Haikuwa uamuzi sahihi kusitisha ajira hata kwa Walemavu, hili kundi linataabika sana mtaani

Haikuwa uamuzi sahihi kusitisha ajira hata kwa Walemavu, hili kundi linataabika sana mtaani

Ila wewe had ukafunguke upeo wako sio leo...kwahyo uko hapo ukisubiri serikali ikukwamue?
Mwenzako kasema kamaliza degree..nikamwambia kumaliza degree ameshajitofautisha na walemavu wengine by far..ni yy kuanza kuitumia degree yake huko mtaani...
Unashindwa nn kuanzisha kituo cha tuition au hata nursery school? Kalaghabaho
Shida yako wewe hautoi masuluhisho ukiwa unafahamu hali za walemavu. Kwa mfano kufungua kituo cha twisheni au hiyo nassary ni gharama. Unamkuta mtu hata mia hana. Naomba unisaidie mtu wa aina hii anaanZia wapi.
 
Shida yako ww hautoi masuluhisho ukiwa unafahamu hali za walemavu. Kwa mfano kufungua kituo cha twisheni au hiyo nassary ni gharama. Unamkuta mtu hata mia hana. Naomba unisaidie mtu wa aina hii anaanZia wapi.
Ubaya haupo postive, ungekuwa postive ningekufungukia hapa ungejiona ulikua wapi. Bye
 
Inasikitisha sana, ivi sheria inasemaje kuhusu hili suala la ajira kwa walemavu hata kama haifuatwi.

Hili kundi haitakiwi kusahaulika kiasi hiki hata kama mambo mengi makubwa yanatekelezwa
Wangefuata sheria inavyosema hakuna mtu mwenye ulemavu na sifa za kuajiriwa ambae angekuwa hajaajiriwa. Sikumbuki ni sheria ya mwaka gani lakini inasema taasisi yenye wafanyakazi kuanzia 100 na kuendelea basi inatakiwa kuwa na wafanyakazi walemavu angalau 3%. Sasa chukua Serikali Kuu, Serikali za Mitaa pamoja na taasisi zake zote, hapo kuna wafanyakazi angalau 500K; huko peke yake kulitakiwa na wafanyakazi walemavu angalau 15,000. Kabla hatujaangalia taasisi binafsi, je huko serikalini walemavu walioajiriwa wanafika 15K?!
 
Serikali imetoa ajira kwa walemavu walimu ila kada nyingine zimesahaulika.
Tunaomba wafikirie na kada zingine kunusuru hili janga la ukosefu wa ajira kwa walemavu.

Ikumbukwe pia, serikali ndio tumaini la walemavu maana mashirika yasiyo ya serikali ukiwaeleza/wakikuona una ulemavu kupata nafasi ni nadra sana kwani wao wanachoangalia ni faida kwenye shirika lao jambo ambalo wanahisi mlemavu anaweza kuchelewesha malengo yao na hatimaye hupati nafasi
 
Ila wewe had ukafunguke upeo wako sio leo...kwahyo uko hapo ukisubiri serikali ikukwamue?
Mwenzako kasema kamaliza degree..nikamwambia kumaliza degree ameshajitofautisha na walemavu wengine by far..ni yy kuanza kuitumia degree yake huko mtaani...
Unashindwa nn kuanzisha kituo cha tuition au hata nursery school? Kalaghabaho
Tuchukue mfano kuanzisha tuition, pale itahitajika vitendea kazi kama darasa/ukumbi, mabench ya kukalia. Hivi vitu viwili huwezi kuvipata bure na ukiwa huna hata senti ni janga. Ndio maana tunasema tuwezeshwe kulingana na hali zetu.

Mtu kama huyu ni rahisi kumuwezesha na akainuka vizuri tu, hicho ndicho cha muhimu(kushikwa mkono)
 
Wangefuata sheria inavyosema hakuna mtu mwenye ulemavu na sifa za kuajiriwa ambae angekuwa hajaajiriwa. Sikumbuki ni sheria ya mwaka gani lakini inasema taasisi yenye wafanyakazi kuanzia 100 na kuendelea basi inatakiwa kuwa na wafanyakazi walemavu angalau 3%. Sasa chukua Serikali Kuu, Serikali za Mitaa pamoja na taasisi zake zote, hapo kuna wafanyakazi angalau 500K; huko peke yake kulitakiwa na wafanyakazi walemavu angalau 15,000. Kabla hatujaangalia taasisi binafsi, je huko serikalini walemavu walioajiriwa wanafika 15K?!
Daa, hilo ndio tatizo kubwa sasa, sheria haifuatwi kabisa. Na siku hizi bila kujuana kupata kazi imekuwa jambo ngumu sana
 
Tuchukue mfano kuanzisha tuition, pale itahitajika vitendea kazi kama darasa/ukumbi, mabench ya kukalia. Hivi vitu viwili huwezi kuvipata bure na ukiwa huna hata senti ni janga. Ndio maana tunasema tuwezeshwe kulingana na hali zetu.

