Kapeace
JF-Expert Member
- May 26, 2017
- 24,514
- 65,521
🤔🤔Me wa kiume mzee wangu Sina pigo hzo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
🤔🤔Me wa kiume mzee wangu Sina pigo hzo
Ikiendelea nitag ila inanyegesha story yako wenzio tuko single hatuna hao madoctor wa kutunyonya chuchu [emoji12]
Tatizo hutugawii namba yako. Tutakunyonyaje chuchu.
OhooooHadithi fupi!
SITOSAHAU ALICHONIFANYA DAKTARI WA SARATANI YA MATITI
SEHEMU YAA NANE
TULIPOISHIA
“Bhana tutawasiliana….” Nilionga huku nikishuka kitandani na kuanza kuvaa nguo zangu halafu nikambusu ninataka kuondoka akanivuta mkono na kuniambia “Pendo”
“Abee”
“Nataka nikuoe” alisema maneno ambayo yalinishangaza, yaani ndo kwanza siku moja tu imepita tangu tuonane kwa mara ya kwanza, sawa tulikuwa tumefanya mapenzi lakini kweli siku mbili tu mtu anataka anioe
Nilijikuta nimestaajabu namtazama tu usoni, naye anavyoangalia ni kama vile yuko serious, halafu kikubwa zaidi ni kwamba alishaniambia ana mke sasa sikuelewa anamaanisha nini
ENDELEA
Niichukua wastani wa dakika moja namuangalia tu, naye ananitazama kisha akasema “Please” huku akininong’oneza
“Hivi Hemed kwanini unaamua kuwa muongo muongo?” nilimuuliza
“Muongo kivipi? Ninahitaji uwe mke wangu naomba unipe hiyo nafasi”
“Niachie embu” nilisema nikiuvuta mkono wangu kwa nguvu ndipo akaniachia na kuinuka
Akaniuliza “Kwanini unanikatalia nisikuoe, penzi lako ni tamu nahitaji mke kama wewe”
“We hemed acha basi mambo yako? Mimi umeniona jana tu, ulikuwa hunijui, sawa tume-share penzi lakini kweli siku moja tu wewe ushataka kunioa? Kuna mapenzi ya hivyo?” nilimuuliza
“Pendo, usifikirie yote hayo. Mapenzi hayana nafasi ya kusubiri yakija ni kuchukua hatua mapema kabla hayajabuma”
“Hata kama lakini siwezi kukurupuka kiasi hicho” nilisisitiza “Halafu nikuambie kitu kimoja, wewe una mke mi huwezi nioa mke wa pili” nilisema
“Sina mke” aliniambia halafu akajikoholesha
“What??? Si umesema una mke wewe?” nilimuuliza “Tena na watoto wawili?”
“Pendo, sina mke”
“Unamaanisha nini? Na hilo gauni ulilonunua unapeleka wapi?” nilimuuliza
“Gauni ni la binti yangu, nimezaa na mwanamke mmoja ambaye yuko Tabora”
“Ina maana hujaoa wewe? Mbona unaonekana mtu mzima?”
“Ni kweli nina miaka 36 lakini sijaoa”
“Huyo mwanamke uliyezaa naye ameolewa?”
“Hapana, ni wiki mbili tu zimebaki mimi naye tuweze kuoana” aliniambia
Nilibaki namshangaa tu anaongea mambo ya ajabu ambayo siyaelewi elewi, nikaweka mikono yangu kifuani halafu nikaendelea kumtazama huku nikianza kupata hasira akaendelea
“Ninafosi tu kuoana naye, hanipendi japo tuna watoto nimefosi kwa muda mrefu umri unaenda ninahitaji kuwa na mke sasa”
“Kwanini unafosi?” nilimuuliza
“Sasa kama mtu ninamuuliza kuhusu ishu za kuoana anasema kama kuna mtu mwingine ananipenda nimuoe….maana ake nini?”
“Mh” niliguna, nilikuwa njia panda, sikumuamini hata kidogo, niliona ni drama kabisa.
Kutokana na kutokumuamini nilijikuta namkatalia “Siwezi kuolewa na wewe…bora tungekuwa tuna hata mwaka, lakini kwa siku mbili tu nitakuwa nakudanganya” nilisema na kugeuka “Mimi ninaenda nyumbani”
“Okay, shika hela ya nauli pamoja na malipo ya nguo yako” alisema ndio nikakumbuka kumbe hajanilipa.
