa MakinI kwa kila hatua,
alikuwa akitembea na damu ya watu
nane mikono mwake. Alihitaji kuilipa
damu iliyomwagwa kwa mikono yake.
alikuwa pekee Katika HilI. Alitakiwa
kulimaliza pasipokuimwaga damu ya
mtu mwingine. Hakutaka kumshirikisha
mtu katika hili. Hakumuamini mtu
kabisa. Kwa alichotendewa na Teddy
hakutaka kumuamini tena mtu.
Alumpenda teddy, akamthamini kutoka
ndani ya moyo wake. Lakini Teddy
hakuliona hilo. Akafanya usaliti na kuja
kumuua mama yake mzazi. Akaona
haitoshi akawajeruhi watoto ambao
hawakuwa wakijua chochote
kilichokuwa kikiendelea. Alitaka
kuutumia usiku ule kuichukua roho ya
mwamvita. Hii ilikuwa mission ngumu
kwake, mission ambayo haikuwa na
msaidizi. Hakutaka kumtafuta msaadizi
kutoka idara nyeti ya usalama. Mama
yake alikuws amelala na hata Dee plus
hakuwa macho tena. Mara hii alikuwa
akipita pale Lugalo military Base usiku
ule. Alikuwa akiiangalia kambi ile.
Kambi iliyompokea kwa mara ya
kwanza wakati alipotoka kwenye
mafunzo ya awali. Kambi ambayo
ilimpa ujasiri na nguvu ambazo
ziliwafanya wakuu wake wamhamishie
Idara ya usalama wa Taifa. Aliitizama
kambi ile kwa makini sana.
Akamkumbuka major general Hayati
Imran Hussein kombe, ambaye alikuja
kuwa mkurugenzi wa Idara ya usalama
wa Taifa. Ndio huyu aliyekuja kuuawa
na polisi walipomhisi kuwa alikuwa
mwizi wa magari. Licha ya
kujitambulisha kwake lakini polisi wale
walimpiga risasi mbele ya mkewe.
Mkewe pekee ndiye aliyepona baada
ya kutoroka kupitia kwenye mashamba
ya mahindi. Hata pale wauaji
walipohukumiwa kifungo cha
kunyongwa lakini walikuja kuachiwa
huru pasipo maelezo yoyote. Kuliwaza
hilo likamtoa machozi.. Punde alikuwa
akiipita lugalo na kukipandisha kilima
cha kuifikia Mbezi. Baada ya kufika
tangi bovu, akamuomba Dereva yule
amshushe hapo. Dereva akaegesha
pembeni kisha kumruhusu masimba
kushuka. Baada ya kushuka alimuacha
yule dereva aondoke, kisha naye
akaondoka pale akitembea kwa miguu.
Ulikuwa usiku wa malipo na usiku wa
kupeleka tiketi na hata usafiri. Mbezi
yote ilikuwa kimya sauti za pekee
zikisikika. Hapakuwa na sauti ya mkazi
ama mpita njia yoyote yule isipokuwa
magari machache tu yaliokuwa
yakipita barabarani.. alitembea na
kivuli cha miti wakati mwingine
akikwepa taa za magari mpaka
alipoifikia Africana. Kufika hapo
akaangalia huku na huko lakini leo
hapakuwa na watu, kwani hata ile bar
ambayo jana aliikuta wazi. Leo ilikuwa
imefungwa na hapakuwa na kitu
chochote. Wakati akiendelea
kuchunguza hiki na kile, mara akauona
mwanga wa taa za gari zikusogea
maeneo yale. Akajibanza kwenye
jumba fulani bovu, hapo akaliona gari
ya kifahari ikipita. Aliitizama kwa
sekunde kazaa akaondoka pale
akiifuata nyuma nyuma. Alikuwa
akihama hapa na kuhama pale. Alikuwa
akitembea kama mcheza sinema.
Mpaka gari ile inasimama Nje ya geti la
jumba analoishi Mwamvita, masimba
naye alikuwa umbali wa hatua tatu tu.
Mlango ukafunguliwa akashuka
mwamvita akiwa sambamba na watu
wawili. Kati ya hao mmoja tu ndiye
aliyemtambua. Alikuwa yule
mwanamke alikuja ofisini kwa chief
mchana ule na ndiye aliyehusika na
kifo cha yule teja. Wote wakaingia
ndani pasipokuacha mtu yeyote nje.
