Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari zenu wanaJF wenzangu,
Hawa jamaa wawili ni kama vile wamepewa majukumu makubwa wasiyoyaweza. Watu wanatekwa, wanauwawa na wengine kupotezwa kimya kimya wao wanaangalia tu. Sasa sijui jukumu la waziri wa mambo ya ndani na IGP ni nini?
Sikatai kwamba inawezekana polisi au serikali haihusiki na yanayoendelea, sikatai kwamba inawezekana kuna kundi la majambazi na watu wasioitakia mema nchi yetu wanaweza kufanya haya ili zigo liiangukie polisi na serikali, lakn wao kama serikali kupitia vitengo vyao vya upelelezi wamefanya nini kuzuia haya yasiendelee kutokea?
Inashangaza katika nchi tunayosema ni ya amani askari anashindwa hata kuvaa sare kwenda kumkamata mtuhumiwa kweli!! Je sare za polisi zilishonwa kwa ajili ya kina nani?
Unakuta kundi la watu wanne au watatu likiwa limevaa nguo za kawaida, eti linaenda kumkamata mtu mwembe chai, likiulizwa nyinyi ni kina nani linasema sisi ni askari kutoka mwenge tumekuja kumkamata mtuhumiwa.
Sasa unajiuliza inakuaje askari atoke mwenge kuja kumkamata mtuhumiwa mwembechai, je magomeni askari wameisha, kwanini wasitumiwe askari wa magomeni kumkamata mtuhumiwa? Hiyo tisa, kumi je kwanini hawana sare za polisi, RB, barua ya mjumbe au mwenyekiti wa serikali ya mtaa nk.
Sasa kwa style hii ya ukamataji mnafikiri watu wabaya hawatokosa kujipenyeza ni kufanya haya kwa maadui zao wakijua kwamba jumba bovu litawaangukia polisi na mamlaka?
Kwanini hamrudishi utaratibu mzuri wa ukamataji wa kufuata sheria? Au mpaka mtumbuliwe ndo muanze kufikiria ambayo mngefanya. Maana tumeshaanza kusikia mpaka wanafunzi na viongozi wa dini wanapotea na wengine kukutwa wameuwawa.
Kuna uwezekano mkubwa wa Masauni na Wambura kukalia kuti kavu. Very soon time will tell us...