Haikuwa kazi rahisi kumng'oa Dr. Eliona Kimaro Kijitonyama, tulitumia mbinu nyingi ziligonga mwamba

Viongozi wa kanisa la KKKT walikesha kwa waganga ili kushusha nyota ya Kimaro

Kimaro ana nyota gani?. Msikuze mambo kijinga. Mwambie I aanzishe kanisa lake atoke KKKT. Mbona mwikali kaondoka na wafuasi wake na KKKT inaendelea.
 
Tunaoelewa tumekupata katika ulimwengu wa Roho. Mambumbumbu wa kiroho hawajui kinachoendelea katika ulimwengu wa roho. Endelea kutufungua bwana Kiranja Mkuu.

Acheni kujificha kwenye ulimwengu wa Roho. Hakuna Cha ulimwengu wa Roho. Huwezi kuita kanisa lako Ni madalali halafu wakakuchekea. Yani wewe ni kiongozi wa KKKT, halafu bado unalitukana kanisa lako kupitia video. Tena wamestahi walitakiwa wamfukuze kabisa. Huwezi kisema katoliki ndio misheni ya kweli wengine madalali.

Lazima afute hiyo kauli hadharani. Halafu atambue yeye ni mchungaji sio motivational speaker.
 
hayaa mambo.yapo kabisaa ukiwa na uamsho kkkt lazima ufanyiwe figisu.

kuna muinjilisti wetu alikuwa mtu wa maombi sana ila alifanyiwa figisu mpaka akatimuliwa kkkt na RC hawataki kabisaa maombi uamsho.

Hivi unajua chanzo cha yeye kasimamishwa?. Hivi mchungaji analitukana kanisa lake ni la madalali halafu aachwe hivi hivi. Wangemfukuza aende aanzishe kanisa lake akatukane vizuri huko.
 
Wengi wanaweza kufikiri umeandika ujinga sababu ya ufupi wa akili zao kuhusu mambo ya kiimani!

Ila kwa mtu muelewa na haya mambo hili uliloandika lina maana kubwa sana.

Hakuna ujinga wa kiimani kila mtu anaijua imani yake. Yule kujirusha you tube na ibafa zake kajiona yeye ndio star. Hadi kulidharau kanisa lake na kuliita kanisa la madalali. Wewe unajua kanisa lako la madalali si uondoke Kama sio unafiki ni Nini?. Huyo alitaka kufungua kanisa lake akaona aropoke ili asimamishwe aondoke.
 
Sisi waumini wake tuna jambo letu. Tutamfata na tutaanzisha kanisa letu tutaliita TRUE CHRISTIANS CHURCH.
 
Kwani Kimaro anashindwa nini kuendelea kuharibu biashara za watu akiwa Kijitonyama!!!! Acha uongo!!!!
 
Japo umetafuta tension ila ktk huu mgogoro lipo jambo la namna flani hivi maana fitina na husda zipo sana makanisani...so nyuma ya pazia lipo jambo ambalo msukumo wake ni siri ya wachache kati ya kimaro na uongozi....Mungu ataingilia kati na haki itasimama hata isipokuwa sasa itasimama tu kwa yeyote kati ya hizo pande mbili....
 
Hapa ndio umedhihirisha zaidi kwamba una akili fupi kuhusu mambo ya kiroho

Kilichomponza Kimaro ni kuongea ukweli
 
Hivi unajua chanzo cha yeye kasimamishwa?. Hivi mchungaji analitukana kanisa lake ni la madalali halafu aachwe hivi hivi. Wangemfukuza aende aanzishe kanisa lake akatukane vizuri huko.
Kiuitwa madalali sio tusi. Angeitwa aulizwe kwa nini kasema hivyo. Wajenge hoja na yeye ajibu hoja.
 
Kama ni kweli na nyie mna mwisho wenu.
 
KKKT mna bahati ya kuwa na waumini wengi nchini, mngekuwa na waumini wachache mgeipata fresh na kushika adabu juu ya migogoro yenu. Maana wachungaji kama kimaro wana ushawishi mkubwa kiasi cha kumega kanisa na kujitenga na ulutheri kwa kuanzisha kanisa jipya, kkkt ingetikisika kiuchumi na kimaendeleo kama yalivyo makanisa mengine yenye waumini wachache. Uwingi wa waumini na idadi kubwa ya wachungaji ndio kiburi cha kkkt kuedekeza migogoro na wachungaji wake kila uchao. Mara migogoro sharikani, mara jimbo, mara dayosisi, mara taifani yaani ni migogoro ya kipuuzi isiyo na tija kwa kanisa la Kristo. Anayefukuza mchungaji ni Mungu pekee, ni dhambi kubwa kumng'oa mchungaji kwa mbinu yeyote ile
 
hayaa mambo.yapo kabisaa ukiwa na uamsho kkkt lazima ufanyiwe figisu.

kuna muinjilisti wetu alikuwa mtu wa maombi sana ila alifanyiwa figisu mpaka akatimuliwa kkkt na RC hawataki kabisaa maombi uamsho.
Acha uongo alokwambia RC hawataki ni nani? Charismatic wanafanya nn sasa ndani ya kanisa? Wanachokataa ni janja janja ya hao mitume na manabii wenu wenye kuwauzia mafuta, maji, michupi mnayoiita ya upako ambayo hta nyie waumini wao hamjui imefanyiwa nn. Hakuna kanisa la Mungu linalopingana na maombi au sala.
 
Huna lolote, wewe ni mpambe wake unaejifanya kuandika kwa codes. Kimaro ni mchungaji kama wachungaji wengine. Anaweza kupelekwa popote kufanya kazi ya uchungaji, na hili halipaswi kuwa la ajabu.
 
Kwa waliosomea cuba wamekuelewa. Tumekuelewa team Kimaro. Kweli kuna viongozi wa dini wana madhabahu ndo maana hawapendi semina za maombi maana huko mnafundishwa kusali kwa kujikomboa. Sio kusali kutokana na ibada za vitabu utasema taifa zima tuna matatizo yanayofanana
 
Wewe ndiye unayetaka kuchochea hiyo migogoro kanisani. Kwani kanisa la kijitonyama ni la kwake? Akihamishwa kuna ubaya gani? Yeye kama mchungaji atahudumu popote pale atakapopelekwa kwani nako kuna wana wa Mungu wanaohitaji huduma. Acheni kuingilia majikumu ya askofu wa jimbo. Yeye ndiye aliyemleta hapo na ana haki ya kumpeleka pengine pia. Ninyi kumpenda si kigezo cha kutohamishwa kwake. Acheni roho ya ubinafsi.
 
Ameonewa gere na akina Malasusa kwasababu yupo mahali pazuri na anapiga pesa ndeefu pamoja na kukua kwa umaarufu kila uchwao. Aaanzishe kanisa late KKK(K)T, hiyo (K)=Kimaro, au KKKT Kimaro.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…