Ulikuwa muda wa sekunde mbili
zilizotumiwa na Masimba kuifunua buti
ya gari na kujitupa ndani yake. Akatulia
kama Dakika mbili akawasikia watu
wakirudi wakiongea.
"Huyu Teddy itabidi itafutwe popote na
kuuawa. Hawezi kujiondoa katika
mpango huu. Ni lazima mzigo tuupate
na lazima Masimba na Teddy
tuwasafirishe kuzimu. Nimejisikia raha
sana kumuua Dee kwa mkono wangu.
Ndio maana hata mama wa masimba
alipoleta ujinga sikumkopesa. Teddy
atafutwe popote sambamba na yule
mtoto." Alijitapa mwamvita bila kujua
maneno yake yalikuwa yakimchoma
Masimba. Alitamani kufungya buti na
kutoka. Lakini kitendo cha kusikia
teddy haonekani, kilimpa faraja ya
kutambua kuwa France alikuwa hai.
"Teddy tutampata nyie msijali.
Tunachotakiwa kufanya ni kuendelea
kumlaghai Chief aweze kuitisha
Mkutano na Wana Habari ili aionyeshe
ile video inayomuonyesha Masimba
akimuua waziri. Tukilifanikidha hilo
tutakuwa tayari." Akaongea
mwanamke mwingine huku wakiingia
kwenye gari na muda mfupi akaliona
gari likitembea. Hakujua wapi
walipokuwa wakielekea. Na pia
hakuwa akiyasikia tena mazungumzo
ya watu wale. Muda wote alikuwa
akifikiria jinsi ya kulimaliza hili. Ilikuwa
ni lazima azuie chief kuitisha mkutano
na waandishi wa habari na pia
alitakiwa kuizuia hiyo video ama aipate
na iwe mikononi mwake. Alikuwa
lazima afanye hivyo huku akiamini
kuwa angemsaka Teddy hata pale
atakapo wamaliza hawa. Gari ilitembea
kwa dakika kama Ishirini na tano ama
thelathini. Ghafla akasikia likipunguza
mwendo na kupiga honi kadhaaa. Mara
lango likafunguliwa akahisi gari
ikiingizwa ndani. Punde gari ilikuwa
ikisimama. Akaisikia milango
ikifunguliwa kisha akasikia hatua za
watu zikitembea kuelekea ndani.
Baada ya ukimya fulani kutawala,
akafunua buti na kuchungulia kwa nje.
Hapo akauona uwazi wa kuweza
kutoka. Sekunde ya pili alikuwa
akiangukia pembeni na kuchupa tena
mpaka sehemu fulani ambayo ilikuwa
na mbaombao. Akatulia hapo kwa
muda akitazama kila kitu
kinachoendelea mle ndani. Alikaa hapo
kwa muda wa kama dakika tano
akawaona watu walewale wakitoka.
Wanne kati yao wakajipakia ndani ya
gari lakini Mwamvita hakufanya Hivyo.
Baada ya maongezi Mawili matatu gari
ile ikaondoka huku mwamvita yeye
akirudi ndani. Baada ya mwamvita
kuingia Masimba naye aliianza
kutambaa kwenye ukuta mpaka
penbeni mwa jumba lile. Kufika hapo
akaliona dirisha Moja la kioo likiwa
wazi. Akasogea mpaka hapo na
alipolifikia akachungulia kwa ndani.
Macho yake yakakutana na mwamvita
akiwa hana hata nguo maungoni
mwake. Alikuwa akielekea bafuni
kuoga. Baada ya Mwamvita kutoka mle
chumbani Masimba akasogeza kioo na
kujitumbukiza ndani tayari kumsubiri
mwamvita. Akachepuka mpaka kando
ya mlango na kutulia hapo. Akatulia
hapo kwa Dakika Tano. Punde akasikia
nyayo za mtu zikisogea pale mlangoni.
Punde akamuona mwamvita akiingia
akiwa mtupu vile vile.
No photo description available.

