Kisiwa cha Hainan hakifahamiki kwa waafrika wengi, kama ilivyo miji mingine ya China kama vile Beijing, Shanghai au Guangzhou, lakini inaaminika kuwa katika siku za usoni, kisiwa hiki kitakuwa moja ya maeneo mapya yenye motomoto ya ushirikiano kati ya China na Afrika, haswa katika sekta ya sayansi ya kilimo.
Rais Xi Jinping wa China hivi karibuni alipofanya ziara ya ukaguzi mkoani Hainan, alisisitiza kwamba mbegu ni msingi wa usalama wa chakula. Usalama wa chakula wa China unaweza kuhakikishwa, kama mbegu zitadhibitiwa kithabiti na wachina wenyewe.
Hainan, kisiwa cha tropiki kilichopo kusini mwa China, na hali ya hewa yake inafanana na ya nchi nyingi za Afrika. Kwa hiyo, katika miaka ya hivi karibuni, mawaziri wa kilimo, mabalozi wa nchi za Afrika hapa China na wataalamu na wasomi zaidi ya elfu 2 kutoka karibu nchi 30 za Afrika, wamekwenda Hainan kubadilishana maoni na wenzao wa China katika sekta ya sayansi ya kilimo cha kitropiki. Wakati huo huo, katika mapambano dhidi ya umaskini uliokithiri, Hainan nayo imepata mafanikio na kuungana na sehemu nyingine za China kuingia katika jamii yenye maisha bora. Inaaminika kuwa katika siku zijazo, Hainan iatakuwa ni mahali penye uzoefu wa kueleza mafanikio yake ya jinsi ya kupambana na umaskini kupitia kilimo na watu wa sekta mbalimbali barani Afrika.
Hali ya sasa ya kimataifa yenye utatanishi imefichua umuhimu wa kuhakikisha kwamba kujitegemea kwenye rasilimali za mbegu na chini ya udhibiti bora, ni lazima kufikiwe katika teknolojia ya mbegu.” Wachina husema mafanikio yanatokana na jasho, na kwamba nchi za Afrika zinapaswa pia kufanya vizuri kazi hii kubwa na kuimarisha kithabiti msingi wa usalama wa chakula.