Safi sana.haya mambo wakubwa muwe mnasema kuna vi-broiler vinahisi Simba na Yanga ni maadui wa kupigana mpaka kuuwana.
Hakuna kitu kama hicho, hakunaga upendo wa dzaini hiyo kwenye hizi d3rby
Hapa tu, tulipo bado tunaombeana kufungwa na timu za nje katika mashindano ya kimataifa
Tunaombeana dua timu zitolewe mapema na timu za nje ili mradi tu kumuona mtani wako ana safa
Niambie huo upendo wa Yanga kumuachia Simba amfunge ili asishuke daraja unakujaje?
Wakati hata hapa kuna watu wanataka timu ishushwe daraja ili wao watambe
Katika huo mwaka ambao mtoa mada kautaja siku ya hiyo mechi ilikuwa inamtegemea Yanga kutangazwa ubingwa endapo atashinda au kutoa sare
Dakika ya 21 simba alipachika bao lakuongoza kwa mchezaji Edward Chumila
Kumbuka hapo simba alihitaji matokeo ya ushindi ili kuweza kusalia ligi kuu
Yanga wakaja kusawazisha dakika ya 36 na kufanya mpira uende mapumziko kwa droo ya moja moja
Dakika ya 58 kuna player wa simba alijulikana kama zigzag huyu alitupia kamba bao la pili la kuongoza na hili ndio lilidumu mpaka mwisho wa mchezo
Sio kweli kuwa Yanga aliisaidia simba isishuke daraja kwasababu kichapo walichopigwa Yanga kiliwafanya wakose ubingwa ambao nao walikuwa wanautegemea
Kongole ya mtu aliyeinusuru Simba isiweze kushuka daraja ni huyo zigzag kwa kufunga bao la pili, the rest ni kujipa ujiko ambao wote tunajua haiwezekani hata kwa namna yeyote Yanga kumsaidia Simba