 
NITAKUPA TU
SEHEMU YA 044
Punde akamuona Mwamvita Akiingia
tena akiwa mtupu. Alikuwa kama
alivyozaliwa. Hilo halikumfanya
masimba ashtuke. Bado alitulia huku
bastola yake aina ya Revolver colt 48
ikiwa mkononi. Akamuacha mwamvita
aingie kwanza. Na alipohakikisha
ameingia Masimba akaufunga mlango
kwa ndani. Mwamvita hakukitegemea
kitendo hicho. Kwani baada ya kuusikia
mlango ukifungwa akageuka akiwa
mtupu vile vile. Akakutana na Mdomo
wa bastola ukimtizama. Alikuwa
akiangalia na masimba. Alikuwa
akiangaliana na mtu ambaye alijua na
kuhisi labda alikuwa Tanga kwenye
mzima. Masimba hakuongea wala
hakuwa anafanya chovhote. Bado
alimuangalia Mwamvita kwa utulivu
huku macho yake yakicheza pande
zote. Kidole kikashuka taratibu kwenye
kitufe cha kufyatulia Risasi. Rukia
alikuwa akitokwa jasho jingi, alikuwa
akikiogopa kifo. Akatamani kuongea
kitu lakini akashindwa. Punde risasi ya
kwanza akafyatuka na kutua kwenye
kifua cha mwamvita. Risasi ya pili
ikatua kichwani na kukifumua kichwa
cha Mwamvita. Risasi ya tatu na nne
zilitua kwenye matiti yake yote. Kila
ilipokuwa akiifyatua risasi alikuwa
akikumbuka kifo cha mama yake.
Alikuwa akipiga risasi kwa Hasira, mwili
mzima wa mwamvita ulikuwa
umetapakaa damu. "Wasalimie
kuzimu.. waambie bado naendelea
kuwakusanya wote tayari kwa
kuwapeleka huko." Aliongea Masimba
huku akiuangalia mwili wa mwamvita.
Baada ya kuhakikisha mwamvita
amekwishakukata roho akauacha mwili
pale pale kitandani kisha yeye akatoka
Nje kupitia pale pale Dirishani. Safari hii
aliamua kurudi Sinza kumekucha tayari
kukijua kile ambacho kinaendelea
ndani ya Saloon ile kilichosababisha
mpaka Teja yule kuuawa. Alifanikiwa
kutoka pasipokuonekana. Akaanza
kuutafuta usafiri katika eneo lile
ambalo bado hakujua ni wapi.
Alitembea usiku usiku pasipokupata
usafiri mpaka karibu na kijimji fulani
Hivi. Hapo akafanikiwa kuiona pikipiki
ambayo ilikuwa akipita. Alichokifanya
ni kuisimamisha kisha kuwambia
Dereva wapi anapoelekea. "Duh Bro
mbona Huku ni Mbali sana na Sinza!!
Alishangaa Dereva yule huku akianza
kuonyesha wasiwasi Juu ya Masimba.
Ndio kwanza masimba alikuwa
akishtuka kwamba kumbe hakuwa
ndani ya Jiji. "Kwani hapa ni wapi
ndugu Yangu? Hatimaye Masimba
akauliza huku akitabasamy ilikumtoa
hofu kijana yule. "Hapa ni Bagamoyo
brother, kwani unatokea wapi? Akajibu
kijana yule kisha kuuliza tena.
Ikabidi masimba adanganye ili kupata
usafiri wa kumrudisha jijini Dar es
salaam. Hakutaka kuchelewa kwa
kuwa bado kazi ilikuwa ngumu. Bado
alikuwa na mission ngumu sana katika
usiku. Usiku wa malipo ya damu ya
watu wasio na hatia. Alitamani sana
kuwamaliza wote kwa usiku ule ili
aanze kumtafuta Yule Malaya Teddy.
