Hadithi fupi!
SITOSAHAU ALICHONIFANYA DAKTARI WA SARATANI YA MATITI
UKURASA WA KUMI NA TATU
Kesho yake mcha muda wa saa saba, nikiwa ofisini kwangu alikuja yule mwanadada ambaye alikuwa amepanga pale kwa Hemed, ambaye nilikuwa nimemuona jana yake nikahisi kama nilishawahi kumuona mahali.
Yule dada aliingia ndani ya ofisi na kunichangamkia sana “Hallo mambo mrembo” ndivyo alivyoniambia
“Safi tu dada karibu” nilimuambia huku nikiinuka kwenye kiti nilichokuwa nimekalia
“Asante…..Nilihisi nimekufananisha jana, kumbe ni wewe kweli” alisema dada
“Hahha…mimi mwenyewe nahisi hii sura sio ngeni kwangu lakini hata mpaka sasa nashindwa kukumbuka vizuri, labda ulishawahi kuniungisha nguo si ndio?” nilimuuliza
“Ndio shoga angu, kuna siku nilikuja hapa nikawa nimenunua nguo kadhaa nikiwa mimi na mwanangu mdogo”
“Hahaa….itakuwa kweli maana hii sura niko familiar nayo kabisa dada angu….karibu sana”
“Asante”
Yule dada alianza kukagua nguo pale dukani kwangu, lakini hakuona aliyoipenda hivyo akaamua kuniaga na kuniambia atarudi siku nyingine.
Akatembea hatua kadhaa na kugeuka akaniuliza “Hivi unaitwa nani vile?”
“Mi naitwa Pendo” nilimjibu.
“Okay Pendo….sasa mimi naitwa mama Numra”
“Sawa” nilisema huku nikimkagua ikabidi mimi naye nimpachike swali “Hivi jana kwanini yule housegirl wa Hemed alikuwa analia et?”
Mama Numra alitabasamu halafu akaniambia “Mdogo wangu….pale umeingia cha kike kabisa….yule mwanaume ana hatari, wanawake ni wengi sana,….ila nashangaa kwanini amekupa thamani kubwa hadi kukuleta nyumbani” alisema yule mama na kuingia tena dukani, alionekana mbea sana
“Mh kumbe ni Malaya yule?” niliuliza
“Mh….sijajua kama kwako amebadilika lakini yule mwanaume amekuwa hatari, umesema Jacque alikuwa analia?” aliniuliza
“Ndio”
“Masikini mtoto wa watu anapitia mengi pale ndani” alisema mama Numra
“Kivipi??” nilimuuliza
“Nafikiri kilichomuuma Numra ni kwa sababu wewe ulifika pale nyumbani kiukweli wanatoka pamoja, ni kama mke wake tu”
Haya maneno yalinishtua sana, kumbe Hemed alikuwa anatoka na dada wa kazi, ni kweli ni mzuri yule Jacqueline lakini si angeniambia tu kwamba yuko naye
Nilimtazama mama Numra na kusema “Jamani anisamehe tu mimi sikujua chochote kumbe ni mtu wake?” nilisita kidogo na kuendelea “Duuh lakini kwanini anipeleke pale nyumbani wakati kuna mpenzi wake? Ah au alikuwa anataka kumkomoa au kunikomoa mimi?”
“Ndio maana nikasema amekupa thamani kubwa sana, huwa ana wanawake wengi lakini kamwe hawaleti nyumbani…kwa sababu anatoka na yule msichana”
“Duuuh….nilihisi tu maana yule msichana ni mzuri sana…….asingeweza kuvumilia Hemed”
“Hahaa…ni kweli ni MashaAllah mtoto yule…sio mtanzania”
“Oh…haya dada…..nashukuru sana kwa ujumbe wako”
“Haya mdogo wangu kwa heri” alisema
“Ok”
Mama Numra aliondoka zake kuelekea nyumbani kwake lakini aliniacha katika mawazo makubwa sana, yule Hemed alionekana sio muaminifu hata kidogo. Alionekana ana wanawake wengi sana, nilishangaa kwa kujua kumbe yule msichana wa kazi alikuwa analia kisa aliniona mimi pale kwao….maumivu yalikuwa sio ya nchi hii.
