Hadithi: Sitosahau alichonifanyia daktari wa saratani ya matiti

Hadithi: Sitosahau alichonifanyia daktari wa saratani ya matiti

Hadithi fupi!
SITOSAHAU ALICHONIFANYA DAKTARI WA SARATANI YA MATITI
SEHEMU YA KUMI NA NANE
BAADA YA WIKI MOJA
Nilikuwa na binamu yangu napiga naye story mbili tatu, alikuwa anajua natoka na Hemed licha ya kutokupendwa na wazazi wangu hasa mama. Sikujua kwanini mama alikuwa hampendi mwanaume yule, lakini baba kidogo alikuwa anampenda.

“Shazma unajua mdogo wangu sielewi kwanini hawataki niolewe na Hemed”

“Achana nao wanakuonea wivu, mimi ningepata mwanaume kama yule mwenye maisha mazuri kama yule ningemganda sana…nisingekubali aniachie hata hatua moja” alisema

“Kweli ee? Lakini sijui kama ananipenda kweli”

“Anakupenda, unadhani kuna mwananume ambaye anaweza kukununulia simu ya milioni tatu kama hakupendi??? Labda ungekuwa hujampa ningesema may be ni tamaa lakini kumbuka umelala naye mara kibao”

“Mh kweli eeh?” tukiwa tunazungumza mara akaingia mama, ikabidi tunyamaze na kumtazama.

Ilikuwa ni wiki imepita tangu Hemed aninunulie simu lakini sikuonyesha mapenzi ya dhati kwake kwa sababu nilikuwa nimepewa onyo, nilikuwa namjibu kwa mkato mara kwa mara na hata baada ya mama kuingia pale Hemed alinipigia simu, sikupokea

Akanitumia ujumbe “Babe uko wapi? Nataka kuongea na wewe kuna surprise yako” alisema na kupiga tena

Ilinibidi nitoke nje ya nyumba na kupokea simu nikawaacha mama na Shazma wakiwa wanapiga story pale sebuleni. Nikapokea simu

“Hallo mke wangu vipi?” aliuliza

“Nambie” nilijibu

“Njoo tukutane”

“Wapi??”

“Njoo hospitalini hapa”

“Kwani nije kuna nini?”

“Kuna sehemu nakupeleka ukaone” alisema

“Mh tena??”

“Ndio”

“Haya basi nijiandae”

“Okay”

Baadaye niliondoka nyumbani bila kumuaga mtu yoyote, nikaenda mpaka hospitalini nilipokutana na daktari alinipeleka mtaa fulani unaitwa CCM nilipofika hivi alinionyesha kiwanja kipya ambacho alikua amekinunua, baada ya kunionyesha kiwanja kile aliniambia ni kwa ajili ya mtoto wetu wa kwanza, alisema ameweka majina yetu mi na yeye.

Nilijisikia faraja akanipeleka mpaka nyumbani ila nikiwa sijashuka kwenye gari tulianza kupigana denda pale pale getini, nilijisikia vizuri akaniuliza’

“Kwanini siku hizi hunijibu vizuri message zangu na mara kadhaa simu hupokei??”

Sikuwa na cha kumjibu, ,mimi nilikuwa nafanya vile kwa sababu nilikuwa najaribu kujiweka mbali naye tangu mama alipokuwa ameniambia kwamba yule mwanaume hafai kuwa mume sahihi kwenye maisha yangu.

Aliniomba nimjibu swali hilo kwenye simu, nilikuwa nimeshampenda lakini vizingiti vilikuwepo.

Nikiwa nyumbani nilipokea simu kwenye namba mpya nikapokea na kuuliza

“Nani???”

Sauti ya kike ikasikika upande wa pili “Hivi umeamua kabisa kuvuruga mahusiano ya watu???”

Nikashtuka na kuuliza “Mahisiano ya nani tena?”

Akajibu “Unamuumiza mtoto wa watu, bado anampenda Hemed embu waachie maisha yao bana” alisema yule mwanamke

Nikamuuliza “Nimevuruga mahusiano ya nani??”

Akanijibu “Wewe sisi tulikuambia kwamba Hemed anatembea na yule binti wa Kiarabu (Jacque) lakini bado unamng’ang’ania, kila siku mtoto wa watu analia huku….embu acha hayo mambo bana”

“Mh” nilihuzunika sikujua ipo hivyo lakini nakumbuka baadaye niliamua kumpigia Hemed nikiwa nje barazani nikaanza kuongea naye nikamuuliza “Hemed kwanini ninapigiwa simu za vitisho kwamba ninaharibu mahusiano yako wewe na Jcque??”

“Khe?? Mahusiano yapi mimi na Jacque?? Mbona sikuelewi??”

“Nimepigiwa hapa simu na mtu ambaye simfahamu, ananiambia naharibu mahusiano yako kati yako na Jacque lakini wewe unakana kwanini sasa??”

“Nitumie hiyo namba iliyokupigia” alisema

“Okay”

Nilikata simu na kumtumia ile namba, nilipomtumia tu yule mwanaume nikasikia sauti ya mama nyuma yangu

“Unaona sasa?? Mimi ninakuambia ukweli kwamba yule mwanaume hakufai lakini unanipuuzia, ona sasa??” alisema

“Mama kwani ….”

“Nikuambie tu ukweli mwanangu….huyu kijana alishawahi kunisumbua sana nitembee naye” alisema mama. Macho yalinitoka, nikashindwa kuelewa ni kweli au ni uongo….MAKUBWAAA!!!! 😳😳
 
Haya enjoy simulizi ndugu yangu
Aaaaah..... Hizi za kusoma madogo... Story nyepesi. Mi napenda story ambazo mtunzi anatumia akili. Nimeitwa kwa ajili ya kuja kusimamia maslahi ya wasomaji. Heading ni nyepesi nimesoma page ya kwanza nikaona nayo story ya kawaida. Basi nikawa nasubiria kama kutakuwa na malalamiko ikiwa hujamaliza au unadanganya sana hapo ndo nitakuja kuku saidia ujirekebishe.
 
Aaaaah..... Hizi za kusoma madogo... Story nyepesi. Mi napenda story ambazo mtunzi anatumia akili. Nimeitwa kwa ajili ya kuja kusimamia maslahi ya wasomaji. Heading ni nyepesi nimesoma page ya kwanza nikaona nayo story ya kawaida. Basi nikawa nasubiria kama kutakuwa na malalamiko ikiwa hujamaliza au unadanganya sana hapo ndo nitakuja kuku saidia ujirekebishe.

Lete ya kwako nzito za kusoma makubwa za madogo tuachie sisi. Pita kule muone
 
hahaha hi noma sasa.hizi sitori za kulambana nyeti zimekuwa nyingi sana zita fanya si tusiopenda kudeki mbususu tuonekane hatujui mapenzi...kiujumla hadithi ni kali sana ina sisimua sana.
 
Aaaaah..... Hizi za kusoma madogo... Story nyepesi. Mi napenda story ambazo mtunzi anatumia akili. Nimeitwa kwa ajili ya kuja kusimamia maslahi ya wasomaji. Heading ni nyepesi nimesoma page ya kwanza nikaona nayo story ya kawaida. Basi nikawa nasubiria kama kutakuwa na malalamiko ikiwa hujamaliza au unadanganya sana hapo ndo nitakuja kuku saidia ujirekebishe.
Pamoja Sana mkuu
 
Back
Top Bottom