Haitopita miezi miwili bila Waziri Masauni au IGP Wambura kung'olewa ofisini

Yaani wanamuaminisha Mh Rais mambo uongo na bado wapo Ofisini hadi leo ni ajabu kabisa.
 
Yaani wanamuaminisha Mh Rais mambo uongo na bado wapo Ofisini hadi leo ni ajabu kabisa.
Hawa dawa yao ipo jikoni. Wangesoma dalili za nyakati kabla hawajatumbuliwa na kuaibishwa kwa kutumbuliwa kwao.
 
Hawa dawa yao ipo jikoni. Wangesoma dalili za nyakati kabla hawajatumbuliwa na kuaibishwa kwa kutumbuliwa kwao.
Hakuna lolote, rais anajua kila kitu na haya yanayofanyika sasa ni mpango wake kutisha wapinzani kuelekea uchaguzi chaguzi. Hata akiwatumbua hao itakuwa ni funika kombe mwanharamu apite, lakini huu utekaji na mauji ya wapinzani yeye ndio msimamizi.
 
Mwanzoni kama wewe na wengine wengi, Masauni na Wambura nilidhani Watakalia kuti kavu.
Lakini baada ya kusikiliza hotuba ya Malkia chura kiziwi... Naomba tu nikwambie... MASAUNI, WAMBURA & Co. wana baraka zote!
 
Nani Kakudanganya!?
 
Hawa walipaswa kuondoshwa mwezi uliopita.
 
Ana wake wawili huyo, wanahitaji mpunga.
 
Hakuna lolote, rais anajua kila kitu na haya yanayofanyika sasa ni mpango wake kutisha wapinzani kuelekea uchaguzi chaguzi. Hata akiwatumbua hao itakuwa ni funika kombe mwanharamu apite, lakini huu utekaji na mauji ya wapinzani yeye ndio msimamizi.
Inawezekana ikawa kweli anahusika, au inawezekana pia akawa hausiki. Lakini kama anahusika atakuwa anahusika kwa sababu ipi ikiwa inaaminika kuwa katiba iliyopo hata wapinzani wakimsimamisha malaika, na CCM ikasimamisha jiwe, bado jiwe litamshinda malaika kwa kura nyingi zaidi katika uchaguzi.

Mimi nahisi kuna watu fulani, au wanasiasa fulani wanatumia ukimya wa serikali kufanya yao, kwa vile wanaona serikali haina muda wa kushughulikia haya yanayoendelea, hivyo kila mtu anatumia mwanya huo ku deal na adui yake kwa kisingizio cha wasiojulikana.

Hata panya road walipokuwa wanauwa na kujeruhi watu, serikali ilikuja kuingilia kati baadae kabisa baada ya kelele nyingi kutoka kila kona ya nchi. So sidhani kuwa na wao walikuwa wanatumwa na raisi.
 
Hawa walipaswa kuondoshwa mwezi uliopita.
Kama ni waerevu wangetoka mapema kabla ya kusubiri kuvuliwa nguo kama kina January. Na wao ilikuwa ni hivi hivi wakavimba vichwa na kujiona kuwa hawawezi kufanywa lolote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…