Hadithi ya mashimo ya mfalme Sulemani

Safi Mkuu ikiwezekana tupia kama zote
 
Aisee[emoji39] [emoji39]
 
Hii kitu ni tama wakuu

Pamoja sana mkuu blackstarline
 
[emoji119] [emoji119] hii kitu ni kali wakuu
 
Hainichoshi kuisoma riwaya hii ingawa nimekuwa nikiisoma tangu ningali kijana mdogo hadi salsa!
Hakika ni riwaya nzuri na yenye milima na mabonde yenye kusisimua moyo na akili pia bila kusahau kuongeza imani juu ya uwepo wa Mungu, Muumba mbingu,ardhi na vyote vilivyomo humo (vilivyo bayana na vya siri)
Ahsante sana mtoa Uzi wenye mtiririko huu! Umenipa mapumziko mazuri ya mwishoni mwa juma hili!
Ningefarijika pia iwapo ungeweza kunikumbusha namna ninavyoweza kuipata riwaya ya Kiswahili iliyoitwa "USO WA MAUTI"
Ni riwaya niliyotokea kuipenda sana tangu nikiwa mdogo ingawa kwa bahati mbaya sana jina la mtunzi limenitoka,ingawa nakumbuka ilikuwa na mandhari ya Tanzania Visiwani hivi (Zanziba) ingawa sina hakika sana juu ya hili!
 
Kweli kabisa hii riwaya inafundisha sana, pia mafanikio ya mtu yanaweza kuja kwa njia tofauti.Riwaya “USO WA MAUTI” sijawahi kuisoma! Pengine siku nitakutana nayo ikitoke nitakujulisha mkuu.
 
Kweli kabisa hii riwaya inafundisha sana, pia mafanikio ya mtu yanaweza kuja kwa njia tofauti.Riwaya “USO WA MAUTI” sijawahi kuisoma! Pengine siku nitakutana nayo ikitoke nitakujulisha mkuu.
Pamoja sana chief tupe muendelezo umetuweka sana Mkuu wikiend hii wengine ndo starehe zetu hizi mkuu
 
Mkuu mwaga madude, galula anasema ukweli , kuna mwanawali mmoja atahitajika kuuwawa kwenye ngoma ya usiku ila watamwokoa .bila kusahau wataponea chupuchupu kuuwawa katika mashimo ya suleman.mkuu dondosha vitu jumapili hii
 
SURA YA KUMI

Tulipofika nyumbani nilimwashiria Infadus aingie pamoja nasi, nikamwambia, ‘Infadus, tunataka kusema nawe.’ Akajibu, ‘Semeni, mabwana zangu.’ Nikasema, ‘Tumeona kuwa huyu Mfalme Twala ni mtu katili.’ Akajibu, ‘Ni kweli, mabwana zangu.

Nchi yote inalalamika kwa sababu ya ukatili wake. Usiku huu mtaona. Itakuwapo ngoma kuu ya kutambulisha wachawi na wengi watatambuliwa kuwa ni wachawi na kuuawa. Hapana mtu anayeweza kusema kuwa maisha yake yapo salama.

Mafalme akiwatamani ng’ombe wa mtu, au mke wa mtu, au akishuku kuwa atawashawishi watu kumwasi basi Yule Gagula mliyemwona au wanawake wengine katika wanawake wanaotambulisha wachawi, watamchagua usiku huu naye atauawa. Wengi watakufa kabla ya mwezi kufifia usiku huu.


Kila mara ni hivyo. Labda hata na mimi nitauawa. Mpaka sasa nimeokoka kwa kuwa ni hodari katika vita, nami napendwa sana na askari; lakini sijui hesabu ya siku zangu za uhai.

Nchi inaugua kwa ajili ya ukatili na maovu ya Mfalme Twala; imechoka naye na mambo yake ya kumwaga damu.’

Nikamuuliza, ‘Infadus, kwa nini watu hawamwondoi? Akajibu, ‘Mabwana zangu, yeye ndiye mfalme, na akiuawa, Skraga atatawala mahali pake na moyo wa Skraga akitawa nira itakayowekwa shingoni mwetu itakuwa nzito kuliko ile ya Twala.


