Haifai: Mtu akikueleza tatizo usikimbilie kumshauri.

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
11,884
Reaction score
21,175
Wengine wanataka tu mtu wa kumsikiliza ajihisi nafuu. We kukimbilia kumshauri ni kama unadogosha tatizo lake. Unakuwa kama unamuona hana akili anahangaika na katatizo kadogo ambako wewe unaweza kusolve ndani ya dk chache tu.

Mtu akikueleza tatizo au changamoto anayopitia kwanza acknowledge kuwa ni tatizo hata kama unaona ni dogo. Watu tumetofautiana mtazamo na ile kuwa likiwa kwa mwenzako linaonekana dogo. Mpe ushauri kama tu ameomba au muombe ruhusa ya kumpa ushauri.

Kitu kingine. Jiepushe kutangaza ishu ya mtu aliyokuambia kwa kukuamini, wala usitumie hilo jambo kuja kumdhihaki.
 
Kuna watu wakisikia kitu ni kama wamemwagiwa upupu aisee wanawashwaaa

Alhamdulillah naweza kusikia kitu na nikanyamaza

Mimi naweza kua najua hunikubari
Unanisema vibaya na hutokaa ujue kama najua nakuangaliaa tu unavyojikomba then naendelea na issue zingine

Nia rahisi sana kwangu kuongea mambo yangu binafsi kuliko ya watu wengine
 
Kawaida masikini huwa wanapenda sana kutoa ushauri hasa kwa matajiri wakati yeye choka mbovu
Tusichokielewa tulio wengi ni kuwa, 'wazo' ni jambo linalozalishwa na ubongo wa mtu.

Mtu anaweza kuwaza jambo lenye thamani sana lakini asiwe na uwezo wa kipesa ama wa kulitekeleza.

Pia mtu mwenye uwezo wa kiuchumi si lazima awe na uwezo wa kuzalisha mawazo yenye tija.

Kwa hiyo mawazo ama ushauri si lazima utoke kwa mtu mwenye ukwasi.
 
Wengine wanataka tu mtu wa kumsikiliza ajihisi nafuu. We kukimbilia kumshauri ni kama unadogosha tatizo lake. Unakuwa kama unamuona hana akili anahangaika na katatizo kadogo ambako wewe unaweza kusolve ndani ya dk chache tu.
Upo sahihi, sana sana wanawake, kuna manzi mmoja nilikua na mahusiano nae mazuri sana tu sasa kuna siku akaniletea kesi moja fulani ya yeye na ndugu yake fulani wa kike kwamba huyo ndugu yake kuna vitu vitu anamfanyia sio vizuri na yeye hapendi huyo ndugu yake kumfanyia hivyo vitu si nikajikologa nikatoka kumpa ushauri ili tu nimalize mzozo wake nikamwaga lecture safi kabisa nikajua nimefanya kitu kizuri kitu chema jambo jema kumbe nimeharibu manzi akaanza kunichukia mimi rasmi yaan ile chuki haswa mpaka ya kupigwa na block juu nikiuliza sababu eti ni hio nimekua km nimeegemea upande wa yule niliekua namwambia asiendelee kumchukia yaan manzi akaniona km sijakaa upande wake vile kwa hio yeye alitaka yule alieniletea malalamiko yake aidha nimfanye kitu mbaya au nimuanzishie zogo kitu ambacho mimi siwezi kukifanya,

lastly mtu yoyote akija kwako kukueleza issue zake au jambo lake hua hataki kabisa ushauri wako kikubwa anachokitaka ni wewe kumsikiliza na kukaa upande wake tu basi mengine mwachie mwenyewe ili kuitatua changamoto yake km ni issue ya kifedha basi acha maneno mengi km unayo mpe km huna mwambie tu sina kisha ishia hapo acha kumjazia maushauri utaishia kumkwadha zaidi tu

Nishaishiwa maneno ya kuandika.
 
Kwahiyo tumekubaliana tusishauri, bali tusikilize tu na kusikitika.
 
Umenena vyema sana mkuu.
 
Sasa ukimwambia kweli hilo ni tatizo maana yake si nawe linaonekana kukulemea!.

Lazima ulidogoshe ili umpe kujiamini mwenye tatizo halisi ajue kweli una dawa yake.

Sasa kama daktari unaletewa mgonjwa kisha unaanza kukuna kichwa hapo mgonjwa lazima ahisi kazi anayo.
 
Mheshimu sana daktari unayemueleza ugonjwa kisha anaanza kukuna kichwa au kufungua mavitabu.
 
Back
Top Bottom