Malaika Gabrieli
JF-Expert Member
- May 28, 2020
- 3,637
- 6,896
Hatuwezi jua kuwa ni yeye au mapepo!Aiseee huyu ameonyesha wazi ndio tatizo.... Alafu ndio mke wako anaenda kumsikiliza🙆
Muhimu ni kuwa kuna mahali walifunga ndoa kabla ya kuachana... "Mwaka 2001 Phares Magesa na Haika tulioana na ndoa ilifungwa katika Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT)" akaombe toba kwa Muumba kwa kukataa kusimamia agano, la sivyo, kitamlamba!
Tatizo siyo kumiliki, je! baada ya kumiliki 100% nini kinachofuata? ubinafsi au ushirika!? kupeana talaka tu ni kuvunja agano au ushirika katika ndoa. AOMBE TOBA KWA MUNGU OR THE WORST WILL COME.
"Mke mwema, ni nani awezaye kumwona?
Maana thamani yake yapita thamani ya marijani.
11Moyo wa mumewe humwamini,
Wala hatakosa kupata mapato.
12Humtendea mema wala si mabaya,
Siku zote za maisha yake.
13Hutafuta sufu na kitani;
Hufanya kazi yake kwa moyo wote.
14Afanana na merikebu za biashara;
Huleta chakula chake kutoka mbali.
15 Tena huamka, kabla usiku haujaisha;
Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula;
Na wajakazi wake sehemu zao.
16Huangalia shamba, akalinunua;
Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
17Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi;
Hutia mikono yake nguvu.
18Huona kama bidhaa yake ina faida;
Taa yake haizimiki usiku.
19Hutia mikono yake katika kusokota;
Na mikono yake huishika pia.
20Huwakunjulia maskini mikono yake;
Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.
21Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake;
Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.
22Hujifanyia mazulia ya urembo;
Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.
23 Mume wake hujulikana malangoni;
Aketipo pamoja na wazee wa nchi.
24Hufanya nguo za kitani na kuziuza;
Huwapa wafanya biashara mishipi.
25 Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake;
Anaucheka wakati ujao.
26Hufumbua kinywa chake kwa hekima,
Na sheria ya wema iko katika ulimi wake.
27 Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake;
Wala hali chakula cha uvivu.
28 Wanawe huondoka na kumwita heri;
Mumewe naye humsifu, na kusema,
29Binti za watu wengi wamefanya mema,
Lakini wewe umewapita wote.
30 Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili;
Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.
31Mpe mapato ya mikono yake,
Na matendo yake yamsifu malangoni."