Hafla ya utiaji saini Mkataba wa Ukarabati wa Kivuko cha MV Magogoni
Hii serikali ina watu wapumbavu sana wamepewa nyadhifa humo serikalini. Wao kila kitu wanataka show offs za kipumbavu.
 
Inasikitisha sana kuona jambo dogo la utiaji saini kwa ajili ya kwenda kwenye matengenezo ya Mv Magogoni ukifanyiwa sherehe kitu ambacho hakikufanyika kwa Mv kazi japokuwa ilitengeneza hapa hapa na mzawa Songoro marine.

Leo pale kivukoni wamezuia magari na kuleta usumbufu mkubwa kwa wananchi ili uweza kufanya hiyo hafla ya utiaji saini,ukiliangalia hili jambo kiundani utakuja kugundua inaonyesha wazi wazi jinsi viongozi wetu wa zama hizi wasivyokuwa serious na kazi, kivuko cha Mv Magogoni ni cha muda mrefu kidogo na kilipaswa kupelekwa mapema sana kwenye matengenezo bila kuchelewa kwa sababu ni kikubwa na ni msaada mkubwa kwa wananchi wa Kigamboni sasa kimeegeshwa ni wiki ya 3 sasa na leo ndio inafanyika hiyo hafla kwanza kabla ya kupelekwa Mombasa kwa matengenezo.

Kilichonisukuma kuandika uzi huu ni malalamiko na minongono mingi ya wananchi mbalimbali waliokuwa wanavuka hakika wameshangazwa sana na hilo jambo wamebaki wakijiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu.

Tunaomba serikali ijaribu kuwa inaangalia umuhimu wa jambo kabla halijafanyika kwa maslahi mapana ya Taifa.

Mungu ibariki Tanzania.
Na hiyo kandarasi kapewa nani maana mombasa wamekua wanatumika na vigogo kupiga sana hela ya umma. Kila kazi ya vyombo vya majini utasikia mombasa wakati bandari na mafundi hadi wajenzi wa meli mpya tunayo tz.
 
1676562133025.jpeg
 
Duh.. Bilioni 7? na hapo ni mkataba wa awali wakianza kazi na sababu zao mara mvua zilikuwa nyingi mara vifaa vilipanda bei....sijui iutafika ngapi... lakini kwani kivuko kipya ni shilingi ngapi kama sikumbuki vizuri JK wakati anakizindua 2009 au 2010 hivi kilikuwa Bilioni 8 kama sikosei... mtaniongezea maarifa wajuzi
 
Bilioni 7 ?
Wanatengeneza nini ?
Vyuma shingapi?
Injini mpya tuseme tumebadilisha hata milioni 100 labda?
Mafundi na vitu vingine tuseme milioni 70.

Bilioni 7 ni pesa kuwezesha mashule huku watu bado wapo chini ya mawe
 
kuna Mpumbavu mwenzangu aliwahi kuniambia baadhi ya ofisi huko Serikalini hata ukiwaambia watumishi wasiwe wanalipwa mshahara ule wa TGS wapo tayari kuendelea kuhudumia watanzania wenzao hata kwa wao kuwa ndio wanalipa fee kama chuoni
 
Nakumbuka Kivuko hiki kilikuwa tia Maji tia Maji tangu enzi za Nyerere

Tupo hapa na mzee Mgaya tunajiuliza hiki Kivuko bado kipo hadi leo?

Hatari sana!
 
Mv magogoni ya Sasa sio Ile ya enzi zile
Hiki kinachotumika sasa Kilijengwa 2009,
Piga hesabu mpk sahv kina miaka mingapi
 
Huo ujinga kwa jpm haukuwepo, kama taifa,tunayo safari ndefu,na tatizo kubwa wapiga firimbi wameungana na wezi,sijui nani atapaaza sauti kulisemea taifa,

Vyama vya upinzani ni zaidi ya bunge,ndio wanatakiwa kuiamsha serikali na kuwapigia kelele watawala,cha ajabu paka na panya wameweka makubaliano,

Twaaaafaaaaaa,
sio kweli
 
Inasikitisha sana kuona jambo dogo la utiaji saini kwa ajili ya kwenda kwenye matengenezo ya Mv Magogoni ukifanyiwa sherehe kitu ambacho hakikufanyika kwa Mv Kazi japokuwa ilitengeneza hapa hapa na mzawa Songoro marine.

Leo pale kivukoni wamezuia magari na kuleta usumbufu mkubwa kwa wananchi ili uweza kufanya hiyo hafla ya utiaji saini,ukiliangalia hili jambo kiundani utakuja kugundua inaonyesha wazi wazi jinsi viongozi wetu wa zama hizi wasivyokuwa serious na kazi, kivuko cha Mv Magogoni ni cha muda mrefu kidogo na kilipaswa kupelekwa mapema sana kwenye matengenezo bila kuchelewa kwa sababu ni kikubwa na ni msaada mkubwa kwa wananchi wa Kigamboni sasa kimeegeshwa ni wiki ya 3 sasa na leo ndio inafanyika hiyo hafla kwanza kabla ya kupelekwa Mombasa kwa matengenezo.

Kilichonisukuma kuandika uzi huu ni malalamiko na minongono mingi ya wananchi mbalimbali waliokuwa wanavuka hakika wameshangazwa sana na hilo jambo wamebaki wakijiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu.

Tunaomba serikali ijaribu kuwa inaangalia umuhimu wa jambo kabla halijafanyika kwa maslahi mapana ya Taifa.

Mungu ibariki Tanzania.
ati "...Tunaiomba serikali kuwa ijaribu ..."!! ni wajibu au fadhila? WaTz tumefikishwa mbali... dah!
 
Back
Top Bottom