Alitaka kumuua mwisho kabisa. Hapo
ndipo alipoona umuhimu wa
kumdanganya kijana huyu. Uongo
ambao ulimlainisha kijana na kukubali
kumbeba Masimba kumpeleka Jiji Dar
es salaam. Pikipiki ikaendeshwa usiku
kwa usiku kwa mwendo wa kutisha na
kuogopesha. Ilikuwa ni lazima aimalize
mission katika muda wa masaa mawili
yaliobaki, kwani saa yake ya mkononi
ilikuwa ikimwambia ilikuwa saa saba
na nusu usiku. Wakati wanaikaribia
Bunju wakaiona gari ikija kwa mbele
yao. Dereva akaupunguza mwendo
kwa kuogopa kukamatwa. Masimba
alimsisitiza aendelee kuendesha na
Asiogope. Dereva akatii na kuanza
kuendesha. Mbele kidogo kuikaribie ile
gari wakapigwa mkono. Masimba
akamwambia kijana yule asimame na
Asiogope chochote. Kijana yule
akasimamisha pikipiki na kutulia.
Punde wakawaona watu watano
wenye makoti makubwa wakisogea.
Mkono wa Masimba Ukashuka taratibu
alipoihifadhi bastola. Lakini watu wale
waliposogea sans akagundua kwamba
ni Askari. Akautoa mkono kisha
akashuka. Polisi nao Wakawasogelea
mpaka pale.
"Naomba Leseni yako ya udereva."
Polisi mmoja akaamuru. Dereva yule
hakuwa na leseni ya udereva. Baada ya
Masimba kuona dereva wake ana
hangaika. Akasogea karibu na kumuita
askari mmoja pembeni. Askari yule
akasogea kwa umakini sana huku SMG
ikiwa mkononi. Kumfikia masimba tu
akapewa kitanbulisho kimoja kati ya
vingi alivyonavyo masimba. Baada ya
kukipokea na kukiangalia, askari yule
akakamaa kwa Saluti. Kitambulisho
kikarudishwa kwa mwenyewe kisha
wakaruhusiwa waendelee na Safari
yao. Askari wote walikuwa
wakintizama Masimba kwa mshangao.
Hawakuwahi kumuona Zaidi ya
kumsikia. Hawakuwahi kumuona Zaidi
Ya kuona na kusoma sifa zake.
Wakaendelea kumuangalia mpaka
anatokomea. Hawakuwa wameamini
na licha ya kutokuamini macho yao
lakini walifarijika sana kumuoba mtu
huyu.
*********
Kama ilivyo kwa maeneo mengi ya Jiji
la dar es salaam kutokukosa watu hata
iwe usiku wa maneno, ndio hali
ambayo aliikuta Masimba Baada ya
kufika hapo. Bado madada poa
walikuwa kwenye biashara za kuuza
miili yao. Mateja wengi bado walikuwa
barabarani wakipiga debe na hata
usafiri wa kukupeleka popote bado
ulikuwa ni wakumwaga. Alishuka
kumekucha na kumlipa dereva wa
pikipiki pesa yake. Basda ya hapo
akamwambia anaweza kurudi na asiwe
na wasiwasi. Baada ya kuachana na
dereva yule, masimba akatembea
kama mtu wa kawaida mpaka nyuma
ya Jengo ambalo kwa mbele ndio
kulikuwa na Ile flemu yenye saloon.
Cha ajabu lilikuwa jengo kubwa sana.
Jengo ambalo lilikuwa na vyumba vingi
sana. Na kingine kilichokuwa
kikimshangaza ni miguno ya watu
wanaofanya mapenzi kila pale
alipokuwa anasogea. Hilo likampa
shaka na kuamini labda jumba hili
lilikuwa na danguro ama ni gesti bubu.
Akaendelea kutembea na ukuta wa
jengo lile mpaka alipofika mbeli kidogo
ndio akauona mlango wa kuingilia.
Kuuona mlangoni huo kuliendana na
kuwaona walinzi watatu waliokuwa
wakizunguka hapo, mikononi wakiwa
na Bunduki kubwa. Kuwaona walinzi
wale kukampa picha halisi kuwa
sehemu ile haikuwa gesti wala
danguro bali kulikuwa kukifanyika
Biashara nyingine zaidi, tena biashara
kubwa na ya hatari. Akaongeza
umakini safari hii akiamua kupambana
kwa Mikono. Akatafuta njia nzuri ya
kuwakabili walinzi wale. Akaendelea
kuwatizama kama atawaona walinzi
wengine, lakini aligundua walikuwa
walewale watatu. Muda huu alikuwa
amehama pale na kuhamia huku.
