Vijana wengi mtakuwa hamna kumbukumbu ya huu msimu.
Yanga ilikubali kufungwa na Simba mechi ya mwisho ili simba isishuke daraja na kwa kufungwa huko Yanga ikakosa ubingwa.
N.B kwa new school aka "soccer Google" nawakumbusha "zamani" game moja ilikuwa na pointi 2 ukishinda!
Upendo huu haujawahi kutokea na haitokuja kutokea tena.
Mtu na Mai Wake [emoji172][emoji169]
View attachment 2230677
Utopolo Msijifiche kwenye kichaka cha huruma.
Hii gemu mlifungwa kihalali na Simba na wala hamkuwa na suala lolote la kuisaidia Simba isishuke daraja.
Nakumbuka Yanga walikuja na Ngoma pamoja na kinyago aliyejipaka masizi uso mzima,
Pia walishaandaa t-shirts za yanga bingwa -1988..
Yote hayo yalikuwa ni maandalizi ya kusheherekea ubingwa ..
Matokeo yake kinyago alisubiri Giza liingie ndy aweze kuondoka.,na Ngoma zilifuatwa siku ya pili.
Hyo ni baada ya lile genge zima la kikundi cha mdundiko wa maleft kusambaratika,na kutelekeza vifaa vyao na kukimbia kusikojulikana.
Hizo t-shirts zao za ubingwa walizivaa nyumbani kama night dress..
Nakumbuka kama sio John makelele( zig zag)
Au Edo boy ndy aliyepeleka kilio kwa utopolo.
Yanga alifungwa sababu ya kujiamini kwake..
Simba waliondoka kishujaa huku mashabiki wao wakisukuma bus la wachezaji hadi Msimbazi ,
Makao makuu ya Simba sports club.
Sasa hebu fafanua vizuri,
Ilikuwaje timu iliyopanga kuiokoa Simba ijiandae na mambo yote hayo?