Nilikaa kimya, roho inaniuma, penzi halijafikisha hata juma, lakini limeanza kunichoma. Sikuwa na cha kufanya zaidi ya kuamua kuachana na Hemed kabisa, ndiyo yalionekana maamuzi sahihi kwenye maisha yangu.
Niliendelea na kazi yangu mpaka ilipofika muda wa saa kumi na moja ndipo Hemed aliponipigia simu, sikusita, niliipokea na kuongea
“Hallo” nilisema
“Niambie Pendo, mzima wewe?” aliniuliza
“Mzima” nilijibu kwa mkato kidogo
“Mbona umekuwa kimya sana mke wangu?” aliniuliza
“Hamna” nilijibu
“Sawa sawa, jana ulifika salama lakini?” aliniuliza
“Ndio lakini nikuulize swali tu, kwanini yule househelp wako alikuwa analia kiasi kile?” hamna
“Hahaha….nilijua tu hilo swali litafuata, anyway yule anadeka sana anasema amemmiss mama yake anataka kwenda kwao”
“Mh….ndo alie hivyo?” niliuliza
“Yaah…ni mtu wa tofauti kidogo”
“Duh haya” nilisema
Nilikuwa na wasiwasi na Hemed , hata yale mapenzi niliyokuwa nimeanza nayo ya moto sana yalikuwa yameshashuka kwa kiasi kikubwa, nikaona ni kheri nikatafuta namna nyingine ya kuishi bila yeye, niliona ni bora kumkaushia.
Hemed alikata simu kisha akanitumia SMS “usiwe na wasiwasi, penzi lako liko salama, naomba unijibu lile suala la kukuoa mpenzi”
Niliisoma ile SMS mara mbilimbili lakini kamwe sikupata jibu lenye faida, niliishia tu kumjibu hivi “Kwa jinsi nilivyoona wadada wanavyokusumbua huko njiani, na mambo mengine ambayo sitaki kuyaandika hapa, naomba suala la mapenzi yangu mimi na wewe liishie hapa”
Kiukweli nilikuwa natamani kuwa na mwanaume wangu lakini yule hakuwa wangu, niliona ni wetu ndio maana niliamua kumkaushia ili nikae kwa amani moyoni mwangu.
Hemed hakunijibu ule ujumbe alikausha kimya mpaka saa nne usiku ndipo alinitumia ujumbe uliokuwa unasema hivi
“NAJUA UNANIHISI VIBAYA KWA SABABU JANA ULIONA NINA MAZOEA NA BAADHI YA WANAWAKE BARABARANI. KIUKWELI SIO KWAMBA NAWATUMIA LAKINI NIKUAMBIE TU KWAMBA NINAHITAJI UWE MKE WANGU NINAAHIDI KUKUPA FURAHA…NAOMBA ULIFIKIRIE HILI UNIJIBU KESHO ILI NIAHIRISHE NDOA AMBAYO NINATAKIWA KUFUNGA NA MAMA NASRA”
Nilishangaa kwanini anang’ang’ana tuoane? Yaani hata hatujachunguzana yeye anataka akaniue na presha tu? Nilimjibu
“LALA HUKO, MIMI SINA RATIBA YA KUOLEWA NA WEWE…..ENDELEA NA JACQUE SITAKI KESI NA MTOTO WA MTU”…………………ITAENDELEA
Hadithi fupi!
