Hai: Zaidi ya Wafanyabiashara 36 wathibitisha kuwa na Nyaraka za uhakika kuthibitisha tuhuma za Sabaya. Waomba kukutana na mamlaka inayomchunguza

Hai: Zaidi ya Wafanyabiashara 36 wathibitisha kuwa na Nyaraka za uhakika kuthibitisha tuhuma za Sabaya. Waomba kukutana na mamlaka inayomchunguza

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hii ndio habari mpya inayosambaa Wilayani Hai kwa sasa baada ya Taarifa ya kufutwa kazi kwa aliyekuwa DC wa hapo bwana mdogo bilionea mpya Sabaya (miaka 34) , ambaye anachunguzwa kwa makosa mbali mbali ikiwemo uvamizi , uporaji wa pesa na wizi wa kuaminiwa ikiwa ni pamoja na ulevi wa madaraka , ambao kistaarabu unaitwa kutumia madaraka vibaya.

Kiongozi wa Wafanyabiashara wenye nyaraka za kusaidia uchunguzi wa Tuhuma za Sabaya ni Ndugu Swai ambaye ni Mmiliki wa hotel kadhaa za kitalii kwenye wilaya hiyo .

Nachukua nafasi hii kuwapongeza Wafanyabiashara na wananchi wote wa Hai kwa kujitolea kuanika uchafu wote wa Sabaya bila kulipwa chochote kwa lengo la kusaidia vyombo vya uchunguzi .
 
Anakwenda Jela, Good job!!
obama.png
 
Yule alosema Eti mama AJITAFAKARI ,natamani uchunguzi ukamilike alafu uanikwe wazi ndo wajue nani ajitafakari.

Tatizo ccm ya Magu ilikuwa inaona ukiwa na mawazo tofauti,basi wewe ni adui hata kama niyenye haki
 
Duh hii nchi ya ajabu sanaa mm najiuliza izo mamlaka Je zilikuwa wapi siku zote kusema mfanyabiashara alikuwa na vibali ? Yaan leo ndio wana jitokeza na kusema eti mfanyabiashara alikuwa sahihi
Mambo ya kurudishana nyuma tu.
 
Back
Top Bottom