Kasiano Muyenzi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,858
- 22,729
Na watu hufanya kazi kupitia shetaniShetani anafanya kazi kupitia watu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na watu hufanya kazi kupitia shetaniShetani anafanya kazi kupitia watu
Msome kati kati ya mistari mleta mada.Utaelewa point yakeSioni uhalisia wowote wa hiki ulicho wasilisha hapa.
Na wewe ndio lichawi lenyewe.Hadithi za kutunga,utaambiwa ni mambo ya ulimwengu wa roho [emoji16][emoji16]
Wachawi mmefura.Acheni kujificha kwenye ulimwengu wa Roho. Hakuna Cha ulimwengu wa Roho. Huwezi kuita kanisa lako Ni madalali halafu wakakuchekea. Yani wewe ni kiongozi wa KKKT, halafu bado unalitukana kanisa lako kupitia video. Tena wamestahi walitakiwa wamfukuze kabisa. Huwezi kisema katoliki ndio misheni ya kweli wengine madalali.
Lazima afute hiyo kauli hadharani. Halafu atambue yeye ni mchungaji sio motivational speaker.
Siku hizi wanaume wanaendeshwa kwa HISIA kama wanawake. Hawatumii kabisa ubongo waliopewa na Mungu. Mtu anameropoka ujinga halafu kanisa limchekeeAcheni kujificha kwenye ulimwengu wa Roho. Hakuna Cha ulimwengu wa Roho. Huwezi kuita kanisa lako Ni madalali halafu wakakuchekea. Yani wewe ni kiongozi wa KKKT, halafu bado unalitukana kanisa lako kupitia video. Tena wamestahi walitakiwa wamfukuze kabisa. Huwezi kisema katoliki ndio misheni ya kweli wengine madalali.
Lazima afute hiyo kauli hadharani. Halafu atambue yeye ni mchungaji sio motivational speaker.
Mbona kajianika jamani , fungueni machoHeeee.. who are you?
Wewe chawa wa Kimaro acha kupotosha umma.Kwa msio na ufahamu wa biashara, hamna biashara isiyo na madhabahu (iwe ya asili au hizo kama za Kimaro), hamna biashara isiye na kuhani, na wala hamna biashara isiyotolewa sadaka/kafara.
Mi sidhani kama viongozi wamekurupuka. kama alikuwa anaingiza mapato makubwa na kupata waumini wengi ilikuwa jambo zuri kwa jimbo.itakuwa kuna vitu walikuwa wanamkataza katika uendeshaji wa ibada na pengine matumizi mabaya ya pesa akawa mkaidi.Maybe hiyo ime mcost.Niseme tu, hakuna marefu yasiyo na ncha.
Kilichokuwa kinatakiwa kufanyika ni kum demolish Kimaro tangu akiwa Usharika wa Kariakoo.
Kwa miaka mingi tumefanya mbinu na njama mbalimbali kumuondoa lakini hazikuwq na matokeo tuliyo yatarajia. Hivyo tukajaribu mbinu nyingine na nyingine tena, hatimaye leo mbuyu haujaanguka ila umemwagika.
Mara ya kwanza tulipofanya yetu akiwa pale Kariakoo alikimbia usharika na kwenda kujificha kwa Mapadre, na mapadre ndio waliofanya jitihada hadi akarudi tena usharikani, ila hii ya sasa harudi, na akirudi basi itakuwa zamu yetu kusalimu amri.
Kimaro alipokuwa Kariakoo, sio kwamba aliharibu taratibu za ibada hapana, hii ni cover tu, tunayoitumia.
Kimaro alipokuwa Kariakoo aliharibu biashara za wengi kwenye ulimwengu wa roho.
Watu walikuwa na madhabahu zao kubwa ambazo ziliprovide ulinzi wa pesa na mali, pia zikikuwa zikivuta mali kutoka kwa maboya wengine.
Alipofika Kimaro, wale ambao tulikuwa tukizivuta mali zao, wakaanza kumiminika kule kila alfajiri, ulinzi wa mali zao ukaanza kuongezeka, na zile biashara zao ambazo tulizifanya zisionekane na wateja zikaanza kuonekana, na taratibu taratibu wakaanza kukua na kutupora wateja wetu.
Kwa msio na ufahamu wa biashara, hamna biashara isiyo na madhabahu (iwe ya asili au hizo kama za Kimaro), hamna biashara isiye na kuhani, na wala hamna biashara isiyotolewa sadaka/kafara.
Watu wakaanza kufundishwa kutoa sadaka za maneneo na manuizi kwa ajili ya biashara zao, tukapata upinzani sana.
Kwa kushirikiana na wenzetu ndani ya kanisa, tukaanza figisu. Ibada hizo mpya zifutwe na ikiwezekana Kimaro ahamishwe Kariakoo.
Tukafanya Kimaro apitie magumu, tukakausha kabisa hali ya utoaji wa sadaka hadi kanisa likashindwa kulipia umeme na maji, tukahakikisha wanapitia kwenye hali ya ugumu kweli kweli.
Baadae Kimaro anajua alichokifanya, akapindua meza, hali ya uchumi wa kanisa ikaimarika sana, likawa pigo lingine kwetu.
Kipindi kile mkuu wa kanisa alikuwa yule jamaa wa Mbeya, tukafanya kila liwezekanalo ahamishwe. Ndipo akapelekwa Kijitonyama.
Zama zile Kijitonyama alikuwepo dogo mmoja anaitwa Kinyaha, hayo mambo ya ibada za asubuhi yalikuwa hayapo au yamekufa kabisa.
Ibada ilikuwa ikihudhuriwa na vizee vienne, wakizidi sana sita. Sasa alipokuja Kimaro sijajua alikuja na mguu upi, akaleta ibada za asubuhi na usiku.
Watu wakaanza kufurika, akaanza kununua nyumba za watu wetu na kuzifanya kuwa za kanisa. Kijitonyama yote ilikuwa ni ngome yetu.
Kata ya Kijitonyama ndio kata ina vijiji viwili mjini kati Dar es Salaam. Kijiji cha Mwenge na Kijiji cha Makumbusho. Jina na asili Kijitonyama sitaki kulielezea leo, lakini kaa ukijua kuwa ile ni ngome yetu na sehemu yetu ya kulia nyama na vitu vyetu vya kutuongezea nguvu. Kijitonyama ndiko kwenye madhabahu ya kuteketeza, ndio maana hata Wahindi miili yao huchomewa Kijitonyama.
Pale tulijaribu mbinu za kishushu, kuna kipindi tulitaka kumfitinisha na serikali kwa kupitia kijana aliyejinyonga kwa madeni aliyokuwa nayo, lakini alikwepa vihunzi kwa namna ya ajabu kabisa.
Kwetu sisi ni furaha, watu waharibifu aina ya KIMARO hawafai, wakakae huko vyuoni wafundishe. Na tutammaliza kwa njia hiyo.