Hemed alichukua suruali akatoa wallet na kunipatia kiasi cha shilingi elfu arobaini. “Bye” nilisema
“Okay” alinijibu
Niliondoka pale, nilikuwa najisikia vizuri, nilikuwa na muda sijafanya mapenzi, kwa hiyo kitendo cha kufanya mara mbili, kilinipunguza kabisa genye nikajikuta nimekuwa mpya. Nilifika nyumbani nikiwa na furaha tele, nikakuta wote wameshalala lakini nilipoingia tu ndani mama alitoka sebuleni na kuniuliza
“Mbona umechelewa sana nyumbani?”
Nikamdanganya “Kuna rafiki yangu alikuwa na birthday ndo nilitoka kwenye party”
“Sasa kwanini hukusema tumekupigia simu hupatikani?” aliniuliza
“Mh” niliguna na kuangalia simu kwenye pochi kumbe ilishazima chaji “Samahani mama ilizima chaji kumbe”
“Okay siku nyingine uwe makini” aliniambia
“Sawa”
Mama aliondoka akarudi ndani kwake, na mimi nilienda bafuni kuoga, na nilipomaliza kuoga nilirudi na kulala, sikuwa na njaa maana nilikuwa nimekula vizuri kule Mbuzi On Target nilipokuwa na Dr. Hemed.
Niliweka simu chaji nikausaka usingizi mpaka asubuhi……ITAENDELEA
Hadithi fupi!
SITOSAHAU ALICHONIFANYA DAKTARI WA SARATANI YA MATITI
SEHEMU YA TISA
Saa kumi na mbili nilishtuka usingizini, na jambo la kwanza nililolifanya ni kuitafuta simu yangu ilipo nikakuta ina chaji asilimia 100 ndipo nikaiwasha, na kuingia mtandaoni.
Nikiwa mtandaoni nilikuwa nilikumbuka nina namba ya hemed, nikamtext WhatsApp “Hi”
Ule ujumbe ulipofika ulichukua sekunde kadhaa tu ukafunguliwa akajibu.
“Hi umeamkaje baby?” aliniuliza moja kwa moja nafikiri aliangalia kwenye picha ya wasifu nilikuwa nimeweka picha yangu ndipo akajua ni mimi
“Mh….umeshanijua tu?”
“Nimeona dp yako, kwanza nikasisimka mwili mzima”
“Hahaha…kisa?” nilimuuliza
“Mtoto mtamu sana”
“Hahha acha mambo yako bana”
“Mambo gani”
“Kweli mi mtamu?”
“Mno, yaani nilipokuona tu ny*ge zikanijaa natamani nipate angalau tena”
“Mmmh mi sio mtamu kama wewe….yani basi tu ni vile hujui unavyojua kumfanya mwanamke achanganyikiwe”
“Daah sawa” aliniambia
Nilitulia dakika tatu akanitumia screenshots ambazo alikuwa akichat na mwanamke ambaye niliamini ndiye alikuwa amezaa naye, zilikuwa hivi
Hemed alimuuliza yule mwanamke “Kwanini usihamie Mwanza tukioana?”
Yule mwanamke akamjibu “Siwezi kuacha biashara zangu nihamie huko, kama unaona hatufai kufunga ndoa ukaishi huko na mimi huku, basi tafuta mwanamke ambaye anakufaa huko”
“Duuh…sasa mbona unasema hivyo?”
“Unataka nisemeje? Huo ndo ukweli tena mimi ni kwa sababu tu unang’ang’ania ila nilikuwa nishaamua kuishi peke yangu”
“Duuh lazima nikuoe”
“Sawa, ukinioa ukae huko na mimi nikae huku, tukikutana mara moja moja sawa”
Hizi messages zilionyesha kwamba mwanamke ndiye aliyekuwa hamtaki mwanaume, nikajikuta naanza kumhurumia hemed na kumpa pole
“Asante Pendo…nakupenda”
“Nakupenda pia” nilimjibu
“Naomba nikuoe pendo nitakupa kila kitu”
“Mmmmh wewe….sawa kama unataka tuoane, basi subiri tujuane”
“Hapana kipi ambacho unataka kukijua zaidi kwangu….mimi ninakujua vizuri tayari nimeshafahamu vingi kwa muda mfupi….naomba ukubali nikuoe kwa kipindi hiki cha haraka haraka ili niachane na huyu mwanamke”
“Duuh….”
“Nini?”
