Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umerogwa wewe ambae unalazimisha kuwa uchaguzi haukua huru na haki wakati ulikuwa fair.Hii nchi yetu ya ajabu sana, na wote tuliomo tunatakiwa kuwekwa makumbusho vizazi vijavyo waje kutushangaa; hawa wanafurahia ushindi feki, na wale wengine wanaogopa kudai haki zao uchaguzi urudiwe kwasababu haukuwa huru na haki.
Sijui tumelogwa?!
Utalalamika mpaka hata akienda kanisaniBiblia inakataza kuapa; Mathayo 5:34, lakini jamaa anaapa kwa kuishika hiyo hiyo Biblia!
Ukiona Mtu anasema CCM ni Wezi basi jua hata Yeye pamoja na Chama chake nao ni Wezi 'Wabobezi' wa 'Kura' ila safari hii wamezidiwa tu Mbinu.Hii nchi yetu ya ajabu sana, na wote tuliomo tunatakiwa kuwekwa makumbusho vizazi vijavyo waje kutushangaa; hawa wanafurahia ushindi feki, na wale wengine wanaogopa kudai haki zao uchaguzi urudiwe kwasababu haukuwa huru na haki.
Sijui tumelogwa?!
Yuko mkuu.Makonda amekaribishwa...!?
Aende tu mama mzaa uovu.Hatimae baada ya Leo ile taarifs ya Msiba wa bibi yetu utatangazwa rasmi.
[emoji23][emoji23][emoji23]Umerogwa wewe ambae unalazimisha kuwa uchaguzi haukua huru na haki wakati ulikuwa fair.
Kwa nini unapiga porojo hapa Jf badala ya kwenda Dodoma kuzia bendera ya rais isipandishwe awamu ya pili?
Kwa Jpm kuapa kwa kutumia Biblia mi kunajisi kitabu kitakatifu.Leo November 5, 2020 anaapishwa Dkt. John Magufuli kumalizia muhula wake wa mwisho kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika October 28 mwaka huu. Wageni kadhaa wameshafika akiwemo Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.
Kuwa nami kukujuza yanayojiri.
======
09: 44, Dkt. Magufuli anaingia uwanja wa Jamhuri Dodoma. Waliohudhuria uwanjani wamesimama na kupeperusha bendera za Taifa na Dkt John Pombe Magufuli anazunguka uwanja kabla ya kwenda jukwaani.
09: 49, Dkt. Magufuli anapokea salamu ya heshima kutoka kwa majeshi ya ulinzi na usalama na wimbo wa taifa unaimbwa.
09:53, Wimbo wa taifa umemalizika kuimbwa na sasa Gwaride linakwenda kukaa katika umbo la Alfa kwa ajili ya kukaguliwa hii inaonesha kwamba mamlaka ya awali yamekwisha.
09:59, Rais amemaliza kukagua Gwaride na ameagwa na bendera yake(bendera ya rais) inashushwa ili kuyavua madaraka yake ya urais wa awamu ya tano kipindi cha kwanza. Bendera sasa inashushwa rasmi polepole na mamlaka yake yanakuwa yameondoka na anabaki kuwa rais mteule anaesubiri kuapishwa.
10:05, Anaelekea jukwaani kwa ajili ya kusubiri taratibu za kuapishwa ili kuchukua mamlaka mapya ya urais baada ya yale ya kwanza kumalizika.
10:07, Rais Mteule anasogea kwenye meza ya kiapo, sasa Rais mteule anaapa. Rais mtele amemaliza kula kiapo na anatia saini kwenye hati ya kiapo. Amekabidhiwa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na sasa makamu wake anakwenda kula kiapo, na kwa sasa ameketi kwenye kiti cha jaji.
10:12, Makamu wa Rais mteule anaapa, Mama Samia Suluhu Hassan amemaliza kula kiapo na sasa anaweka saini kwenye hati ya kiapo na kisha jaji anaweka saini kuwa yeye ndie aliemuapisha.
10:15, Rais anakabidhiwa ngao na mkuki. Na sasa tukio linalofuata ni dua na sala , na viongozi wa dini wako tayari kuanza zoezi hilo.
10:32, Maanadamo rasmi kuelekea jukwaa kuu maandamo haya yatawahusu wote isipokuwa raais baada ya kukamilika kwa dua na sala, na maandamo hayo yanafuata utaratibu maalum. Rais kwa sasa hatakwenda jukwaani mpaka bendera ya rais ipandishwe na ndio zoezi linalosubiri sasa.
10:40, Wimbo wa taifa unaimbwa na bendera ya rais inapandishwa na Dkt John Pombe Magufuli rasmi sasa ni rais wa Jamhuri ya Tanzania kwa awamu ya pili. Wananchi wanapunga mikono juu kuonesha kushangilia zoezi hilo.
10: 47, Sasa gwaride linakwenda kuweka umbo la Alfa kuonesha mamlaka mapya ya Rais yanakwenda kuanza. na sasa Amiri jeshi mkuu, Rais John Pombe Magufuli anakwenda kukagua gwaride hilo likiwa katika umbo la Alfa. Sasa rais anapanda jukwaa kuu baada ya kumaliza kukagua gwaride na anasalimiana na baadhi ya viongoi wakiwemo kutoka nje ya nchi. Wimbo wataifa unaimbwa. Gwaride maalum linapita mbele ya Rais.
11:25, Rais na makam wake wanapongezwa kwa makofi na kisha utambulisho wa viongozi mbalimbali waliohudhuria kuapishwa kwa rais Dkt. Magufli unafanyika . Wimbo maalum wa kumpongeza rais na makamu wake unaimbwa, pia utafatiwa na burudani nyingine mbalimbali.