Alitaka kuwazunguka na kuwatokea
kwa nyuma. Aliwaangalia kwa hatua
zao na ukaaji wao. Akahamisha macho
kwa kila mmoja aliyekuwa pale. Wote
walikuwa wamesimama sehemu moja
wakiongea. Alikuwa na uwezo wa
kuwachapa Risasi wote lakini hilo
akaliacha baada ya kuyaona mazingira.
Akatembea na giza mpaka karibu
kabisa na walinzi wale. Sekunde hii
alikuwa akisogea kwa karibu zaidi.
Ulikuwa ni muda wa kuwaonyesha kwa
nini Aliaminiwa na Taifa. Akawatokea
pale pale kwa kushtukiza. Yaani
sekunde hii walikuwa wenyewe
wakiongea, lakini sekunde ya pili
walijikuta wakiwa wanne. Alikuwa
ameongezeka mtu mmoja katikati yao.
Mtu ambaye aliwashangaza na hata
kuwafanya wababaike. Haiwezekani
muda huu waongee watatu, harafu
sekunde ile ile aongezeke wa nne.
Mikono yao ikataka kushuka kwenye
tufe la kuachia Risasi. Ni wakati huo
kila mmoja alikuwa akiugulia
maumivu. Yalikuwa mapigo
yaliompigwa katika namna ambayo
hakuna ambaye aliiona. Kila mmoja
alikuwa ikigugumia kwa maumivu
huku akishika kwenye korodani.
Hakutaka kuwapa nafasi ya kujiuliza.
Lakini wakati akijiandaa mmoja
akarusha teke lakini likapita hewani
baada ya kukwepwa kwa ustadi.
Akarusha tena ngumi tano mfululizo
lakini zilipita hewani. Safari hii
akakutana na teke la Taya. Akajikuta
mlinzi yule akiisalimia sakafu. Wakati
huo walinzi wengine walikuwa
wamekaa sawa. Yakafuata mapigano
yaliochukua dakika mbili tu. Walinzi
wote walikuwa chini wakiwa hawana
uhai.
Akawaacha chini wakiwa wamelaliana.
Sasa akawa anaingia ndani ya jengo lile
kwa kupitia mlango wa ule ule. Bado
miguno ya mapenzi ilikuwa ikisikika.
Bado malalamiko ya mahaba yalikuwa
yakitamalaki katika ngoma za masikio
yake. Hapo akahamisha mawazo yake
kwa Teddy, alimkumbuka Teddy kwa
mengi. Alikuwa msichana wa kipare
lakini alikuwa akiyajua mapenzi kama
mzaramo ama mngoni. Alikuwa akijua
kuutumia mwili wake mwembamba
kwa utulivu na ufundi mkubwa.
Ukimuona akiwa kwenye uwanja wa
fundi seremala ungehisi labda alitokea
Tanga yalikozaliwa mapenzi. Akapita
akiyalazimisha masikio yake yatii kile
ambacho alikwenda kukitenda.
Akalifungua geti taratibu na
kuchungulia kwa ndani, hapo
akakutana na giza totoro. Akalifungua
zaidi na zaidi kisha kujipenyeza ndani.
Bado utulivu haukuwepo, bado miguno
iliendelea. Akatembea sambamba na
ukuta mpaka karibu kabisa na kibanda
ambacho kilionyesha kilikuwa ni cha
walinzi. Akatulia hapo akaangalia kila
kona kwa chati. Kwa kuwa alikuwa
amezoea giza, kwa kuwa macho yake
yalizoea hali hiyo. Akafanikiwa
kuwaona watu waanne katika sehemu
tofauti. Licha ya uwepo wa watu wale,
lakini hawakuonyesha kama
walimuona Masimba. Hilo likamfanya
masimba asonge mpaka karibu na
mlango wa kuingilia ndani. Kufika hapo
akaisikia minong'ono ikitokea ndani.
Masimba akachomoa bastola kisha
kuiweka Tayari. Bado minong'ono
iliebdelea tena na tena. Punde akahisi
ukimya lakini ukimya huo haukudumu
sana, kwani Ndani ya Sekunde kumi
miguno ikaanza kusikika kutoka
ndani...
ITAENDELEA
May be an image of 1 person

 
Back
Top Bottom