Mtu kama huyu ni rahisi kumuwezesha na akainuka vizuri tu, hicho ndicho cha muhimu(kushikwa mkono)

Hamuelewi tu siri ya kuanza mwenyewe then ndo uwe pushed...hv sasa nin maana ya kuwa kwenye jamii inayokuzunguka? Yaan umekaa hapo una idea ya kufungua tuition lakin unakaa unasubiri mtendaji akuletee vitendea kazi?? Hv uko serious kweli? Unashindwa nn kupita nyumba kwa nyumba mtu kwa mtu kuomba akuchangie dawati? Anza kwanza kuoambna mwenyewe thrn atatokea mtu atakupush...mngekuwa mnasadiki tungeweza kuwekaga shuhuda humu msadiki ..hakuna mafanikio rahis..kubali kuteseka..kubali kukataliwa..hata hiyo mifuko ya jimbo sijui mafungu ya walemavu unadhan yatatosha sasa kwa aina hii ya mawazo? Aisee safari bado ndefu..nakuhakikishia ukiendelea kusubiri kuwezeshwa na serikali utaishia kuwa maskini...tena fukara mno! Maisha yako yako kiganjani mwako...amka..simama on your feet...
Unashindwa kuomba kikuku ki1 kwa jirani ukakilea ukaanza ufugaji kutafuta mtaji? Walau upate kuku 40 ukiuza kila kuku 10000 huna laki 4 hapo? Hujapata madawati ya tuition hapo hata m5? Au viti vya plastick hata 6?Shida mnataka hela za papo kwahapo...HAKUNAGA🙋
 
Shida yako wewe hautoi masuluhisho ukiwa unafahamu hali za walemavu. Kwa mfano kufungua kituo cha twisheni au hiyo nassary ni gharama. Unamkuta mtu hata mia hana. Naomba unisaidie mtu wa aina hii anaanZia wapi.
Kuhusu kukosa mtaji hata tusio walemavu inatuhusu, mtaji hakuna lkn ndo tunapaswa kutumia akili kutafuta huo mtajji. Mkuu wewe ni mlemavu wa kiungo gani?
 
Kuhusu kukosa mtaji hata tusio walemavu inatuhusu, mtaji hakuna lkn ndo tunapaswa kutumia akili kutafuta huo mtajji. Mkuu wewe ni mlemavu wa kiungo gani?
Kwanza serikali haiwez ikakupa mtaji kizembe namna hiyo...yaan maisha haya bora uchanwe live tu... maisha magumu kweli lakini napinga kbs serikali kuja kukupa mtaji...umekaa tu eti unasubirinkushikwa mkono..lol
 
Kupewa mtaji na serikali ni kujiendekeza, na wengi watapewa lkn hawatafanyia kitu zaidi ya kula na kunywa ..tatizo litabaki pale pale.
Siku hizi jamani kuna biashara za kila Aina..hata kwa 20,000 mtu anaanza biashara..ukipambana unapata mtaji ambao unataka. Vijana mjini wameamka yaani kila biashara inafanywa Ili mradi maisha yaende.
Binafsi sijafikia ninapotaka ila namshukuru Mungu naiona mbele yangu. Nilishalia mtaji weee Lkn nikaona ni kazi bure..hatakuja tokea mtu akupe mtaji hata ndugu yako hakupi.
So nikupambana kuanzia chini kabisa.

Walemavu ninaowaonea huruma ni wale wasioona. Ila mlemavu alie na mikono inayofanya kazi tena msomi mwenye degree yake kulilia kupewa mtaji kwa kigezo cha ulemavu sio sahihi. Apambane Kama sisi..
Ukute alikuwa anapata mkopo..angeweza kutoa hapo 200,000 ya mtaji. Ila ndo hivyo vijana tunawaza kupata mtaji mamilioni ili tufungue makampuni makubwa. Kwa maisha ya sasa haitatokea...pesa imekuwa ngumu kupita maelezo.
Tuache kulialia kila siku..tumesharahisishiwa biashara kitambulisho Cha mjasiriamali 20,000 kwa mwaka. Tufanye chochote kile ila ndo hivyo sie tunaojiita wasomi tunaona aibu.
** Wengi wanaolalamika (hata wasio walemavu) ni wale tunaojiita wasomi. Tunawaza mambo makubwa ingawa kiuhalisia hayapo hivyo.

**Kuna shughuli kibao za kutengeneza vitu...YouTube imejaa madini kibao yaani ukiwa mtu wa kupenda kutengeneza vitu Kama mimi hukosi cha kufanya. Kinachobakia ni kutafuta wateja tu..na Kama kazi yako nzuri hukosi wateja ingawa changamoto hazikosekani pia, kikubwa ni kujaribu na sio kulialia.
Ajira hakuna watu wajiongeze
 
Back
Top Bottom