Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 23,234
- 28,473
Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete amekutana na Mwanafunzi wa Udaktari kutokea Chuo Kikuu cha Kairuki, Catherine Conrad ikiwa ni miaka 18 imepita tangu alipomuona katika Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI).
Dkt. Kikwete alikutana na Catherine, Novemba 14, 2008 akiwa na umri wa miaka minne baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo akiwa mmoja wa Wagonjwa wa mwanzo kufanyiwa upasuaji katika Taasisi hiyo.
Mei 29, 2026 Catherine alimtembelea Dkt.Kikwete ofisini kwake kwa lengo la kumsabahi na kumshukuru kwa mchango wake katika kuanzisha na kusimamia Taasisi hiyo inayotoa huduma za matibabu ya moyo Nchini.
Katika mazungumzo yao, Dkt. Kikwete alimpongeza Catherine ambaye atatimiza miaka 22, Julai 2026 kwa kutimiza ahadi aliyompa miaka 18 iliyopita ya kusomea Udaktari huku akieleza furaha yake kumuona akiwa ameendelea vizuri baada ya kuwa mmoja wa Wagonjwa wa kwanza kufanyiwa upasuaji wa moyo akiwa Mtoto.