Ingalikuwa Imotu hakuuawa, au Ignosi mwana wake angalikuwepo, ingalikuwa bora; lakini wote wawili wamekufa.’ Hapo tukasikia sauti; tukageuka tukaona kuwa ni Umbopa, akasema, ‘Unajuaje kuwa Ignosi alikufa?’ Yule Infadus akasema, ‘Je, namna gani we mtoto? Nani aliyekupa ruhusa ya kusema?’


Akajibu, ‘Sikiliza, Infadus, nami nitakwambia hadithi. Zamani, wakati alipouawa Mfalme Imotu katika nchi hii, mke wake alikimbia pamoja na mtoto Ignosi, sivyo?’ Akajibu, ‘Ndiyo.’
Umbopa akasema, ‘Ilisemwa kuwa mwanamke huyo na mtoto wake walikufa katika milima, sivyo?’ Infadus akasema, ‘Ndiyo.’


Umbopa akaendelea, ‘Basi ilivyo ni kuwa Yule mama na mtoto Ignosi hawakufa. Walivuka milima wakaongozwa na kabila la watu wanaotembea tembea jangwani mpaka kufika katika nchi yenye maji na majani na miti.’

Infadus akauliza, ‘Je, unajuaje hayo?’ Umbopa akajibu; ‘Sikiliza. Walisafiri mbali kwa muda wa miezi mingi mpaka kufika nchi ya watu waitwao Amazulu, nao ni ukoo mmoja na Wakukuana.

Watu hawa kazi yao ni vita, Wakakaa nao miaka mingi mpaka mama mtu akafa. Basi alipokufa, Yule mtoto Ignosi akawa msafiri tu, akasafiri katika nchi za ajabu wanapokaa watu weupe, akakaa nao miaka mingi, akajifunza maarifa yao.’


Yule Infadus akasema kwa sauti ya kutosadiki, ‘Ni ‘hadithi nzuri, lakini ya nini?’ Basi Umbopa akaendelea, akasema, ‘Miaka mingi alikaa akifanya kazi ya utumishi na uaskari, lakini katika moyo wake alikumbuka yote aliyoambiwa na mama yake juu ya nchi yake, alitamani sana namna ya kufika tena katika ile nchi, ili apate kuwaona watu wake na nyumba ya baba yake, kabla hajafa.


Miaka mingi alikaa akingoja, na halafu alipata nafasi, maana alionana na watu weupe waliokusudia kutafuta nchi ile isiyojulikana, akafuatana nao. Wale watu weupe walisafiri wakaenda mbele tu wakimtafuta mtu mmoja tu aliyepotea.


Walivuka jangwa lenye joto, wakavuka milima yenye theluji, wakafika nchi ya Wakukuana, na pale ndipo walipokuona wewe, Ee Infadus.’

Yule Infadus akashangaa, akasema, ‘Kweli, wewe, una wazimu kusema hivyo.’ Umbopa akasema, ‘Unafikiri tu hivyo; tazama nitakalokuonyesha, Ee wewe mjomba wangu. Mimi ni Ignosi, Mfalme wa haki wa Wakukuana!’

Basi hapo alifungua nguo yake akasimama uchi mbele yetu, akasema, ‘Tazameni, hii ni nini?’ Akaonyesha kiunoni mwake amechanjwa alama ya nyoka anayezunguka kiuno. Infadus akatazama, na macho aliyakodoa kwa kushangaa, kisha akampigia magoti akasema, ‘Koom!Koom!

Ndiye mtoto wa ndugu yangu; ndiye mfalme.’ Umbopa akasema.’ Umbopa akasema, ‘Ee mjomba wangu, sikukwambia hayo? Inuka; mimi sijawa mfalme, lakini kwa msaada wako pamoja na msaada wa hawa watu weupe mashujaa walio rafiki zangu, nitakuwa mfalme.