SITOSAHAU ALICHONIFANYA DAKTARI WA SARATANI YA MATITI
SEHEMU YA KUMI NA NNE
TULIPOISHIA
Hemed hakunijibu ule ujumbe alikausha kimya mpaka saa nne usiku ndipo alinitumia ujumbe uliokuwa unasema hivi
“NAJUA UNANIHISI VIBAYA KWA SABABU JANA ULIONA NINA MAZOEA NA BAADHI YA WANAWAKE KADHAA BARABARANI. KIUKWELI SIO KWAMBA NAWATUMIA LAKINI NIKUAMBIE TU KWAMBA NINAHITAJI UWE MKE WANGU NINAAHIDI KUKUPA FURAHA…NAOMBA ULIFIKIRIE HILI UNIJIBU KESHO NILI NIAHIRISHE NDOA AMBAYO NINATAKIWA KUFUNGA NA MAMA NASRA”
Nilishangaa kwanini anang’ang’ana tuoane? Yaani hata hatujachunguzana yeye anataka akaniue na presha tu? Nilimjibu
“LALA HUKO, MIMI SINA RATIBA YA KUOLEWA NA WEWE…..ENDELEA NA JACQUE SITAKI KESI NA MTOTO WA MTU”…………………
ENDELEA
“Jacque????” aliniuliza kwa mshangao kidogo
“Ndio, ulifikiri mimi sifahamu?”
“Hahaah….acha mambo yako” aliniambia
“Mambo gani Hemed? Mimi nimeshaambiwa kila kitu, kumbe ndio maana mtoto wa watu alikuwa analia” nilisema
“Waliokuambia hivyo wamekudanganya, mimi sina mahusiano na binti yangu wa kazi jamani”
“Hahahaa eti ee” niliuliza
“Ndio, kwanini unakuwa hivi Pendo? Hivi kweli wewe utaolewa??”
“Ni kheri nisiolewe kuliko kuolewa nikaenda kuzeeka kabla ya muda wangu”
“Haya poa”
Tuliachana kirahisi rahisi tu namna ile, lakini vile haikupita siku mbili, nilikuwa nimekaa zangu kazini kwangu naweka midoli ya nguo nje ya ofisi yangu, ndipo akapita yule msichana ambaye pia ni mpangaji wa pale kwa Hemed, alipoona nguo alisogea karibu na mdoli mmoja na kunichangamkia
“Jamani mambo”
“Safi…..karibu” nilisema huku nikimtazama
“Mmh….nimeona hili gauni jekundu ni zuri nikasema nije hata niulizie bei”
“Hahah…karibu ni shilingi elfu ishirini na nane tu”
“Mmmmh…ni zuri lakini beii mmmh”
“Mh sio pesa nyingi jamani”
“hahaa….nikikupa ishirini hautanipatia shogaa??” aliniuliza
“Hapana mama,….ishirini mbali sana. Labda ishirini na tano jamani”
“Daaah” alisema huku akiligusa, mara ghafla nilimuona Jacque akiwa anakatiza barabarani. Ndipo akamuita “We Jacqueeee….Jacquee” binti Jacque akageuka kwa mshangao, nadhani moyoni alikuwa anajiuliza ni nani anamuita.
Alipomuona yule msichana mwingine, alichangamka na kumnyooshea kidole akicheka “Halafu wewe” alisema Jacque huku akivuka barabara na kuja kwenye upande wa duka langu
“Umetoka wapi??” yule msichana mwingine aliuliza
“Nimetoka kwa bwana angu” alisema huku akicheka mimi nikawa namuangalia kwa kifupi moyoni ni kama nilikuwa adui yake, alishaninyima tunda langu kwa Hemed lakini sikuwa na namna maana yeye ndiye aliyetangulia.
“Kumbe una bwana huku?” aliuliza yule msichana mwingine ambaye baadaye niligundua anaitwa Farida
“Hahaha…hapana bana, kuna sehemu kaka aliniagiza nimepeleka hela” alisema Jacque na kuniangalia.
Sasa ghafla yule binti akanitazama na kushtuka kidogo halafu akasema “Shikamoo dada”
Nilitabasamu kisha nikaitika “Marahaba mdogo wangu, mbona umeshtuka uliponiona?”
