Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Piganieni katiba mpya tupate viongozi wazuri. Mnawapa kina Jokate uongozi halafu mnategemea tuwe na maendeleo?Kitendo cha kuagiza mchele nje ya nchi siyo kitendo cha kukiacha kipite hivi hivi tu kama ni jambo la kawaida na halina maana yoyote. Jambo hili ni ishara mbaya sana na siyo dalili nzuri sana huko tuendako kama taifa.
Haiingii akilini kabisa kuona nchi kama Tanzania eti tunaagiza mchele nje ya nchi! Yaani kivipi? Kwamba Tanzania imeshindwa kuzalisha mchele wa kutosha ? Kwamba Tanzania mavuno ya mpunga hayakuwa mazuri au ni nini? Kwamba idadi ya watu imeongezeka ghafla binu vuu? Kama haya ni sahihi sasa je? Zile takwimu tunasomewaga pale bungeni na waziri bashe huwa anazitoa wapi? anapika takwimu? Anadanganywa? Au ni nini haswa?
LAKINI haya tuliyaonya mwanzoni kuwa Tanzania inauza sana chakula nje ya nchi na mazao ya chakula yanasafirishwa sana kwenda nje ya nchi ,tukajibiwa kuwa hayo ni mambo ya soko la EAC na hatujui kitu tukae kimya.
Round ya Kwanza, Mwaka 2021-2022 tuliagiza Mchele from Japan.
Round ya pili, 2024.
Sasa ivi tunaagiza kutoka India, wa Indi wenye maghala ya kuhifadhia chakula hapa Dar watapiga Sana mpunga kupitia Wazir bashe
Hali hii ni ishara mbaya sana na siyo ya kubeza kwa kuwa tunajua muda wowote tutatangaziwa kuwa kuwa uhaba wa mafuta ya kupikia nchini. Tulishakuwa na uhaba wa kila kitu hii ni dalili kuwa uchumi wa nchi yetu una suffocate na taifa liko kwenye CRISIS. Tujipange mapema na hakuna haja ya kufichaficha mambo.
Ivi ni lini SSH atakuja kugundua kuwa bashe anafanya biashara ya chakula kupitia wafanya biashara wa kubwa, pasipo Halali na kuliingiza nchi kwenye hasara ya kutumia fedha nyingi za kigeni kununua chakula na pembejeo .
Sasa hatuwezi kukaa kimya na kutohoji nchi inapita kwenye majanga ya kila aina na kila kona watu wanalalamika halafu tuone ni suala la kawaida tu . Hapana haiwezikuwa kawaida na lazima tuwe wakweli na wawazi kuwa tuna shida mahali na tuwe na majibu ya kuwapa wataanzania.
Hili suala la kuagiza mchele kutoka nje siyo la kubeza na ni suala linalotaka majibu na tafakari nzito sana.
Na mafuta ya kupikia wataanza kuyaficha Muda si mrefuKwenye wizara ya kila kuna
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula
Na majukumu yao ni haya:
i. Kuhifadhi akiba ya chakula toshelevu kwa mahitaji ya nchi;
ii. Kununua, kuhifadhi na kutoa akiba ya chakula ili kukabiliana na majanga;
iii. Kuzungusha na kutafuta masoko ya chakula ili kupunguza mfumuko wa bei na kuingiza mapato;na
iv. Kutoa huduma mbalimbali za uhifadhi ili kuongeza mapato.
Hivyo basi, kama tumetoka kuagiza sukari , na sasa mchele
Basi nchi kama nchi hatuna akiba ya chakula.
Mama anaupiga mwingi, mwendo ameumaliza
Miaka 10 mingine kwa mama
Mkuu waliokuwa kwenye ngazi ya maamuzi ni wakimbizi, ndio maana wanafanya maamuzi ya kuwaumiza wa tz 🇹🇿 makusudi.Piganieni katiba mpya tupate viongozi wazuri. Mnawapa kina Jokate uongozi halafu mnategemea tuwe na maendeleo?
Ukienda TRA upande wa custom utapata data mchele wa Tz umeuzwa wap i quantities value na mwakaMkuu umenielewa vibaya,
Haya niambie Mchele abao wakulima wa tz wameunza nje ya nchi ni $ ?
hawakui wapi? umetembea mkoa upi na upi kufanya research zako?Sawa nimekuelewa,
Sasa kama wakulima wanauza chakula nje ya nchi, inamaana wamepata soko la uhakika na wanaingiza Sana faida .
Je mbona uzalishali haukui uko vile vile kila siku ?