Lakini Yule kichawi Gagula alisema kweli, yaani nchi italowa kwa damu kwanza, naye damu yake italowesha nchi pia, yaani ikiwa anayo damu, kwani ndiye aliyemuua baba yangu kwa maneno yake, ndiye aliyemfukuza mama yangu. Na sasa wewe Infadus, imekupasa uchague. Utakubali kuweka mikono yako katika mikono yangu uwe mtu wangu?


Wewe utakubali kushirikiana nami katika hatari zilizo mbele yangu, na’ kunisaidia nimwangushe huyo jeuri na muuaji, au huwezi kukubali? Chagua.’


Yule mzee alikamata kichwa akafikiri, kisha akaondoka akamjia Umbopa, yaani Ignosi, akapiga magoti mbele yake akamshika mkono, akasema, ‘Ignosi, mfalme wa haki wa Wakukuana, naweka mikono yangu katika mikono yako, nami ni mtu wako mpaka kufa.


Ulipokuwa mtoto nilikupakata nakakulea, na sasa mkono wangu ulio dhaifu utapigana kwa ajili yako na uhuru.’


Umbopa akajibu, ‘Vema, ewe Infadus. Nikishinda wewe utakuwa mtu mkubwa katika ufalme wangu chini ya mfalme mwenyewe.

Nikishindwa, hapana ila kifo, na wewe tangu hapo si mbali na kufa sasa. Simama, mjomba wangu. Na nyinyi watu weupe, mtanisaidia? Je yale mawe meupe sitaweza kuwapa? Hakika nikishinda yale mawe meupe mtayaona na kuchukua kwa kadiri ya nguvu zenu. Je, mtakubali?

Nikatafsiri maneno yake, na Bwana Henry akajibu, ‘Mwambie kuwa hafahamu tabia ya Mwingereza. Mali ni njema, nayo ikitujia tutaiokota; lakini mungwana hajiuzi kwa mali. Lakini mimi binafsi nasema haya:

Tokea mwanzo nilimpenda Umbopa, na kwa kadiri ya nguvu zangu nitamsaidia. Nitafurahi sana kujaribu kumtia adabu Yule shetani mwovu Twala.
 
Je, nyinyi Bwana Good na Quatermain, mwasemaje?’
Bwana Good akasema, ‘Waweza kumwambia ya kuwa mimi nipo tayari kabisa kumsaidia, lakini neno moja nalitaka, nalo ni kuruhusiwa kuvaa suruali zangu.’


Basi nikatafsiri maneno hayo yote, na Ignosi ambaye ndiye Umbopa akasema, ‘Vema rafiki zangu, nawe Makumazahn wewe utakuwa pamoja nami? Maana wewe ni mwindaji wa zamani mwenye uerevu kupita ule wa nyati aliyejeruhiwa.’


Nilifikiri kwanza nikajikuna kichwa, kisha nikasema, ‘Umbopa au Ignosi, mimi sipendi vita, ni mtu wa amani na tena ni mwoga kidogo (na hapo Umbopa akacheka) lakini napenda kuambatana na rafiki zangu.


Wewe ulitusaidia sisi, nami nitakusaidia wewe. Lakini mimi ni mfanyabiashara na kwa hiyo, ikiwa tutapata almasi, basi nakubali ahadi yako. Na tena, kama ujuavyo, sisi tulikuja kumtafuta ndugu yake Bwana Henry aliyepotea; lazima utusaidie kumtafuta.’

Basi Ignosi akajibu, ‘Nemekubali, lakini wewe, Infadus, apa kwa alama hii ya nyoka iliyochanjwa kiunoni mwangu kisha uniambie kweli. Mtu mweupe yeyeto ameingia katika nchi hii?

Akajibu, ‘Hapana, Ignosi.’
Ignosi akasema, ‘Mtu mweupe angalionekana au habari za mtu mweupe zingalivuma, wewe ungalipata habari?’ Akajibu, ‘Hakika ningalipata habari.’


Akamwambia Bwana Henry, ‘Umesikia, Inkubu, hakufika katika nchi hii.’ Bwana Henry akasikitika akasema, ‘Basi, basi, ni hivyo. Naona hakufika hata hapa, masikini, masikini! Tumefanya safari ya bure. Lakini ndiyo Mungu alivyo panga.’