Jacque akatabasamu kwa aibu kisha akaniambia “Sikujua ni wewe”
“Mh haya bwana” nilisema
Waliendelea kuangalia nguo wakawa wanazisifa ila hawakununua
FARIDA: Basi nisindikize sokoni tutarudi wote shogaa
JACQUE: Mh…mbali kote kule na jua hili? Unataka niwe mweusi (akiwa anachezea nywele zake ndefu)
FARIDA: Mh twende bwana huwezi ukawa mweusi
JACQUE: Haya
FARIDA: (Huku akinigeukia) Kwa heri tutarudi siku moja kununua bwana
MIMI: Sawa karibuni jamani
JACQUE: Kwa heri dada
MIMI: Okay
Jacque na Farida waliondoka kwenda zao lakini hakufika mbali nikaamua kumuita Jacque ili niweze kumaliza tofauti zetu.
Jacque aligeuka na kunitazama kisha akaniuliza “Mimi?” nikasema
“Ndio wewe….. nakuomba mara moja” nilisema
“Mh” Jacque aliguna na kunisogelea lakini akamuacha farida akiwa anamsubiri mbali kidogo na pale, Jacque akanisogelea kisha nikamuambia
“Samahani kipenzi, mimi naamini unanikumbuka nilikuja pale kwenu siku mbili zilizopita”
“Ndio nakukumbuka dada”
“Okay, nilikuja kusikia kwamba nilikukwaza, kwani nilikuacha ukilia pale ndani sikujua kwamba chanzo ni mimi”
“Mh” alisema huku akinishangaa kidogo yule msichana mdogo na mzuri sana “sijakuelewa dada” aliniambia
“Yaani ninamaanisha kwamba Hemed hakuniambia kwamba yuko na wewe kimapenzi ndio maana nilikuja pale, mimi sikujua ana mpenzi mwingine maana hakuniambia, naomba unisamehe nimeamua kuachana naye ili niwaache na mapenzi yenu” nilisema
“Mh mimi??” aliniuliza tena kwa mshangao
“Ndio….nimeambiwa wewe ni mpenzi wake, ndio maana siku ile nilipokuja ukaanza kulia nakuomba unisamehe mdogo wangu”
“Hahahaaa…bhaana” alisema yule binti kwa mshangao kidogo “Mimi mbona sina mahusiano yoyote na boss wangu” alisema
“Kivipi J??” nilimuuliza
“Ninashangaa habari ulizoniletea, najua wewe ni mpenzi wake…mi sipo naye kimapenzi mbona, mh nitamuweza kweli mtu mzima kama yule mimi nina miaka 18 tu” aliniambia nikamshangaa kwanza nikaguna halafu nikashika kiuno
Nikamuuliza “sasa siku ile kwanini ulikuwa unalia?”
“Ahahahaa….kwa hiyo ulidhani nalia kwa sababu ya wivu??” aliniuliza
“Ndio, hasa nilipokuja kuambiwa anatoka na wewe, basi nilijua kabisa ndiyo sababu iliyokupelekea kulia siku ile”
“Hapana dada yangu….nina matatizo yangu binafsi tu yalipelekea mimi kulia siku ile ninaumia sana”
“Tatizo nini?”
“Nina miaka minne tangu nije hapa Tanzania nimefanya kazi na hii familia kwa utiifu mkubwa, lakini hawajawahi kunilipa pesa, kiukweli nakula vizuri navaa vizuri lakini hata nyumbani sijawahi kuwatumia chochote, ninadai zaidi ya milioni sita za mshahara lakini pia nilitamani wanipe hata hela kidogo mwishoni mwa mwaka huu niende nikamuone mama anaumwa, ila wao hawaonyeshi kunijali, nimepamiss kwetu sana”
“Mh…kweli??” nilimuuliza
“Ndio”
“Oh pole sana my dear….”
“Asante” alisema “Kwa hiyo wewe usiwe na wasiwasi kwamba mimi natoka naye hapana, sina hata ratiba hiyo mimi ya kuwa naye usijali….” Aliniambia
JE NI KWELI BINTI HANA MAHUSIANO NA HEMEDI??