“Sijui nikujibu vipi…..ila mimi ninahisi haiwezekani….halafu pia dini”
“Sawa. Utakuwa hujanipenda kweli” aliniambia
“Kweli nakupenda lakini kiukweli sio kwa haraka haraka kama unavyodhani wewe…naomba nipe muda, mapenzi ya uchumba hata mwaka mmoja basi sasa kweli siku moja sijui mbili unataka unioe kweli?”
“Duuh okay asubuhi njema” alinitumia ujumbe ambao kidogo ulionyesha kama amekasirika
“Umekasirika?” nilimuuliza lakini alikuwa ameshatoka mtandaoni jumbe hazikumfikia nikamtumia mwingine “Sorry kama nimekuudhi ila nipe muda kidogo nifikirie hili”
Nilipotuma hizi jumbe niliondoka online na kuamka nimsaidie mama usafi nyumbani halafu niende kwenye kazi yangu ya kila siku.
Nilifanya usafi kiuvivu ndipo mama akanifuata nikiwa nimesimama kwenye ukuta, kichwani namuwaza tu Hemed yaani, kilichokuwa kimenipa raha zaidi ni baada ya kupata taarifa kwamba hajaoa, nilitamani nithibitishe zaidi maana kwa dini yake inawezekana anataka kunifanya mke wa pili wakati mimi nilikuwa sitaki
“Unawaza nini?” aliniuliza mama nikashtuka na kumtazama
“Mama shikamoo” nilimuamkia
“Marahaba, nimekaa pale dirishani naona unacheka mwenyewe, vipi?” aliniuliza
“Hamna mama” nilisema na kuinama nikaendelea kufagia, mama akaninyooshea kidole akisema “Wewe” halafu akaanza kuondoka. Sikuweza kuvumilia nilimuita “Mama”
“Nini” mama alisema na kunigeukia, sijui kwa nini wiki ile alianza kuwa rafiki yangu, nafikiri alichoka kuniona kwake alitamani niolewe lakini sijui
“Hivi mama?” nilimuuliza huku nikiogopa, mama akanitazama nikasema “Au basi”
“Mjinga wewe” mama alinitukana
“Hamna mama, hivi mwanaume mliyekutana siku mbili tu anaweza akaahidi kukuoa na akaoa kweli?” niliuliza lakini mama hata hakushtuka alinipachika swali
“Mmeshalala na huyo mwanaume?” aliniuliza nikaogopa kumjibu ndio nikatikisa kichwa kuonyesha kwamba sijalala naye lakini kiukweli siku hizo mbili tu alikuwa ameshaninyandua mara mbili mama akasema “Wanaume ni viumbe wenye tamaa ukikutana naye siku moja tu anachotamani ni penzi kama hajalipata anakuwaga na mapenzi ya kweli na anaweza kukuahidi vitu vingi sana, sio kwamba hamaanishi lakini mara nyingi zinakuwa ni ahadi za kushawishi ili apewe penzi, akishapewa hubadilika….lakini kama mwanaume akikuahidi wakati mshafanya, basi huyo anaweza akawa anamaanisha maana tamaa yake ameshaipata lakini bado anatamani”
“Mh”
“Unaguna nini?”
“Ah maelezo yamekuwa mengi kweli kweli”
“Kama hamjafanya anakudanganya….kama mmeshafanya anaweza akawa anamaanisha” mama aliniambia halafu akaondoka zake
Ulikuwa ni ushauri mzito, nilikuwa nimeshalala na daktari, nilipata ahueni moyoni mwangu na kumfikiria zaidi hemed, nikawa nimeanza kujihisi ninahitaji mume.
Nilimaliza usafi, nikaoga na kuondoka nyumbani kwenda kazini kwangu. Nikiwa natembea niliamua kumpigia nimuulize kama yupo serious na suala zima la kutaka kunioa, simu ikakatwa, nilishtuka sana nikajaribu kupiga tena nikijua amekasirika lakini hakupokea.
Nilimtumia ujumbe “Mbona hutaki kupokea simu yangu, nisamehe mume wangu” nilimuita kimahaba hivyo. Kweli haikuchukua muda akapiga.
Nilipopokea simu nilimuita kwa hisia “Mume wangu” lakini cha kushangaza nilisikia nimejibiwa na sauti ya kike ikiniuliza
“Wewe nani???” niliishiwa nguvu……JE NI NANI HUYO ALIYEPIGA SIMU USIKOSE UKURASA WA 10
Shukrani mkuu na itaendelea mpk mwishoHadithi nzuri
Nitaendelea kuifuatiliaShukrani mkuu na itaendelea mpk mwisho