Haiingii akilini kabisa kuona nchi kama Tanzania eti tunaagiza mchele nje ya nchi! Yaani kivipi?

Nani atalima wakati nyie mnashinda mjini mnalalamika? Mkiambiwa mwende kijijini hamtaki. Fursa hiyo. Unataka nani alime?
Sensa inasema Zaidi ya 75% idadi ya watu Tanzania ni wakulima, Je bado hiyo idadi haitoshi ?πŸ˜‚
 
Na hiyo ndio Kazi Waziri anatakiwa kufanya, kutengeneza mazingira Mazuri Kwa wakulima wa tz πŸ‡ΉπŸ‡Ώ kuunza mazao Yao Kwa wingi Kwa fedha za kigeni
 
Wakenya warwanda wako wananunua mazao shamban Kwa TSH
 
Haitakaa itokee Bashe kuwa rais wa TZ.
Hata ingekuwa ni wewe BBT bajeti yake ni $600ml , ungekuwa na kiburi cha kugombea urasi,
Bashe ametuona wa tz πŸ‡ΉπŸ‡Ώ πŸ˜‚ mazoba
 
Wakenya warwanda wako wananunua mazao shamban Kwa TSH
Na wengi hawalipi hata ushuru kuna njia za panya zaidi ya 100 mipakani mwetu
Mazao yanapita kimagendo sana na ndio maana wao wanapata faida sana
 
Makonda karudishwa hushangai unashangaa "NCHELE".
 
Kuna watu mnafikiri import ni dhambi au dalili ya kushindwa. Import na export ni pande mbili za sarafu. Hakuna nchi duniani ambayo haiimport hata zile zilizoendelea. Kinachotakiwa nchi iuze zaidi nje ili ipate pesa za kuahgiza bidhaa.

Kuna watu wana taste tofauti ya kitu hicho hicho hata kama kinazalishwa nchini mwao hivyo inabidi watumie kinachoagizwa toka nje na wana haki; mfano ukienda ujerumani utakuta ntu ameagiza toyota toka Japan na ukienda Japan kuna mtu anaagiza benz tika Ujerumani. Ndivyo uchumi ulivyo nchi inachofanya inatumia nfumo wa kodi kufanya kile knachotoka nje kuwa ghali kuliko vinavyozalishwa ndani ya nchi ili kulinda viwanda vya ndani japokuwa hii inaweza kusababisha mlaji apate bidhaa mbovu za ndani kwa sababu ya kubweteka kwa wazakishaji wa ndani.
Comparstive advantage ndiyo basis ya biashara baina ya nchi na nchi. Pia ukumbuke kuna julipiziana kisasi kati ya nchi na nchi; ukizuia bidhaa ya nchi fulani naye anazuia ya kwako.

Huo mchele nenda kalime kwanza ili uone ugumu wake kabla ya kupiga kelele nchi izuie kuuza chakula nje. Mkulima analima kwa ajili ya soko kama serikali inataka hayo mazao iyabunue kupitia NFRA.
 
Kabla ya kuandika pumba kumhusu Bashe ungeuliza Je Uzalishaji Wetu vs mahitaji vikoje?

Pili Serikali inaendelea na uwekezaji wa Kilimo Cha Umwagiliaji Ili Kuzalisha zaidi na lengo sio tuu kujitosheleza Bali kuwa muuzaji Mkuu wa Nje ya Nchi
Ni aibu ya Taifa kuagiza Mchele.

Ccm hii imetufikisha pabaya
 
Mkuu umenielewa vibaya,
Haya niambie Mchele abao wakulima wa tz wameunza nje ya nchi ni $ ?
 
Kwenye wizara ya kila kuna

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula​

Na majukumu yao ni haya:

i. Kuhifadhi akiba ya chakula toshelevu kwa mahitaji ya nchi;
ii. Kununua, kuhifadhi na kutoa akiba ya chakula ili kukabiliana na majanga;
iii. Kuzungusha na kutafuta masoko ya chakula ili kupunguza mfumuko wa bei na kuingiza mapato;na
iv. Kutoa huduma mbalimbali za uhifadhi ili kuongeza mapato.

Hivyo basi, kama tumetoka kuagiza sukari , na sasa mchele
Basi nchi kama nchi hatuna akiba ya chakula.

Mama anaupiga mwingi, mwendo ameumaliza
Miaka 10 mingine kwa mama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…