Basi nikaona afadhali kumtoa katika fikira za huzuni, nakasema, ‘Haya, sasa tufanye kazi.

Ni vizuri kuwa mfalme wa haki, Ignosi, lakini utafanya nini upate kuwa mfalme kweli?’ Akajibu, ‘Hayo mimi sijui; je, Infadus unalo shauri linalofaa?’

Mjomba wake akajibu, ‘Ignosi, Mwana wa Umeme, usiku wa leo itakuwapo ngoma kuu ya kutambulisha wachawi. Wengi watatambuliwa na kuuawa, na wengi zaidi watajaa huzuni na masikitiko na hasira juu ya mfalme Twala.


Ngoma itakapokwisha nitasema na wakubwa, na ikiwa nitaweza, wao watasema na watu walio faraghani, nami nitawaleta kwako wapate kushuhudia kuwa kweli wewe ni mfalme. Nadhani kabla ya jua kuchomoza kesho utakuwa na mikuki ishirini elfu tayari kutii amri zako.

Na sasa lazima niende nikafikiri na kusikiliza na kuweka yote tayari. Baada ya ngoma kwisha ikiwa nita kuwa hai, tukutane hapa hapa, tutaweza kuongea zaidi. Lakini haikosi kutakuwa na vita.’


Basi hapa mazungumzo yetu yalivunjika kwa kuwa matarishi wa mfalme walikuja. Tukakaribia mlangoni na tukawapa ruhusa kuingia, kisha watu watatu waliingia na kila mtu alikuwa kachukua nguo za minyororo ya chuma iliyong’aa na iliyofumwa, na shoka zuri la vita.

Wakasema, ‘Hizi ni zawadi kutoka kwa mfalme, za watu weupe waliotoka katika nyota.’ Nikajibu, ‘Tunamshukuru mfalme.’ Basi wakatoka wakaenda zao nasi tukazitazama nguo zile. Kazi yake ilikuwa nzuri mno kupita zote tulizoona.

Nikamuuliza Infadus, ‘Je, hizi nguo zina tengenezwa hapa kwenye hii nchi?’
Akajibu, ‘Hapana, bwana wangu, tumezirithi kutoka kwa mababu zetu.

Hatujui ni nani aliyezitengeneza, na sasa zimebaki chache tu. Waana wa mfalme tu ndio wanaoruhusiwa kuzivaa. Zina nguvu kama zile za uchawi na mkuki hauwezi kuzipenya. Mtu akivaa nguo hizi katika vita yu salama.


Mfalme amependezwa sana, au ameogopa sana, maana asingewaleteeni nguo hizi. Mabwana zangu, afadhali mzivae usiku wa leo.’

Basi tulipumzika siku ile tukaongea juu ya mambo yaliyotokea. Jua lilipotua tuliona mwangaza wa mioto mingi na katika giza tulisikia vishindo vya nyayo za watu wengi na vya mikuki yao, vikosi vilipokuwa vikipita na kujipanga katika utaratibu wa kujitayarisha kwa ngoma kuu ya usiku.


Baadaye kidogo mwezi ulitoka ukaangaza nchi yote, tukasimama na kutazama mbalamwezi; akaja Infadus amevaa nguo zake nzuri za vita, amefuatana na askari ishirini, kutupeleka kwenye ngoma.

Tulikuwa tumekwisha vaa zile nguo za minyororo ya chuma kama alivyotushauri, na juu yake tukavaa nguo zetu za kila siku.

Tukajifunga bastola zetu, tukachukua mikononi mashoka yale ya vita aliyotupa mfalme, tukaondoka.

Tulipofika kwenye jumba kuu tuliona mahali palipojaa watu kiasi elfu ishirini waliopangwa kwa vikosi.

Vikosi hivyo viligawanywa katika makundi, na katikati ya kila kundi na kundi waliacha njia ili kusudi wale watakaotambulisha wachawi wapate nafasi ya kupita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…